Nicholas,
Mimi nadhani wengi tunachukulia kama vile jamii zetu kabla ya ukoloni existed in a vacuum. Hii sio sahihi. Vile vile aidha kwa makusudi au bahati mbaya, wengi tuna mazoea ya kutazama jamii zetu kwa jicho la "WEST", kwani hoja zetu nyingi zinaleta tafsiri kwamba mkoloni aliikuta TANU madarakani, akaipokonya madaraka kwa nia ya kuiboresha nchi na watu wake, lakini TANU wakavuruga mipango hiyo, hivyo mkoloni akamrudishia mtanganyika nchi yake kupitia TANU, lakini TANU wakaharibu kila kitu in the long run. Ni vizuri umetaja societies kama zile zilizokuwa zinaongozwa na Mkwawa. Ebu tuzitazame kwa undani kidogo.
Kabla ya ukoloni, kulikuwa na jamii kuu za aina mbili: Kwanza ni zile
centralized and highly politicized; pili ni zile zilizokuwa decentralized and stateless.
- Tuanze na Decentralized societies: Hizi zilikuwa made of jamii/vijiji vidogo vidogo vilivyokuwa vinaishi jirani jirani na havikuwa na any meaningful political units na pia hazikuwa na political connection na jamii kubwa kama za mkwawa zaidi ya mahusiano ya kibisahara;
- Tukija kwenye Centralized & Politicized Societies: Hizi zilikuwa chini ya himaya ya machifu (e.g Mkwana). Key characteristics za jamii hizi that differentiates na zile decentralized ni kwamba - the chiefs had absolute power; and there was no separation of powers- machifu na washauri wao controlled mfumo wote wa utawala as they carried both the Executive, Judiciary and Legislative duties.
Kumbuka,
mpaka hapa hakuna Mkoloni, TAA, TANU wala Nyerere, na jamii hizi zilipiga hatua kubwa sana kimaendeleo. Jamii hizi zilikuwa na uwezo mkubwa kujiendesha kisiasa na kiuchumi, na uwezo huu ulitokana na ukusanyaji wa kodi na tributes mbali mbali hasa kupitia trade control; pia ziliweza kulinda mipaka isivamiwe na maadui. Jamii hizi zilikuwa na ndoto na malengo ya kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujitosheleza kwa chakula), kujitosheleza kifedha (kiuchumi) ili kuendesha shughuli za utawala, na muhimu zaidi, kudumisha uhuru wake kwa kulinda mipaka yake yake. Muhimu hapa ni kwamba Jamii hizi:
- Zilifanikiwa kukuza sana sekta ya uzalishaji wa Kilimo;
- Zilifanikiwa sana kuendeleza tekinolojia ya chuma/new metals technologies;
- Vile vile zilifanikiwa sana kukuza sekta ya biashara (trade expansion);
Mkoloni alipoingia Tanganyika, lengo lake kubwa ilikuwa ni kuvuruga mfumo na mafanikio yote haya, hasa uwezo wa kiuchumi uliotokana na efficient revenue system, nguvu za kijeshi, uhuru wa jamii kujiamulia sera kisiasa, kiuchumi, kijamii n.k; Mkoloni alifanikiwa kufanya haya kwa kuwarubuni machifu kadhaa, pia kupitia sera ya ‘divide and rule', na mara nyingine ‘military coercion'.
Kwa kifupi, mkoloni alifanikiwa kuzima ndoto za Watanganyika na badala yake, akaleta muundo mpya kabisa wa mahusiano katika uzalishaji (uchumi), mahusiano katika utawala, huku pia akivuruga utamaduni wa mwafrika and install utamaduni na mfumo wake ambao ulilenga to serve interest za serikali ya kikoloni na pia za mataifa mama.
Mkoloni akaanzisha a new government, New Political Practices and New Political Institutions ambazo zilikuwa ni ngeni kabisa (so alien) kwa jamii ya watanganyika;
Nahimiza kwamba hadi hapa hapakuwepo TAA, TANU wala Nyerere bali jamii iliyorundikwa kwa pamoja bila ya ridhaa yao, ikapewa jina la
"Tanganyika", kisha kuanza kutawaliwa katika kila nyanja bila ya hiyari yao;
TANU na Harakati za Uhuru
Tujitahidi kutazama harakati za uhuru kwa kina zaidi kuliko ndani ya mazingira ya TANU. Harakati kama za
Kinjeketile (Maji Maji) na
Mkwawa dhidi ya mjerumani zililenga kuondokana na utawala wa kikoloni ambao ulivuruga taratibu za maisha ya watanganyika, huku ikizidi kupoteza uhuru wao wa kisiasa na kiuchumi.
