You might have a valid point. Lakini naomba nikuulize: Je kwanini imechukua miaka 15 (1995-2010) kwa chadema kuwa na nguvu kwenye umma, kiasi cha kupelekea kuaminiwa kwamba Chama kipo tayari kuchukua madaraka ya nchi 2015? Je, kuna strategy maalum ambayo Chadema walikuwa wanaitumia consistently? Kwani hoja yako inaashiria kwamba kuna mkakati maalum ambao Chadema waliuweka miaka 15 iliyopita na ndio umezaa matunda leo. Ningependa kujua hili kwani binafsi sina taarifa yoyote na badala yake nadhani mafanikio ya Chadema yametokana na Chama kufanikiwa ku link umaskini wa wananchi na ufisadi, wakati ukweli wa mambo ni kwamba ufisadi explains only a fraction of the story – kwanini watanzania maskini. The bigger story ni sera zinazoshinikizwa na mataifa matajiri, sera ambazo hata chadema wataenda kuzitekeleza Ikulu kama CCM inavyofanya sasa. In short, we talk of development but we do not own our development agenda!
Unachoshindwa kuelewa hapa ni kwamba TANU ilitoa ahadi ya kuwakomboa watanganyika kisiasa na kiuchumi, ilifanikiwa kisiasa lakini imeshindwa kuwakomboa kiuchumi.
Watanzania wanahitaji the second independence kwani the first one chini ya TANU haikukamilika. Ni bahati mbaya tu CCM ya sasa inahusishwa na TANU lakini ukweli ni kwamba hizi ni taasisi mbili tofauti kabisa, kwa mfano, TANU haikumkomboa mzanzibari. Mtu anaetatizwa na Chadema kufananishwa na TANU basi sio muelewa wa matatizo ya watanzania.
Pengine itasaidia iwapo tutaita chama kilichoikomboa tanzania kwa jina lingine lisilohusiana na CCM ndipo itaeleweka vizuri kwanini changamoto za TANU na Chadema ni zile zile.
Unachoshindwa kuelewa hapa ni kwamba TANU ilitoa ahadi ya kuwakomboa watanganyika kisiasa na kiuchumi, ilifanikiwa kisiasa lakini imeshindwa kuwakomboa kiuchumi. Watanzania wanahitaji the second independence kwani the first one chini ya TANU haikukamilika.
Ni bahati mbaya tu CCM ya sasa inahusishwa na TANU lakini ukweli ni kwamba hizi ni taasisi mbili tofauti kabisa, kwa mfano, TANU haikumkomboa mzanzibari. Mtu anaetatizwa na Chadema kufananishwa na TANU basi sio muelewa wa matatizo ya watanzania.
Pengine itasaidia iwapo tutaita chama kilichoikomboa tanzania kwa jina lingine lisilohusiana na CCM ndipo itaeleweka vizuri kwanini changamoto za TANU na Chadema ni zile zile.
Well said Mchambuzi.
Hata hivyo, kumbuka kuwa itafikia mahali, of all the situations ulizosema may not apply kwa watu kuchoka....hapa ndipo changes hutokea regardless ya nini!refre, mapinduzi ya Ufaransa, kuondolewa wakoloni Afrika..na hivi sasa yaliyotokea Misri, Libya, Syria na kwingineko.
Lakini pia hujaangalia CCM wanavyoandaa anguko lao kwa mambo ambayo wengi wanayasahau kuyaona: shule za kata (uwingi wa wasomi hata kama wanapata zero, lakini ni chachu ya mabadiliko), mitaala ya elimu, matatizo makubwa ya wafanyakazi katika kila nyanja..na hata hayo maisha magumu uliyoyasema!
Hii quote ndio msingi wa mada yangu. Ningependa nieleweke kwamba naposema "utayari wa chadema", haina maana kwamba najaribu kujenga hoja kwamba chadema haipo tayari.Kwa utaratibu wa mabadiriko unavyoendelea sina uhakika wa lengo la mada yako kwamba haitafuti mikakati ya CDM. Ila mimi binafsi nawaamini CDM kwa mikakati yao kwa lengo langu moja tu NIMECHOSHWA NA CCM NAHITAJI MABADIRIKO
Naona kama hizo dhana mbili zinapingana, mwanzo umesema kuwa Chadema inaweza kuongoza kwa ridhaa tu bila pesa baadae umesema Chadema kimefika kilipofika kutokana na viongozi kadhaa kuwa na uwezo wa mkubwa wa kifedha.
Mchambuzi, umeleta sredi ambayo kama Watanzania tungekua watu wa kujadili hoja za manufaa kwa taifa letu,ingepata wachangiaji wengi.
