CHADEMA Special Thread

CHADEMA Special Thread

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA Taifa (BAVICHA), Deogratius Mahinyila , amesema vijana wa chama hicho hawatakubali kile alichokiita siasa za udalali na usaliti ndani ya chama, akisisitiza umuhimu wa kulinda mshikamano wa wanachama.

Mahinyila ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika Nyamongo, ambapo amesema vijana wa CHADEMA wataendelea kusimamia masuala wanayoamini ni muhimu kwa chama na kwa wananchi.

Amesema mwanachama yeyote anayefanya vitendo anavyodai vinaweza kuvuruga mshikamano wa chama, kuwakwamisha viongozi au kuwasaliti Watanzania katika mapambano ya kisiasa hatapata uungwaji mkono kutoka kwa vijana wa CHADEMA.

“Sisi vijana wa CHADEMA kauli yetu ni kwamba yoyote anayefanya siasa za udalali, yoyote anayefanya mambo ya kumsaliti mwenyekiti wetu aliye gerezani bila hatia, yoyote anayewakwamisha, yoyote anayewasaliti Watanzania, yoyote anayewakera Watanzania kwenye mapambano tuliyonayo, sisi vijana wa CHADEMA, hata kama atakuwa na mapembe makubwa kwenye uongozi, tutampita juu,” amesema Mahinyila.

Aidha, Mahinyila amesema vijana wa chama hicho hawatakubali kuona wanachama wakifanya vitendo ambavyo, kwa mtazamo wake, vinaweza kudhoofisha mshikamano wa CHADEMA, akisisitiza kuwa hata viongozi waliowahi kushika nafasi ndani ya chama wanaweza kukataliwa iwapo wataenda kinyume na msimamo huo.

Amesisitiza kuwa tofauti za kisiasa ndani ya chama zinapaswa kushughulikiwa kwa namna inayolinda umoja na mshikamano wa CHADEMA.
1791515372949.jpg
 
‼️HABARI MBAYA‼️

Mwanachama wa CHADEMA Edson Malyo Myinga amekamatwa na Polisi leo majira ya asubuhi akiwa eneo la Mji mdogo wa Ilula Kitongoji cha Ding'inayo Jimbo la Kilolo, Mkoa wa Iringa.

Kwasasa anashikiliwa katika kituo cha Polisi Central Iringa mjini lakini Polisi hawataki kusema kosa lake ni nini.

Hii picha frame ya kwanza huyu anaengia kwenye gari ndo Edson.

Kwa trend ya matukio yanayoendelea sasa ni wazi kwamba kuna operation inaendelea kimya kimya ya kukamata Viongozi na Wanachama wa Chadema.

Jana usiku Mwenyekiti wa Bavicha Kanda ya Pwani John Nguti Wa Chadema alinusurukia kutekwa na watu wasiojulikana.

Leo asubuhi kwa nyakati tofauti wamemkamata Pambalu na Edson halafu Mchana wakamkata Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Kigoma Colleta Ntidyicha.

Ni muhimu kila mmoja akachukua tahadhari maana hatujui kesho itakuwa zamu ya nan??

#FreeEdsonMyinga #FreeCollethaNtidyicha
#FreeJohnPambalu
1792043506661.jpg
 
Back
Top Bottom