CHADEMA: Ole wenu mkiipokea Mizoga ya CCM!

CHADEMA: Ole wenu mkiipokea Mizoga ya CCM!

Si wote walioachwa ni mizoga maana mshindi lazima awe mmoja. Unaweza ukawa na wagombea 10 wote ni wazuri lakini kwa vile mgombea lazima awe mmoja haina mana kuwa wale waliochwa wote hawafai. Kumbuka pia CCM ni chama cha mafisadi kwahiyo wengine wanaweza kuwa wameachwa kwa kuwa wako kinyume na maslahi ya wanamtandao wanaojinufaisha wao wenyewe bila kujali maisha ya watanzania kwa ujumla.

Swali la Rev. kwamba kwa nini wamesubiri mpaka watoswe ndio wajiunge na upinzani bado hujalijibu.

Ukilichunguza sana swali hilo utaona wanataka kujiunga na upinzani kwa sababu wanataka kuingia bungeni tu, by hooks and crooks, na si lazima wawe na mapenzi ya kweli na kazi ya wananchi.

Nilisema kuhusu hili kwenye thread ya tetesi za Shibuda kuhamia CHADEMA. Wananchi wanaiangalia CHADEMA na kuipima kwa mambo kama haya.Wanajiuliza, CHADEMA ni chama imara au ni desperate kupata wagombea wenye "name recognition" hata kama hawa rejects wa CCM wananuka kabisa.
 
Azimio,

If we have people with crediility and nobility, why are they clinging to CCM a rotten party which everyone knows will never reform?

Mchungaji naona unachomaanisha..!

Lakini ni Mchakato..! tulisha sema tena unahitajika MSUGUANO NDANI YA CCM ... Msuguaono ambao uko controlled au Hata vurugu kabisa kwa ajili ya jambo la maana kutokea pale.

Ni Msuguano wa aina fulani utakao tenganisha hayo makundi mawili kutokea .... Yaani Pale CCM pale ... kuna makundi mawili ... moja la watu sahihi kabisa. ... Na definetly litakuwa la watu wachache.... Hata hayati JKNyerere alilisubiri sana na hata wengi tunalisubiri lijiengue.... Lipo kundi sahihi pale.... That is why I say NI MCHAKATO!!

.... Ni Msuguano gani utalitoa na kulifanya Kundi sahihi lijitenge ..nafikiri ndio jambo la kujadili!!

.... Ni hao wabunge wachahe walio temwa? Ni kweli wabunge walioachwa nao wako kwenye makundi mawili niliyo ya elezea kabla...!

.... Tungetakiwa sote tujaribu kugundua namana ya kuharakisha kupata kundi sahihi toka pale CCM ...Hata kama ni wachache ... lipatikane kundi lijiunge na Chama Kama CHADEMA nk.

Ni vugumu sana, Kupata CHAMA kilichokomaa kabisa ... tayarari kuchukua Nchi bila extracts from CCM kwa namna fulani .... Na pale CCM wapo watu wetu pale..! Namna gani sahihi kujitoa? Mbinu gani? Wakati gani? Hiyo ndio hoja kamili.....Wakifanya jambo hili kwa Makosa.... We are all done!!! Jiulize iko wapi ile CCJ??????? Timing?????? Lakini ...Pale CCM pale ....Kuna Watu sahihi pale ...wasiotakiwa kuwepo pale...!! Wapeni ushauri na lorgistics WATOKE VIPI!!! Na WAKATI GANI.
 
Chadema hakikisheni mnawachukua wale waliotoswa kwa makusudi kura za maoni ccm.
 
Rev. Kishoka,
Je, what if hao wagombea unawaona ni mizoga walikuwa wahamie Chadema longtime isipokuwa wakabakia hadi mwisho wa bunge kufungwa. Kisha kutokana na vitisho vya CCM ambayo ilihakikisha yeyote atakayetaka kuhama CCM hatakuwa na muda wa kufanya hivyo wakabakia hadi dakika hizi za majeruhi..Kumbuka hawa wabunge wanawakilisha wamnanchi wa majimbo yaliyowachagua mwaka 2005 sio kutumikia CCM ya Mafisadi, hivyo wangeondoka CCM mapema wange loose Ubunge wao mapema vile vile..Mkuu hapa inakuwaje?
 