Kama kuna kipindi viongozi wa chama changu CDM wanapaswa kujadili mambo ya msingi nchi yetu itaongozwa vipi baada ya 2015 ni sasa! Hizi stori za watu kutafuta urais,binafsi zinakwaza sana. Siyo wakati wake sasa, tujenge chama! Kikichukua dola kionyeshe tofauti.
Mchambuzi nakubaliana na wewe..lkn ninaushauri wa ziada CDM kabla ya kuwaza kutawala lazima wawatolee uvivu mapandikizi kwao..maana bila kuwatolea uvivu hawawezi shika dola.
Nawashauri watafute kura 100 za wanachama CDM JF za kuwashinikiza viongozi wao Mbowe na Slaa wahudhurie mdahalo humu kisha watoe onyo kali kwa wale wote wanaosaliti chama kwa kuacha kukijenga chama na kujijenga wao.
Hii itawasaidia viongozi wao pia kuwatoa nduli wanaoharibu chama chao ambacho wananchi tunaamini wanania ya dhati kuleta maendeleo. Mie sio CDM lkn nachukia sn vijana iwe wa CCM au CDM sijui NCCR ambaye anacheza siasa za mbimnu ya kuwanyonya wananchi nachukia sn.
CDM mdharau mwiba????.........................
Mchambuzi ukiniuliza na mawazo gani kuhusu kesho ya Nchi yangu, naweza kukujibu hivi:
Nafuu hata Paka awe raisi lakini siyo kiongozi yoyote toka CCM sababu CCM wote hawana uwezo wa kusema Hapana.Hakuna Rais wetu dhaifu wala msaidizi wake hakuna, wote walio CCM wanasubiri ni namna gani apate uongozi ili afilisi zaidi.
Ile dhana ya vyama vya upinzani vitaleta vita imepitwa na wakati, iangalie Zambia, Malawi mbona vinavyotawala leo ni vilivyokuwa vyama vya upinzani?
Watanzania tuondoe woga,tuone uchungu na Maliasili zetu tubadilishe mtawala ili hata anayekuja awe mwoga ajue kesho yake ipo kwenye hatihati.
lakini Dr.slaa hakuyasema hayo kwa bahati mbaya, wanajua udhaifu wa chama cha magamba kuwa kadri unavyowakosoa ndivyo wanavyozidisha makosa ujue jinsi walivyozeheka, hiyo inasaidia kuwajulisha wananchi kuwa magamba wanatupeleka ndiko siko, hivi wasipowakosoa watakuwa wanafanya siasa gani?
CDM hawahitaji kuzama sana katika itikadi za TANU.VIjana hawaijui TANU, na TAnu haikuwa perfect kihivyo.Ila kuna vifaida vidogo vidogo na kujihusisha nayo , pamoja na vitu fulani ambavyo ni universal vilivyokuwepo katika TANU.
Kukimbilia sana TANU ni kuwapa CCM comfort zone.Kwani watapunguza nguvu kwa kusema kuwa ni ya TANU, halfu warudi sema kuna ni ya CCM kwa vile ilizaliwa katika TANU.Sasa inabidi pawe na New creations.Ili CDM waseme kuwa wana nia na mshikamano kama TANU ila wanafanya Mambo makubwa kuliko TANU.
Hii ndio sababu ya mimi kusema itachukua miaka mingi sana ccm kuangushwa, CDM bado kuwa chama mbadala,wanasafari ndefu. Hawajajipanga kikamilifu, wanapata nguvu kutokana na uzembe wa ccm lakini ki sera bado wako nyuma sana. Wametoka kwenye chama cha msimu na wamerudi kwenye sera za msimu.utawasikia wakati ccm imekosea jambo. Je ccm wakijipanga vizuri CDM watajadili nini?
Ufisadi ni janga kwa uchumi wetu kwani umedumu tangu enzi za Sokoine. CHADEMA muhimu walivalie njuga. Ufisadi is highy linked to developed nations (mikataba mibovu, forced policies in monetary, employment, health, etc). Angalia fujo kutoka kwa wananchi (grassroot) katika maeneo ya uwekezaji hasa migodi ya dhahabu!
Ni dhahiri wananchi wamechoka. If corruption is used as a weapon by CHADEMA and is understood and appreciated then it is perhaps a leeway towards developing a realistic national agenda. In any case the ruling party CCM if truly wishes Tanzania well, should have shown genuine cooperation with the opposition to make the dream Tanzania they have failed to provide instead of cursing and childish propaganda towards the opposition which is a waste of precious time.