Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,434
Kilichonipa hamasa ya kuja na mjadala huu ni kauli ya Mwenyekiti wa Chadema (Taifa), Freeman Mbowe, aliyoitoa hivi karibuni ambapo alitamka (nanukuu):
"Iwapo CCM itashinda uchaguzi mwaka 2015, basi nitajiuzulu Siasa."
Ifikapo mwaka 2015, CCM itakuwa imetawala Tanzania kwa miaka 54 mfululizo. Kwa Mtanzania aliyeajiriwa, huu ni umri wa kustaafu na kujipanga kula pensheni. Umri huu pia unalingana na wastani wa maisha ya mtanzania (life expectancy). Kwa kila hali, miaka 54 ni miaka mingi sana. Katika mazingira ya kisiasa, jambo hili sio rahisi kutokea katika nchi yoyote ile inayofuata mfumo wa vyama vingi, hasa katika nyakati hizi za demokrasia ya kiliberali (liberal democracy), soko huria (free market) na utawandawazi (globalization).
Utawala wa CCM kwa miaka zaidi ya hamsini (50) umeambatana na uwepo wa &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];amani' na &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];utulivu', suala ambalo ni moja ya mafanikiio makubwa ya kisiasa kwa CCM. Lakini ni vizuri tukaambiana ukweli &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; hatuna utulivu Tanzania bali uvumilivu. Vinginevyo kama alivyotamka Nyerere mwaka 1987, ipo siku bomu litalipuka kwani kufaulu kwa CCM kisiasa kunaenda sambamba na kufeli katika nyanja za kiuchumi na kijamii. Kwa mfano, pamoja na kuishi katika mazingira ya amani na utulivu, Mwanakijiji wa Tanzania amekuwa mvumilivu sana kusuburi pengine ipo siku ahadi za TANU wakati wa harakati za uhuru zitatimizwa. Vinginevyo, maisha ya mwanakijiji leo sio tofauti sana na yale ya 50 iliyopita. Isitoshe, tofauti na enzi za Ujamaa, leo wageni wale wale tuliowafukuza kutokana na kuiba rasilimali zetu wanapokewa kwa mikono miwili; wizi wa fedha za walipa kodi ni umeongezeka; matumizi ya rasilimali za nchi yanafaidisha wachache zaidi; tofauti ya kipato baina ya walio nacho na wasio nacho imekuwa kubwa zaidi; dira na mwelekeo kama taifa havipo tena; na hakuna dalili zozote kwamba hali hii inaweza kubadilika katika muda mfupi na wa kati ujao. Ndio maana hata viongozi wengi wa CCM wanakiri chini kwa chini kwamba &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];The Country is Suffering From CCM Fatigue'. Huu ndio msingi wa kauli ya Freeman Mbowe!
Kuna tofauti kubwa baina ya "Doing the Right Things" na "Doing things Right", na ili ufanikiwe, nilazima kufanya yote mawili. Chadema has been doing the right things ambayo ni kutumia kikamilifu mapungufu ya CCM kujijenga kisiasa. Lakini tatizo linakuja kwenye "doing things right" &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; ambapo, mbali na kutumia mapungufu ya CCM, kuna umuhimu wa kufanyia kazi viambato (ingredients) vinavyoiwezesha CCM kuwa na mafanikio ya kisiasa. Ushindi wa Chadema utatokana na umahiri wake kufanyia kazi mambo kuu tisa kama ifuatavyo:
Tume ya Nyalali ilikusanya maoni yaliyoonyesha kwamba watanzania wengi walipendelea nchi iendelee na mfumo wa chama kimoja. Lakini CCM ikaamua kuruhusu maoni ya wachache ndio yatawale. Ni dhahiri kwamba suala la vyama vingi lilikuwa haliepukiki lakini mkakati wa CCM wa kuhakikisha mageuzi ya kisiasa hayatokani na nguvu ya umma bali CCM na serikali yake imekijenga sana chama hasa vijijini kwani nimetembea maeneo mengi na kushangazwa na maoni ya wengi kwamba wanachofanya chadema ni "shukrani ya punda ni mateke". Katika nchi nyingi maskini, chaguzi kuu zilifanyika muda mfupi baada ya umma kufanikisha kuleta demokrasia ya vyama vingi, hivyo kupelekea vyama vingi tawala kuanguka na kupotea katika medani za siasa. Nchini Tanzania, mbali ya kuruhusu vyama vingi kinyume na matakwa ya wengi, CCM pia ilijiwekea muda wa kutosha (miaka mitatu) kujiandaa kabla ya kuitisha uchaguzi wa vyama vingi. Hili ni jambo la kwanza la Chadema kulifanyia kazi.
