Wakili wa shetani
JF-Expert Member
- Nov 22, 2022
- 1,726
- 3,391
CDM ni chama chenye uuchwara mwingi sana, na wala siyo chama cha maana. Lakini kwenye uuchwara huo nashangaa wameshindwaje kuwateka wakulima ukiaangalia jinsi mkulima wa nchi hii anavyoteseka. Asilimia 70 ya watz wanategmea kulima, lakini sera na harakati za CDM zinawagusa kidogo sana. Watu wanaishia kusema watu wa vijijini wanachagua CCM sababu ya ujinga, kumbe ni sababu sera za wapinzani hazijaeleweka kwa watu hao.
Watu wa vijijini wanataka bei nzuri za mazao yao. Lowassa na Mwalimu walizungumzia tu kwa mbali suala hilo kwenye chaguzi mbili zilizopita, lakini si kwa namna ya watu kuwachukulia serious. Watu wa vijijini hata usipowaambia habari ya zahanati, barabara, maji na shule, ukawaambia tu jinsi watakavyopata pesa za kutosha kutokana na mazao yao watakuelewa na kukubali mara mia. Mtu mwenye pesa mfukoni anaweza kujitatulia mambo mengi.
Fanyeni kama wataalamu, ni aibu mpaka leo kwa chama chenu kutoeleweka vijijini.