Msichanganye na ku complicate mambo, hii siasa, hamna formula kwamba ikiwa hivi lazima iwe hivi, lililopo ni mwenzio akikosea unatake advantage.

Kuna watu wanakuwa wanakubalika na wananchi kama wao na sio kama Chama, yaani we hata umuweke Chama gani wanamkubali, na kama ulivyosikia wagombea binafsi hamna, sasa we unataka kuacha machine kama hizo zinazovutia umma wote jimboni kisa kwa nini katubu na katufuata (akiwa yeye na wafuasi wake) eti tu kwa nini hakuja mapema...its non sense! HUYO KESHATUBU MSAMEHE TWENDE KAZI MBATIZE....
 
Rev. Kishoka,
Je, what if hao wagombea unawaona ni mizoga walikuwa wahamie Chadema longtime isipokuwa wakabakia hadi mwisho wa bunge kufungwa. Kisha kutokana na vitisho vya CCM ambayo ilihakikisha yeyote atakayetaka kuhama CCM hatakuwa na muda wa kufanya hivyo wakabakia hadi dakika hizi za majeruhi..Kumbuka hawa wabunge wanawakilisha wamnanchi wa majimbo yaliyowachagua mwaka 2005 sio kutumikia CCM ya Mafisadi, hivyo wangeondoka CCM mapema wange loose Ubunge wao mapema vile vile..Mkuu hapa inakuwaje?

ukishatishwa na ukakubali manake wewe si mtetezi wa wananchi bali ni mwitikia mwito wa mwenye mbwa.... nao pia hawafai

HIVI NANI ALISEMA UPINZANI NI LELE MAMA?? KWANI ZITTO HAKUTAMANI HIZO RUZUKU NA TAX EXPMPTIONS??
 
So definition yako ya mizoga ni kuhama chama akibaki ndani ni mzoga usionuka makubwa, Bilal alikuwa reject ya zanzibar nyie bara mkaudaka mzoga mnalo litawanukia hilo.
I can confirm wewe ni imbecile.... sasa akibaki ndani ya CCM anakua vipi mzoga???? mzoga ni anayekufa chamani na kutamani kufufukia nje ya CCM

wewe ni kabila gani??? au huelewi maana ya mzoga??? mzoga ni mfu, na kwenye siasa mfu hufia chamani yani kaondoa chamani, pole sana mkuu... i thought you'd be antimalarial in action but i see you as a person who needs clinical care
 
Rev. Kishoka naomba uwe na adabu ya kuwaita wazee wetu mizoga, watu wazima (kina malecela) waliolipigania taifa hili kwa moyo mmoja ni juzi tu walikuwa watunga sheria za kukuruhusu wewe kuwa dual citizenship ufaidi huko uliko leo unawaita mizoga nafikiri si bure lakini sadaka yake ni kubwa utaipata tu.
 
ukishatishwa na ukakubali manake wewe si mtetezi wa wananchi bali ni mwitikia mwito wa mwenye mbwa.... nao pia hawafai

HIVI NANI ALISEMA UPINZANI NI LELE MAMA?? KWANI ZITTO HAKUTAMANI HIZO RUZUKU NA TAX EXPMPTIONS??
Mkuu nadhani una mis my point hapa.. Kwanza kubali kuwa mgombea yeyote wa Ubunge ni mwakilishi wa wananchi.. Pili huwezi kuwakilisha wananchi wako pasipo kupewa nafasi hiyo na chama chako na ndipo ushindani wao unapoingia kati.

Kwa hiyo, huyu mgombea wa CCM ambaye wewe unamwita mzoga kumbuka ndiye aliyewakilisha sehemu zile kwa miaka mitano iliyopita na khakika ubora wake umepokelewa na wananchi wote. Katika kura za maoni za CCM ambazo ni only asilimia chini ya 10 ya wapiga kura wote jimboni wamemchagua mgombea mpya.. Mathlan Mzee Selelli kashindwa na mgombea mwenza kwa kura nyingi sana na pengine niseme kwa asilmia 80 lakini hii ni asilimia ya wapiga kura wa CCM..na sio kura za maoni ya wilaya nzima ambao wangeweza kumchagua mghombea kutokana na uwakilishi wake.

