NAPE AWAPONDA CHADEMA
>.Asema ni vibaraka waliobobea.
>.Adai wanawapotezea watu muda mikutano ya Katiba
>. Ajivunia utaratibu uliotumiwa na CCM
>. Adai wanachofanya Chadema ni uhuni
>. Ampongeza Warioba kukataa maoni ya helkopta
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndg. Nape Nnauye amewaponda Chadema na utaratibu wanaotumia kukusanya maoni ya wananchi juu ya rasimu ya kwanza ya katiba kuwa ni uhuni na kuwapotezea watu muda.
Nape akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma alipokuwa akielezea ratiba ya vikao vya CCM vya kitaifa alisema,"sisi tunakutana kupitia maoni ya wanaCCM waliotoa maoni yao juu ya rasimu ya kwanza ya katiba, lakini wakati sisi tunafanya hivyo watani zetu wameamua kuwapotezea muda wananchi kwa kufanya uhuni wa mikutano ya hadhara huku wakijua kuwa ni kinyume na sheria inayoongoza mijadala ya rasimu hiyo ya katiba"alisisitiza Nape.
Lakini Nape pia alimpongeza mwenyekiti wa Tume ya mabadiliko ya katiba nchini Jaji Warioba kufuatia kauli yake kuwa atapokea maoni ya taasisi sio ya helkopta.
"Jaji warioba kawatendea haki hawa watani, sheria inataka taasisi ikae kama baraza sio ikafanye mikutano ya hadhara.Kasema sawa sawa, hawatapokea maoni ya helkopta ila ya taasisi sasa sio busara hawa jamaa kuendelea kupoteza muda wa watu".
"Lakini najua wataendelea tu kwasababu inabidi watoe hesabu ya pesa walizopewa kwa kazi hii.Watafanyaje sasa zaidi ya kuruka na chopa ili wakidhi matakwa ya waliowatuma,ndo tabu ya vibaraka!"alisisitiza Nape.
Kuhusu vikao alisema sekretariete ya CCM imekutana kwa siku tatu mjini Dodoma kuandaa kamati kuu inayokutana kesho na Halmashauri kuu inayokutana tarehe 24 -25/08/2013.
Big up Nape,naona umewafundisha kazi hawa vijana wadogo kwenye siasa,naomba watambue kua siasa sio mchezo wa kukurupuka,kwanza inabidi Chadema wauambie Umma fedha hizo wamepata wapi wanazotumia kuzunguka kwa helikopta nchi nzima,ni nani anaewatumilia ili watoe maoni waliyotumwa na bwana wao.
Hawa Chadema ndio vibaraka aliowaona Mugabe,western Puppets.
'KURUKA RUKA KWA MAHARAGE NDIO KUIVA KWAKE'ccm mtaondoka tu madarakani hata ingekuwa vipi.Mlianza na kuipakazia Chadema kuwa ni ya kidini/ya kikabila/ya kikanda/Ya kigaidi na sasa mnaiita ni ya kihuni na wewe umepigilia msumari kwa kuiita shetani!!!!!.
nampongeza Nape kwa kauli yake hiyo. chadema si tu vibaraka bali ni wahuni na waladi wakubwa