2. Umiliki na Udhibiti wa Vyombo Vya Habari
Sina haja ya kujadili hili sana kwani lipo wazi, lakini muhimu hapa ni mambo mawili: kwanza ni ile sheria ya mwaka 1976 ambayo hadi leo bado inatumia na madhara yake yapo wazi; pili, ni kwamba muundo na utaratibu wa ufanyaji kazi wa Wizara ya Habari haujabadilika sana na ule enzi ya kimoja. Wizara hii kwa kiasi fulani bado ni extension ya idara ya propaganda na uenezi ya CCM. Chadema ina waziri kivuli wa Habari ambae he/she is supposed to do "things right" in that regard.
3. Uchumi Mkubwa wa CCM
Hili lipo wazi kwa Chadema, kwa mfano, katika ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2000, chadema iliazimia kurudisha mali zote za CCM serikalini kwa hoja kwamba mali hizi ziligharimiwa na watanzania wote chini ya mfumo wa chama kimoja. Iwapo hoja hii ina mashiko kisheria, basi kosa linakuja pale Chadema inapoliweka hili kama ahadi nyakati za uchaguzi badala ya kulishughulikia kama chama cha upinzani. Isitoshe, tofauti hii ya kiuchumi baina yake na CCM inachangia sana Chadema kutofanikisha malengo yake za kisiasa. Kupitia rasilimali hizi, CCM pia inafaidika sana na &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];political branding'. Siasa ni bidhaa kama nyingine sokoni, kwahiyo wananchi wanapoona au kusikia &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];brands' kwa mfano &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];CCM kirumba', au maeneo kuitwa "CCM Makao" etc, brand awareness kupitia macho, masikio na memory, haina utofauti mkubwa na ile ya bidhaa nyingine sokonikama Vodacom, CRDB n.k. Isitoshe, kuna watanzania wengi ambao wanaamini kwamba Chadema haistahili kuongoza nchi kwa sababu bado haina fedha. Hii ni imani potofu na ni muhimu kwa chadema kuanza kutoa elimu kwa umma kwamba chama chochote cha siasa kikipewa ridhaa na umma kuongoza nchi, uwezo wake kufanikisha malengo ya kuendeleza taifa unatokana na fedha za walipa kodi na kwamba hivyo ndivyo CCM imekuwa ikifanikiwa kutawala.
4. Ujamaa Bado ni Relevant (unaendana) na Maisha ya Wengi Vijijini
Itikadi ya Ujamaa imebakia kuwa nadharia, kwani kivitendo, CCM inatekeleza sera za soko huria zinazoendekeza ubepari na elements zote zinazoendana na mfumo huo. Lakini pamoja na hayo, bado Ujamaa unaendana na maisha ya asili aliyokuta mkoloni vijijini. Ndio maana TANU ilipata wafuasi wengi walioamini kwamba lengo kuu la TANU ni kumuondoa mkoloni na kuwarudishia wananchi utamaduni na maisha yao ya awali. Hali hii pia ilichangia sana Nyerere kuamua kufuata sera ya Ujamaa mwaka 1967 kwani Tanganyika huru ilikuwa dominated zaidi na vijiji vilivyosheheni wakulima wadogo wadogo waliokuwa wanaishi katika umaskini uliopindukia. Mazingira haya provided "excellent material and social basis for Ujamaa to flourish" &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; kwani dhana ya Ujamaa iliakisi maisha halisi ya walio wengi; lakini pia malengo ya sera ya Ujamaa na kujitegemea yaliendana na ndoto za wananchi wengi.
Tatizo lililopo sasa ni kwamba - Chadema haijafanikiwa kuja na itikadi ambayo wananchi wengi (wale waliounga mkono TANU) wanaweza kuikubali kama ndio mbadala wa kweli wa sera ya Ujamaa. Ni muhimu kwa Chadema kujipanga mapema na kurekebisha itikadi yake ya sasa ili iendane na uhalisia wa maisha ya watanzania walio wengi, lakini muhimu zaidi, iendane na ndoto ya watanzania hawa kwani kwa ujumla, hali zao na ndoto zao hazipishani sana na zile za enzi ya TANU na uhuru (1950s-1960s), na uliberali kama sera na itikadi, ambayo hata Chadema inaifuata, na pia CCM kuitekeleza kwa miaka zaidi ya 20 sasa, ni chanzo kikubwa cha umaskini Tanzania.