Pili, kushindwa kwa Wabunge wengi wa CCM kumetokana na wao kuonekana walitaka kukivuruga chama. Wale woote walioweka wazi mabaya ya viongozi iwe Ufisadi au utumiaji wa mbaya wa madaraka walionekana ni watu waliotaka kukivunja chama. Na hakika ukimwambia Mlalahoi kwamba hawa watu walitaka kukiua chama sidhani kama watapita lakini kama uwakilishi wao bungeni pamoja na kukubalika kwao kwa wananchi wote ndio kungekuwa kigezo cha upigaji kura nina hakika Wapiganaji wengi wangeweza kupita...
 
Rev. Kishoka,
Je, what if hao wagombea unawaona ni mizoga walikuwa wahamie Chadema longtime isipokuwa wakabakia hadi mwisho wa bunge kufungwa. Kisha kutokana na vitisho vya CCM ambayo ilihakikisha yeyote atakayetaka kuhama CCM hatakuwa na muda wa kufanya hivyo wakabakia hadi dakika hizi za majeruhi..Kumbuka hawa wabunge wanawakilisha wamnanchi wa majimbo yaliyowachagua mwaka 2005 sio kutumikia CCM ya Mafisadi, hivyo wangeondoka CCM mapema wange loose Ubunge wao mapema vile vile..Mkuu hapa inakuwaje?

Bob Mkandara,

Mwaka jana niliandika thread kuwahoji hawa wanaoitwa wapiganaji kuwa kwa nini wanang'ang'ania kubakia CCM? Kwa nini wasijiondoe CCM kama kweli wao wana nia ya kuleta mabadiliko ya kweli? Hawakujigusa na wengine wakawashabikia kuwa tuwaache wana sikio la Mwenyekiti.

Leo hii, CCM wameonyesha ukweli kuhusu wao. Nenda mkoa wa Tabora, mizengwe imetumika tangu awali na watu wamekuwa wakilia kuhusu mizengwe ndani ya chama, ooh Rostam kashikilia mkoa na bado matokeo yametoka kama tulivyojua miaka miwili iliyopita kuwa wanaojiita wapiganaji watapigwa kata funua.

Sasa suali ni hili, kama wao walikuwa ni watu makini tangu awali? kwa nini hawakuona maandiko kwenye ukuta na wangejiondokea CCM mapema na kwenda iwe Chadema, CUF au TLP? Kwa nini wasubiri wapigwe mweleka kweye kura za maoni au kuangushwa kwa mizengwe kutoka Lumumba ndipo wagutuke kuwa wako kwenye chama mbofumbofu?

Sasa Shalom anadai kuwaasa Chadema wasikimbilie mizoga hii ambayo nia yao si kumlinda Mtanzania bali ni maslahi yao binafsi, eti nami ni mzoga uliokaa Marejani kwenye mtandao. Badala ya kua na shukrani kuwa kuna watu wenye nia njema hata kwa kukikosoa Chadema ili kisigeuke kuwa CCM, yeye anaona Mchungaji ni CCJ au ni mpuuzi fulani.

Nitawaambia hivi, nendeni mkasome alichosema Jussa kuhusu Chadema kisha mjiulize n i wapi Mchungaji anakosea!

Nikirrudi kwenye Mizoga, sitajirudi kauli. Seleli, Kaboyonga, Shelukindo, Kimaro na wengine walijua mapema kuwa hawana lao ndani ya CCM, kwa nini waliendelea kukaa ndani ya CCM hadi Bunge liishe? Ili wapate mshiko na kulipwa marupurupu? Kwa nini wlipoona msuguano ambao ni dhahiri haukuwa kwa ajili ya maslahi ya Taifa ndani ya CCM, hawakuondoka na kwenda upande mwingine na kuwekeza nguvu za kutetea maslahi ya Taifa?

Mfano, wapiganaji hawa hawa, walikaa kimya Zitto alipoliongelea suala la Buzwagi na wote wakaafiki Zitto asimamishwe Ubunge, jje ni maslahi gani walikuwa wakiyapigania na kualinda?

