Sangarara,
Nashukuru sana kwa mchango wako uliojaa mawazo mazuri sana; Lakini kabla sijaenda mbali, naomba niseme kwamba huu ni mtazamo wangu tu, hivyo nategemea mgongano mkubwa sana wa mawazo, lakini ninacho thamini zaidi ni kwamba mwisho wa siku, sote tunajifunza mengi toka kwa kila mmoja wetu, hivyo kuibuka waelewa zaidi; Nitajibu post zako mbili (post number 98 na number 99 kwa pamoja kama ifuatavyo:
Nianze na suala la wapiga kura wa mijini vi-a-vis wa vijijini; Kimsingi nakubaliana na wewe ila ningependa kuongeza tu kwamba – ni muhimu kwa Chadema kuanza kufanya an examination juu ya nani ni mpiga kura mijini na vijijini in terms of income, occupation, kiwango cha elimu, jinsia n.k, na kubaini factors zinapelekea wananchi wawe na tabia zinazotofautiana kwenye upigaji kura, hasa kwanini wapo wananchi wenye mazoea ya kupiga kura na kwani wengine hawana mazoea hayo, kote mijini na vijijini; Pengine nifafanue zaidi ni nizidi kueleweka juu ya hili: Kwa mfano, Chadema kama chama cha siasa,
JE ni AGENT of mobilization au representation? Kwa mtazamo wangu, M4C inaegemea zaidi on Mobilization na kwa kiasi kikubwa ignores Representation; Ndio maana ukitazama umati wa M4C, wengi ni wanaume, wakati uhalisia wa mambo ni kwamba watanzania wengi (up to 54% of the population ni Wanawake), lakini muhimu zaidi, wapiga kura wengi (karibia 60%) ni wanawake;
Tukiwa bado kwenye suala la wapiga kura wa mijini versus vijijini, kumekuwa na trend katika chaguzi karibia zote barani Afrika kwa watu wa mijini kupigia kura zaidi vyama vya upinzani huku wale wa vijijini wakipigia kura zaidi vyama tawala; kwa kiasi kikubwa katika hoja zako umejaribu kulizungumzia hili, hasa katika jitihaha zako za kujaribu kubaini juu ya motivations za wapiga kura vijijini vis-à-vis mijini ni zipi; kwa mfano, umezungumzia suala la Ujamaa, illiteracy n.k, hoja ambazo binafsi pia nazikubali; Lakini tujiulize,
JE: Wananchi wa mijini wanachagua vyama vya upinzani kwa sababu gani nje ya conventional factors tunazoelezwa: JE, is it because they feel the pinch of injustices kiuchumi, kisiasa na kijamii kwa kiwango tofauti na wenzao wa vijijini? Kwa maana nyingine, je, madhara ya soko huria na ubepari kwa wananchi/wapiga kura wa vijijini ni madogo kuliko kwa wenzao wa mijini? Hii itasaida sana kuzidi kutupatia uelewa juu ya relevance ya Ujamaa vijijini versus mijini;
Kwa mtazamo wangu ambapo pengine ni finyu, nadhani utofauti huu baina ya jamii za mijini na vijini unachangiwa sana ukweli kwamba - Wananchi wengi wa vijijini wana ufahamu mdogo sana kuhusu their civic duties (wajibu wao kama raia) na pia ufahamu mdogo sana juu ya state duties (wajibu wa serikali kwa wananchi), tofauti na wenzao wa mijini; Kwa mfano, among the most important civic duties ni katika any democracy ni pamoja na: VOTING & PAYING TAXES;
- VOTING
Huu ni wajibu mkubwa sana kwa mwananchi kwani wajibu huu unampa mwananchi fursa/ unamsaidia mwananchi kufanya maamuzi muhimu kuhusu mwenendo wa uongozi husika katika kumwendeleza yeye kiuchumi na kijamii; Ndio maana ni muhimu sana kwa wananchi wa vijijini kuanza kuwa na uelewa/kutofautisha kupigia kura MTU vis-à-vis MASUALA;
2.PAYING TAXES
Kulipa Kodi ni wajibu mwingine muhimu wa mwananchi; Pia Kodi ndio kiunganishi kikuu baina ya wajibu wa serikali na wajibu wa raia; ni katika uhusiano huu, suala la LEGITIMACY & CREDIBILITY ya serikali ndio hujitokeza kwani – credibility na legitimacy inatokana na jinsi gani serikali ipo accountable na kodi za wananchi wake; lakini tatizo lililopo Tanzania, hasa katika uhusiano baina na serikali na wanavijiji ni kwamba serikali kuu haiwajibiki moja kwa moja kwa wananchi kupitia kodi, na pia wananchi hawawajibiki moja kwa moja kwa serikali kuu kupitia kodi, na ni hapo ndipo mianya inayodumaza demokrasia hujitokeza;
Pengine nifafanue zaidi kidogo: Kodi represents mkataba baina ya serikali na wananchi ambapo wananchi hutegemea kuona faida ya kodi zao kwa serikali kupitia kwa mfano ongezeko au uboreshwaji wa huduma za kijamii, ongezeko au uboreshwaji wa miundo mbinu n.k, na haya yakitokea, ndio legitimacy na credibility inazidi kujengeka kwa serikali husika; Lakini huko vijijini kwetu Tanzania, contract ya namna hii haipo that straight forward; Ni katika mkanganyiko huu unakuta mara nyingi wananchi vijijini wanashindwa kufanya maamuzi ya maana during their civic duties, na mara nyingi huishia kupigia kura aidha MTU badala ya MASUALA anayosimamia au kupigia kura AHADI badala ya kuchambua practicalities za hizo ahadi. Suala la ahadi umelijadili na kimsingi tupo pamoja. Mwalimu Nyerere katika uchaguzi mkuu wa 1970 alipata kunena yafuatayo:
"I hope that both candidates in each election will be intelligent enough to recognize that not everything can be done at once, and that nothing in this world is FREE. For the fact is that if a person is urging more communal services or better communal services, he or she is probably also urging that you, as the voter, should be willing to pay more local rates or more taxes. For is they are promising lots of new activities if they are elected, and if they are promising that these will be done without any cost to you, or effort on your part, they are either deliberately misleading you – thinking you are fools or they themselves are fools."
