CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

Hili la serikali 2 ni la kuangalia kwa mtazamo mpana

Upo ushahidi , wabunge wa CCM katika bunge maalum waligawanyika. Waliitwa na kupewa msimamo, jambo lilozaa Ukawa

Rais Kikwete,aliwaambia CCM wajiandae na mabadiliko ya serikali 2 kwenda 3. Hii ilikuwa ni baada ya rasimu ya kwanza

Jaji Warioba ni muumini wa serikali 2. Hata hivyo, alisema ameshawishika kuunga mkono serikali 3 kutokana na mabadiliko ya hali ya kisiasa nchini na duniani na kwamba jambo hilo haliepukiki

Ni mbadiliko ya dunia anayosema Warioba ndiyo yaliyomlazimuNyerere kukubali uwepo wa mfumo wa vyama vingi, jambo alilolikataa miaka 30 kabla ya kutokea kwake

Asha Rose alikuwa mjumbe wa tume ya Kisanga iliyopendekeza serikali 3.
Kwa maneno mengine anaamini katika serikali 3. Ni Asha huyo ndiye aliyegawa nakala za katiba yao pendekezwa iliyokufa akiwa anaamini 3 nakutekeleza serikali 2

Da'Amina naye ni kama Asha. Mkuu JokaKuu kaeleza hapo juu

Hivyo, kumsema Lowassa na kufumbia macho wengine ni double standard and unfair

That said and done, haiondoi ukweli kua anapotaka kubeba dhamana kubwa ni vema akaeleweka.

Ni katika kuondoa mashaka kama alivyouliza Alinda hapo juu
Tuseme kwamba tusiwafumbie macho wengine, tuwajumuishe nao katika huo "uwajibishaji".
Je, hiyo kweli ni point ya kumsafisha mtu?
Yaani usimuhukumu mwizi kwa sababu kuna wezi wengine.
Jamani Kubalini tu kuwa in principle, Lowassa siyo the best flag-bearer wa UKAWA. This is good news to me, even my uneducated self can debate the hell outta this dude.
Yes, I can debate Lowassa and make him look vague.
 
Last edited by a moderator:
Jamani Kubalini tu kuwa in principle, Lowassa siyo the best flag-bearer wa UKAWA.
So says who, UKAWA or Kobello? For your info Lowassa is the flag bearer of UKAWA so bear it and like it!
This is good news to me, even my uneducated self can debate the hell outta this dude.
So what? What stopped you from entering the ring? it's hard to imagine...Kobello vs Lowassa, that would be the day!
Yes, I can debate Lowassa and make him look vague.
Keep on blowing your own trumpet dude, Lowassa has a huge following and what do you have? Family, dog and cat?

Dont be offended friend, this is but with a light touch! Just laugh it off! See ya at the ballot box come October 2015.
 
Hivi ni lipi na wapi Lowassa alitamka mambo ya serikali 2 au 3?

Huu uumini wa Lowassa wa serikali mbili hauwezi kubadilika kuwa serikali tatu?

Kama huyu Lowassa amezaliwa na kulelewa na CCM lakini leo hii kahama CCM je kinachomshinda ni nini kuwa muumini wa serikali 3?

Hivi wakati anajiunga na Ukawa si alifahamu kuwa Ukawa wanapigania katiba ya Wananchi ambayo ni rasmu ya Warioba?

Simpendi Lowassa, lakini napenda kumhukumu kwa haki si kwa maneno ya kulishwa na CCM Kama ni mla rushwa tuambiwe ni rushwa ya nini, ni lini ilitokea na ni wapi na serikali ilimchukulia hatua gani na kama serikali haikuchukua hatua tuambiwe ni kwanini? zaidi ya hapo yatakuwa ni majungu ya akina Nape und co.
 
Kobello,

..lowassa ni muumini wa serikali 2 lakini sasa ni mwanachama wa cdm ambayo sera yake ni serikali 3.

..kuna uwezekano lowassa akabadilika, au akaibadilisha cdm.

..lakini suala la uumini wa serikali 2 vs 3 lipo zaidi kwa wana-ccm. Labda tunaweza kujufunza kwa mifano iliyoko ccm.

..balozi amina salum aliongoza tume iliyotoa mapendekezo ya muungano wa serikali 3. Dr
Asha migiro alikuwa mjumbe wa tume ya jaji kisanga iliyopendekeza serikali 3. Dr.mwakyembe aliandika thesis ya phD kutetea serikali 3. Lakini wote hao leo ni waumini wa serikali 2.