Likaja suala la Mafisadi na Dr. Slaa aliponguruma MwembeYanga kuhusu EPA na takataka nyingine, wao walikaa kimya na kujiunga nyuma ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa CCM na watumishi wao kuubeza upiinzani na kudai tuhuma hizo ni za kizushi.

Tuliwaona wakajaribu ujasiri kwenye suala la Richmond pekee kutokana na mvutano wao wa kugombea madaraka ndani ya Bunge na Serikali kuu na wala si kuleta uwajibikaji kwa waliohusika na uzembe na uhujumu wa Richmond.

Sasa kwa nini leo eti wapokelewe kwa shangwe Chadema, TLP au CUF kisa wamenyimwa kura? Mbona hawakuyafanya yale ya Mrema kugoma kuafiki na kupoteza kazi na kufukuzwa uanachama?

So they are Mizoga, Makapi na Pumba!
 
Rev. Kishoka naomba uwe na adabu ya kuwaita wazee wetu mizoga, watu wazima (kina malecela) waliolipigania taifa hili kwa moyo mmoja ni juzi tu walikuwa watunga sheria za kukuruhusu wewe kuwa dual citizenship ufaidi huko uliko leo unawaita mizoga nafikiri si bure lakini sadaka yake ni kubwa utaipata tu.

Kwinini,

Kakuambia nani nategemea maamuzi ya watunga Sheria za Tanzania niweze ishi? Kakuambia nani kuwa nataka uraia wa nchi mbili? Umemleta Mzee Malecela, ni baba yangu mkubwa kwani kasema anakwenda Chadema? Kaangushwa Mtera hajasema anatafuta Chama kingine. Yeye hataondoka CCM, huko ni nyumbani kwake.

Acha kuchanganya mambo, inaonyesha una upeo mdogo wa kuelewa. Mizoga ni ile inayotafuta vyama vipya sasa baada ya kutemwa na CCM! Hivyo wala usikosee na kumtusi Mzee wangu Cigi!
 
Mkuu nadhani una mis my point hapa.. Kwanza kubali kuwa mgombea yeyote wa Ubunge ni mwakilishi wa wananchi.. Pili huwezi kuwakilisha wananchi wako pasipo kupewa nafasi hiyo na chama chako na ndipo ushindani wao unapoingia kati.

Kwa hiyo, huyu mgombea wa CCM ambaye wewe unamwita mzoga kumbuka ndiye aliyewakilisha sehemu zile kwa miaka mitano iliyopita na khakika ubora wake umepokelewa na wananchi wote. Katika kura za maoni za CCM ambazo ni only asilimia chini ya 10 ya wapiga kura wote jimboni wamemchagua mgombea mpya.. Mathlan Mzee Selelli kashindwa na mgombea mwenza kwa kura nyingi sana na pengine niseme kwa asilmia 80 lakini hii ni asilimia ya wapiga kura wa CCM..na sio kura za maoni ya wilaya nzima ambao wangeweza kumchagua mghombea kutokana na uwakilishi wake.

Pili, kushindwa kwa Wabunge wengi wa CCM kumetokana na wao kuonekana walitaka kukivuruga chama. Wale woote walioweka wazi mabaya ya viongozi iwe Ufisadi au utumiaji wa mbaya wa madaraka walionekana ni watu waliotaka kukivunja chama. Na hakika ukimwambia Mlalahoi kwamba hawa watu walitaka kukiua chama sidhani kama watapita lakini kama uwakilishi wao bungeni pamoja na kukubalika kwao kwa wananchi wote ndio kungekuwa kigezo cha upigaji kura nina hakika Wapiganaji wengi wangeweza kupita...