5. CCM imejenga Coalition na Taasisi zote nchini zenye nguvu kiuchumi, kijamii na kijeshi.
Kwa mfano, sekta binafsi (wafanyabiashara); majeshi ya ulinzi na usalama; vyama vya ushirika; watumishi wa umma; mashirika ya umma n.k. Tukianza na sekta binafsi, sekta hii ni muhimu sana katika kusaidia Maendeleo ya vyama vya siasa na sio kwa Tanzania tu, bali hata mataifa makubwa. Ingawa sekta hii haikupewa nafasi wakati wa mfumo wa chama kimoja, Tanzania huru ilikuwa na tabaka hili ambalo liliwezeshwa na mfumo wa kikoloni, hasa wahindi. Sasa ili waendelee na shughuli zao katika mazingira ya Ujamaa, wengi wao walitegemea kulindwa na baadhi ya viongozi wa TANU/CCM, ambao kwa kumzunguka Nyerere, walianza kuwa washirika wakubwa wa wafanyabiashara, hasa katika wizi wa rasilimali za umma. Mfumo wa vyama vingi ulipoingia mwaka 1992, na pia sekta binafsi kuhalalishwa, sehemu kubwa ya wafanyabiashara hawa ilikuwa tayari loyal kwa CCM, hivyo ikawa vigumu kwa vyama vipya vya siasa kujenga mahusiano na kada hii.
Kumekuwa na kelele nyingi kwamba CCM imenunuliwa na wafanyabishara, lakini lazima tukubaliane kwamba hakuna chama cha siasa kinachoweza kufanikiwa bila kuwa na uhusiano wa karibu na wafanyabiashara. Hata Chadema ikipata mwanya huo, ni muhimu ifanye hivyo, ili mradi iwe katika mazingira transparent, incorrupt na yanayozingatia taratibu zilizopo. Isitoshe, ni sahihi nikisema kwamba bila ya Chadema kuwa na viongozi kadhaa wenye uwezo mkubwa wa kifedha, isingefanikiwa kufika ilipo leo.
CCM pia ilishajijenga kwenye vyombo vya ulinzi na Usalama, kwa mfano, ilikuwa ni kawaida kwa viongozi wa juu wa jeshi kuwa wajumbe wa halmashauri kuu ya taifa (NEC) na Kamati Kuu (CC); vyombo ambavyo hadi leo vina maamuzi ya juu katika nchi yetu. Nafasi hizi pia walipewa viongozi wa taasisi za umma (mfano NBC, NIC/Bima); viongozi wa vyama vya wafanyakazi; viongozi wa vyama vya ushirika n.k; Pamoja na mabadiliko ya kutenganisha siasa na utumishi wa umma, majeshi ya ulinzi na usalama n.k, CCM bado ina mkono mrefu katika taasisi hizi, hasa kupitia mamlaka ya uteuzi ya Rais.
6. Katiba ya Sasa ya nchi inaipa CCM nguvu kubwa kisiasa
Jambo hili tayari linaeleweka lakini nitalijadili kidogo. Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 msukumo wake mkubwa ulikuwa ni muungano wa CCM na ASP (1977), kwani kabla ya muungano wa vyama hivi viwili, Tanzania haikuwa na katiba rasmi bali ya mpito kwa miaka karibia kumi tatu: 1964 &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; 1977. Katiba ya Tanzania (1977) ilitungwa ili kuhalalisha ufalme wa CCM. Moja ya mambo muhimu yanayopiganiwa katika michakato ya katiba mpya katika nchi yoyote ni "Democracy/democratization of the the society." Maana rahisi ya democratization ni - mabadiliko ya sheria/kanuni/taratibu za msingi za kuongoza mwenendo na utawala wa nchi husika. Katika mchakato unaoendelea wa kupata katiba mpya Tanzania, ni muhimu chadema ikaelewa mambo mawili:
i. Kwanza ni kukumbushana tu kwani tayari linajulikana: there has to be a compromise baina ya nini CCM inataka kiwepo/kisiwepo ndani ya katiba mpya na nini Chadema pamoja na wadau wengine wa demokrasia wanataka kiwepo/kisiwepo ndani ya katiba mpya. Ni vigumu kushawishika kwamba Chadema (na upinzani kwa ujumla) itafaidika na mchakato huu kuliko CCM, hasa ikizingatiwa kwamba uteuzi wa wajumbe wa tume husika kwa kiasi kikubwa una mkono mrefu wa CCM. Pia ni vigumu kuelewa kwanini mwanazuoni incorrupt and sober katika masuala ya sheria ya katiba, Professor Issa Shivji ambae anaheshimika kimataifa katika fani hiyo, hakuteuliwa kwenye tume ya Warioba.
