DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
TAARIFA KWA UMMA
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinalaani vikali kitendo cha Jeshi la Polisi kumshemlulia na kumdhalilisha Wakili Deogratius Mahinyila mmoja wa mawakili wa Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mhe. Tundu Lissu, baadhi ya viongozi na wanachama wengine.Leo Jumatatu, Agosti 15, 2025, wakili Mahinyila ameshambulikiwa, kujeruhiwa vibaya na kudhalilishwa na Askari wa Jeshi la Polisi katika eneo la Mahakama Kuu alipokuwa akihudhuria kesi ya uhaini inayomkabili Mhe. Tundu Antipius Lissu. Polisi walimshambulia, na kisha kumpeleka Kituo Kikuu cha Polisi (Central Police), ambako bado anashikiliwa.
Ifahamike kuwa, Mahakama ni eneo la haki na siyo himaya na uwanja wa Jeshi la Polisi kunyanyasa na kuwafanyia ukatili Watanzania.
Chadema kinalitaka Jeshi la Polisi liheshimu eneo la Mahakama na Watanzania wanaofika eneo hili kufuatilia kesi mbalimbali. Hivyo basi, bila masharti Chama kinawataka Jeshi la Polisi kumuachia wakili Mahinyila pamoja na wanachama wengine (8), walioshambuliwa eneo la Mahakama wakifuatilia kesi inayomkabili Mh. Tundu Antipus Lissu.
Imetolewa leo Jumatatu, tarehe 15 Septemba 2025
^saini
Brenda Rupia
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi