Uchaguzi 2020 CHADEMA tuwekeze nguvu mkoa wa Njombe, bila hivyo tutaaibika

Endeleza tu propaganda uchwara Mataga ila jua kanda ya nyasa CCM mnapotezwa vibaya mwaka huu. Si iringa si Mbeya si songwe si njombe. Watu wa kule wana uelewa sana. Nimewapenda kwa kweli!!
 
Hapo ni mtaa unaitwa Kibena-kata ya Ramadhani. Na huyo jukwaani ni mgombea udiwani ambaye pia alikua diwani miaka mitano iliyopita. Watu wa huo mtaa wengi si wahudhuriaji wazuri wa mikutano yoyote ile. Hapo hata CCM wakiweka mkutano hawapati watu.
 
Hapo ni mtaa unaitwa Kibena-kata ya Ramadhani. Na huyo jukwaani ni mgombea udiwani ambaye pia alikua diwani miaka mitano iliyopita
Asante mkuu kwa ufafanuzi. Na je ni kweli chadema huko imekufa na kuzikwa kabisa?
 
Njombe tungeweza kupata jimbo this time kama Edwin Sware asingeunga juhudi.

Makambako pia almanusura tuchukue jimbo 2015 sijui uchaguzi huu ushawishi wa mgombea.

Mbeya zamu hii tunachukua majimbo matatu
 
Njombe tungeweza kupata jimbo this time kama Edwin Sware asingeunga juhudi.

Makambako pia almanusura tuchukue jimbo 2015 sijui uchaguzi huu ushawishi wa mgombea.

Mbeya zamu hii tunachukua majimbo matatu
majimbo yapi matatu ???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante mkuu kwa ufafanuzi. Na je ni kweli chadema huko imekufa na kuzikwa kabisa?
Hapana, Upinzani haujafa. Nilipita hilo eneo. Ni kati ya maeneo ambayo yanashida kubwa ya maji licha ya kuzungukwa na vyanzo vikubwa vya maji( kuna mabwawa makubwa matatu). Wakazi wengi wa hiyo kata ni kama wamekata tamaa ya kupiga kura na kujihusisha na siasa kwani wanaamini kuwa hata umchague mpinzani hawezi kushinda. Haya niliyasikia toka kwa baadhi ya watu na wengine wakasema uchaguzi huu hawawezi kwenda kupiga kura kwa sababu hizo. Mwaka 2015 Diwani wa eneo hilo alikua Chadema na mwenyekiti wa mtaa alitoka Chadema lakini akaja kuhamia CCM. Upinzani hasa Chadema ungewekeza nguvu kubwa katika kutoa elimu ya Uraia kwa watu, ili wajue umuhimu wa wao kushiriki kwenye chaguzi mbali mbali. Kikubwa upinzani upo nafikiri uliona mapokezi makubwa aliyopata Lissu wakati akitafuta wadhamini Njombe.
 
Shukurani mkuu. Nadhani kuna haja ya kutuma watu wakafanye amsha amsha huko ili kuamsha ari na kuwatia matumaini ya kwamba mamluki Sasa basi.
 
Shukurani mkuu. Nadhani kuna haja ya kutuma watu wakafanye amsha amsha huko ili kuamsha ari na kuwatia matumaini ya kwamba mamluki Sasa basi.
Hiki ndicho nimekisema kwenye hii mada, badala yake kama kawaida ya makamanda wengi kupenda kuropoka
 
Njombe Mjini walifanya kosa kubwa kumuweka Emanuel Mwasonga kugombea ubunge, watu wa njombe wanajua ni mchaga, bora mngemuweka dada yangu Rose Mayemba
 
Jimbo la Njombe mjini wangeligawa vizuri CCM wasingekaa walipate.Ila wajanja,sehemu kubwa ya Njombe mjini ipo vijijini.Mtu ukisikia unaenda Njombe mjini usifikiri pote Ni mjini.Kama Jimbo la Njombe mjini lingechukua lile eneo la mjini tu CCM wasingekaa washinde hata Mara moja.
Ukienda Jimbo la Lupembe,lile pale siasa bado zipo CCM Sana japo 2015 Kuna mgombea wa CDM Edwin Swalle alileta ushindani mkubwa bahati mbaya kaunga juhudi na ndiye mgombea kwa upande wa CCM mwaka huu.Jimbo la Makambako angalau ndio Jimbo pekee ambalo CCM huwa hawana uhakika nalo.
Njombe mjini Masonga anajulikana Sana pale mjini lakini ukienda pembezoni hapati kura za kutosha. Yote kwa Yote pale Njombe Mjini na mji wa Makambako Tundu Lissu atapata kura nyingi.
 
Njombe Mjini walifanya kosa kubwa kumuweka Emanuel Mwasonga kugombea ubunge, watu wa njombe wanajua ni mchaga, bora mngemuweka dada yangu Rose Mayemba

Mayemba angebebwa na Jina Mayemba pia Mwanyika wa CCM jina Mwanyika Ni kubwa hivyo linambeba pia kale Kataito kwamba jamaaa Ana noti za kutosha kanambeba.
 
Njombe hali ni mbaya
Wewe tapeli sijawahi kukuamini na haitatokea kamwe nikuamini, Njombe ya Rose Mayemba sio hiyo uliyoweka kwenye picha, sijui unaokota wapi hizo picha na nyungine unavizia kabla watu hawajafika kwenye mikutano unapiga picha unaleta huku, wewe ni MUONGO.
 
Ndio maana huwa simuamini huyu tapeli na hizi thread zake, hajui lolote, siku zote anafanya mind games kuonesha Chadema haina nguvu, amefeli.
 
Ruzuku imepigwa yote kampeni zitafanywa na pesa zipi,ukiuliza bwana Yule anakwambia wanafanya kampeni kimkakati,wanakodi ndege wanaruka juu wanaenda mikoa yenye ushawishi tuu,wananchi wengi wanawaacha chini,wakishindwa utasikia wanasema wameibiwa kura,lakini mwwnzao ana piga mpaka kwenye kata,wao wameruka hata wilaya
 
Utayaoga matusi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…