..maswali ya msingi ni haya: does lowassa care enough about serikali 2 kiasi cha kupelekea kujaribu kuibadilisha cdm? Je, ana uwezo wa kihoja ktk kutekeleza azma hiyo? Je, ana watu wa kutosha ndani ya cdm watakaomuunga mkono kubadilisha msimamo kwenda serikali 3? Nini future ya ukawa ikiwa cdm itabadilika na kuunga mkono serikali 2?

Cc Mag3, Nguruvi3, Mwalimu
Lowassa hawezi kuibadilisha CDM na wala CDM hawawezi kumbadilisha.
Lowassa anataka kutawala JMT na siyo Tanganyika au a watered-down JMT.You get more power when you rule Tanzania as it is, hawezi kujiondolea madaraka wakati Ana veto power.
He has spent a lot of money and time to do that. Atakayepinga atakuwa anatafuta mtafaruku ambao sidhani kama watanzania wengi wanautaka.
Ni hatari.
 
Last edited by a moderator:
Hivi ni lipi na wapi Lowassa alitamka mambo ya serikali 2 au 3?

Huu uumini wa Lowassa wa serikali mbili hauwezi kubadilika kuwa serikali tatu?

Kama huyu Lowassa amezaliwa na kulelewa na CCM lakini leo hii kahama CCM je kinachomshinda ni nini kuwa muumini wa serikali 3?

Hivi wakati anajiunga na Ukawa si alifahamu kuwa Ukawa wanapigania katiba ya Wananchi ambayo ni rasmu ya Warioba?

Simpendi Lowassa, lakini napenda kumhukumu kwa haki si kwa maneno ya kulishwa na CCM Kama ni mla rushwa tuambiwe ni rushwa ya nini, ni lini ilitokea na ni wapi na serikali ilimchukulia hatua gani na kama serikali haikuchukua hatua tuambiwe ni kwanini? zaidi ya hapo yatakuwa ni majungu ya akina Nape und co.
Dada, tafadhali pitia hansards za bunge au type Lowassa/serikali tatu in a Google search bar.
These things are not hearsay, they are facts.
It's also logical to want more power, thats second to life itself. A 3 tier government will always be an enemy of any incumbent in Tanzania.
 
So says who, UKAWA or Kobello? For your info Lowassa is the flag bearer of UKAWA so bear it and like it!

So what? What stopped you from entering the ring? it's hard to imagine...Kobello vs Lowassa, that would be the day!

Keep on blowing your own trumpet dude, Lowassa has a huge following and what do you have? Family, dog and cat?

Dont be offended friend, this is but with a light touch! Just laugh it off! See ya at the ballot box come October 2015.
Just because you have a huge following, doesn't make you smart.
Keep on liking him .... He ain't going nowhere, and you can't grow enough ballz to use "other" means.

Your little words don't move me. I suggest we talk politics or just be a gentlemen and read between the lines.
 
Hivi ni lipi na wapi Lowassa alitamka mambo ya serikali 2 au 3?

Huu uumini wa Lowassa wa serikali mbili hauwezi kubadilika kuwa serikali tatu?

Kama huyu Lowassa amezaliwa na kulelewa na CCM lakini leo hii kahama CCM je kinachomshinda ni nini kuwa muumini wa serikali 3?

Hivi wakati anajiunga na Ukawa si alifahamu kuwa Ukawa wanapigania katiba ya Wananchi ambayo ni rasmu ya Warioba?

Simpendi Lowassa, lakini napenda kumhukumu kwa haki si kwa maneno ya kulishwa na CCM Kama ni mla rushwa tuambiwe ni rushwa ya nini, ni lini ilitokea na ni wapi na serikali ilimchukulia hatua gani na kama serikali haikuchukua hatua tuambiwe ni kwanini? zaidi ya hapo yatakuwa ni majungu ya akina Nape und co.

Humpendi Lowasa?kakukosea nini,ni kwa sababu ya siasa au lingine tu.ufisadi wa Lowasa Leo umekua majungu,wakati Padri Slaa alisema kwa UMMA pale mwembe Yanga.. Leo nimeamini fedha Sabuni ya Roho
 
Humpendi Lowasa?kakukosea nini,ni kwa sababu ya siasa au lingine tu.ufisadi wa Lowasa Leo umekua majungu,wakati Padri Slaa alisema kwa UMMA pale mwembe Yanga.. Leo nimeamini fedha Sabuni ya Roho

Nafikiri nilishakwambia kuwa huwa sijibu kashfa na kejeri....Pole...
 
