13 August 2020
Tunduma, Tanzania
UMATI WA WATU WAMPELEKA MWAKAJOKA KUCHUKUA FORM YA KUGOMBEA UBUNGE.
Source: DSS Tunduma
Tuliwaambia CCM Mpya wananchi wanataka sera bora zitakazowafanya wawe watu huru katika kujiletea Maendeleao ya Watu.
Mfano wa Maendeleo ya Watu kwa mtu huru ni serikali kuweka mazingira bora katika kilimo. Siyo wao wanalima Korosho kama watoto yatima halafu siku ya mavuno serikali inakuja kuyanyakuwa kwa mkopo wakati wamefanya kazi kwa bidii na jingi bila msaada wa Mkuu wa wilaya DC, RC, Waziri wa Kilimo, Ofisi ya Waziri Mkuu wala Ofisi ya Rais. Huo ni mfano mmoja wa unyanyasaji.
Wananchi wanaona unyanyasaji wa wazi kwa wabunge wao waliowatuma huko ndani ya Bunge na nje ya Bunge. Chaguzi ndogo kati ya 2015-2019 zilizofanyika kukuta Ofisi ya Mkurugenzi imefungwa! Mwaka 2019 November Uchaguzi wa serikali za Mitaa na Vijiji wagombea wa upinzani kunyimwa fomu au kuenguliwa kihuni wananchi waliona. Vyombo vya habari kutishwa kurusha habari za wapinzani...
Wananchi wanalipa kodi lakini viongozi wanasema wazi na kwa vitendo vya kibaguzi kuwa hawatapata barabara kwa vile wamechagua viongozi bora ambao wametokana na upande mbadala ambao licha ya kuwa unatambulikana kisheria kupitia katiba lakini wanaadhibiwa na CCM Mpya kwa kunyimwa huduma muhimu za Maendeleo ya Watu.
Sasa wananchi wameamua kusema basi!