Mkandara,

Swali ni hili, kama Wananchi bila chama wanawaridhia hawa jamaa, kwa nini waling'ang'ania kurudi CCM ambako inajulikana wazi hawana nafasi na watahujumiwa na hakuna atakayejitikisa? Ndipo tunarudi kwenye ile mada nilianzisha wakati kikao cha bajeti kilipoanza cha kutaka Wote wenye nia nzuri na Tanzania, wasusie kikao cha bajeti kutokana na ukweli kuwa bajeti haikujengwa ka manufaa ya Mtanzania na ilikuwa na mianya mingi ya kuendeleza deni la Taifa na ufisadi.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ue-patriots-should-take-a-stand-and-walk.html
 
Kwinini,

Kakuambia nani nategemea maamuzi ya watunga Sheria za Tanzania niweze ishi? Kakuambia nani kuwa nataka uraia wa nchi mbili? Umemleta Mzee Malecela, ni baba yangu mkubwa kwani kasema anakwenda Chadema? Kaangushwa Mtera hajasema anatafuta Chama kingine. Yeye hataondoka CCM, huko ni nyumbani kwake.

Acha kuchanganya mambo, inaonyesha una upeo mdogo wa kuelewa. Mizoga ni ile inayotafuta vyama vipya sasa baada ya kutemwa na CCM! Hivyo wala usikosee na kumtusi Mzee wangu Cigi!
Ndiyo maana nasema wewe hujui maisha ya bongo yalivyo ndiyo sababu hutegemei sheria zetu wewe endelea kutegemea za Canada, tumemaliza kura za maoni ndiyo unaanza kutukana watu ulikuwa wapi.

Si ulidai unanzisha chama kiko wapi unaanza kuwashwa na vya wenzako hivi kinachokuuma nini ulichangia hata senti moja kukianzisha. Hata wakichukua makapi hukisaidii wala hakikusaidii. Na kesho wengi tu wana ingia utajiju.
 
Hello Kishoka
watu wote wanaokatiliwa ni mizoga?
support jibu lako!
 
ccm wameshaamua nani watawawakilisha kwenye ubunge, wamechuja chuya, wametupa makapi na mizoga.

Sasa natoa tahadhari kwa chadema; ole wenu mkiipokea hii mizoga ya ccm na kuipa kadi na hata kuwafanya wagombea wenu kwenye majimbo, mtajishushia hadhi na kuonekana chama kisicho na maana na ni hifadhi ya mizoga na makapi.

Jiulizeni kwa nini hawa mizoga, makapi na pumba kwa nini walisubiri kuenguliwa na ccm ndipo wakakimblia kwenu? Kwa nini tangu awali hawakufanya uamuzi wa kuhamia chadema kabla ya kushindwa ndani ya ccm na hivyo baada ya kutalikiwa wanakuja kwenu nanyi mnawapa ufestiledi kwenye majimbo?

chadema wangekuwa na fikra kama zako leo wasingekuwa na dr. Slaa.
 
Mkiikimbilia hii mizoga na kuifanya wagombea wenu, mnautangazia umma kuwa nyie bado hamna uwezo wa kujijenga na kuongoza Tanzania! Mnasubiri makapi na pumba visalie mziokote mjitape kuwa mmepata lulu!
Samahani nimechelewa kuiona hii thread ila ningependa kuchangia kujibu posts kadhaa zilizotolewa na wateteaji wa waliochujwa na kukataliwa na CCM. La msingi ni kuwa mwanachama halisi hajiungi na chama kwa ajili ya kupata uongozi tu, ni lazima awe na mapenzi ya dhati kwa chama. Sasa hawa waliokuwa watetezi wa CCM siku zote hadi dakika ya mwisho wanapokimbilia CHADEMA kwa vile wamekosa uongozi huko CCM, hao hawawafai kabisa kwani hawan mapenzi na chama, wakishakosa uongozi hapo kwenu watawakimbia pia. Kumbukeni kuwa mwaka 1995 Wassira alitupwa nje ya CCM akajiunga na upinzani kusudi arudi Bungeni, baada ya hapo akarudi CCM tena. Huhitaji kuwa na wanachama wa aina hiyo wanaokuja kutafuta ulaji tu. Watawaletea ule ugonjwa wa rushwa ulioko CCM. Mwanachama halisi ni lazima awe tayari kutumikia chama hata kama hana uongozi, hao wa CCM wameshaonyesha kuwa wao wanachotaka ni uongozi kwa namna yoyote, ndiyo maana walikuwa wanatoa rushwa. Muwapokee kama wanachama tu lakini msiwape uongozi mara moja labda hadi hapo baadaye.