Hivi ni lipi na wapi Lowassa alitamka mambo ya serikali 2 au 3?

Huu uumini wa Lowassa wa serikali mbili hauwezi kubadilika kuwa serikali tatu?

Kama huyu Lowassa amezaliwa na kulelewa na CCM lakini leo hii kahama CCM je kinachomshinda ni nini kuwa muumini wa serikali 3?

Hivi wakati anajiunga na Ukawa si alifahamu kuwa Ukawa wanapigania katiba ya Wananchi ambayo ni rasmu ya Warioba?

Simpendi Lowassa, lakini napenda kumhukumu kwa haki si kwa maneno ya kulishwa na CCM Kama ni mla rushwa tuambiwe ni rushwa ya nini, ni lini ilitokea na ni wapi na serikali ilimchukulia hatua gani na kama serikali haikuchukua hatua tuambiwe ni kwanini? zaidi ya hapo yatakuwa ni majungu ya akina Nape und co.
Mkuu,
Gonga na soma hapa,
Au hapa,
Mh. Edwad Lowassa (a.k.a Rais ya Monduli) alipoulizwa kuhusu sababu za mvutano wa kisiasa nchini, alijibu:

"Kuna mchakato wa uundwaji wa katiba mpya, watu wanataka serikali tatu, wengine moja, wengine wanataka zibaki mbili, lakini mimi kwa maoni yangu naona bora zibaki serikali mbili kama ilivyo sasa, kwa sababu serikali tatu, ile ya muungano itamezwa na Serikali za Tanganyika na Zanzibar na huko ni kuvunja muungano. Kuna watu wameoana pande zote mbili sasa muungano ukivunjika hawa tuta wafanyaje? lakini tuwaachie wananchi watoe maoni".

Alipo ulizwa kuwa wanachi wakipendekeza serikali tatu itakuwaje? Alicheka na kujibu: "Hiyo ni bahati mbaya, itakuwa bahati mbaya sana!"

Source: VOA.
Baada ya maelezo ya Lowassa, mpambambanaji mmoja wa CHADEMA alinukuliwa akisema.
Huyu mzee ni mtu wa kufuata mkumbo na hajawahi kuwa analytical.Aseme tu anachanganyikiwa na mapendekezo ya serikali tatu maana hajui atagombea wapi.Uroho wa madaraka ndiyo uliomsukuma kutoa maoni hayo kwa hoja dhaifu zilizopitwa na wakati
 
Wanaukumbi.

Mabilioni yatengwa kumsafisha Lowassa

Mabilioni yatengwa kumsafisha Lowassa

Na Saed Kubenea - Imechapwa 30 March 2011

WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya mkataba tata wa Richmond, Edward Lowassa ameelezwa kuwa na mradi wa karibu Sh. 8 bilioni wa “kujisafisha” na kumwingiza ikulu.

Lowassa alipoulizwa na gazeti hili kuhusu mradi huo, alijibu kwa mkato, “Mimi sijui.”

MwanaHALISI limeelezwa kwamba fedha za “kumsafisha” Lowassa zimeahidiwa na swahiba wake, Rostam Aziz ambaye wamesimama pamoja muda wote wa sakata la kashfa ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond iliyothibitika kuwa feki.

Richmond ilipewa mkataba wa kufua umeme ikiwa haina fedha, wataalam wala uzoefu katika eneo hilo; huku nyaraka zilizopo juu ya kashfa hiyo zikionyesha kuwa mkataba ulipatikana kwa njia ya upendeleo – tuhuma ambazo zinamwangukia Lowassa.

Taarifa zinasema mabilioni hayo ya shilingi yamelenga kutumika kulegeza wajumbe wa vikao vya maamuzi vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) hasa kuelekea, na wakati wa mkutano mkuu ndani ya chama hicho ambao utafanyika mwaka kesho.

Fedha hizo pia zinadaiwa kulenga kuyumbisha jumuiya za CCM – Umoja wa Wanawake (UWT), Jumuiya ya wazazi na Umoja wa Vijana (UV-CCM). Wengine ambao wanadaiwa kulengwa katika hatua ya kushawishi, kulegeza na kushirikisha katika mradi wa kusafisha Lowassa ni wabunge, vyombo vya habari na waandishi wa habari mmojammoja.

“Mradi wa kumsafisha Lowassa” umeelezwa kuwa chini ya kundi la watu watano. Mbali na Lowassa mwenyewe na Rostam, wengine waliotajwa ni Andrew Chenge, Makongoro Mahanga na Peter Serukamba.

