CHADEMA ni vibaraka - Nape

CHADEMA ni vibaraka - Nape

NAPE AWAPONDA CHADEMA
>.Asema ni vibaraka waliobobea.
>.Adai wanawapotezea watu muda mikutano ya Katiba
>. Ajivunia utaratibu uliotumiwa na CCM
>. Adai wanachofanya Chadema ni uhuni
>. Ampongeza Warioba kukataa maoni ya helkopta

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndg. Nape Nnauye amewaponda Chadema na utaratibu wanaotumia kukusanya maoni ya wananchi juu ya rasimu ya kwanza ya katiba kuwa ni uhuni na kuwapotezea watu muda.

Nape akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma alipokuwa akielezea ratiba ya vikao vya CCM vya kitaifa alisema,"sisi tunakutana kupitia maoni ya wanaCCM waliotoa maoni yao juu ya rasimu ya kwanza ya katiba, lakini wakati sisi tunafanya hivyo watani zetu wameamua kuwapotezea muda wananchi kwa kufanya uhuni wa mikutano ya hadhara huku wakijua kuwa ni kinyume na sheria inayoongoza mijadala ya rasimu hiyo ya katiba"alisisitiza Nape.

Lakini Nape pia alimpongeza mwenyekiti wa Tume ya mabadiliko ya katiba nchini Jaji Warioba kufuatia kauli yake kuwa atapokea maoni ya taasisi sio ya helkopta.
"Jaji warioba kawatendea haki hawa watani, sheria inataka taasisi ikae kama baraza sio ikafanye mikutano ya hadhara.Kasema sawa sawa, hawatapokea maoni ya helkopta ila ya taasisi sasa sio busara hawa jamaa kuendelea kupoteza muda wa watu".
"Lakini najua wataendelea tu kwasababu inabidi watoe hesabu ya pesa walizopewa kwa kazi hii.Watafanyaje sasa zaidi ya kuruka na chopa ili wakidhi matakwa ya waliowatuma,ndo tabu ya vibaraka!"alisisitiza Nape.

Kuhusu vikao alisema sekretariete ya CCM imekutana kwa siku tatu mjini Dodoma kuandaa kamati kuu inayokutana kesho na Halmashauri kuu inayokutana tarehe 24 -25/08/2013.

Ingawa mimi sina chama chochote lakini kwa hili la Chadema bwana security guard umeongea la msingi sana. Mpaka sasa hivi hakuna chama cha kweli cha ushindani. CCM hawana mshindani wa kweli. Chadema wanaendesha mambo kama wanatumwa vile. Sijawaona wakionyesha uzalendo hasa kwa Taifa lao. Naona bado wana kazi sana ya kukifanya chama chao kiimalike na kujipatia watu wenye uwezo na moyo wa uzalenda na maarifa ya kiuongozi. Mpaka sasa hivi mimi binafsi bado sijaona mtu mwenye uwezo wa kuongoza Taifa. Labda yule kijana wetu Mheshimiwa Kabwe ndiye namuona kuwa na hekima ya kiutu uzima. Mimi nimevunjwa moyo na uchochezi na fujo zinazosimamiwa na viongozi wa hiki chama kwa kutumia neno "NGUVU YA UMMA" naona kama kuna ka upuuzi vile. Huwa najiuliza hivi kwani siasa ni lazima ziendeshwe kwa fujo? ukiendesha kiustarabu haziwi siasa za upinzani? kwani upinzani ni nini? si nitofauti ya mawazo tu? kwani ni kufanya fujo? mimi hata raha imeondoka kwa hivi vyama...
 
Warioba anaposema hapokei maoni ya helikopita anamanisha nini hasa?
 
Ndo napompendea nape hapo. Anawapa za uso bila kupepesa macho
 
Chadema hawatofautiani na MDC ya Morgan Tsvangirai. Baba yao Tonny Blair. Kitawakuta kama kilichowakuta Tsvangirai na Raila
 
ndiyo maana anaitwa nape nauye maana yake napepea naauye(kikwetu kokote kuelekea kubaya kuzuri naauye)
 
Big up Nape,naona umewafundisha kazi hawa vijana wadogo kwenye siasa,naomba watambue kua siasa sio mchezo wa kukurupuka,kwanza inabidi Chadema wauambie Umma fedha hizo wamepata wapi wanazotumia kuzunguka kwa helikopta nchi nzima,ni nani anaewatumilia ili watoe maoni waliyotumwa na bwana wao.

Hawa Chadema ndio vibaraka aliowaona Mugabe,western Puppets.

Acheni kushabikia kitu ambacho hakina manufaa kwa Taifa.Kuwaita CHADEMA kuwa ni vibaraka au wahuni ndiyo hicho ambacho Nape na CCM yake wametumwa na wananchi kwenda kukifanya?au inamaana CCM imekosa maoni ya kupeleka kwenye tume ya katiba kiasi cha kuanza kutafutiza mipasho ya kupeleka kwenye tume?au CCM wanarasimu tofauti na ile iliyotolewa na tume ya katiba inayowataka wapeleke maoni hayo mafu wanayoyajadili kwenye vikao vyao.
 
Basi hili nalo ishauriwe ccm iweke hiki nalo ktk katiba hhhhh chadena vibaraja. Heru kibaraka asiye fisadi. Wanataka kutumia uchaguzi wa zimbabwe say tz !=zmbw
 
Vipi lile swala la madiwani kule Bukoba? Nape utawasilisha zile barua walizowasilsha kwako za kukata rufaa? nina wasiwasi kesho utakanusha kwamba hujasema Chadema Wahuni. umemnukuu Warioba wakati ulisema ni mzee anasubiri kufa. wanaosubiri kufa nao wana mawazo mazuri? Hivi Warioba alisemaje kuhusu yale mavitabu yenu mliyogawia watu ili kuwafundisha ya kuongea. Nyani haoni kundule.
 
Km ni uzalendo khs rasimu ya katiba cdm wanastahili pongezi ni iwapo tu utalipima hili kimawazo ya kitaifa zaidi na si kichama mm nimebahatika kuhudhuria ktk misafara yote i mean wa mwenyekiti na wa katibu nilihudhuria wa m/kiti nikiwa mwz na wa katibu nikiwa dodoma kuna kijitabu cha kijani chenye alama ya jembe na nyundo kinapinga mambo mengi mazuri ya tume ya mzee warioba mf kuhusu uwazi, maadili ya viongozi wa umma na mengine mengi, wao wanajaribu kuelimisha tena kwa kuwatumia wanasheria weledi km marando, edson mbogolo, tundu lissu nk. Nafikiri ccm kwa suala hili nyeti la katiba wamepotoka na hawana jipya wanataka waturudishe enzi za chama kushika hatamu(patamu). Ni mtazamo wangu tu!
 
tsvangirai aw Tanzania wanaongojea kichapo 2014/2015. Hawana jinsi lazima wapewe Chinje Chiiiiii
 
Nyie endeleeni kukipaisha CHADEMA
2015 ndo mwisho wa kila kitu

CHADEMA twende kazi

attachment.php




nape ameona mbali chadema sio chama cha siasa ni kundi la wafanyabiashara
 
Hivi HEBU NISAIDIE UNAWEZA KUMUHUBIRI YESU/MUNGU BILA KUMLAANI NA KUMTAJA SHETANI? CHADEMA KAMA SHETANI KILA AKITOKEA TU WATU....ushindwe na ulegee shetani!!!

Mifano mingine......!!!!! Mhh! Ata shetani atakushangaa kumfananisha na CDM.
 
Back
Top Bottom