CHADEMA sasa ni tishio la amani na utulivu nchini...

CHADEMA sasa ni tishio la amani na utulivu nchini...

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,468
Reaction score
911,184
Mikutano karibu yote ya chadema ina wasifu wa jazba, hoja za nguvu na kufoka kunakopita kiasi na hivyo kuwafanya wafuasi wao kuonyesha nia ya kujichukulia sheria mkononi na haya kama hatutaelezana mapema nionavyo uhuru wa wengineo ambao hawaafiki misimamo ya cdm uko njia panda.....

CDM wanapatwa na taswira hii ya kuuandaa umma kuvunja amani ni kwa sababu zifuatazo:-

1) HAWAJIAMINI/ INSECURE!

Viongozi wengi wa cdm ni makapi ya ccm na hivyo kujiona ni bidhaa choka na hivyo kutafuta mbinu mpya ya kujirudish a ulingoni kama hii ya jazba, hasira, kufoka na kudai hata yale ambayo hawastahili.

2) VISASI/ VENGEANCE.

kawaida ya makapi ni kuwinda mwanya wa malipizi na huo mwanya usipopatikana kwa haraka basi "hasira za mkizi" hutawala kama tunavyoona sasa kwenye mihadhara yao.

3) UTAPELI WA KISIASA/ POLITICAL HYPOCRISY

Unapoona vinara wao bungeni wanakuja na khoja binafsi ambazo zimekithiri kwa kukiri hatua za serikali katika kutatua kero kama ile ya maji ya Dar kwenye khoja ya Mnyika lakini bado wanadai nayo ni khoja binafsi kwa vile mkakati wa serikali umepungua bilioni mia! Basi ujue taifa limeingiliwa na matapeli wa kisiasa ambao kwa raia wasiojua lolote wanafikiri cdm ndiyo mkombozi kumbe khoja tajwa hazina ufumbuzi ila malalamiko yasiyo na kichwa wala miguu........

Mnyika alipaswa kutathmini mkakati wa serikali na kubaini mianya ya wizi na ubadhirifu ambayo ni lukuki na hivyo kutoa ushauri wa kuiziba.............................hilo hakufanya sasa purukshani za cdm kupeleka khoja tajwa kwa wananchi kama siyo ulimbukeni ni nini?

4) USHAWISHI FINYU \ LIMITED PERSUASIVE POWER!

Ukifuatilia manung'uniko mengi ya CDM bungeni yanatokana na madai potofu kuwa wao wako wachache kama vile ukubwa wa pua ndiyo wingi wa makamasi badala ya kujikita katika kuajiri wataalamu wawasaidie katika kujenga khoja zenye mashiko na kubuni mikakati endelevu. Unapoona cdm wanatafuna ruzuku badala ya kuwekeza kwenye utalaamu jiulize ni masilahi ya nani ambayo wanayapigania? Wabunge wote bila ya kujali vyama vyao wanalengo la kuona nchi inasonga mbele na cdm kudhani ni wao tu nao ni kukosa dira ya kisiasa.

Wakati umefika tukawaelimisha cdm kuwa wabunge waachie nafasi ndani ya chama ili wazame kwenye shughuli ya kuibana serikali badala ya utaratibu uliopo wa kujirundikia madaraka ndani ya serikali na ndani ya chama.

pia watendaji ndani ya chama wawe wataalamu badala ya sasa upayukaji kwenye mihadhara sasa ndiyo sifa ya kukwaa madaraka chamani.

5) KUWADHARAU WAPIGAKURA/ UNDERESTIMATING AND ABUSING VOTERS!

CDM ni magwiji wa kutengua sauti ya wapigakura lakini wakifika majukwaani huwahadaa kuwa kuna kitu kiitwacho "people's power"...........huu ni uzandiki usiyo na kifani.

tatizo la uongozi wa CDM ni kuwaona wapigakura ni mbumbumbu na wao ndiyo wajuaji na kwa kufanya hivyo wamewadharau na ni wale tu ambao kweli ni mambumbumbu wataendelea kufuata hilo giza nene ndani ya kivuli cha CDM.