ii. Pili, pamoja na Chadema kufanikiwa kuwa sehemu ya historia ya katiba mpya, wasijisahau na kudhania kazi ndio imekwisha kwani kazi ndio kwanza imeanza. Siasa za katiba mpya zitatawala sana uchaguzi wa 2015, hasa suala la muungano. Mwisho wa siku kutakuwa na referendum, hivyo na suala muhimu kuzingatia ni kwamba &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; bado Chadema haina uhakika wananchi wengi wataegemea upande gani kuhusu masuala mbali mbali katika referendum kwa maana ya &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; hatujui masuala yepi yatapata kura nyingi za NDIO au HAPANA. Sasa, iwapo leo chadema tayari wana misimamo ya wazi kuhusu masuala fulani fulani, halafu baadae, aidha kwa uhalali au kwa kuchakachua, referendum ikatoa matokeo kwamba wananchi wengi wapo upande tofauti na msimamo wa Chadema, haya yatakuwa ni maafa makubwa sana kwa Chadema kwa 2015 and beyond.
7. Mbinu za upinzani zinazotumiwa na Chadema Hazipo Consistent na Coherent
Kwanza Chadema wanastahili pongezi kwa kuonyesha ukomavu wa kisiasa kwa kuwa politically active majira yote, tofauti na zamani ambapo kilikuwa ni chama cha msimu wa uchaguzi tu. Lakini pamoja na mafanikio haya, bado Chadema kinaonyesha udhaifu mkubwa kwenye mbinu inazotumia kuendesha siasa za upinzani. Mbinu za Chadema kwa kiasi kikubwa hazina consistency (uthabiti) na coherence kwani zinabadilika mara kwa mara. Hili ni tatizo, hasa pale chama kinapokuwa hakina mvuto unaotokana na itikadi bali masuala ya mpito (mfano ufisadi) au mvuto wa wapiga kura unaotokana na personalities za viongozi kadhaa. Katika mazingira ya namna hii, umma (hasa wenye uelewa mdogo wa mambo), unaofuatilia siasa za chadema unaishia kuchanganyikiwa, huku ukizidi kuwa vulnerable na propaganda za vyama vingine vinavyoishambulia Chadema.
Yapo masuala ambayo chadema huwa na msimamo kama chama, lakini huwa inatokea mara nyingine individual leaders wanasimamia mambo ambayo mara nyingine yanapishana na mtazamo wa chama, au wa viongozi wengine. Kuna mifano kadhaa:
· Kwanza, Upinzani wenye utiifu na uaminifu kwa CCM &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; kuna nyakati viongozi wa Chadema huwa wanahubiri sera mbadala wa CCM huku wakiendelea kukitambua CCM kama ni chama halali chenye kuendesha serikali halali.
· Pili, Upinzani wa kuasi &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; Mara nyingine Chadema huonyesha umma kwamba chama kimejenga disloyalty na utawala wa CCM, lakini unakuta sio viongozi wote wanaoshikamana katika misimamo kama hii. Kwa mfano mwaka 2010 wabunge wa chadema walipotoka bungeni kukacha hotuba ya Rais Kikwete kufungua bunge, Zitto hakushiriki.
· Tatu, Upinzani dhidi ya muundo wa kisiasa (hasa katiba ya nchi) &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; Chadema wamekuwa wanapinga vipengele vingi vya katiba ya sasa, hasa vinavyohusiana na mapungufu ya current political system (mfano suala la muungano n.k), huku wakiendelea kuitambua serikali iliyopo madarakani kwamba ni halali kwa mujibu wa katiba ya nchi iliyopo sasa.
· Nne, Upinzani dhidi ya Itikadi ya CCM, lakini bila ya kutoa dira na itikadi mbadala iliyo practical &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; Chadema wamekuwa wanapinga sera nyingi za CCM bila ya kutoa itikadi na dira mbadala kwa Ujamaa; mpaka sasa hawana itikadi yenye kusisimua na kuvutia wananchi walio wengi (vijijini) &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; [rejea mjadala wangu wa awali kuhusu relevance ya Ujamaa katika vijiji vya leo Tanzania].
