CHADEMA tumewapigania sana, hakuna mnalotudai bali mna deni kubwa kwetu

CHADEMA tumewapigania sana, hakuna mnalotudai bali mna deni kubwa kwetu

Kindus

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2014
Posts
3,384
Reaction score
2,073
Wakuu hiki Chama mi kimenitia majeraha makubwa hakika. Nakumbuka miaka nane ilopita tukiwa na mama yangu kijijini tukisikiliza radio five ghafla ikatangazwa break news mtangazaji Alli Shemdoe akatangaza kupigwa kwa bomu kwenye mkutano wa CHADEMA wa NMC moja kati ya majeruhi alikuwepo Abdi Madava Kaka yangu kipenzi alotegemewa mno na mama.

Kuanzia hapo mama yangu alipatwa na heart attack iliosababisha kifo chake mwaka 2013 walichofanya CHADEMA ni kuwatelekeza majeruhi swala la kumtibu kaka yangu tuliachiwa sisi familia hakuna Mbowe wala Lema alotusaidia.

Mimi nadiriki kusema CHADEMA mlisababisha kifo cha mama yangu ingawa bado naichukia sana CCM ila CHADEMA bado si chama sahihi kwa ukombozi wa Tanzania.
 
Apumzike kwa amani.

humtendei haki kaka yako,maana yy alikuwa na maamuzi ya kuamini anachoamin

swala LA Mbowe kutokuja kukuona,Fanya kusamehe..

...maana kwa dhoruba za awamu5, mara wabunge kutimka na jambajamba nyingine wanazopitia itakuwa wanalipia kosa la kumtelekeza bro wako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
pole sana mkuu, in short vyama vyote vya siasa vipo pale kusaidia watu na sio kusaidiwa, wewe zaidi ya kupiga kura utakuwa umefanya ziada.., kwahio in short upo right CCM kutokuleta maendeleo inawaangusha wananchi na Chadema kutokufanikiwa kile ambacho ilipanga ikifanye bado ina deni vilevile..
 
CHADEMA ndio waliokupiga bomu? Wakati huyo ndugu yako anaenda kwenye mkutano wa siasa hakuna yoyote aliyemlazimisha, na matangazo yalikuwa ni mkutano wa siasa, na hakuna popote cdm waliposema watatoa mafunzo ya matumizi ya mabomu. Serikali ndio ilipaswa kukupa majibu ya hilo bomu na sio CHADEMA.

Isitoshe CHADEMA sio taasisi ya kutoa huduma ya matibabu, kiasi useme kwamba ukipata matatizo yaliyo nje ya wajibu wa cdm basi wawajibike. Huwa tunaona watu wakipata ajali kwenye vyombo vya moto wengine kuwa vilema na hata kupoteza maisha, mbona hatuoni wamiliki wa hivyo vyombo wakiwatibu wahanga wa hizo ajali?

Unajifunza kuichafua taasisi kwa mbinu za kizee ile mbaya.
 
Huo ndio ujinga wa siasa unapata kilema cha maisha kama sio kupoteza maisha kwa kumpigania mwanasiasa apate kujaza tumbo lake na familia yake

Ukipata ajali kwenye chombo cha usafiri wakati unapigania mmiliki alishe familia yake, huwa anakutibu? Msitake kupotosha maana wakati ukweli tunaujua.
 
Kwa mujibu wa maelezo yake ana chuki dhidi ya chama ambayo chanzo chake hata yeye hakijui. Ila tumpe pole tu inamtosha wakuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli ana chuki kwa sababu kaka yake alikua msukule wa chadema yaani mwanachama wa chadema kajeruhiwa kwenye mkutano wa ufipa hajasaidiwa na ufipa kwenye matibabu
 
Huo ndio ujinga wa siasa unapata kilema cha maisha kama sio kupoteza maisha kwa kumpigania mwanasiasa apate kujaza tumbo lake na familia yake
Nishasema huu ujinga stakaa niufanye maisha yangu yte! Mambo ya kuitwa makamanda na kuvalishwa t-shirt bila bima wala salary slip! Mda huo wake na watoto wao wanakula bata ugaibuni! Huu niujinga wa FUSO.
 
Huo ndio ujinga wa siasa unapata kilema cha maisha kama sio kupoteza maisha kwa kumpigania mwanasiasa apate kujaza tumbo lake na familia yake

..kumuua mtanzania mwenzako au kumtia kilema kwa kuitumikia au kutumwa na ccm ni ujinga, unyang'au, na unyama.
 
Hijja Madava,
Loo, haya nayo ni makubwa!

Unadai. Sasa wafanyeje?

Waitishe michango ya wananchi ili ulipwe deni?

Wakisema wewe umetumwa na mahasimu wao wakuu, CCM utadai si kweli?

Kwa hiyo ujumbe huu ulioweka hapa, unataka wahanga woooote, waliowahi kupata majanga ambayo hata hayakusababishwa na CHADEMA, wakadai madeni yao kwa chama? Akili hii kama sio matope ni kitu gani?

Na hao waliopo huko ndani ya CHADEMA, kama akina Mbowe na wenzao na majanga yanawapata, na wao wakadai wapi?

Wazazi wa Akwilina, Ben Saanane, wakadai CHADEMA?

Hii CCM yako hii itakufikisha wapi kama hali ndiyo iko hivi! Mwisho hata Ngoyai na Sumaye wakadai CHADEMA, kwa mda waliopoteza wakiwa huko!

Mada za ajabu hizi, nazo zinahitaji kujadiliwa JF!

Mbona sasa ni kama wafamaji..., wanawaangukia hata wasiojua mbinu za kushambulia chama.

Ngoja nikuulize swali: wewe na 'Masanjaone' hapo juu #21; kazi yenu ni moja?
 
Back
Top Bottom