6) KWELI MWAMBA NGOMA HUVUTIA KWAKE/ TWISTED SELF EVALUATION!

CDM kamwe hawako tayari kukemea maovu ndani ya CDM lakini ni magwiji wa kuinyoshea vidole serikali ya CCM!
Huu ni unafiki haswa pale ambapo jazba, ukelele, mayowe, ndulu, na kupayuka kwatumika kufukia mashimo ya mapungufu ndani ya CDM na wajanja hawa kujipatia mtaji wa kuonekana wao ni swafi huko wananuka na ufisadi mashabiki wao humezwa na hilo wimbi la kitapeli na hatari yake ni kuwa viashiria vya kukosekana amani vimeanza kushamiri kama sasa tunasikia hata spika Anne Makinda anapigiwa simu na watu wasiojulikana na kutukanwa matusi ya nguoni.

Ni juzijuzi tu CDM kwenye mikutano yao Dar waligawa namba za simu za wabunge wa CCM kwa mashabiki wao bila ya hata ya kuomba kibali cha wabunge tajwa. Unapopewa namba ya simu na mtu ujue hiyo ni dhamana na wala siyo kuitumia dhamana hiyo utakavyo na hata kuhatarisha maisha ya mwenzio ili wewe upate mkate wako wa kisiasa.

Ni vyema polisi wakakamata viongozi wote wa cdm waliokuwa wanagawa namba za simu za wabunge wa ccm kwa wanachama wao na kuwafungulia kesi za kuchochea uvunjikaji wa amani na matumizi mabaya ya dhamana ya simu walizopewa.........Ikiwa na pamoja ya wale wote ambao itabainika namba zao tajwa zilitumika kuwakashifu wabunge wa CCM ambao wanatumia haki yao kidemokrasia kuyatekeleza yale ambayo wanaona yanatija kwa taifa............

7) MAJEMADARI WA LAWAMA LAKINI HAWANA MAJIBU YA KERO/ GRUMBLING WITHOUT ALTERNATIVES!

Ukihudhuira mikutano mingi ya CDM utakuta ni malalamiko dhidi ya serikali ya CCM lakini hata siku moja hawatoi ufumbuzi wa kero husika na kudhani kama wakifanikiwa kuing'oa CCM basi shida zetu nazo zitakuwa zimefikia ukingoni jambo ambalo ni udanganyifu mkubwa. Kenya walikuwa wakidai upinzani "YOTE YAWEZEKANA BILA MOI" lakini miaka 10 tangu Moi atoke madarakani tunaona ulikuwa ni utapeli wa kimataifa kabisa!!! ........................tatizo siyo mtu bali mfumo wa kuendesha nchi...........................acheni CDM kutupotosha juu ya hili.

8)............nitaendelea wakati mwingine...............
 
zumbemkuu labda tusaidie kabla ya cdm kugawa namba za simu za wabunge wa ccm lini Spika wa Bunge alikwisha kuwahi kupigiwa simu na watu wasiojulikana na kutukanwa matusi ya nguoni? jibu hili kwa umakini khalafu ujiulize wewe ni shabiki wa cdm au ni mwanachama wa haki?
 
maagizo ya chama na ambayo yalirushwa live kwenye taarifa ya habari ni kumtumia spika na naibu wake wajiudhuru,
ila kwa hasira za wananchi wenyewe (wafuasi na wasio wafuasi wa chadema, wakristo kwa waislam) wakaenda mbali zaidi
kwa kumaliza au kupunguza hasira zao kwa kuwapa matusi, binafsi sijatuma msg, ningetuma isingekuwa tofauti na hizo msg 400 alizotumiwa, huenda mimi ningezidisha zaidi,
hivi unajua asaiv watu wanapigana vita ya kidini Geita sababu ya hao hao wapuuzi?
umesahau ni juzi tu bunge hili hili lilitaka kuidhihaki madhabahu kwa kujadili mambo yanayohusu dini??
ulikuwa umelala Rutha? hukusikia?
 
