CHADEMA: Tujadili Utayari wa Kutawala Nchi 2015

CHADEMA: Tujadili Utayari wa Kutawala Nchi 2015

Hii ndio sababu ya mimi kusema itachukua miaka mingi sana ccm kuangushwa, CDM bado kuwa chama mbadala,wanasafari ndefu. Hawajajipanga kikamilifu, wanapata nguvu kutokana na uzembe wa ccm lakini ki sera bado wako nyuma sana. Wametoka kwenye chama cha msimu na wamerudi kwenye sera za msimu.utawasikia wakati ccm imekosea jambo. Je ccm wakijipanga vizuri CDM watajadili nini?
 
You might have a valid point. Lakini naomba nikuulize: Je kwanini imechukua miaka 15 (1995-2010) kwa chadema kuwa na nguvu kwenye umma, kiasi cha kupelekea kuaminiwa kwamba Chama kipo tayari kuchukua madaraka ya nchi 2015? Je, kuna strategy maalum ambayo Chadema walikuwa wanaitumia consistently? Kwani hoja yako inaashiria kwamba kuna mkakati maalum ambao Chadema waliuweka miaka 15 iliyopita na ndio umezaa matunda leo. Ningependa kujua hili kwani binafsi sina taarifa yoyote na badala yake nadhani mafanikio ya Chadema yametokana na Chama kufanikiwa ku link umaskini wa wananchi na ufisadi, wakati ukweli wa mambo ni kwamba ufisadi explains only a fraction of the story – kwanini watanzania maskini. The bigger story ni sera zinazoshinikizwa na mataifa matajiri, sera ambazo hata chadema wataenda kuzitekeleza Ikulu kama CCM inavyofanya sasa. In short, we talk of development but we do not own our development agenda!

Ufisadi ni janga kwa uchumi wetu kwani umedumu tangu enzi za Sokoine. CHADEMA muhimu walivalie njuga. Ufisadi is highy linked to developed nations (mikataba mibovu, forced policies in monetary, employment, health, etc). Angalia fujo kutoka kwa wananchi (grassroot) katika maeneo ya uwekezaji hasa migodi ya dhahabu!

Ni dhahiri wananchi wamechoka. If corruption is used as a weapon by CHADEMA and is understood and appreciated then it is perhaps a leeway towards developing a realistic national agenda. In any case the ruling party CCM if truly wishes Tanzania well, should have shown genuine cooperation with the opposition to make the dream Tanzania they have failed to provide instead of cursing and childish propaganda towards the opposition which is a waste of precious time.
 
Nimemsoma kwa makini sana Ndugu Mchambuzi. Ana hoja nzito sana.

Amefanya uchambuzi mwanana...amefanya kile kinachojulikana kama 'a critical analysis' ameandika kisomi kweli kweli.

Kwa jitihada kubwa ya wazi aliyochukua kukamilisha andiko lake, namwona kama ''an intellectual giant''. Kazi za namna hii ndizo zinazozalisha mawazo na fikra mpya, wala tusitake kumwona Mchambuzi kama mtu mwenye nia ovu na CHADEMA. Nafarijika sana kuona kuwa wenzangu kadhaa wamejadiliana naye kwa hoja, naye amewajibu kwa hoja.

Panapo majaliwa, nitafanya review kidogo ya bandiko lake kesho ama keshokutwa. Kwa sasa nafanya maandalizi.
 
Last edited by a moderator:
Unachoshindwa kuelewa hapa ni kwamba TANU ilitoa ahadi ya kuwakomboa watanganyika kisiasa na kiuchumi, ilifanikiwa kisiasa lakini imeshindwa kuwakomboa kiuchumi.

Watanzania wanahitaji the second independence kwani the first one chini ya TANU haikukamilika. Ni bahati mbaya tu CCM ya sasa inahusishwa na TANU lakini ukweli ni kwamba hizi ni taasisi mbili tofauti kabisa, kwa mfano, TANU haikumkomboa mzanzibari. Mtu anaetatizwa na Chadema kufananishwa na TANU basi sio muelewa wa matatizo ya watanzania.