Chenge ni mbunge wa Bariadi Magharibi; Mahanga ni mbunge wa Segerea na Serukamba ni wa Kigoma Mjini. Taarifa zinasema tayari baadhi ya wajumbe wa kundi hilo wamefanikiwa kushika nafasi za juu za Kamati za Kudumu za Bunge.

Walioshika nafasi hizo ni Lowassa (Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama) na Serukamba (Miundombinu).

Gazeti hili limeelezwa kuwa mgogoro unaoendelea ndani ya UV-CCM, unatokana na “kasi ya mbio za Lowassa kugombea nafasi muhimu” ndani ya chama chake na baadaye urais.

Kwa wiki mbili sasa, viongozi wa vijana wamekuwa wakisutana, kulaumiana na kutuhumiana kujenga makambi ndani ya umoja huo. Wiki iliyopita walimrukia waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye wakimtuhumu kuhujumu chama “kwa kuzungumza nje ya vikao.”

“Sikiliza bwana ee, vurumai hii ya vijana ni ya kutafuta kujenga kundi la kumsafisha Lowassa. Wapo wanaofanya kazi hiyo kwa kujua na wapo wanaofanya hivyo bila kujua,” ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi wa CCM.
Hatua ya baadhi ya viongozi wa vijana, kurukia kila wanayeona ana uwezekano wa kupinga Lowassa na kundi lake, inaelezwa kutokana na waliokuwa wapinzani wao wakuu kubaki serikalini na wao (akina Lowassa) kuwa nje ya utawala.

Wanaotajwa kuwa serikalini, lakini wanadaiwa kuwa wapinzani wa Lowassa katika mgawanyiko wa wanaopinga ufisadi na wanaoutetea, ni pamoja na Samwel Sitta, ambaye hivi sasa ni waziri wa Afrika Mashariki.

Wengine ambao akina Lowassa hawakutegemea kuwemo serikalini, ni waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, Benard Membe; naibu waziri wa ujenzi, Dk. Harisson Mwakyembe na mkuu wa wilaya ya Masasi, Nape Nnauye.

Lowassa hakuwa na simile pale alipohojiwa kwa njia ya simu kuhusu “mradi wa kujisafisha.”

Swali: Mheshimiwa, tumepata taarifa kuwa una mradi wa Sh. 8 bilioni kwa ajili ya “kujisafisha kisiasa.” Je, hii ni kweli?
Lowassa: Muulizeni huyo mpuuzi aliyewaambieni.

Swali: Gazeti linakuliza wewe kwa kuwa ndiyo mwenye mradi.
Lowassa: Mimi sijui. Sitaki kusikia mambo ya kijinga…”

MwanaHALISI liliripoti katika toleo lake la Machi 9 – 15 mwaka huu, chini ya kichwa cha habari kisemacho, “ Siri ya Edward Lowassa nje,” juhudi za mbunge Beatrice Shelukindo “kumsafisha” Lowassa.

Katika ujumbe wake wa maandishi kwa mbunge mwenzake, Pindi Chana, Shelukindo alisema ameambiwa na Nabii Joshua wa Nigeria kuwa “rais ajaye ni Edward Lowassa” na kwamba maisha yake ya nyuma yanayomhusisha na kashfa ya ufisadi, “si kitu.”

Joto la Shelukindo katika mawasiliano haya lilitokana na kile alichoeleza kuwa, “Mungu ni wa ajabu. Lowassa ameniombea kura pasipo maelezo. Ameandaa lunch na dinner (vyakula vya mchana na usiku) ambako amekuwa akiniombea kura. Mungu ana njia za ajabu za kufanya mambo.”

Shelukindo alikuwa akirejea fadhila za Lowassa kumwombea kura wakati wa kugombea nafasi ya kamishena wa bunge. Alishinda. Naye Rostam alitafutwa kwa simu bila kupatikana. Hatimaye alipelekewa swali kwa njia ya sms.

Swali: Kuna taarifa kuwa umeahidi kumwezesha Mhe. Edward Lowassa kwa Sh. 8 bilioni katika kile kinachoitwa “mradi wake wa kujisafisha kisiasa.” Je, hii ni kweli? Simu yako haiitiki.

Tofauti na Lowassa aliyesema hataki kusikia “mambo ya kijinga,” Rostam alijibu kwa sms, “Sidhani Lowassa anahitaji mradi wa kumsafisha maana si mchafu,” kauli ambayo haikushangaza kwa kuwa ilitoka kwa swahiba mkuu wa wakati wa jua na mvua.

