CHADEMA tupeni Ratiba ya Mikutano ya Lissu

CHADEMA tupeni Ratiba ya Mikutano ya Lissu

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Kufuatia mikutano ya vyama vya siasa kuruhusiwa na Mh. Tundu Lissu kurejea nyumbani, kujua atakuwa wapi mheshimiwa huyu kwa mikutano hii ingependeza sana.

"Si waswahili wanasema mgeni aje mwenyeji apone? Pia si kipya kinyemi?"

Tayari kwa mujibu wa kitabu cha Mkapa (Maisha Yangu) sasa tunajua kumbe tuna Marais wezi.

Tunajua matatizo yetu ya maisha magumu, bei za vyakula juu, tozo na kodi zisizokuwa na idadi kuongezeka Kila uchao, serikali kutowajibika kwetu nk, ni matokeo ya katiba hii mbovu.

"Ikumbukwe katiba hii inapigiwa kelele leo tangia miaka ya 90."

Tukijua atakakuwa wapi mheshimiwa huyu, wengi tutajipanga ikibidi kufika aliko physically.

"Kwa maana kwetu wengine kwa madini aliyo nayo, alipo tupo."

Nani asiyetaka kujua chanzo cha matatizo yetu? Nani asiyetaka kujua suluhisho la matatizo yetu? Nani asiyetaka kuwa sehemu ya ufumbuzi wa matatizo yetu?

"Mlete mdhunguuu. (×2)
mlete mdhungu (×2)" 🎵🎵

Katiba mpya ni sasa!
 
Chanzo cha matatizo yetu wao, suluhisho letu sisi, hakuna njia nyingine zaidi ya hiyo..
 
Chanzo cha matatizo yetu wao, suluhisho letu sisi, hakuna njia nyingine zaidi ya hiyo..

Mikutano ya huyu bwana ni muhimu na ni tofauti. Hakuna jipya analosema ambalo hatukulijua. Tofauti Iko kwenye presentation na ufafanuzi.

Chawa hawa walidhani katiba mpya haiwahusu. Sasa hivi wameamka na wengine kama joni hatimaye wanaupiga mwingi Wala si mama tena.
 
Back
Top Bottom