Pengine itasaidia iwapo tutaita chama kilichoikomboa tanzania kwa jina lingine lisilohusiana na CCM ndipo itaeleweka vizuri kwanini changamoto za TANU na Chadema ni zile zile.

Ha ha...saa kama unafahamu kuwa TANU haikumkomboa Mzanzibar(Ingawa nafahamu walimkomboa na walituma askari polisi wengi kulinda mapinduzi baadaye pia) kwa nini unataka watu wapoteze muda ku refer to their failed promises?

Pia ujue dunia ya leo uchumi ni kikwazo cha mambo mengi, kuanzia knowledge transfer, geting ana edge in an anya business , sports, medical researches etc someone need money.

Back to my earlier posting, utaona nilitaka CDM waingie kwa tahadhari katika issue ya kulink na TANU.Tusiwe naive and militant.Tayari Mh. Nape na wengine waliwahi sema mambo kadhaa yalifanaywa na kuasisiwa na TANU na si CDM. So next ni kuweka link ya CCM na TANU, hapatakuwa na time kwa watanzania wasioweza chambua hayo.Hembu fikiria CCM wakisema kuwa "Wao ni TANU iliyoboreshwa kwa kuongezea ASP na kuhama toka kugombea uhuru na kuingia katika leta maendeleo".

Halafu wakaelezea mapungufu ya TANU na kusema kuwa CDM hawana Jipya zaidi ya kuenda anzia kule walipoanzia CCM na hivyo watachukua miaka kama ya CCM ili wafikie CCM walipo? Sijui utaanzia wapi waelimisha watu kuwa CDM haikupata inspiration kwa TANU, na badala yake wamepata katika parties nyingine za Kisasa Duniani.

Kwanza TANU ilikuja na ujamaa ambao ulishindwa kwa kila kitu duniani, ikiwepo pia kuwatenganisha watu na Imani zao Kuhusu uwepo wa Mungu na Umuhimu wake kwa taifa.Sasa hivi tupo katika 21 century na matatizo yetu si yaleyale na masuluhisho yake si yale ya zamani tena.

Nasiktika kuwa na wewe unacheza mchezo niuchukiao sana wa kublack mail. Kuwa mtu anayetaka Tenganisha CDM na TANU kuwa hajali matatizo ya watu, ili umjengee mtu sense ya kuwa guilty.Ila ulichoandika kinaonyesha kuwa factor iliyokuvutia ni ahadi(Tena ahadi zilzioshindwa), lakini katik amaisha kila mtu na taasisi zinaahidi, na nyingi hufanikisha ahadi zake. Nadhnai CDM wangejinadi kuwa wanakauja kamilisha kile, TANU na baadaye CCM walichoshindwa fanikisha.

Ukombozi pia una mipaka na tafsiri yake CCM nao wanaweza ita system yao iliyomtolea matanzania jukumu la kufikiri kuhusu hatima ya Taifa.Kwa kuwaletea zidumu fikra za mwenyekiti, kufanya ila raia aamini kuwa serikali ndiye mlezi na tegemeo lake.So kwa wajinga wata agree na hii nortion, kwani wapo wengi hawapendi fikiri kuhusu namna ya kuandaa maisha, ku support wategemezi wao na kuwa responsible.Hawa wataipenda CCM wakidhani inawasaidia kuhusu familia yake.

So hawa amaa wanaweza claim kuwakomboa raia kutoka utumwa wa kuwaza jinsi gani watapata riziki ya kila siku, ila hawatasema utumwa wa kuwa na ubongo ila hautumiki kupata fikra huru za mwenye ubongo. Ndio maana wabunge wa chama tawala hawajui kuwa wana utumwa mkubwa sana wa kifikwa, kiuchumi, na baadaye wa kisiasa.
 