Ni muhimu nisisitize kwamba tatizo sio mbinu hizi za upinzani bali the inconsistency na incoherence katika hilo.
8. Tanzania inakabiliwa na Udhaifu wa Civil Society
Leo, watanzania wengi wanaishi kama ndugu, hasa wakati wa shida, lakini hawana &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];associational life', hata kwa standard za bara la Africa. Nitafafanua.
9. Na Mwisho ni tatizo la Political Culture Tanzania.
Kila jamii inaongozwa na values, norms na ethics &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; ambazo husaidia kutoa mwongozo juu ya mwenendo au tabia za kuzingatiwa katika mazingira ya siasa (political behavior), hasa mahusiano baina ya viongozi na wananchi. Historia ya nchi yetu inaelezea vizuri sana jinsi gani viongozi wengi wa kimila walivyokuwa na maadili mema kabla ya ukoloni na jinsi gani hali ilivyoanza kubadilika baada ya kuja mkoloni, hasa kutokana na sera yake ya &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];divide and rule'. Huo ndio ukawa mwanzo wa kuporomoka kwa maadili yetu ya uongozi hadi leo.
Baada ya uhuru, makabila mbali mbali yalikuwa yameshakuwa polluted na corrupted na ukoloni. Ili kuepuka madhara mengi zaidi, Nyerere alitumia mbinu mbalimbali ili kuondoa tofauti zetu kwa misingi ya ukabila, udini, ukanda na badala yake kujenga jamii yenye kuheshimiana kama binadamu, hali ya umoja, undugu, na usawa. Lugha ya Kiswahili pia ilikuwa muhimu katika kufanikisha lengo hili. Sera Ujamaa ilitupatia itikadi na dira inayoeleweka, na pia maadili ya uongozi, hivyo baadhi mapungufu ya utamaduni wa Kiswahili hayakuweza kujitokeza sana wakati wa ujamaa (tukumbuke kila kabila/utamaduni una faida na mapungufu yake), hivyo tulifanikiwa kujenga political culture bora, juu ya utamaduni wa kiswahili, bila matatizo makubwa. Lakini tatizo ni kwamba hatukuwa tumejiandaa kwa siku za mbeleni:
Kwa mfano, yale yote Nyerere aliyojitahidi kuyadhibiti (hasa suala la ukabila katiak uongozi/siasa), yameanza kushamiri kwa kasi kubwa ndani ya jamii yetu. Leo hii masuala ya uongozi na siasa yametawaliwa sana na misingi ya Ukanda, Ukabila na Udini. Nje ya fedha, ni vigumu kwa Mtu kufanikiwa kupata uongozi bila ya vigezo hivi vitatu (pamoja na fedha). Inawezekana baadhi ya watu wasikubaliane na mimi katika hili, lakini pengine mifano midogo itasaidia. Kwa mfano, katiba ya sasa ya Tanzania inaruhusu mtanzania yoyote kwenda kugombea nafasi yoyote ya uongozi katika sehemu yoyote ya Tanzania &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; bara na visiwani. Lakini sote tunajua ukweli kwamba ukiachilia maeneo machache ya mijini, ni vigumu kwa watanzania wa maeneo mengi ya Tanzania kumchagua mtu bila kwanza ya kuangalia vigezo vya ukanda, udini au ukabila.
Hata katika ngazi ya urais, hali ni hiyo hiyo. Kwa mfano, wengi tumeshasikia kauli kwamba Rais ajaye mwaka 2015 hatatokea kanda fulani; Vile vile kwa miaka mingi, kuna sumu iliyosambaa kwamba Rais wa Tanzania kamwe hatatokana na makabila matatu: (1)Wachaga, (2) Wanyakyusa na (3) Wahaya. Pia, katika siku za hivi karibuni, tumesikia wanasiasa kadhaa wakiapia kwamba rais ajaye 2015 lazima atoke mkoa fulani etc etc. Tumeanza kujenga na kulea tatizo kubwa sana katika jamii yetu; ukosefu wa ushindani wa kisiasa kwa njia ya itikadi, ukosefu wa dira na mwelekeo kama taifa, na uchaguzi wa viongozi unaofuata vigezo vya personalities za wagombea (badala ya misimamo yao), haya yote yanazidi kuimarisha mizizi ya ukabila, udini na ukanda.
