Rev. Kishoka,
Je, what if hao wagombea unawaona ni mizoga walikuwa wahamie Chadema longtime isipokuwa wakabakia hadi mwisho wa bunge kufungwa. Kisha kutokana na vitisho vya CCM ambayo ilihakikisha yeyote atakayetaka kuhama CCM hatakuwa na muda wa kufanya hivyo wakabakia hadi dakika hizi za majeruhi..Kumbuka hawa wabunge wanawakilisha wamnanchi wa majimbo yaliyowachagua mwaka 2005 sio kutumikia CCM ya Mafisadi, hivyo wangeondoka CCM mapema wange loose Ubunge wao mapema vile vile..Mkuu hapa inakuwaje?
Bob Mkandara,
Mwaka jana niliandika thread kuwahoji hawa wanaoitwa wapiganaji kuwa kwa nini wanang'ang'ania kubakia CCM? Kwa nini wasijiondoe CCM kama kweli wao wana nia ya kuleta mabadiliko ya kweli? Hawakujigusa na wengine wakawashabikia kuwa tuwaache wana sikio la Mwenyekiti.
Leo hii, CCM wameonyesha ukweli kuhusu wao. Nenda mkoa wa Tabora, mizengwe imetumika tangu awali na watu wamekuwa wakilia kuhusu mizengwe ndani ya chama, ooh Rostam kashikilia mkoa na bado matokeo yametoka kama tulivyojua miaka miwili iliyopita kuwa wanaojiita wapiganaji watapigwa kata funua.
Sasa suali ni hili, kama wao walikuwa ni watu makini tangu awali? kwa nini hawakuona maandiko kwenye ukuta na wangejiondokea CCM mapema na kwenda iwe Chadema, CUF au TLP? Kwa nini wasubiri wapigwe mweleka kweye kura za maoni au kuangushwa kwa mizengwe kutoka Lumumba ndipo wagutuke kuwa wako kwenye chama mbofumbofu?
Sasa Shalom anadai kuwaasa Chadema wasikimbilie mizoga hii ambayo nia yao si kumlinda Mtanzania bali ni maslahi yao binafsi, eti nami ni mzoga uliokaa Marejani kwenye mtandao. Badala ya kua na shukrani kuwa kuna watu wenye nia njema hata kwa kukikosoa Chadema ili kisigeuke kuwa CCM, yeye anaona Mchungaji ni CCJ au ni mpuuzi fulani.
Nitawaambia hivi, nendeni mkasome alichosema Jussa kuhusu Chadema kisha mjiulize n i wapi Mchungaji anakosea!
Nikirrudi kwenye Mizoga, sitajirudi kauli. Seleli, Kaboyonga, Shelukindo, Kimaro na wengine walijua mapema kuwa hawana lao ndani ya CCM, kwa nini waliendelea kukaa ndani ya CCM hadi Bunge liishe? Ili wapate mshiko na kulipwa marupurupu? Kwa nini wlipoona msuguano ambao ni dhahiri haukuwa kwa ajili ya maslahi ya Taifa ndani ya CCM, hawakuondoka na kwenda upande mwingine na kuwekeza nguvu za kutetea maslahi ya Taifa?
Mfano, wapiganaji hawa hawa, walikaa kimya Zitto alipoliongelea suala la Buzwagi na wote wakaafiki Zitto asimamishwe Ubunge, jje ni maslahi gani walikuwa wakiyapigania na kualinda?
Likaja suala la Mafisadi na Dr. Slaa aliponguruma MwembeYanga kuhusu EPA na takataka nyingine, wao walikaa kimya na kujiunga nyuma ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa CCM na watumishi wao kuubeza upiinzani na kudai tuhuma hizo ni za kizushi.
Tuliwaona wakajaribu ujasiri kwenye suala la Richmond pekee kutokana na mvutano wao wa kugombea madaraka ndani ya Bunge na Serikali kuu na wala si kuleta uwajibikaji kwa waliohusika na uzembe na uhujumu wa Richmond.
Sasa kwa nini leo eti wapokelewe kwa shangwe Chadema, TLP au CUF kisa wamenyimwa kura? Mbona hawakuyafanya yale ya Mrema kugoma kuafiki na kupoteza kazi na kufukuzwa uanachama?
So they are Mizoga, Makapi na Pumba!