Unachoshindwa kuelewa hapa ni kwamba TANU ilitoa ahadi ya kuwakomboa watanganyika kisiasa na kiuchumi, ilifanikiwa kisiasa lakini imeshindwa kuwakomboa kiuchumi. Watanzania wanahitaji the second independence kwani the first one chini ya TANU haikukamilika.

Ni bahati mbaya tu CCM ya sasa inahusishwa na TANU lakini ukweli ni kwamba hizi ni taasisi mbili tofauti kabisa, kwa mfano, TANU haikumkomboa mzanzibari. Mtu anaetatizwa na Chadema kufananishwa na TANU basi sio muelewa wa matatizo ya watanzania
.

Pengine itasaidia iwapo tutaita chama kilichoikomboa tanzania kwa jina lingine lisilohusiana na CCM ndipo itaeleweka vizuri kwanini changamoto za TANU na Chadema ni zile zile.

Mkuu Mchambuzi heshima yako.

Hapa naona unaenda nje kabisa ya mstari unaposema kwamba TANU na ASP zisihusishwe na kwamba hizi ni taasisi mbili fotauti kabisa, mkuu umesoma historia ya Tanzania ipi?

TANU na ASP ni vyama vilivyoshirikiana kwa hali na mali kuhakikisha mwafrika anajikomboa na kuwa na uhuru wake kamili, Hayati Nyerere TANU na hayati Karume ASP.

Isitoshe Nyerere ndie aliemsaidia Karume katika harakati zake za kuiimarisha ASP Zanzibar na baadae Nyerere kumshawishi Karume na ingawa alikataa hadi alipokufa ni TANU na ASP walioungana na kuundwa CCM mwaka 1977.

Hii sehemu ya historia mkuu usiisahau hata kidogo na muhimili wa CCM umeanzia TANU na ASP.

Mbali ya hii kasoro ndogo uchambuzi wako ni makini.
 
mchambuzi bado hujaonesha kuwa CDM kujiingiza katika legacy ya TANU kuna zaidi ya vifaida vidogovidogo.Na vingi vinavutia wazee waathirika wa CCM, ambao sasa ndio wanaona kuwa walichoaminishwa kuhsu CCM si kile wanachovuna.watu walitoa kila kitu ch afamilia kujenga office za CCM, kuchangia mwenge, viawanja vya michezo, Jumuia ya Wazazi etc.Leo ni vya CCM na wanaofaidi ni wengine katik tabaka lao nadnai ya CCM.Hawa wazee hata bila wakumbusha TANu wanashikika, kwani Meru walishikwa vipi?

Si kazi ya CDm kufufua ndoto za TANU ambazo nyingi zilikuwa applicable enzi za cold war, enzi za uhuru, na vuguvugu la Pan Africanism.Leo tuna changamoto nyingine.Na ujamaa tuujuao si kitu leo unless tunataka ingia katika inward spiral waliyopo CCM, na si ajabu nchi tuziteteazo kuwa Kinyume chetu baada ya msaada wetu kwao.Ho wmany countries zinatukumbuka lets alone kuwa na mahusiano nasi baada ya kutoa kila kuwasaidia?South africa?Nigeria?Malawi? palestina?Lebanon,syria?Sychelles?Commoro?
 
Well said Mchambuzi.


Hata hivyo, kumbuka kuwa itafikia mahali, of all the situations ulizosema may not apply kwa watu kuchoka....hapa ndipo changes hutokea regardless ya nini!refre, mapinduzi ya Ufaransa, kuondolewa wakoloni Afrika..na hivi sasa yaliyotokea Misri, Libya, Syria na kwingineko.

