NAPE AWAPONDA CHADEMA
>.Asema ni vibaraka waliobobea.
>.Adai wanawapotezea watu muda mikutano ya Katiba
>. Ajivunia utaratibu uliotumiwa na CCM
>. Adai wanachofanya Chadema ni uhuni
>. Ampongeza Warioba kukataa maoni ya helkopta
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndg. Nape Nnauye amewaponda Chadema na utaratibu wanaotumia kukusanya maoni ya wananchi juu ya rasimu ya kwanza ya katiba kuwa ni uhuni na kuwapotezea watu muda.
Nape akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma alipokuwa akielezea ratiba ya vikao vya CCM vya kitaifa alisema,"sisi tunakutana kupitia maoni ya wanaCCM waliotoa maoni yao juu ya rasimu ya kwanza ya katiba, lakini wakati sisi tunafanya hivyo watani zetu wameamua kuwapotezea muda wananchi kwa kufanya uhuni wa mikutano ya hadhara huku wakijua kuwa ni kinyume na sheria inayoongoza mijadala ya rasimu hiyo ya katiba"alisisitiza Nape.
Lakini Nape pia alimpongeza mwenyekiti wa Tume ya mabadiliko ya katiba nchini Jaji Warioba kufuatia kauli yake kuwa atapokea maoni ya taasisi sio ya helkopta.
"Jaji warioba kawatendea haki hawa watani, sheria inataka taasisi ikae kama baraza sio ikafanye mikutano ya hadhara.Kasema sawa sawa, hawatapokea maoni ya helkopta ila ya taasisi sasa sio busara hawa jamaa kuendelea kupoteza muda wa watu".
"Lakini najua wataendelea tu kwasababu inabidi watoe hesabu ya pesa walizopewa kwa kazi hii.Watafanyaje sasa zaidi ya kuruka na chopa ili wakidhi matakwa ya waliowatuma,ndo tabu ya vibaraka!"alisisitiza Nape.
Kuhusu vikao alisema sekretariete ya CCM imekutana kwa siku tatu mjini Dodoma kuandaa kamati kuu inayokutana kesho na Halmashauri kuu inayokutana tarehe 24 -25/08/2013.
Ingawa mimi sina chama chochote lakini kwa hili la Chadema bwana security guard umeongea la msingi sana. Mpaka sasa hivi hakuna chama cha kweli cha ushindani. CCM hawana mshindani wa kweli. Chadema wanaendesha mambo kama wanatumwa vile. Sijawaona wakionyesha uzalendo hasa kwa Taifa lao. Naona bado wana kazi sana ya kukifanya chama chao kiimalike na kujipatia watu wenye uwezo na moyo wa uzalenda na maarifa ya kiuongozi. Mpaka sasa hivi mimi binafsi bado sijaona mtu mwenye uwezo wa kuongoza Taifa. Labda yule kijana wetu Mheshimiwa Kabwe ndiye namuona kuwa na hekima ya kiutu uzima. Mimi nimevunjwa moyo na uchochezi na fujo zinazosimamiwa na viongozi wa hiki chama kwa kutumia neno "NGUVU YA UMMA" naona kama kuna ka upuuzi vile. Huwa najiuliza hivi kwani siasa ni lazima ziendeshwe kwa fujo? ukiendesha kiustarabu haziwi siasa za upinzani? kwani upinzani ni nini? si nitofauti ya mawazo tu? kwani ni kufanya fujo? mimi hata raha imeondoka kwa hivi vyama...