Uchaguzi 2020 CHADEMA tuwekeze nguvu mkoa wa Njombe, bila hivyo tutaaibika

Uchaguzi 2020 CHADEMA tuwekeze nguvu mkoa wa Njombe, bila hivyo tutaaibika

Countrywide

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2015
Posts
20,694
Reaction score
32,527
Wakuu nina imani mko powa, leo kuna jambo limenistaajabisha sana. Moja ya ngome zetu kuu kama chama ni nyanda za juu kusini, ikiwemo mikoa ya Mbeya, Iringa na Njombe. Kama tunavyofahamu sasa hivi kuna kampeni zinaendelea kila mahali za urais, ubunge na udiwani.

Chama chetu ninaona kabisa kuna sehemu hakijajiandaa au kuna tatizo lipo ambalo pengine viongozi hawataki kuliweka wazi. Mkoa wa Njombe ni moja ya mikoa ya kimkakati lakini nguvu iliyopelekwa huko haitoshi kabisa.
Kampeni za ubunge na udiwani hazina watu wa kusikiliza na kuishia kubaki mgombea na viongozi wachache.

Ni lazima tuangalie wapi tumejikwaa na sio kulalamika tulipoangukia. Njombe tunaenda kupoteza kura nyingi sana kama hali itaendelea kuwa hivi.

Picha chini ya mkutano wa kampeni huko Njombe.

IMG_20200906_222638.jpg
IMG_20200906_223324.jpg
 
CDM hawezi kushinda mkoa wa Njombe na Ruvuma hata jimbo Moja na hawatawekeza nguvu Huko maana haiwezekani kushinda maeneo hayo.
ACT wanaweza kuweka upinzani majimbo ya Tunduru ila kushinda pia ni ngumu.
Nafikiri wameshafanya tathmini maeneo wanayoweza kushinda ni Iringa mjini na Mbeya mjini.
Ukisema Ngome ya CDM ukaijumuisha na Njombe nitashangaa.
Iringa pia ni jimbo moja tu la Iringa mjini ambalo linahistoria Toka NCCR likarudi CCM sasa CDM.
kwahiyo sio mkoa Mzima. Majimbo mengine yote uwezekano wa CDM kushinda ni mdogo Sana.
CDM iwekeze sana nguvu Iringa mjini na Mbeya mjini haya majimbo ni muhimu Sana. Iachane na maeneo isiyo na nguvu Kama Njombe.

Sent from my Infinix X603 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom