Uchaguzi 2020 CHADEMA Tunduma: Wananchi wakimsindikiza Mwakajoka kuchukua fomu za Ubunge

Huwa tathimini yangu nilioipiga nimeona nikama mikoa ya mbeya songwe chadema niwengi kuliko mikoa mingine yote

Ni kweli kabisa Mbeya na Songwe ccm ilikufa zamani sana. Kwanza kunapakana na nchi ambazo zimekomaa kidemocrasia kama vile Malawi, Zambia na DRC
 
Yapo majinga mengi yalitia Nia ccm, na Pasco Mayala akiwemo, kwa kudhani kuw a CCM itawabeba kiulaini. lakini shughuli ya October hata kasimu majaliwa huenda asirudi bungeni
Ka-simu ameanza vituko vya kuteka watu!
 
Hivi hawa hawana habari za ndege kununua kwa cash? Hawajui SGR?
Mbona wako hivi hawa? Jee hawana habari za kuunga mkono juhudi kwa kina Nasari, Gekule, Silinde, na madiwani wengi tuu? Hata daraja la mfugale ambalo ni la aina yake barani Afrika?
Hawa ni wapiga dili
 
Ushauri : Mgombea wa ccm Tunduma ajitoe .
 
Nyie chadema kwenye sanduku hatuwawezi, ila inshaalah wakurugenzi wanalipwa na gari zao zinajazwa mafuta kwa hela kutoka mfuko wa mwenyekiti wetu naamini jambo haliwezi haribika!
Alishawaambia hakuna kuwa neutral
 
Watu walikuwa wagonjwa,wanaugulia ndani ya nafsi zao. Tume isiingize siasa kupitisha wagombea;kusiwe na double standard,vinginevyo vichaa watakuwa wengi,,,sonona. Tunahitaji umoja wa kitaifa,hoja zitawale,hatutaki matusi
 
jiwe awaze mambo mengine ya maendeleo, aache kupoteza muda na pesa kujaribu kuua upinzani...haiwezekani watz wote KAMWE hatuwezi woote kuwa CCM, hata kama mabomba ya maji yangetoa maziwa nchi nzima!.
 
Hapo unakuta wanaopiga kura ni wachache tu
mkuu kuwa honest kwenye nafsi yako, hebu jiulize inawezekana vp pamoja na mazingira ya upinzani kubanwa sana awamu hii lakini kumbe bado wapo tu kwa wingi hivyo?!. na hapo hakuna cha wasanii wa muziki wala wananchi kusombwa kwa mabasi/malori!!.
 
Kati ya makosa makubwa CCM watajilaumu kumuacha akazuia Shughuli za Vyama vya siasa na kudhulumu uchaguzi wa Serikali za mitaaa mwaka jana ndio matokeo yake tunayaona leo
WANANCHI KOTE NCHINI BARA NA VISIWANI WAMEKUA NA SHAUKU KUBWA SANA YA KUWASIKILIZA WAPINZANI KINYUME KABISA NA MAWAZO KUWA WANGEKATA TAMAA

Kiukweli kupitia hili ccm wajifunze ;ingekua wapinzani wanapata muda wa kusema miaka mitaano hii bila kunyanyaswa leo hawangekua na la kuwaambia watu

Binadamu huna jipya la kuwafanyia au kuwapa ; WAPE KILA KITU ILA USIWANYIME MDOMO KUSEMA NA MASIKIO KUSIKIA ......Dola na Vyama vyenye Nguvu duniani zilifanya Maendeleo makubwa Lakini zilianguka kwa sababu tu waliziba watu midomo ...

Leo CCM haipo kwa watu kabisa zaidi ya kwenye Dola tena kwenye dola sio wote bali wale wenye mamlaka

Wanamikakati wa CCM wamempotosha Sana Mwenyekiti

Mwaka Huu ni maeneo machache Sana ccm inaweza kushinda kihalali Hii ni tofauti kabisa na miaka mitano nyuma Pamoja na kazi nzuri iliyofanywa

SEKRETARIET ya CCM imeuwa Chama kwenye mioyo ya watu !!!!!

Baada ya uchaguzi Huu lazima mabadiliko makubwa yafanyike kwenye sekretariet ya CCM ile ya kina Kinana na Nape was far better kwakua ilikua na approach ya kutumia siasa zaidi kuliko kutegemea kubebwa na Dola nzima .
 
Magufuli hakushauriwa na yeyote , aliamua mwenyewe binafsi kwa kudhani ana akili kuliko wengine , Sisi wengine tulijua kitakachotokea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…