Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
-
- #41
unaweza kunifafanulia hapo kwenye nyekundu?
Rutashubanyuma kwa members wageni wanaweza kuiona hii kama hoja ya msingi lakini usisahau kwamba nimeanza kusoma maandishi yako hapa JF tangu mwaka 2010 tukielekea uchaguzi mkuu na baada ya uchaguzi mkuu. Sihitaji kukukumbusha jinsi ulivyokuwa ukiishambulia Chadema na viongozi wake hasa Dr. Slaa huku ukijiita political analyst.Mwita Maranya thibitisha tuhuma zako hiziz kama unaweza...............and make my day!
Kwa mara ya kwanza nimeona mada ya ajabu katika jukwaa hili. Yaliyoongelewa na mleta mada inaonekana kama vile walioko madarakani ni watakatifu sana kiasi kuonekana kufanyiwa fujo na wale wanaotaka kuingia madarakani. Mwenyekiti wa ccm anapoongea huku akitabasamu na kushangiliwa kuwa hayuko tayari kuachia nchi kwa wapinzani kwa namna yoyote; yuko sawa? Kiongozi wa cdm anapoongea kwa 'jazba' na msisitizo kuwa ccm inatumia hela za wanachama wa mashirika ya hifadhi ya jamii katika kutekeleza ilani za ccm; anakosea? Ni wakati gani mtu anatakiwa azungumze kwa bashasha na wakati gani mtu azungumze kwa kauli kavu na thabiti? Ndugu Rutashubanyuma umekosea sana katika hili.
Rutashubanyuma kwa members wageni wanaweza kuiona hii kama hoja ya msingi lakini usisahau kwamba nimeanza kusoma maandishi yako hapa JF tangu mwaka 2010 tukielekea uchaguzi mkuu na baada ya uchaguzi mkuu. Sihitaji kukukumbusha jinsi ulivyokuwa ukiishambulia Chadema na viongozi wake hasa Dr. Slaa huku ukijiita political analyst.
Labda nikufahamishe kwamba mara moja moja nikijisikia huwa napoteza muda kubisha na wewe lakini mara zote sisomi thread zako kwa matarajio ya kuona kitu chochote kipya ama constructive. Hauna hata ile constructive criticism zaidi ya chuki tu zilizoujaza moyo wako, na hiyo haishangazi kwakuwa wako wengi wa aina yako ambao wamekuwa wakijaribu kufanya hadaa ili kuharibu reputation ya Chadema na viongozi wake bila mafanikio.
Kama wananchi wangekuwa wanakubaliana na hadaa zenu bila shaka sasahivi Arusha (mahali ulipo wewe, kama hujahama) pasingekuwa uwanja wa nyumbani wa Chadema kwakuwa hapo ndipo mmefanya kila aina ya songombingo lakini wananchi wamesema hatudanganyiki.
Umeongea too general na kutoa lawama za jumla jumla kwa CHADEMA bila kufanya upembuzi yakinifu!
This is too low for you Rutashubanyuma.
Ruta,
Nakubaliana zaidi na hoja zako No.1, No.2 na No.7.
Hii hoja namba 7, ni mbaya zaidi kwani siku CDM wakipata ridhaa ya kuongoza nchi hii basi ni hoja ambayo itawa-cost sana! Kwa jinsi ilivyo, wananchi wamejengewa dhana kwamba matatizo yote haya ni kwa ajili ya CCM na as if, endapo CDM itaingia tu madarakani basi matatizo yote hayo yataisha! For me, this's purely political robery. Wakati wa kipindi cha bunge la bajeti 2012/2013; nilitoa changamoto ya kutaka kuona bajeti mbadala ya CDM itakayoainisha mapato(ongezeko la mapato). Nilichoona kwa bajeti ile, ni ON & OFF ya entries; kwamba...say, Matumizi X ni ufisadi, so X should transfered to....! Baada ya On & OFF ambayo waliifanya bajeti yao ikaonekana ime-save about TZS 900bn.....simply means, kama bajeti ya CCM ilikuwa TZS 10 Trilion, basi ya CDM ingekuwa somwehere very close to 11 Trilion!! Ongezeko hilo la mapato yaliyokaribia kiasi cha Trilioni moja, kisingetosha hata ku-run ile project ya Minimum Salary ya TZS 315,000/= ambayo nayo kuna siku niliwaomba wanidadavulie vile ambavyo wangeweza kulipa minimum ya 315,000 lakini ambacho kililetwa jukwaani hapa kilikuwa ni kituko cha mahesabu ambacho kisingeweza kufanywa hata na mwanafunzi wa darasa la 5!!
So, siku CDM wakishika dola, basi ni hoja hiyo namba 7 ndiyo itawarudisha kwenye dawati la upinzani unless CCM wasambaratike baada ya wao kushindwa! CDM wamejenga matumaini makubwa mno kwa wananchi kama matumaini ambayo Watanganyika walikuwa nayo mara baada ya kupata uhuru!! Sioni namna CDM inavyojenga spirit ya kujituma kwa Watanzania kama njia njia ya kuepukana na umaskini na badala yake wamewajengea wananchi imani ya namna gani CCM inavyosababisha umasikini wao wakati wao(CDM) bado hawajajiandaa kuondosha umasikini zaidi tu ya kujiandaa kuiondoa CCM! It will take one or two terms kwa Wananchi kushituka kwamba wameingizwa mkenge kwani yale wanayoyatarajia kutoka kwa CDM hawatayaona ingawaje sina shaka kwamba utetezi wa CDM utakuwa "Tumeichukua nchi ikiwa katika hali mbaya sana so we need more and more time to rebuild it!
