Kumbe Mzilankende Magufuli alikuwa hakubaliki Hadi kwao πππ
My Take: Chadema acheni kutoa Siri za Wakubwa ππ
====
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeeleza nia yake ya kulitwaa Jimbo la Chato kwa kushinda viti vingi katika uchaguzi wa serikali za mitaa baadaye mwaka huu na ule wa ubunge na madiwani mwakani.
Jimbo hilo ambalo kwa muda mrefu tangu likiwa Biharamulo Magharibi mwaka 1995 hadi lilipoitwa Chato baada ya kuanzishwa wilaya, lilikuwa chini ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dk. John Magufuli mpaka mwaka 2015 na baada ya hapo Dk. Medard Kalemani mpaka sasa.
Mwenyekiti wa Kanda ya Victoria, Hezekiah Wenje, ambaye anawania tena nafasi hiyo, amesema kuwa Chato ni moja ya majimbo yaliyoko katika kanda hiyo ambayo wamepania kushinda yote katika uchaguzi ujao.
"Kwa kanda nzima ya Victoria katika majimbo 25, mpango wetu ni kupata majimbo si chini ya 16 likiwamo la Chato na uwezekano upo. Tumeshafanya tathmini na utafiti wa kutosha.
"Kwa mfano Jimbo la Chato tumewahi kuongoza serikali za vijiji vingi kuliko Chama Cha Mapinduzi (CCM) tena kipindi cha Magufuli," amesema.
NIPASHE