Kumbuka tena, hapa hapakuwa na TAA, TANU wala Nyerere. Pia niseme kwamba kidogo umenishangaza unapo downplay harakati za Nyerere kwamba ‘it was an easy walk to freedom' huku ukisahau kwamba kwa ujumla wake, Tanganyika na Kenya kwa mfano, hazipishani sana when it comes to umwagaji wa damu wakati wa mapambano dhidi ya ukoloni; tofauti kubwa iliyopo baina ya harakati za Kenya ni only in contextual terms (especially dates), lakini content wise, hatuna tofauti kubwa sana;
Bottom line mkuu Nicholas ni kwamba, aspirations za watanganyika zilikuwepo kwa muda mrefu sana, hata kabla ya ujio wa TANU na Nyerere, na ushahidi ndio huu wa Kinjeketile na Mkwawa. Kilichotokea ni kwamba TANU ilikuja kuongezea nguvu vuguvugu hili na ikafanikiwa kuwaletea watanganyika uhuru wa kisiasa (somewhat) na kuahidi kuwaletea uhuru wa kiuchumi.
TANU ndani ya Tanganyika huru ilikuwa na majukumu mawili:
a) To restore/reconstruct Tanganyika.
b) To Develop Tanganyika.
Tumeona katika historia jinsi gani Europe was reconstructed baada ya vita vikuu vya pili vya dunia. In actual fact, walijiundia chombo special kwa kazi hiyo – IBRD (International Bank for Reconstruction and Development), ambayo baada ya kufanikiwa, IBRD ikapewa jina jipya – the World Bank kwa lengo la kufanya shughuli ya reconstruction and development in the third woorld (former colonies) kama ilivyofanya kazi Europe. Lakini ili Tanganyika na mataifa mengine huru yafanikiwe to reconstruct and develop, ilikuwa ni lazima wajengewe mazingira kama yale ya Europe chini ya IBRD, lakini haikuwa hivyo, na badala yake, mfumo ule ule wa kikandamizaji ukaendelezwa, na ndio maana Nyerere ajijaribu to delink jamii yetu na mfumo huu wa kidhalimu, hence Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea ili tuweze kuanzia pale mkoloni alipokuja na kutuvuruga, na hii ndio moja ya sababu kubwa kwanini Ujamaa uliungwa mkono nna wengi. Logic ya Ujamaa was a simple as that! Tatizo likaja pale Nyerere aliposhindwa na mradi huu wa delinking, na badala yake kupelekea wananchi kuzidi kuumia;
Mfumo wa kibepari ulishaotesha mizizi mirefu sana, kwahiyo isingekuwa rahisi wa Nyerere kufanikiwa. Na sio kwa Tanzania tu, kwani hakuna nchi yoyote Africa iliyofanikiwa katika hili. Kilichofanya wenzetu kwa mfano wa Kenya au Zimbabwe watuzidi ni kwamba Kenya kwa mfano - mkoloni alitumia muda na rasilimali nyingi kujenga a an indigenous bourgeoisie class (hasa wakikuyu) ili wafanane nae in terms of kumiliki ardhi n.k kwasababu mkoloni alilenga kuishi Kenya moja kwa moja, na kwamba at independence, pasiwe na much ‘class struggle'; kwa bahati nzuri au mbaya (depending unaangalia kwa jicho gani), mkoloni hakufanya hivyo Tanganyika kwani hakuwa na nia ya kuishi (we were not a settler economy), ndio maana hakuwaendeleza watanzania kwa namna yoyote ya maana, badala yake aliwaacha as proletariats (wengi as manual laborers) na pia wakulima wadogo wadogo kama alivyowakuta.
Pia ni muhimu tusijisahau na kuanza kuijadili TANU kama vile Nyerere alipokea nchi (1961) ikiwa na:
· Uwezo wa kujiendesha (political capacity) na pia uwezo wa kuboresha maisha ya watanganyika kwa urahisi;
· Kama vile Nyerere alipokea nchi iliyokuwa inaheshimu human rights and democracy practices wakati wa ukoloni;
· Na pia kama vile watanganyika walikuwa ni homogenous society wakati ukweli ni kwamba ilikuwa na makabila mengi huku baadhi yao mkoloni tayari akiwa ameshayavuruga kiuchumi, kisiasa na kijamii kwa kutumia makabila mengine, huku baadhi ya makabila (na dini) yakiwa yame neemekana kuliko mengine - kiuchumi, kisiasa na kijamii.
Tutazame kidogo masuala ya political capacity na human rights.
1.
Political/State Capacity Chini ya TANU: Huu ni uwezo wa serikali kufanya shughuli zake kama to guarantee protection and security kwa wananchi, guarantee haki za binadamu; kuwekeza kwenye miundo mbinu inayohitajika kwa ajili ya shughuli za kiuchumi, to encourage uwekezaji ambao utazaa ajira, kama njia ya kukuza uchumi; kutoa huduma za kijamii kwa wananchi wote – elimu, afya, nyumba, maji safi n.k.