Hivi unadhani tutafikia hatua ya umma kuleta mapinduzi kama nchi za afrika kaskazini kweli? Binafsi sidhani kama tumefikia hali hiyo kwani CCM is not the common enemy - ni kweli kuna tensions kubwa sana kwenye jamii yetu kutokana na competing socio-economic interest between tabaka la walio nacho na wasionacho but again, CCM is not the common enemy kwa tabaka zima la wasio nacho;

Lakini pia hujaangalia CCM wanavyoandaa anguko lao kwa mambo ambayo wengi wanayasahau kuyaona: shule za kata (uwingi wa wasomi hata kama wanapata zero, lakini ni chachu ya mabadiliko), mitaala ya elimu, matatizo makubwa ya wafanyakazi katika kila nyanja..na hata hayo maisha magumu uliyoyasema!

Ni kweli, anguko hili laja na litapitia sanduku la kura lakini ni kwa bahati mbaya sana watanzania wengi hawaelewi kwamba CCM inachangia kidogo sana katika umaskini wao, kuna many other factors ambazo hata chadema wakiingia ikulu wananchi wengi sana watakata tamaa muda mfupi tu baadae kwani Chadema haielezei hadithi yote kwanini nchi yetu maskini, and to make matters worse, chadema itaenda kuendeleza matakwa ya wahisani kwa mwendo usiokuwa tofauti sana na wa CCM hivi sasa; ushauri wangu kwa chadema ni kufanya safari ya ikulu kuwa a project ambayo inawaelezea watanzania kwamba watakaofaidika na ushindi wa Chadema 2015 ni watoto wetu na wajukuu zetu na sababu za msingi to defend hili zipo, bila hivyo, CCM haitakawia kurudishwa tena madarakani 2020 - 2025 na wale wale walioiangusha CCM 2015 (iwapo CCM itaanguka);
 
Kwa utaratibu wa mabadiriko unavyoendelea sina uhakika wa lengo la mada yako kwamba haitafuti mikakati ya CDM. Ila mimi binafsi nawaamini CDM kwa mikakati yao kwa lengo langu moja tu NIMECHOSHWA NA CCM NAHITAJI MABADIRIKO
Hii quote ndio msingi wa mada yangu. Ningependa nieleweke kwamba naposema "utayari wa chadema", haina maana kwamba najaribu kujenga hoja kwamba chadema haipo tayari.

Kama ulinisoma vizuri, nimeweka bayana katika sehemu ya kwanza kabisa kwamba sasa Tanzania ipo tayari kutafuta mbadala wa CCM, lakini tatizo langu kubwa ni kwamba CDM wamewekeza sana on What went wrong for CCM (mapungufu na udhaifu wa CCM) which is okay lakini haitoshi kwani ni muhimu pia kuangalia on What went right for CCM (factors zilizoifanya CCM iwe imara as a brand, as an institution and as a political party), and all along nikajenga hoja kwamba bila ya kuzifanyia kazi factors hizi, hoja juu ya madhaifu ya CCM haitatosha kuipatia Chadema ushindi 2015;

Vinginevyo kimsingi nakubaliana na wewe, hasa kuhusu suala la vyombo vya habari ingawa wewe unaliangalia nje ndani (hata chadema pia wanafanya hivyo), mimi nalitazama ndani nje.

Kwa mfano, sielewi kazi ya waziri kivuli wa habari wa Chadema (nje ya kuandaa bajeti mweizu wa sita) huku inaeleweka wazi kwamba majukumu na utaratibu wa kazi wa wizara ya habari ni ule ule kama enzi za chama kimoja; nachokiona ni Chadema kuisemea serikali kwa wananchi kuhusu rafu za hapa na pale, na nadhani hata wewe utakubaliana na mimi katika hili na kwamba kuisemea serikali kwa wananchi haitoshi.
 
Naona kama hizo dhana mbili zinapingana, mwanzo umesema kuwa Chadema inaweza kuongoza kwa ridhaa tu bila pesa baadae umesema Chadema kimefika kilipofika kutokana na viongozi kadhaa kuwa na uwezo wa mkubwa wa kifedha.

Nadhani hili ni straight forward Mammamia:

Maana yangu ni kwamba - kuna baadhi ya watanzania ambao wanaamini kwamba gharama zote za kuendesha nchi zinatokana na pesa za CCM na kwamba CCM ikianguka itaondoka na hizo pesa, na upinzani hautakuwa na rasilimali za kuendesha nchi.