Rostam aliandika, “Isipokuwa nimetenga pesa kuwasaidia nyie MwanaHALISI mnunue mtambo wa kuchapisha gazeti bila bughdha!”

Hata hivyo, gazeti hili lina uhakika kuwa Rostam hana mtambo wa kuchapa magazeti yake ya Mtanzania, Rai, The African, Bingwa na Dimba. Anayachapia kampuni ya Mwananchi Communications Limited.

Majibu ya Rostam yameelezwa kuwa ya kumfariji swahiba wake kwa msingi mmoja tu; kwamba wameshiriki – kwa njia mbalimbali – katika kutafuta miradi ya kufua umeme, ambayo imeleta kashfa na kumfikisha Lowassa alipo sasa.

Mtoa taarifa amesema kundi la watu watano limekuwa likifanya vikao; lakini ni kikao cha Dar es Salaam cha mwishoni mwa mwaka jana, ambacho kiliweka mkakati wa Lowassa kujitokeza hadharani “kila inapobidi,” kushiriki mikutano na kutolea matamko hoja kadhaa zinazoibuka ili aonekane karibu na wananchi.

Maswali yaliyotumwa kwa wajumbe wengine wa kundi hili ambao simu zao ziliita bila kujibiwa au hazikupatikana, hayakujibiwa.

Wakati hayo yakifanyika, taarifa zinasema baadhi ya wajumbe wa NEC wamejipanga kupeleka hoja katika vikao vya juu kutaka watuhumiwa wote wa ufisadi waenguliwe kwenye nafasi zao za uongozi ndani ya chama.

“Tunakwenda kwenye NEC tukiwa na dhamira moja ya kumuondoa Rostam, Lowassa na Chenge katika vikao vya maamuzi vya chama chetu. Huo ndio mkakati wetu na lazima tuutekeleze ili kukinusuru chama,” ameeleza mmoja wa wajumbe wa NEC.

Katika minyukano hiyo, vijana ambao wasiokubali kuingia katika mradi wa kumsafisha Lowassa wameanza kusakamwa. Tayari mjumbe wa Baraza Kuu la uongozi la UV-CCM kupitia mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesimamishwa uongozi na baraza la vijana la mkoa huo.

Pamoja na kutuhumiwa kuhujumu kampeni za mgombea ubunge wa jimbo la Arusha Mjini, Baltida Buriani, Gambo anatuhumiwa kumweleza mmoja wa watu walio karibu na Lowassa kuwa “hafai kabisa”, akitumia maneno ambayo, kwa kuzingatia maadili, gazeti hili haliwezi kuyachapisha.

Kauli ya Gambo ilipofikishwa kwa mtoto wa Lowassa, Frederick, mtoto huyo alimwandikia Gambo sms ifuatayo: “Gambo unayo haki ya kumchagu mtu yeyote unayemtaka na siyo kumutukana mzee wangu. Hiyo siyo siasa, lakini endelea.” Ilikuwa 4 Machi 2011, saa 2:14:39 usiku. Gazeti hili limeona mawasiliano hayo.

Uhusiano wa Gambo na wafuasi wa Lowassa ulizidi kuwa mbaya kutokana na kunukuliwa akielezea wajumbe wa baraza la vijana la taifa mjini Dodoma wiki mbili zilizopita kuwa, sababu kubwa iliyofanya CCM kufanya vibaya katika uchaguzi uliopita, “ni chama kukumbatia watuhumiwa wakuu wa ufisadi nchini.”

“Lowassa na Rostam ndio wanakipotezea mvuto CCM. Tusitafute mchawi. Watanzania wanakerwa sana na Richmond na Dowans na lazima CCM iwashughulikie wahusika wote ili kujenga taswira mpya kwa chama chetu,” alieleza.

chanzo: Mwanahalisi.
 
Dada, tafadhali pitia hansards za bunge au type Lowassa/serikali tatu in a Google search bar.
These things are not hearsay, they are facts.
It's also logical to want more power, thats second to life itself. A 3 tier government will always be an enemy of any incumbent in Tanzania.

Mkuu,
Gonga na soma hapa,

Au hapa,

Baada ya maelezo ya Lowassa, mpambambanaji mmoja wa CHADEMA alinukuliwa akisema.