Ni vigumu kwa sasa kubaini masuala la udini, ukabila na ukanda yata &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];play out' vipi katika siasa za CCM na Chadema 2015. Kitakachoweza kutokea ni kwamba &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; viongozi kutoka dini au makabila fulani wataanza kuunda makundi yatakayo exploit tofauti zilizopo kihistoria kwenye jamii &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; tofauti za kiuchumi na kielimu, kwani zipo jamii nyingi ambazo zinahisi historia ya nchi na utawala wa CCM haujawatendea haki.
Uwepo wa ombwe la itikadi utasababisha ushindani wa CCM na Chadema mwaka 2015 utawaliwe na siasa chafu sana. Ni dhahiri kwamba Sera za CCM na Chadema hazipishani sana - wote wanaunga mkono (kwa kujua au kutojua) kumnyonya mkulima ili kufaidisha nchi tajiri, and in return kupata fedha (AID), lakini muhimu ili vyama vyao viendelee kuwa in good books na wakubwa wa dunia yetu (tofauti na Nyerere aliyepingana na upuuzi huu); ndio maana katika hali ya leo, wahisani sasa wanakabiliwa na democracy fatigue, kwani wanajua kwamba uwepo wa CCM au Chadema Ikulu hautakuwa na utofauti wowote mkubwa kkwenye interest zao. Kikubwa wanajali zaidi uwepo wa amani ili strategic interest zao zisipate madhara, hasa vitega uchumi.
Vinginevyo ni muhimu Chadema ikafanya marekebisho ya maana kwenye itikadi yake, kwani nje ya uchovu wa wananchi na CCM, nje ya agenda ya serikali ya CCM kutokuwa na maamuzi magumu kutatua matatizo ya nchi, na pia nje ya agenda ya ufisadi, Chadema haina ammunition ya kutosha kisera kuitoa CCM magogoni. Hivi karibuni, chadema imekuwa ikifananishwa na TANU, jambo ambalo ni la kheri kwa Chadema. Lakini ili Chadema iwe TANU iliyokamilika, inahitaji ije na &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];new and a radical orientation' inayo challenge dhana ya soko huria (hasa mapungufu yake), na ambayo inahimiza umuhimu wa umiliki wa mageuzi (ownership of reforms kwa wananchi), badala ya sasa ambapo mageuzi yanafuata mtindo wa &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];Top &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; Down" (badala ya bottom &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; up). Ni muhimu na ni lazima wananchi wahisi kwamba kuna chama ambacho kina nia ya kuwashirikishwa katika kila hatua ya mageuzi i.e. a bottom up and participatory process (badala ya top &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; down), kwani tangia mwaka 1985 Tanzania ilipoachana na mfumo wa Ujamaa, wananchi wamekuwa wanatengwa na kuachwa wapigane vikumbo kivyao vyao na nguvu za soko (market forces). Hili linahitaji kubadilika na ndio kete kuu ya Chadema 2015 itakayowaletea mafanikio yenye mashiko zaidi mbali ya vita dhidi ya ufisadi ambayo sio mwarobaini (panacea) ya matatizo ya wananchi walio vijijini. Tukumbushane tu kwamba CCM enzi za ujamaa ilijitahidi sana kuzuia ufisadi lakini hiyo haikutosha kumletea mabadiliko mwananchi wa kijijini.
Ni mambo haya tisa ambayo nadhani yakifanyiwa kazi na Chadema, basi yatazidi kujenga mazingira ya utayari kwa Chadema kushika madaraka ya nchi 2015 &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; kwani mbali ya "doing the right things", pia watakuwa wametekeleza dhana ya "doing things right"

- CCM ndio iliyoongoza mageuzi ya kiuchumi (political reforms) Tanzania;
- Umiliki na Udhibiti wa Vyombo Vya habari;
- Uchumi Mkubwa Wa CCM;
- Ujamaa Bado ni Relevant (unaendana) na Maisha ya Wengi Vijijini;
- CCM imejenga Coalition na Taasisi zote nchini zenye nguvu kiuchumi, kijamii na kijeshi;
- Katiba ya Sasa ya nchi inaipa CCM nguvu kubwa kisiasa;
- Mbinu za upinzani zinazotumiwa na Chadema Hazipo Consistent na Coherent;
- Tanzania inakabiliwa na Udhaifu mkubwa wa Civil Society; na
- Political Culture ya Tanzania ina matatizo.

- Demographics:
- Social Capital: