Mkuu
Rutashubanyuma,
Nianze kwa kusema, katika Dunia/Ulimwengu huu wa sasa, si jambo la kushangaza kupata namba BINAFSI ya mtu kama kiongozi au raia wa kawaida.
1. Kutojiamini(Insecurity): Sidhani kuwa na sababu moja yaani viongozi wa Chama fulani walikuwa ni wa chama fulani(mf. viongozi wa CHADEMA kuwa walikuwa CCM) na hivyo ni makapi! Hii SI HOJA bali propaganda za kisiasa.
Endapo mtu alikuwa mfuasi wa Chama husika na akahama haimaanishi 'amekwisha' kisiasa, isipokuwa hapa hutakuwa na maana ya Uhuru wa maoni, maamuzi.
Wakati fulani ni kama mchezo wa kuigiza ukitazama Bunge la Tanzania, si kwamba tu wabunge(baadhi) hawaheshimiani bali hawaheshimu na kujali/kupenda kazi yao.
2. Visasi/Vengeance: Mkuu, katika duniana hii mtawaliwa hutumia nguvu yake tu, hapa namaanisha kura. Sasa pale utendaji unapokiukwa, mambo ya msingi kupuuzwa, wakati hoja za msingi zikijengwa na majibu mepesi kutolewa, Hasira hutawala...Hii ni jambo la kawaida kwa binadamu yeyote. Pengine kutohimili hasira hizi ni kutokana na Upuuzwaji wa mambo ya msingi kuendelea.
3.Utapeli wa Kisiasa/Political Hypocrisy:
Binafsi sifurahishwi/kuvutiwa na uendeshwaji wa Bunge, hasa katika hoja binafsi..Kuwekuwa na kipaumbele cha "uchama"..zaidi ya Utaifa. Nikimaanisha ushabiki ndio umetawala.
4.Ushawishi Finyu/Limited Persuasive power.
Sikubaliani na wewe kusema kuwa, "kila mbunge anajali maslahi ya Taifa".
Pili Utakuwa hauko sahihi kusema Viongozi kujirundikia madaraka katika Serikali na Chama. Nasema hivi kwa kuwa, Si wabunge wote wa CHADEMA ni viongozi katika chama.
Tatu nadhani ni viongozi wa CCM wenye tabia hii, achilia mbali ndani ya chama, unakuta kiongozi wa Serikali(mfano mkuu wa mkoa) anaongoza/anasimamia mikoa miwili lakini bado ana majukumu mengine, na hapa unategemea kweli kazi kufanyika.
Achilia mbali hiyo unaweza kukuta naibu waziri/waziri ana wadhifa mwingine, kumbuka habari ya Mh. Lukuvi, Mh. Mwantumu Mahiza!!
Unataka kusema Tanzania yote hii amekosekana mtu wa kushika nafasi fulani, kuepuka kurundikiwa madaraka?
5. Kuwadharau wapiga kura/Underestimating and abuse voters:
Sidhani kwa kutumia msemo(Slogan) Peoples' power, ni kuwadharau wananchi, labda tuwe maana yake ni mpya, yaani uisemayo wewe.
Ni sawa na kusema "Nguvu Mpya, Ari mpya na Kasi mpya" , je unataka kumaanisha hapa kabla ya msemo huu CCM walikuwa dhaifu, goigoi na wakijivuta?!!
6.Mwamba Ngoma huvutia Kwake/Twisted alternative evaluation.
Mkuu hapa ndipo unapokosea, na kiukweli ni kosa la wengi.Hatusemi Serikali ya CCM, Serikali ya CHADEMA/CUF/n.k..unless
i) Definition ya Serikali ni tofauti.
ii) Ni kutafuta majigambo yasiyo na msingi.
iii)Ni kusababisha KUENDELEA kuwepo na mpasuko wa kivyama na wananchi.
Hii ni kwa sababu, Tunapochagua viongozi tunachagua viongozi wa Taifa, sio wananchama wa CCM au chama chochote kile.
Hata Rais/Balozi/W/Nje(kama mwakilishi wa Taifa) awapo huko nje, husimamia serikali ya TANZANIA.
Kuendelea kutumia misemo kama hii, tusitegemee maendeleo kwa sababu, UPINZANI huikosoa Serikali(kama mija wapo ya Kazi yake) na iwapo tutajijenga kiakili(mindset) kuwa ni Serikali YETU WOTE na si ya kwao, Mapungufu yatapokelewa na kufanyiwa kazi, vinginevyo Wabunge na Wafuasi wa CCM watakapokosolewa kwa utendaji wa "Serikali yao" wataona ni uchokozi(attack) na vurugu kuanza upya.
7. Majemadari wa Lawama bila ufumbuzi.
Mkuu, wakati fulani Upinzani ulitengeneza bajeti na ikawasilishwa Bungeni na hata kusomwa, ikiainisha mapato yote yatakavyopatikana na matumizi yake hii ilikuwa na unafuu kuliko bajeti iliyotengenezwa na Bunge zima, lakini hadi leo hii(15.02.2013) hakuna jambo lilifanyiwa kazi.
Dharau kwa kundi fulani kuwa hawawezi(Underestimating) hii ilifanywa na wabunge wa chama tawala, WAKATI hii ilikuwa kusaidia Taifa.
Vivyo hivyo kuhusu magari ya kifahari ya watumishi wa Serikali(wabunge wakiwamo), lakini nini kilifanyika?
wakati fulani pia, majina ya wala rushwa, wabadhirifu yalisomwa na ushahidi kuwa wazi, lakini hakuna kilichofanyika, Simply kwa sababu tu ni Upinzani.
Sasa mkuu
Rutashubanyuma, unataka alternative ipi unayohitaji?