Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Uchaguzi wa ndani ya CHADEMA umeendelea kupamba moto
========================================
Wajumbe wa mkutano mkuu wa taifa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kutoka mkoa wa Shinyanga wamesema watamuunga mkono Tundu Lisu ambaye ametangaza kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama
Msimamo huo umetolewa na Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Kahama Gango Kidero kwa niaba ya Wajumbe hao ambapo wamesema wanatambua na kuthamini mchango wa Mwenyekiti anayemaliza muda wake na kwamba wanatamani apokewe kijiti ili mazuri aliyoyafanya ndani ya Chama yaweze kuendelezwa na mtu mwingine.
Awali akifafanua kuhusu kumuunga mkono Tundu lisu,Mjumbe wa Mkutano Mkuu Jackson Tungu amesema hatua hiyo haiwezi kusababisha mpasuko ndani ya Chama hicho kutokana na uimara wa CHADEMA.