Siyo siri kuwa hii nchi ni ngumu sana. Uwekezaji uliopo dhidi ya haki na usawa ni mkubwa sana.
Kwa makusudi demokrasia na uhuru wa watu vimeminywa vilivyo ili kufanikisha hayo.
Hali hii haitaondoka yenyewe bila ya makabiliano. Ni muhimu kufahamu watesi wetu hujipanga upya kwa kila hatua tunazochukua.
Iwe wanapanga kusuka au kunyoa hiyo na ikawe shauri yao.
Muhimu kwetu ni kujua wazi wazi tunakwama wapi na hali iwe hivi hadi lini:
1. Harakati za kudai katiba mpya kupoa baada ya Aboubakar kukamatwa.
2. Kuweka matumaini yoyote chanya kutokea kwenye kesi za ngedere hakimu akiwa nyani.
3. Kutokuwa na mikakati ya wazi kuhusiana na kuwahami wahanga wetu katika mapambano.
4. Kutokuhakikisha chaguzi zinakoma kama hakuna tume huru. Kususia peke yake hakutoshi.
5. Kutokuiangazia nguvu yetu ya kuyajaza magereza yao kama sera halali na mbadala dhidi ya matumizi yao batili ya nguvu.
Makamanda uelekeo uwe zaidi kutoka mitandaoni. Lissu, Lema, na makamanda wote tukutane Tahrir tuna hisani ya kuifanyia nchi hii.
Tanzania itakombolewa na wenye moyo.