Kwenye hoja yangu ya pili kuhusu uwezo wa kifedha wa viongozi wa Chadema nilikuwa nahimiza umuhimu wa Chadema kama chama kujitafutia vyanzo mbalimbali vya pesa ili mradi katika mazingira safi, kwa mfano kama michango ya wajasiriamali halali kama Mzee Sabodo; Bottom line ni kwamba chama chochote cha siasa kinahitaji fedha za kujiendesha wakati kinatafuta madaraka ya kuongoza nchi;

(1) bila ya fedha za kujiendesha kama chama kikuu cha upinzani, Chadema itapata wakati mgumu sana wa kujijenga, hivyo wajitahidi kutafuta vyanzo vya pesa lakini thanks to uwezo wa baadhi ya viongozi wake kama kina mbowe, mtei, ndesamburo n.k;
(2) wakati wanajipanga kuingia madarakani, wajaribu kuondoa imani potofu kwa baadhi ya wananchi kwamba Chadema ina uwezo wa kuendesha nchi kwenye maeneo yote kasoro fedha kwani wakiingia ikulu, walipa kodi watafanikisha hilo;
 
Tuko pamoja Mchambuzi Mkuu! Kusema kweli nimependa uchambuzi wako wa kujenga, na kama ni wa kusikilizwa utaleta tija kubwa kwa chama.

Tatizo kubwa ninaloliona katika vyama vyetu, ni kuwa watu hukimbilia kupinga kila neno kwa kupinga tu, bila ya kuchukua hata dakika chache za kutafakari mawazo mbadala.

Kitu kilicho wazi ni kwa saa ya mabadiliko Tanzania imewadia - ingawaje njia bado ni ngumu.
 
Mchambuzi, umeleta sredi ambayo kama Watanzania tungekua watu wa kujadili hoja za manufaa kwa taifa letu,ingepata wachangiaji wengi.

Kama kuna kipindi viongozi wa chama changu CDM wanapaswa kujadili mambo ya msingi nchi yetu itaongozwa vipi baada ya 2015 ni sasa! Hizi stori za watu kutafuta urais,binafsi zinakwaza sana. Siyo wakati wake sasa, tujenge chama! Kikichukua dola kionyeshe tofauti.

Hili ndio litaweza kuja kuwa anguko la Chadema 2020 au 2025 kwani wanajisahau kwamba licha ya CCM kuboronga hapa na pale, bado CCM na Chadema have a common enemy anaefanya mtanzania azidi kuwa maskini siku hadi siku; kwa mfano, soko huria ni tatizo kubwa sana kwa mtanzania hasa wa kijijini, halina manufaa yoyote ya maana, yet sio CCM wala Chadema wanao challenge suala hili.

Ndio maana nikasema kwamba wahisani wao hawajali nani ataingia ikulu 2015, wanachojua ni kwamba matakwa yao yatatekelezwa kama yalivyo kwani wakati CCM inayatekeleza ikiwa madarakani, Chadema inaonyesha kila dalili kwamba itaenda kufanya hivyo hivyo; ndio maana lazima tukubaliane kwamba come 2020 au 2025, maisha ya mtanzania wa kijijini (na vijana wengi wa mijini) bado yatakuwa ni yale yale, na wengi watasema kumbe CCM na CDM ni hao hao.

Tazama kwa mfano matumaini yaliyokuja na chama cha MMD cha Chiluba Zambia mwaka 1991 na kuiangusha UNIP ya kaunda; lakini hivi sasa MMD nao wanaonekana hamna kitu; ndio maana huwa nahimiza kwamba watanzania wasijidanganya eti tumeshapata vyama viwili vya upinzani, hivyo tusihangaike na vyama vipya; je, iwapo chama cha patriotic front (PF) cha Satta kingefuata mawazo kama haya, wazambia wangepata wapi mbadala wao to UNIP na MMD???

