CHADEMA ni ngangari, usipoielewa utadhani imedhoofika kwa hama hama ya wabunge na madiwani wake

2015 ulafi wa viongozi wenu kumfukuza Dr. Slaa na kumchukuwa mliemwita fisadi ndo unawatokea puani Sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Ni kweli makosa hayo yalifanyika. Naomba nikiri kuwa kama chama cha siasa wakati mwingine maamuzi ya ki- mkakati (ya haraka haraka), yanaweza kuwa na makosa kwani wahusika hawana muda mwingi wa kufikiri.

Chadema imejifunza kutokana na makosa, sasa hivi kimekomaa kweli kweli na makosa hayo hayatajirudia tena. Wananchi na wapenzi wa chadema wamekielewa chama.
 
Upo sahihi kabisa
 
Kama kawaida yetu wana cdm tuzidi kuwa na uvumilivu wa kukibeba chama chetu bila kusikiliza miruzi ya wapinzani wetu.

Ukiona kila mtu anakuongelea wewe kila siku basi jua kuwa anakuogopa
Shetani kamwe hawapendi walio wa haki na wenye uimara wa moyo.
Huwapenda anaweza kuwayumbisha atakavyo.
Hapa amebuma na mwaka huu atalia kwa kikwao
We shall overcome. Amen
 
Mapandikizi ya ccm yote yanarudi kwao na itafika muda cdm itabakia na wana cdm wenye mapenzi ya dhati
hakika tunahitaji wanachama wenye misimamo wanoamini katika vikao ukionewa unasubiri vikao unatowa dukuduku lako
 
Hizo ni dua za kuku dhidi ya mwewe, na hizo ngonjera zenu hazikuanza leo hii maana walikuwepo kina Wasira na Kombani walio itabiria cdm anguko baya sana lkn leo hii wapo wapi?
 
Ccm ilishajifia kitambo wacha waongee hao vijakazi wa lumumba
 
Nakushauri wacha kupoteza muda wako kumjibu huyo ndumilakuwili wa lumumba
 
Mtoa mada kumbuka kuzeeka na kifo ni sehemu ya ukuaji pia.
 
Jazba haisaidii,ningeona kama ni hekima kutaka kufaham chama chetu pendwa kina fail wapi?matokeo yake mnakuja na ubishi na kebehi+jazba sizokua na mashiko,Chama kisichoshaurika..tunakaa pembeni tunawatazama.
 
Tunataka kwanza kujua zilipo 1.5 trillion
Mbona Prof. Asad alishajibu hilo, kwamba hakuna hela iliyopotea.

Haya sasa tuambie Mwamba keshakwenda kwa Gen Mbungo au bado anapiga vyenga?
 
Kimsingi ukuaji wa CHADEMA toka ianzishwe ni chama kilichokuwa hatua baada ya hatua, kama mtoto mdogo anavyokuwa. Huanza kutambaa, kukaa, kusimama na hatimaye kutembea.
Mkuu, malizia hatua za ukuaji ili tujue kipo wapi na kinaelekea wapi. 😎😎😎😎😎
 
Kimsingi upinzani upo hata katika utawala wa chama kimoja, kinachokosekana katika utawala wa chama kimoja ni katiba tu inayoidhinisha mawazo mbada kuwa na uwanja wake. Ni vyema wenzetu wa Lumumba waelewe kuwa, ni ukweli usiofichika kuwa hata kama mkuu anapendwa kwa aliyoyafanya lakini kuna aliowakwaza vile vile. Miongoni mwao ni pamoja na wasioajiriwa (wahitimu wa vyuo vikuu na vya kati), wakulima, mafisadi, matajiri n.k. Ukidhani kuwa waliokwazwa ni mafisadi peke yao unakosea.

Kwa maana hii ni mawazo mafupi sana kufikiria eti Chadema ikifa ndio mwisho wa kukabiliana na upinzani. CCM inabidi iwe na mawazo marefu zaidi na mapana ya kutatua kero za wananchi, kuliko kudhani kuwa wanapambana na majina ya vyama.

Katika hali ya kawaida si rahisi kwa chama kimoja kiweze kutetea wakulima, masikini, wafanya biashara, wafanya kazi, wasioajiriwa (wahitimu) matajiri na wenye viwanda na wachimbaji wa dhahabu/madini. Kama kipo chama kama hicho basi ni chama cha kichawi.
 
Mkuu, malizia hatua za ukuaji ili tujue kipo wapi na kinaelekea wapi. 😎😎😎😎😎

Chadema sasa hivi inatembea mwendo wa kijeshi 100 meters/min, inatafuta gia ya mwendo kasi. Ikipatikana hiyo, Lumumba watahamia kuzimu.
 
Wacha songombingo hizo twambieni 1.5 trillion ziko wapi?
Mbona Prof. Asad alishajibu hilo, kwamba hakuna hela iliyopotea.

Haya sasa tuambie Mwamba keshakwenda kwa Gen Mbungo au bado anapiga vyenga?
 
Chadema sasa hivi inatembea mwendo wa kijeshi 100 meters/min, inatafuta gia ya mwendo kasi. Ikipatikana hiyo, Lumumba watahamia kuzimu.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Mkuu, jibu swali vizuri bhana. Kipo katika hatua gani ya ukuaji? maana hata watoto wanakufa, vijana, watu wazima na hata wazee pia.
So kwa ulewa wangu kinaweza kufa katika stage yoyote ile.
Kwa maoni yangu, chadema inahitaji kuto dharau yanayosemwa nakuona kama wanakosea kuwakosa. hata mtoto anapokosea huwa analekebishwa. Sasa cdm wanaona tayari wameshapita kuwa watoto sasa ni wazee ambao kijana hapaswi kuwalekebisha ndio maana watapotea tu kama nccr.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…