Ni lazima pia muionyeshe jamii kuwa nyini tayari mnaweza kuongoza nchi bila kuitegemea CCM, sasa kama hap mlipo mnaonyesha kuhitaji watu wa CCM 2nd class, mtakuwa mnaonyesha udhaifu wa hali ya juu sana.

Najua kuwa kuna special cases zinazoweza kupita condition hii lakini hata hivyo msiwakurupukie.
 
Kuongezea alivyosema Kichuguu, hivi CHADEMA itakuwa ina send message gani kwa wanachama wake waadilifu wa miaka mingi wanaotaka kugombea ubunge kama kizito mmoja aliyekataliwa na CCM anakuja na kuchukua ugombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA katika muda wa siku chache? Hii haitakuwa na effect ya kuua morale kwa watu waliomenyeka kutafuta wanachama na ku fanya grassroot campaigns miaka yote hii?

Mimi kama niko katika position ya kugombea ubunge, nimweweka muda mwingi katika kuhughulikia mambo ya CHADEMA, halafu anakuja kigogo mmoja kutoka CCM anapewa ugombea ubunge just like that nitaona kama nimetukanwa.
 
Hello Kishoka
watu wote wanaokatiliwa ni mizoga?
support jibu lako!

Kwangu mimi, ukisubiri kukataliwa ili kujiondoa katika chama kimoja na kujiunga na chama kingine napata maswali mengi kuhusu nia yako. Unaondoka chama kimoja na kwenda kingine kwa nini? Kwa sababu umekataliwa ? Usingekataliwa ungeondoka ? Kama kweli una mapenzi halisi na chama hicho cha upinzani kwa nini hukuondoka kabla ya kukataliwa? Majibu ya maswali haya kwangu mimi yana point zaidi kwenye jibu la kwamba waheshimiwa hawa wanapenda zaidi ubunge kuliko vyama vya upinzani wanavyotaka kuungana navyo, na wanataka kuvitumia tu hivi vyama vya upinzani, kwa sababu kama wangekuwa na mapenzi halisi na vyama vya upinzani wangetangaza kujiunga navyo hata kabla ya kukataliwa na CCM.

Ukingojea kukataliwa na CCM ili ujiunge na upinzani, mimi nitakuona wewe ni opportunist tu unayetafuta kuingia bungeni kwa njia yoyote, mamluki asiye na principle anayeweza kuajiriwa na mtu yeyote, ndiyo maana hata wengine wamediriki kuwaita watu hawa malaya wa kisiasa, kwa maana malaya hana principle, yeye anachojali ni maslahi yake tu, hajali mzee wala kijana.Vivyo hivyo hawa watu wanaohama vyama kwa sababu wameshindwa primaries ni malaya wa kisiasa tu, hawana principles, wanachojali ni kuingia bungeni na kutunisha matumbao yao tu.

CHADEMA ikiwakubali nayo itakuwa inakubali umalaya wa kisiasa tu.
 
Katiba ya CHADEMA haisemi mkatalie muomba uanachama kama katoka kugombea chama kingine.

Akiingia chamani, akafata mchakato wa demokrasia ndani ya chama, akawapiku wanachama wa siku nyingi katika kupata tiketi ya chama, basi mwache awe mgombea.

Vinginevyo ni kuiga mfumo wa CCM ambao vikao vya juu vinaamua nani agombee hata kama wanachama hawamtaki.
 
mizoga huwa imepata muda saa ngapi wa kuzijua sera za chama wanachohamia?

hata selelii aichaguliwa ubunge kwa tiketi ya chadema atakuwa ana represent chadema kweli au mawazo yake binafsi? ( if not mawazo ya ccm aliyoyazowea)

upiganiaji wa haki za wananchi sio lazima uwe mbunge tu, wangeweza pia kutumia umaarufu wao walionao kuwanadi hao wagombea waliowekwa tokea mwanzo na chama.......................hapo nafikiri tungelijua kuwa kweli wana nia thabiti, vinginevyo tunaona ni kuwakosea heshima wananchi.
 
Back
Top Bottom