Chadema kama inataka kufanikiwa, ianzishe project ya kuwaelimisha watanzania kwamba kazi ya mageuzi ya maisha yao kiuchumi ni kazi ndefu na pevu sana, na watakaofaidika na project hii sio wananchi hawa hawa by 2020 au 2025 walioichoka CCM 2015 bali watoto na wajukuu zao; nje ya hapo, tutarajie CCM kurudi tena madarakani 2020 au 2025 na wananchi kutoitoa tena madarakani kwa muda mrefu sana;
 
Mchambuzi nakubaliana na wewe..lkn ninaushauri wa ziada CDM kabla ya kuwaza kutawala lazima wawatolee uvivu mapandikizi kwao..maana bila kuwatolea uvivu hawawezi shika dola.

Nawashauri watafute kura 100 za wanachama CDM JF za kuwashinikiza viongozi wao Mbowe na Slaa wahudhurie mdahalo humu kisha watoe onyo kali kwa wale wote wanaosaliti chama kwa kuacha kukijenga chama na kujijenga wao.

Hii itawasaidia viongozi wao pia kuwatoa nduli wanaoharibu chama chao ambacho wananchi tunaamini wanania ya dhati kuleta maendeleo. Mie sio CDM lkn nachukia sn vijana iwe wa CCM au CDM sijui NCCR ambaye anacheza siasa za mbimnu ya kuwanyonya wananchi nachukia sn.

CDM mdharau mwiba????.........................

Ni kweli, hili ni moja ya masuala ambayo yanaipunguzia chadema kasi, ndio maana nikaelezea katika original post yangu kwamba upinzani unao onyeshwa na chadema haupo consistent kwani mara leo viongozi wanakuwa na msimamo mmoja, mara kesho huyu anakuwa na msimamo mwingine unaoudhi wenzake, mara siku nyingine chadema kinasimama hivi kama chama etc etc!

Hili ni tatizo, na nadhani linatokana zaidi na Chadema kutokuwa inaongozwa na itikadi i.e. umaarufu wa chadema sio kwamba itikadi yake inawapa mvuto wananchi, bali ni mvuto wa personalities (viongozi) mbali mbali, na ndio maana baadhi ya hawa viongozi mara nyingine wanajiona wapo juu ya chama wakati ukweli ni kwamba chama sio mtu mmoja, chama ni watu;
 
Mchambuzi ukiniuliza na mawazo gani kuhusu kesho ya Nchi yangu, naweza kukujibu hivi:

Nafuu hata Paka awe raisi lakini siyo kiongozi yoyote toka CCM sababu CCM wote hawana uwezo wa kusema Hapana.Hakuna Rais wetu dhaifu wala msaidizi wake hakuna, wote walio CCM wanasubiri ni namna gani apate uongozi ili afilisi zaidi.

Ile dhana ya vyama vya upinzani vitaleta vita imepitwa na wakati, iangalie Zambia, Malawi mbona vinavyotawala leo ni vilivyokuwa vyama vya upinzani?

Watanzania tuondoe woga,tuone uchungu na Maliasili zetu tubadilishe mtawala ili hata anayekuja awe mwoga ajue kesho yake ipo kwenye hatihati.