Ili kufanikisha haya, Serikali lazima iwe na vitu kama:
a)
Taasisi (institutions) - zinazojihusisha na kila sekta tajwa hapo juu, mfano shule (kutoa elimu), hospitali (kutoa huduma za afya), polisi na jeshi (kwa ajili ya ulinzi na usalama wa raia na mali zao); Pia ni lazima taasisi hizi ziwe na ufanisi wa hali ya juu. Lakini muhimu pia ni:
b)
Bureaucrats – wenye ujuzi, ari na moyo wa kutumikia nchi yao; kila taasisi inahitaji watumishi wenye uelewa na ujuzi katika maeneo husika, vinginevyo malengo ya serikali hayawezi timia; lakini kumbuka pia kwamba - ili upate watumishi wa namna hii, ni lazima taasisi za afya na elimu ziwe katika ubora wa hali ya juu vinginevyo ili kuzalisha Human Capital ya maana, vinginevyo mambo hayataenda. Lakini pamoja na umuhimu wa taasisi na human capital, pia kuna suala la:
c)
Mapato (Revenue) – bila ya mapato, taasisi na human capital zitakuwa useless unless kuna mapato ya kujenga na ku maintain taasisi hizi, kulipa mishahara mizuri n.k ili huduma bora zitolewe kwa wananchi;
Sasa tofauti na haya, Nyerere hakupokea nchi ikiwa na haya yote in place kwani taasisi, bureaucracy na revenue structure aliyokuta Mwalimu, mkoloni hakuiunda kwa ajili ya kutoa huduma kwa watanganyika milioni tisa on indendepence eve; Sote tunaelewa fika kwamba mkoloni hakufanya lolote la maana kuendeleza wananchi walio wengi kielimu na kiafya; vile vile, mkoloni hakutumia mapato kutoka kwenye kilimo na kodi kuendeleza to diversify uchumi, au to develop miundombinu kwa lengo la kuinua maisha ya walio wengi; Alichorithi Nyerere na TANU ni muundo uliokusudiwa kunufaisha serikali ya kikoloni na mataifa yao makubwa; given haya yote, haina ulazima wa mtu leo hii kujikuna sana kichwa kwa masikitiko kwamba Nyerere's idea to delink us from mfumo wa usiotendea haki wazalishaji wetu, hence sera ya UJAMAA na KUJITEGEMA, was a bad idea. When it comes to Ujamaa, tukijitahidi kutofautisha Malengo, Mchakato, Utekelezaji na Matokeo ya Ujamaa nadhani itakuwa ni hatua muhimu sana katika kuelewa changamoto zetu kama taifa (sio kama wana CCM, Chadema n.k). Tanzania kwanza, siasa baadae!
2. Human rights Chini ya TANU:
Wengi wetu tumekuwa na tabia za kum criticize Nyerere na TANU kama vile mkoloni alimwachia nchi iliyokuwa inaheshimu haki za watanganyika. Je, Nyerere alirithi taifa linalojali rights and freedoms for all individuals - without distinction of any kind, such as race, color, sex, language, religion, political or national/social origin? What about right to life, liberty and security of the people? Jibu ni
HAPANA! Haya yote hayakuwahi kuwepo kabla ya mkoloni na hata baada ya mkoloni kuja. Sasa in the midst ya colonial legacy na madhara yake kwa jamii yetu, ili kusonga mbele ilibidi TANU na Nyerere to compromise mengi. Tutazame baadhi:
a) Political rights- Rights of individuals to participate in their own government and provide protection against abuse and oppression by governments.
[Je. Nyerere alikuta such rights? NO]
b) Freedom of thought and religion – the notion that everyone has the right to freedom of thought, conscience and religion; hii ni pamoja na freedom to worship/practice religion…
[Je. Nyerere alikuta such rights? NO]
c) Economic rights - These include the right to own property, right to employment, rights to an adequate standard of living…
[Je. Nyerere alikuta such rights? NO]
d) Social/Distributive Rights - Includes rights to adequate health care for all, a safe and healthy childhood, adequate housing
[Je. Nyerere alikuta such rights? NO]
e) Cultural Rights - hali ya kila mtu kuwa na right to freely participate in the cultural life of the community, to enjoy the scientific advancement za jamii n.k
[Je. Nyerere alikuta such rights? NO]
Ni kweli Ujamaa ulifeli, lakini in the midst of all this, ningependa kusikia toka kwako je: Nyerere angefanya nini/ au better said – Je kwa mfano Chadema ndiyo ingekuwa Chama mbadala wa TANU, wangeweza kufanya nini? Nadhani majibu yako yatatusaidia kuboresha mjadala wetu juu ya similarities between TANU na Chadema – kwa maana ya changamoto zilizokuwepo waakti ule na zile zilizopo katika mazingira ya sasa. Iwapo utajikita katika kuuponda Ujamaa, jaribu kuujadili in the context of
Malengo, Mchakato, Utekelezaji na Matokeo wa Sera hii.
Naamini hii itatusaidia sana kuzidi kusaidiana mawazo kuhusu changamoto za Chadema 2015, hasa tukiweka watanzania wa vijijini at the centre badala ya the periphery kama wengi wanavyofanya katika mjadala wa kuelekeo 2015.