Hebu zumbemkuu tetea hili hitimisho lako kwa nguvu ya khoja au na wewe ni kama CDM ambao hupayuka lakini hawawezi kujenga na kutetea khoja zao?
kaka nimeamua kupayuka kuanzia sasa baada ya kuona nchi yangu inapelekwa kosovo.
nasema ni wapuuzi, ngoja na mimi nitafute hizo namba zao niongeze idadi ya msg ziwe 401 badala ya 400.
 
hii ni lugha ya utawala kandamizi.

Coercive thinking........na hapa amepotosha kweli kuhusu Kenya......anyway ndio freedom of opinion and speech ilivyo

Kenya walikuwa wakidai upinzani "YOTE YAWEZEKANA BILA MOI" lakini miaka 10 tangu Moi atoke madarakani tunaona ulikuwa ni utapeli mkubwa ........................tatizo siyo mtu bali mfumo wa kuendesha nchi.......................... .acheni cdm kutupotosha juu yahili.

ukweli usio ukweli

Msome Jizalendo hapa anasemaje:

Duniani pote vyama vya siasa na wafuasi wao wanaoitakia mema nchi yao, wamalizapo uchaguzi kazi inayobaki ni moja tu - kuungana na raia wengine waote kuchapa kazi kuijenga na kuiendeleza nchi yao kwa pamoja wakingojea kipindi kingine cha uchaguzi wachuwane wakati huo mwanana. Hivi ndivyo inavyofanyika USA (Amerika), Uingereza, Kanada nk.

Hapa Tanzania vyama vingi vya siasa vinalielewa hilo na vinatenda hivyo; isipokuwa hiki chama kinachojiita M4C ambayo maana yake ni "Movement for Chaos" yaani kuanzisha fujo. Wao wanachotekeleza ni fujo, fujo na kampeni kabla ya wakati. Hawa ni waovu wakubwa wa nchi yetu. Watanzania tuweni macho!
 
kaka nimeamua kupayuka kuanzia sasa baada ya kuona nchi yangu inapelekwa kosovo.
nasema ni wapuuzi, ngoja na mimi nitafute hizo namba zao niongeze idadi ya msg ziwe 401 badala ya 400.

zumbemkuu tatizo siyo wingi wa sms bali ni kudharau haki za wenzio katika kulisukuma gurudumu la maendeleo. SMS za ushauri hazina kero au kuashiria uvunjifu wa amani.............tusaidiane kukemea matusi na kudharauliana ili tuijenge nchi yetu ambayo uvumilivu uwe ndiyo msingi wa kutunganisha badala ya kila mmoja kujichukulia sheria mkononi.........................
 
Coercive thinking........na hapa amepotosha kweli kuhusu Kenya......anyway ndio freedom of opinion and speech ilivyo

Safari_ni_Safari fafanua maana hueleweki hata kidogo...........unataka kusema corruption in Kenya has subsided because Moi is not in power? yesterday you did not watch the live Kenyan presidential debate otherwise you would have a different attitude over this matter.............
 
maagizo ya chama na ambayo yalirushwa live kwenye taarifa ya habari ni kumtumia spika na naibu wake wajiudhuru,
ila kwa hasira za wananchi wenyewe (wafuasi na wasio wafuasi wa chadema, wakristo kwa waislam) wakaenda mbali zaidi
kwa kumaliza au kupunguza hasira zao kwa kuwapa matusi, binafsi sijatuma msg, ningetuma isingekuwa tofauti na hizo msg 400 alizotumiwa, huenda mimi ningezidisha zaidi,
hivi unajua asaiv watu wanapigana vita ya kidini Geita sababu ya hao hao wapuuzi?
umesahau ni juzi tu bunge hili hili lilitaka kuidhihaki madhabahu kwa kujadili mambo yanayohusu dini??
ulikuwa umelala Rutha? hukusikia?

zumbemkuu vita vya geita ni vya ajira na wala havina uhusiano na Bunge........au hata dini...............khalafu thibitisha usemi wako kuwa wasio wana cdm walishiriki huu uvunjifu wa amani....................naona waongea kwa hisia.......................khalafu suala la hasira limechochewa na nani kama siyo Alibaba (read Mbowe) & forty thieves............?
 