Upo sahihi, lakini muhimu zaidi una haki na kuwa na uchungu huo kwani ni dhahiri watanzania walio wengi wamechoka; ila kuhusu upinzani Zambia kwa mfano, hivi unajua CCM ya Zambia (UNIP) ilianguka na Chadema ya Zambia (MMD) ikachukua madaraka lakini nayo ikaja angushwa na (PF) ya Satta? Nani atakuwa Patriotic Front wa Tanzania? Nauliza hivi kwa sababu kuna ombwe kubwa sana la kiitikadi among vyama vya siasa, na hili ni tatizo kubwa ingawa wengi humu hawakubaliani na mimi; ni dhahiri kwamba wakati CCM inajitahidi kutekeleza sera za soko huria ambazo kwa zaidi ya miaka 20 zimekuwa zinazidi kuwamaliza watanzania, Chadema nao wakienda ikulu watatekeleza hizi hizi; usisahau kwamba mzee Mtei alipingana na mwalimu na sera zake za ujamaa na akaja baadae kuanzisha chama chake (Chadema) ambacho nia yake ilikuwa ni kutekeleza sera za soko huria kwa ushirikiano mkubwa na wahisani; leo hii CCM inatekeleza sera ambazo mzee mtei alizitaka, tatizo ni kwamba ndani yake CCM imelea ufisadi mkubwa, lakini pia tusisahau kwamba ufisadi ni sababu ndogo sana ya kuelezea hadithi ya umaskini Tanzania; ni muhimu Chadema wakajifunza kwa MMD ya Zambia ili wasije jikuta kwenye same situation baadae; na moja ya njia ya kujiepusha na balaa hili ni kurekebisa itikadi iweze ku challenge soko huria kwa manufaa ya watanzania walio vijijini;
 
lakini Dr.slaa hakuyasema hayo kwa bahati mbaya, wanajua udhaifu wa chama cha magamba kuwa kadri unavyowakosoa ndivyo wanavyozidisha makosa ujue jinsi walivyozeheka, hiyo inasaidia kuwajulisha wananchi kuwa magamba wanatupeleka ndiko siko, hivi wasipowakosoa watakuwa wanafanya siasa gani?

Upo sahihi, kwani moja ya kazi ya chama cha upinzani ni kuikosoa serikali iliyopo madarakani; lakini nimelieleza hili kwa kirefu - kwamba ni sawa kwa chadema kutumia fursa ilivyojitokeza ya udhaifu wa CCM lakini pia wasisahau kutumia muda mwingi pia katika kuelewa what went right for CCM; huu ndio ulikuwa msingi wa mada yangu;
 
CDM hawahitaji kuzama sana katika itikadi za TANU.VIjana hawaijui TANU, na TAnu haikuwa perfect kihivyo.Ila kuna vifaida vidogo vidogo na kujihusisha nayo , pamoja na vitu fulani ambavyo ni universal vilivyokuwepo katika TANU.

Kukimbilia sana TANU ni kuwapa CCM comfort zone.Kwani watapunguza nguvu kwa kusema kuwa ni ya TANU, halfu warudi sema kuna ni ya CCM kwa vile ilizaliwa katika TANU.Sasa inabidi pawe na New creations.Ili CDM waseme kuwa wana nia na mshikamano kama TANU ila wanafanya Mambo makubwa kuliko TANU.

Chadema haina haja ya kuzama katika itikadi za TANU, upo sahihi, lakini kuna suala la msingi hapa ambalo nadhani unashindwa kulielewa: Watanzania wapo (hasa vijijini) wapo katika mkao wa kupata uhuru wao wa kiuchumi miaka 50 baada ya TANU/CCM kushindwa kufanikisha hilo; kwahiyo nachosema hapa ni kwamba harakati za Chadema limeanza kuwakumbusha wananchi hasa wa vijijini vuguvugu la TANU, na baadhi yao wanaanza kuamini kwamba pengine malengo yale ya TANU ya kuwaletea ukombozi wa kiuchumi yatafanikishwa na Chadema; Kwahiyo Chadema hawana haja ya kuzama kwenye itikadi za TANU bali kuelewa watanzania hasa wa vijijini wamekuwa wanasubiri mapinduzi ya namna gani na kwanini waliamini TANU ingeweza kuwaletea mapinduzi hayo, thats all.

Bottom line is - Chadema wanaweza kabisa kumtupa jongoo (TANU) lakini sio mti wake (mambo ambayo TANU ililenga kimkakati kuwakomboa watanzania hasa wa vijijini).