Mkuu Rutashubanyuma,
Nianze kwa kusema, katika Dunia/Ulimwengu huu wa sasa, si jambo la kushangaza kupata namba BINAFSI ya mtu kama kiongozi au raia wa kawaida.
1. Kutojiamini(Insecurity): Sidhani kuwa na sababu moja yaani viongozi wa Chama fulani walikuwa ni wa chama fulani(mf. viongozi wa CHADEMA kuwa walikuwa CCM) na hivyo ni makapi! Hii SI HOJA bali propaganda za kisiasa.
Endapo mtu alikuwa mfuasi wa Chama husika na akahama haimaanishi 'amekwisha' kisiasa, isipokuwa hapa hutakuwa na maana ya Uhuru wa maoni, maamuzi.
Wakati fulani ni kama mchezo wa kuigiza ukitazama Bunge la Tanzania, si kwamba tu wabunge(baadhi) hawaheshimiani bali hawaheshimu na kujali/kupenda kazi yao.
2. Visasi/Vengeance: Mkuu, katika duniana hii mtawaliwa hutumia nguvu yake tu, hapa namaanisha kura. Sasa pale utendaji unapokiukwa, mambo ya msingi kupuuzwa, wakati hoja za msingi zikijengwa na majibu mepesi kutolewa, Hasira hutawala...Hii ni jambo la kawaida kwa binadamu yeyote. Pengine kutohimili hasira hizi ni kutokana na Upuuzwaji wa mambo ya msingi kuendelea.
3.Utapeli wa Kisiasa/Political Hypocrisy:
Binafsi sifurahishwi/kuvutiwa na uendeshwaji wa Bunge, hasa katika hoja binafsi..Kuwekuwa na kipaumbele cha "uchama"..zaidi ya Utaifa. Nikimaanisha ushabiki ndio umetawala.
4.Ushawishi Finyu/Limited Persuasive power.
Sikubaliani na wewe kusema kuwa, "kila mbunge anajali maslahi ya Taifa".
Pili Utakuwa hauko sahihi kusema Viongozi kujirundikia madaraka katika Serikali na Chama. Nasema hivi kwa kuwa, Si wabunge wote wa CHADEMA ni viongozi katika chama.
Tatu nadhani ni viongozi wa CCM wenye tabia hii, achilia mbali ndani ya chama, unakuta kiongozi wa Serikali(mfano mkuu wa mkoa) anaongoza/anasimamia mikoa miwili lakini bado ana majukumu mengine, na hapa unategemea kweli kazi kufanyika.
Achilia mbali hiyo unaweza kukuta naibu waziri/waziri ana wadhifa mwingine, kumbuka habari ya Mh. Lukuvi, Mh. Mwantumu Mahiza!!
Unataka kusema Tanzania yote hii amekosekana mtu wa kushika nafasi fulani, kuepuka kurundikiwa madaraka?
5. Kuwadharau wapiga kura/Underestimating and abuse voters:
Sidhani kwa kutumia msemo(Slogan) Peoples' power, ni kuwadharau wananchi, labda tuwe maana yake ni mpya, yaani uisemayo wewe.
Ni sawa na kusema "Nguvu Mpya, Ari mpya na Kasi mpya" , je unataka kumaanisha hapa kabla ya msemo huu CCM walikuwa dhaifu, goigoi na wakijivuta?!!
6.Mwamba Ngoma huvutia Kwake/Twisted alternative evaluation.
Mkuu hapa ndipo unapokosea, na kiukweli ni kosa la wengi.Hatusemi Serikali ya CCM, Serikali ya CHADEMA/CUF/n.k..unless
i) Definition ya Serikali ni tofauti.
ii) Ni kutafuta majigambo yasiyo na msingi.
iii)Ni kusababisha KUENDELEA kuwepo na mpasuko wa kivyama na wananchi.
Hii ni kwa sababu, Tunapochagua viongozi tunachagua viongozi wa Taifa, sio wananchama wa CCM au chama chochote kile.
Hata Rais/Balozi/W/Nje(kama mwakilishi wa Taifa) awapo huko nje, husimamia serikali ya TANZANIA.
Kuendelea kutumia misemo kama hii, tusitegemee maendeleo kwa sababu, UPINZANI huikosoa Serikali(kama mija wapo ya Kazi yake) na iwapo tutajijenga kiakili(mindset) kuwa ni Serikali YETU WOTE na si ya kwao, Mapungufu yatapokelewa na kufanyiwa kazi, vinginevyo Wabunge na Wafuasi wa CCM watakapokosolewa kwa utendaji wa "Serikali yao" wataona ni uchokozi(attack) na vurugu kuanza upya.
7. Majemadari wa Lawama bila ufumbuzi.
Mkuu, wakati fulani Upinzani ulitengeneza bajeti na ikawasilishwa Bungeni na hata kusomwa, ikiainisha mapato yote yatakavyopatikana na matumizi yake hii ilikuwa na unafuu kuliko bajeti iliyotengenezwa na Bunge zima, lakini hadi leo hii(15.02.2013) hakuna jambo lilifanyiwa kazi.
Dharau kwa kundi fulani kuwa hawawezi(Underestimating) hii ilifanywa na wabunge wa chama tawala, WAKATI hii ilikuwa kusaidia Taifa.
Vivyo hivyo kuhusu magari ya kifahari ya watumishi wa Serikali(wabunge wakiwamo), lakini nini kilifanyika?
wakati fulani pia, majina ya wala rushwa, wabadhirifu yalisomwa na ushahidi kuwa wazi, lakini hakuna kilichofanyika, Simply kwa sababu tu ni Upinzani.
Sasa mkuu Rutashubanyuma, unataka alternative ipi unayohitaji?