EZZ CHEZZ
JF-Expert Member
- Apr 10, 2011
- 1,230
- 1,352
Mpaka sasa chama hiki ndiyo kikubwa zaidi miongoni mwa vyama vya upinzani. Kwa wanaokumbuka uchaguzi wa 2010 ulionesha umuhimu wa chama hiki kuwa na kituo chake cha television kitakachooneshwa kwenye luninga mbali na vile vya mtandaoni.
Ikumbukwe pia namna kipindi cha TBC cha "mchakato jimboni" kilivyochangia kuipa umaarufu chadema sanjari na wagombea wake. Mwangwi haukuishia kuipaisha chadema bali pia kuishusha ccm na wagombea wake kiasi cha chama hicho kuwapiga marufuku wagombea wao kushiriki midahalo ile! Pia kipindi hakikumwacha salama mtunzi wake!
Kwa kifupi hakuna asiyejua umuhimu wa upinzani kuwa na jukwaa lao huru hususan nyakati za kampeni. Sasa pamoja na kelele za wafuasi wengi wa chadema kuitaka kuwa na TV yake kitu ambacho ikismua inaweza, mpaka sasa ni ngumu kudhani kuwa kuna mpango kama huo ndani ys chama.
Sasa hebu tujadili. Unadhani nini kinawakwamisha watu hawa kuwa na TV station yao? Je ni utashi hafifu? Ni ukata?
Tujadili.