Mkuu umeandika kwa kiasi chake, ukijaribu kuangalia vizuri namna mfumo wa kiuongozi/kiutawala wa nchi hii utagundua yafuatayo;
1. Hii nchi ina mfumo wa hovyo na wa kimakusudi wa kuwalinda watawala na kukandamiza wananchi.
2. Huu mfumo siyo wa jana wala juzi. Ni wa miaka zaidi ya 40 iliyopita, ni kama mti uliopandwa mwaka 1970 na sasa ndio umekomaa na kuzaa.
3. Waanzilishi wa mfumo huu wa hovyo ndio wanaoitwa mashujaa leo hii, na majina kedekede na taswira mpaka kwenye fedha.
4. Kwa mfumo huu ni ngumu kujiita watu huru.
5. Mfumo ulisukwa kwa lengo mahsusi kunufaisha familia/ kundi la watu wachache.
6. Utamu wa matunda ya mfumo huu wa kale ukiyaonja lazima unogewe na kuupalilia mti huo milele.
7. Uchungu wa matunda ya mfumo huu wanaujua wale tuu walio/ watakaojaribu kuyashika na kupeleka mdomoni, haijalishi ni kiongozi wa dini, mwanasiasa, mtawala au raia wa kawaida.
8. Kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo mti unazidi kumea na kutoa matunda kwa wingi na harufu yake inafika mbali zaidi.
9. Asilimia kubwa ya waathirika wa mfumo huu wameamua/ tumeamua kukabidhi hii VITA ipiganwe kwa niaba yetu.
10. Kwa mpaka sasa bado haijaonekana hata chembe ya dalili ya kutoka hapa tulipo, kazi kubwa bado haijaanza kufanyika.