Last edited by a moderator:
zumbemkuu labda tusaidie kabla ya cdm kugawa namba za simu za wabunge wa ccm lini Spika wa Bunge alikwisha kuwahi kupigiwa simu na watu wasiojulikana na kutukanwa matusi ya nguoni? jibu hili kwa umakini khalafu ujiulize wewe ni shabiki wa cdm au ni mwanachama wa haki?

Inakuuma sana spika kutukanwa, hajatukanwa kama makinda . Ninachoona kwako unataka hata akivua nguo zote mbele ya bunge tumpigie makofi. Nadhani we ni moja ya wanamuona kama kama picha ya video screen huku ukichukua rimoti na kumchezesha kama katuni. Ajifikilie na arudi nyuma aangalie mwenendo wake
 
chitambikwa mwenendo wake upi hata atukanwe? Kwahiyo kama mtu kama hakubaliani na Alibaba & forty thieves (Soma Mbowe na wezi wenzie ndani CDM) basi kazi ni moja achukue namba zao za simu na kuanza kuwatukana.....................hiyo si kuwahukumu hata kabla hujawapa haki ya kujitetea na hiyo ndiyo demokrasia ya wapi?
 
zumbemkuu labda tusaidie kabla ya cdm kugawa namba za simu za wabunge wa ccm lini Spika wa Bunge alikwisha kuwahi kupigiwa simu na watu wasiojulikana na kutukanwa matusi ya nguoni? jibu hili kwa umakini khalafu ujiulize wewe ni shabiki wa cdm au ni mwanachama wa haki?

Your skewed thread again!! Why don't you discuss and compare whether the Speakers' Chair actions are justifiable as seen on the TV screen? Those actions are the cause of all of those you condemn. Don't forget ACTIONS AND REACTIONS ARE EQUAL AND OPPOSITE.

Try some other stupid arguements.
 
Your skewed thread again!! Why don't discuss and compare whether the Speakers' Chair actions are justifiable as seen on the TV screen? Those actions are the cause of all of those you condemn. Don't forget ACTIONS AND REACTIONS ARE EQUAL AND OPPOSITE.

Try some other stupid arguements.

Mimibaba unazidi kunithibitishia CDM ni chama cha vurugu tupu.......huwezi kuhalalisha kujichukulia sheria mkononi kwa kisingizio chochote kile..............
 
Mimibaba unazidi kunithibitishia CDM ni chama cha vurugu tupu.......huwezi kuhalalisha kujichukulia sheria mkononi kwa kisingizio chochote kile..............

Kwani maspeaker walichukua sheria miguuni kukandamiza kanuni za bunge? Tulipofikia hapa sasa Serikali iliyoko madarani kupitia chama dhaifu inafanya "provocations" kwa matumaini ya kujificha nyuma ya ujuzi wa kanuni na vyombo vingine vya dola.

By the way umemuona Rage akimshambulia mwanachama wa Chadema, Le Mutuz na Bulembo wanang'oa bendera ya Chadema Chalinze, na mwenyekiti wa ccm kuhukumiwa kwenda jela kwa kung'oa bendera ya Chadema? Toa ushahidi wa vurugu za Chadema.

Mauaji yote kwenye vurugu za siasa yameundiwa tume; hakuna majibu ya hizo tume kwa sababu zinawagusa Chama tawala na serikali yake.

Please usifurahishe jamvi kwa kukosoa bila kuweka mizania. Maspeaker na wenye viti wa bunge wanapokea maagizo ya kuinusuru CCM na serikali yake kuhusu hoja za mshiko za wananchi; si hoja za CDM. Waruhusu mijadala ya Bunge watumie wingi wa wa wabunge wao kutozipigia hoja; mwishowe watafikishwa kwenye mahakama ya umma. Hata wasipoifikisha Chadema wananchi wenyewe watahukumu.
 
Back
Top Bottom