Ni muhimu kwa Chadema kutumia Masomo kama haya Mwalimu aliyotuachia;
Hoja yako Juu ya mtazamo wangu juu ya ‘Consistency & Coherency' of Opposition Strategies
Kimsingi nakubaliana na hoja zako juu ya hili, hasa kuhusu umuhimu wa kutofautisha kauli na misimamo ya kiongozi vis-à-vis CHAMA, lakini pia umuhimu wa kutoa uhuru wa mawazo miongoni mwa viongozi; Nadhani hivyo ndivyo ulimaanisha, vinginevyo kama nimekosea naomba unisahihishe; Kama nipo sahihi, kimsingi tupo pamoja, ila niseme tu kwamba hoja yangu ililenga zaidi juu ya aina ya mikakati ya upinzani inayotumiwa na Chadema na kutafsiriwa na UMMA, hasa pale UMMA unapo consider matamshi na misimamo ya individual leaders kama ndio ya misimamo rasmi ya Chama;
Kama tunavyoelewa, moja ya kazi za chama cha upinzani ni kuja na mtazamo au msimamo tofauti na Serikali iliyopo madarakani, na ni muhimu mtazamo huo mbadala ukaonekana kuwa ni superior kuliko ule wa serikali mbele ya UMMA, mfano taxation policies, employment policies, etc; Ndio maana ili kufanikiwa in a consistent way, mara nyingi huwa ni muhimu sana kwa chama kuwa na mitazamo inayokingwa na itikadi fulani badala ya kuwa na misimamo au mitazamo ambayo haina a ‘strong base'; Chadema kwa bahati mbaya sana haina itikadi yenye mizizi mirefu kwa wananchi walio wengi (hasa vijijini), na badala yake kimekuwa ni chama kinachoendeshwa zaidi kwa personalities za viongozi wake; kwa bahati mbaya, CCM nayo pia imeanza mchezo huu;
Hii ni kutokana na ukweli kwamba Vyama vyote viwili vinakabiliwa na ombwe la Itikadi.
Mwisho naomba nimalizie na suala la UFISADI na kwanini nasema hili ni suala la msimu.
Kwanza, naomba niseme kwamba mimi sikatai kwamba ufisadi unatugharimu kimaendeleo kama taifa; na nimependa sana ulipoliweka tatizo hili on PAR na maadui wengine wa Maendeleo kama vile umaskini, ujinga na maradhi; Ninaposema kwamba Ufisadi ni suala la msimu, maana yangu kuu ni kwamba – ni Kweli RUSHWA ni ADUI WA HAKI, lakini HAKI ina maadui wengi zaidi ya RUSHWA; kama tunakubaliana juu ya hili,
JE, Rushwa ikipata ufumbuzi, suala la HAKI litakuwa limetatuliwa? Jibu ni Hapana; ndio maana huwa nahimiza juu ya umuhimu wa Chadema kuja na programu pana zaidi ya kujiandaa na uchaguzi mkuu wa 2015 ambayo itafanya Rushwa kuwa sehemu muhimu ya programu hiyo lakini huku ikikwepa kufanya UFISADI kuwa kete kubwa kuliko zote as a way ya kujitofautisha na CCM mbele ya wapiga kura; hii itawagharimu chadema, hasa ikizingatiwa kwamba Ufisadi hauna mashiko yoyote ya kiitikadi Kwahiyo chama chochote (including CCM) kinaweza kudandia hoja hiyo nap engine kuitumia kikamilifu kuliko Chadema 2015;
The bottom line hapa ni kwamba: Kwa miaka nenda, miaka rudi, majority of Tanzanians wamekuwa wanaishi kwa kuteseka sana kutokana na ukosefu wa HAKI kiuchumi, kisiasa na kijamii (political economic and social injustice), hivyo ni muhimu kwa Chadema inapoelekea 2015, ‘to approach' suala la HAKI in a more HOLISTIC WAY, kwani kama tunakubaliana kwamba HAKI ni the common denominator ya matatizo mengi kama sio yote ya Watanzania walio wengi, then ni muhimu tukakubaliana pia kwamba
UFISADI is just an atom in the WHOLE;