CHADEMA Special Thread

CHADEMA Special Thread

Walitunyima uwanja wa mjini wakatuto nje ya mji lakini umma umeufata huo uwanja na kuujaza ni uwanja mkubwa balaaaaa,Mh Lema amesema Mungu ana makusudi yake ule uwanja wa mjini pasingetosha hii nyomi
1792523574252.jpg
1792523569750.jpg
1792523565938.jpg
 
Leo, tarehe 21 Oktoba 2026, ujumbe wa CHADEMA ukiongozwa na Katibu Mkuu wa chama, Mhe. John Mnyika ukiwa na Mwanasheria Mkuu, Dkt. Rugemeleza, na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi, Mhe. Brenda Rupia, umekutana na Balozi wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya haki za binadamu, Eleanor Sanders, pamoja na Balozi wa Uingereza, Marianne Young.

Katika mazungumzo hayo, ujumbe wa CHADEMA umewasilisha hali ya haki za binadamu nchini, ukiangazia masuala mbalimbali yanayohusu demokrasia, utawala wa sheria na haki za kisiasa.
1792639221586.jpg
1792639218033.jpg
1792639214868.jpg
 
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) Taifa, Necto Kitiga, ametangaza hali ya Tahadhali na kuanza kwa ufuatiliaji wa mwenendo wa wenyeviti wa Kanda tatu pamoja na mikoa 11, akieleza kuwa hatua hiyo inalenga kufuatilia shughuli na mienendo ya viongozi hao.

Akitoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X, Kitiga amesema BAVICHA inaendelea kuwa imara na yenye ushawishi mkubwa, huku akieleza kuwa ufuatiliaji huo utahusisha pia safari zinazofanywa na viongozi husika.

Aidha, amesema taarifa kuhusu ikiwa biashara haramu zitatolewa, huku akisisitiza kuwa vitendo vya udhalilishaji havitavumiliwa miongoni mwa vijana. Pia ameeleza kuwa BAVICHA si sehemu ya kuhubiri kile alichokiita maridhiano ya ulaghai.

BAVICHA ni Baraza la Vijana la CHADEMA lililoanzishwa kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho, likiwa na jukumu la kuratibu shughuli zinazohusu vijana katika ngazi mbalimbali za uongozi, kuanzia ngazi ya msingi hadi Taifa. Mwongozo wa Mabaraza ya CHADEMA unaeleza kuwa kundi la vijana ni sehemu muhimu katika shughuli za kisiasa, kijamii na kiuchumi.

Katika mahojiano yaliyowahi kuchapishwa na gazeti la Nipashe Aprili 24, 2024, aliyekuwa Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa wakati huo alieleza kuhusu shughuli za baraza hilo, ikiwemo kuhamasisha ushiriki wa vijana katika siasa, kuibua mijadala kuhusu changamoto zinazowakabili vijana na kushiriki katika harakati za kudai Katiba Mpya.

Alieleza pia kuwa BAVICHA imekuwa ikihamasisha vijana wasomi kushiriki katika uongozi na kutoa nafasi kwa vijana kujenga taasisi yao kupitia shughuli mbalimbali za kisiasa na kijamii.

Kwa upande mwingine, CHADEMA kupitia mwongozo wake wa mabaraza imeeleza umuhimu wa vijana kama kundi lenye nafasi katika kujenga na kuendeleza chama, jambo linaloonesha umuhimu wa uratibu na ushirikiano wa viongozi katika ngazi mbalimbali.

Katika muktadha huo, kauli ya Kitiga inaibua suala la uwajibikaji na namna viongozi wa BAVICHA katika ngazi za Kanda na mikoa wanavyoteke
1793464036870.jpg
 
Back
Top Bottom