Nicholas:
Naomba unisaidie kujibu swali hili: je, Chadema wana njia gani mbadala ya kuwakmboa small peasants vijijini ambao waliunga mkono TANU?
 
Hii ndio sababu ya mimi kusema itachukua miaka mingi sana ccm kuangushwa, CDM bado kuwa chama mbadala,wanasafari ndefu. Hawajajipanga kikamilifu, wanapata nguvu kutokana na uzembe wa ccm lakini ki sera bado wako nyuma sana. Wametoka kwenye chama cha msimu na wamerudi kwenye sera za msimu.utawasikia wakati ccm imekosea jambo. Je ccm wakijipanga vizuri CDM watajadili nini?

Hii ndio hoja yangu ya msingi, na kwa kweli binafsi sina nia mbaya kabisa na chadema, kwani ipo siku naweza kuwa mwanachama wa chadema au chama chochote chenye mwelekeo wa kweli wa kuwakomboa watanzania; tunavyoleta mada za kujadili utayari, mimi nilikuwa nadhani ilitakiwa ichukulie kama ni creative criticisms, not destructive; ndio maana hata CCM ya nyerere, pamoja na mapungufu yake, kwenye mwongozo wake ilitamka hivi:

"Kujikosoa na kukosoana ni silaha ya Mapinduzi."
 
Aiseeee baba yangu huu uzi ni mzuri sana namanisha ni chakula cha ubongo cha kushangaza umechangiwa na watu 2 tu embu tuache uvivu wa kusoma,,2some na 2changie


ngoja naweke mbege pembe pembeni kweli
 


Ufisadi ni janga kwa uchumi wetu kwani umedumu tangu enzi za Sokoine. CHADEMA muhimu walivalie njuga. Ufisadi is highy linked to developed nations (mikataba mibovu, forced policies in monetary, employment, health, etc). Angalia fujo kutoka kwa wananchi (grassroot) katika maeneo ya uwekezaji hasa migodi ya dhahabu!

Ni dhahiri wananchi wamechoka. If corruption is used as a weapon by CHADEMA and is understood and appreciated then it is perhaps a leeway towards developing a realistic national agenda. In any case the ruling party CCM if truly wishes Tanzania well, should have shown genuine cooperation with the opposition to make the dream Tanzania they have failed to provide instead of cursing and childish propaganda towards the opposition which is a waste of precious time.

Kinachonifanya nione ufisadi kama ni agenda short-lived ni pamoja na masikitiko yangu naposikia baadhi ya watanzania wakitafsiri ufisadi kama ni baadhi ya Viongozi wa CCM Kuwa na Tabia ya Kula Wenyewe. Hii ni sawa na kusema kwamba kula ni sawa lakini usiwe mchoyo; ndio maana watu wengi wakiwa nje ya madaraka wanapinga sana ufisadi, lakini wakiyapata madaraka, hadithi inabadilika, na wakijitahidi kuwa tofauti, basi hawali wenyewe! ​

Ufisadi usiunganishwe na umaskini tu; chadema has to attack ufisadi in a holistic way;
 
Nicholas

Nadhani tatizo ni kwamba wewe unaiangalia TANU in a top-bottom approach (unaangalia viongozi/wanasiasa wa TANU/CCM) and then base your comparative analysis from that angle, na ndio maana inakuwa na mushkeli kidogo tukianza kuifananisha TANU na CHADEMA.

Lakini ukijitahidi uiangalie TANU based on a bottom - up approach, nina uhakika tutakuwa ukurasa mmoja; bottom - up basically ni kuwaangalia watanganyika wa 1940s-1950s walikuwa na aspirations gani bila hata ya uwepo wa TAA au TANU, kwani ni baada ya Nyerere kuzisoma hizi hopes and aspirations, ndio akaja na TANU...; lazima ujue kwamba issue ya TANU Kufeli doesnt mean kwamba aspirations za wanavijiji nazo zimekufa, zipo pale pale hata kama ujamaa ulifeli, na hii ndio opportunity ya Chadema to tackle;
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom