CHADEMA: Tuna dhamira ya kushika dola 2025

Tatiz
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika amesema chama hicho kitahakikisha kinaimarisha majimbo yote ya Tanzania na Zanzibar ili kufikia dhamira ya kuiondoa CCM madarakani katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

“Tuna dhamira ya kushika dola mwaka 2025, kutokana na dhamira hii kuu, hatuwezi kuliacha jimbo lolote nyuma lazima yote tusonge kwa nguvu kamili. Ujumbe huu sio kwa Geita au kanda ya Victoria bali kanda zote 10 za Tanzania na Zanzibar,” amesema Mnyika.

Mnyika ambaye ni mbunge wa zamani wa majimbo ya Ubungo na Kibamba mkoani Dar es Salaam, ameeleza hayo jana Jumanne Desemba 27, 2022 wakati akihutubia katika mkutano mkuu wa jimbo la Geita Vijijini mkoani Geita.

Katibu mkuu huyo, kwa nyakati tofauti amekuwa akifanya ziara katika majimbo mbalimbali yaliyopo katika kanda 10 za chama hicho, ameshafanya vikao na makongamano na wanachama wa Chadema katika mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara na Dar es Salaam.

Amedai Chadema ndiyo chama cha tumaini kuu la Watanzania, akisema kama kunahitijaka mabadiliko ya uongozi, demokrasia na maendeleo, uhuru, haki za watu lazima kazi ya kujiimarisha ifanyike mahali kote ili chama hicho kiibuke kidedea na kuongoza Serikali mwaka 2025.

“Nyie wa Bukombe na Geita, kama ambavyo sisi wa kitaifa tutakavyozunguka katika majimbo na kata zote, nanyinyi mna wajibu wa kwenda kila kata, kijiji na kitongoji msiache mahali Chadema iamke ili kuwakomboa Watanzania,” amesema Mnyika.

Katika hatua nyingine, Mnyika amewataka wanachama wa chama hicho, kuutumia mwaka 2023 kudai Katiba Mpya na Tume huru ya uchaguzi, akisema ni jambo linalopaswa kuwa la Taifa.

MWANANCHI
o wapinzani wana njaa sana, tukiwapa dola itakuwa ni scramble ya kushiba!!!
 
Walamba asali kweli wamedhamiria kushika dola za kimarekani.
 
Chadema wenyewe wanaosema hivyo ndio hawa?
2826503_1625156235957.png
 
CDM hawapo serious na hawajui wanataka Nini

Ccm ni upuuzi lakini wamekosa watu makini wakuwatoa kwa kura

Ccm hawatatoka madarakani kwa kura, labda useme kingine. Machafuko tu ndio yataitoa CCM madarakani. Mnyika asipoteze muda, kwa tume ya uchaguzi na katiba hii kuitoa CCM madarakani ni kujidanganya.
 
Ajira
Siasa ni ajira kama ajira nyingine tu. Kwa wenye vyeo vya juu.

RIP. Christopher Mtikila. Mpinzani pekee aliyeonyesha nia dhabiti ya kuchukua nchi.
Wengine tupo bado kwenye vikao vya maridhiano na mshindani wetu.
 
Njia za kuitoa Ccm zipo nyingi siwezi ku-share ideas zangu lakini wakijua umuhimu wetu watatuita ili tuwaoneshe njia sahihi

Hizo mbinu za CDM zimepitwa na wakati. That sisi Great thinker tunafahamu what going on kuwa ni upuuzi mtupu unaoendelea hapo ufipa
 
Yes sure Mbowe na genge lake ni wajanja wajanja
Ajira
Siasa ni ajira kama ajira nyingine tu. Kwa wenye vyeo vya juu.

RIP. Christopher Mtikila. Mpinzani pekee aliyeonyesha nia dhabiti ya kuchukua nchi.
Wengine tupo bado kwenye vikao vya maridhiano na mshindani wetu.
 
Hawa watu hawako siliazi , kama wanamaanisha dola ya Zimbabwe wako sahii.
 
Njia za kuitoa Ccm zipo nyingi siwezi ku-share ideas zangu lakini wakijua umuhimu wetu watatuita ili tuwaoneshe njia sahihi

Hizo mbinu za CDM zimepitwa na wakati. That sisi Great thinker tunafahamu what going on kuwa ni upuuzi mtupu unaoendelea hapo ufipa

Uitwe wapi boss, nani anakufahamu kwa hii fake I'd? Hakuna ulazima wa kuwapa hizi mbinu zako hao ufipa, unaweza kuwapa hizo mbinu zako chama kingine. Au kama vipi anzisha chama utumie hizo mbinu zako kuwatoa CCM.
 
Kama mnaleta dharau Kama hivi then mnaamini katika mawazo yenu tu.

Hicho chama chakavu mtakitoa kweli??
 
Dharau za kuona mawazo yenu ni Bora na mkiwadanganya wanachi (Mbumbumbu) kuwa nyie ndo mbadala wa Ccm ni kujilisha upepo
 
Kama mnaleta dharau Kama hivi then mnaamini katika mawazo yenu tu.

Hicho chama chakavu mtakitoa kweli??

Mkuu nimekuambia weka mbinu zako umesema mpaka uitwe. Sasa sijui unataka uitwe na nani, maana hapa ni kwenye mtandao wa kijamii, sio ofisi ya CDM, au ya chama chochote cha siasa. Kama unataka kuwapa mbinu CDM waandikie kwa official email yao ili wakuite. Sasa unaposema unadharaulika, au mawazo yako yanapuuzwa sijui unamaanisha nini. Mimi sio kiongozi wa CDM useme nitakuita ofisini, bali ni shabiki wa CDM. Ndio maana nimekurahisishia, anzisha chama uchukue nchi na hizo mbinu zako.
 
Kuanzisha chama sio Jambo Rahisi , lengo sio kufukuzia Ruzuku. Tu pasipo kuwa na mbinu mbadala

Ngoja tuwe outside watcher tu nothing else

Unaona ni kazi ngumu kuanzisha chama, lakini una mbinu za kuitoa CCM! Haya basi wape hizo mbinu waliokuwa na uthubutu wa kuanzisha chama, napo unataka ubembelezwe.

Mkuu sioni kama una mbinu zozote za maana, kama ungekuwa nazo ungezitoa. Unalaumu maoni yako yanapuuzwa, yatumie mwenyewe basi nayo bado huwezi, ila unalaumu wengine hawana mbinu za kuitoa CCM. Kazi kweli kweli.
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika amesema chama hicho kitahakikisha kinaimarisha majimbo yote ya Tanzania na Zanzibar ili kufikia dhamira ya kuiondoa CCM madarakani katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

“Tuna dhamira ya kushika dola mwaka 2025, kutokana na dhamira hii kuu, hatuwezi kuliacha jimbo lolote nyuma lazima yote tusonge kwa nguvu kamili. Ujumbe huu sio kwa Geita au kanda ya Victoria bali kanda zote 10 za Tanzania na Zanzibar,” amesema Mnyika.

Mnyika ambaye ni mbunge wa zamani wa majimbo ya Ubungo na Kibamba mkoani Dar es Salaam, ameeleza hayo jana Jumanne Desemba 27, 2022 wakati akihutubia katika mkutano mkuu wa jimbo la Geita Vijijini mkoani Geita.

Katibu mkuu huyo, kwa nyakati tofauti amekuwa akifanya ziara katika majimbo mbalimbali yaliyopo katika kanda 10 za chama hicho, ameshafanya vikao na makongamano na wanachama wa Chadema katika mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara na Dar es Salaam.

Amedai Chadema ndiyo chama cha tumaini kuu la Watanzania, akisema kama kunahitijaka mabadiliko ya uongozi, demokrasia na maendeleo, uhuru, haki za watu lazima kazi ya kujiimarisha ifanyike mahali kote ili chama hicho kiibuke kidedea na kuongoza Serikali mwaka 2025.

“Nyie wa Bukombe na Geita, kama ambavyo sisi wa kitaifa tutakavyozunguka katika majimbo na kata zote, nanyinyi mna wajibu wa kwenda kila kata, kijiji na kitongoji msiache mahali Chadema iamke ili kuwakomboa Watanzania,” amesema Mnyika.

Katika hatua nyingine, Mnyika amewataka wanachama wa chama hicho, kuutumia mwaka 2023 kudai Katiba Mpya na Tume huru ya uchaguzi, akisema ni jambo linalopaswa kuwa la Taifa.

MWANANCHI
Pambaneni aiseh tafuteni mtu mzuri wa kumsimamisha lkn sio Lissu aiseh mine mbona ntawapigia kura
 
Unaona ni kazi ngumu kuanzisha chama, lakini una mbinu za kuitoa CCM! Haya basi wape hizo mbinu waliokuwa na uthubutu wa kuanzisha chama, napo unataka ubembelezwe.

Mkuu sioni kama una mbinu zozote za maana, kama ungekuwa nazo ungezitoa. Unalaumu maoni yako yanapuuzwa, yatumie mwenyewe basi nayo bado huwezi, ila unalaumu wengine hawana mbinu za kuitoa CCM. Kazi kweli kweli.
Sawa Mimi ngoja tutazame endless progress ,

Kuitoa ccm ni tofauti na kuanzisha chama ni process ndogo zenye , kuvaa uchungu wanaopitia watanzania , na sio kuvizia Ruzuku na kuomba maridhiano ,

Nimeshawatumia uongozi wa CHADEMA Taarifa lakini wanakataa eti sisi vijana tunabidi kufata utaratibu ambao utapatikana kwa Rais niseme tu .

Hawa nyie mnaowaona Kama mashujaa ni wabinafsi Sana that way wamewa-blind ili msijitambue mbaki na jicho moja la kuona kuwa Ccm itatolewa kwa maridhiano au ballots box .

Haitokaa itokee watu Kama Mbowe and so called wanaharakati mkitoe hiki chama chakavu endapo mkawa na hizi Ego zenu za kuona nyie ni Bora .

Mimi nimecheza sabotage mbalimbali huko Ccm so I don't want to find my self guilty that way nilitaka CHADEMA watupe nafasi na sisi tuweze kufanya kitu .
 
Back
Top Bottom