Mkuu Kobello asante sana kwa angalizo lako, nime"google" na kukuta hizo links mbili alizoleta Ng'wamapalala
Kwanza kabisa nilitgemea kukutana na clips na maandishi mbali mbali ya Mh. Lowassa kuhusu serikali 2 lakini kwa bahati mbaya kabisa nimekutana na hilo andishi la kwanza ambalo Lowassa aliongelea kanisa na hizo la pili alilohojiwa na Voa..

Andishi la pili pamoja na Lowassa kusema serikali mbili lakini bado anasisitiza kuwa wananchi waulizwe wanachotaka sasa basi kusema kuwa msimamo wa Lowassa ni serikali 2 bado hatutendi haki.

Swala la pili "Andishi kutoka kanisani" alichoongea ndio ulikuwa msimamo wa CCM (Si Lowassa) hivyo basi ilikuwa ni wajibu au ni lazima Lowassa kutetea msimamo wa chama. Na hii si kwa Lowassa tu bali wabunge wote wa CCM walikuwa wanatetea serikali 2 kama walivyokuwa wabunge wote wa Ukawa kutetea serikali 3. Laiti kama hawa wabunge wangeachwa huru kuamua ni serikali mbili au tatu basi kama Lowassa angesema kuwa yeye anataka serikali 2 walau tungesema kuwa huu ndio msimamo wa Lowassa.. Lakini tunachokiona ni msimamo wa CCM si wa Lowassa.

Nitajaribu kutoa mfn tu.. Tunafahamu Ukawa watu waliokuwa wako mstari wa mbele kutetea serikali 3 ni Tundu Lissu na Jussa hawa watu walijenga hoja zao na hata tukisoma maandishi au hata kuangalia clips mbali mbali utaona ni kwanini wanatetea serikali 3.

Na pale mtu atakaposema kuwa Tundu au Jussa misimamo yao ni Serikali 3 mtu unaelewa kwanini ni hivyo lakini inapotokea mtu akasema kuwa Mh. Msingwa au Mh Mhonga msimamo wake ni serikali 3 huyu mtu unakuwa unamuonea kwani huo msimamo wa Ukawa ambao hawa waheshimiwa wengine wamelazimishwa kufuata, kitu ambacho mimi nakiona si sawa kwa pande zote mbili maana wabunge hawakuwa uhuru kutoa mawazo yao bali mawazo ya viongozi wa vyama vyao.

Lakini pamoja ya hayo nimeuliza hapo awali kuwa je kwani msimamo wa Lowassa hauwezi kubadilika? Kama Lowassa metoka CCM na kwenda Chadema ni nini kitachomfanya hasibadilishe uamuzi wake wa awali?

Pia ndugu zangu Tanzania muhimu si serikali ngapi umuhimu ni kupata mhafaka kwa pande zote mbili ili kusudi kila upande uweze kutembea kifua mbele ukijivunia Mama yetu Tanzania.

Ng'wamapalala
Unakumbuka hapa""""

Mimi ninaheshimu uwezo wa Lowassa kwenye resource mobilization and mass mobilization kwenye uwanja wa siasa za Tanzania. Hakuna mwingine nchini zaidi ya Lowassa kwenye maeneo haya.

Hata wapinzani walikuwa wanampigia magoti aende kwenye vyama vyao kwa sababu wanafahamu uwezo wake mkubwa katika resource mobilization and mass mobilization kwenye uwanja wa siasa za Tanzania.

Nadhani ameamua kubaki CCM kwa sababu anahofia atapoteza vingi alivyonavyo!"""

Hizo ndio siasa
 
Alinda, nilidhani angeleta clip ya Lowassa akiunga mkono mfumo wa serikali mbili na sababu ya kutetea msimamo huo kwa hoja. Mimi najua kwamba alichosisitiza Lowassa wakati mwingi ni wananchi kuulizwa mfumo upi wanautaka na sababu zao na kwamba uamuzi wao huo uheshimiwe.

Wananchi kupitia Tume ya Warioba walitoa maoni na walionesha wazi kutoridhika na mfumo uliopo wa serikali mbili lakini chama tawala, CCM, kwa kutanguliza maslahi binafsi ya chama wakayapuuza maoni hayo ya wananchi. Wako wana CCM wengi kama Lowassa iliwabidi waheshimu msimamo wa chama ingawaje moyoni hawakukubaliana na huo msimamo na maadam Lowassa kwa sasa hayupo CCM, hafungwi tena na maamuzi ya hovyo yaliyofanywa huko nyuma na chama chake cha zamani.
 
Mkuu Kobello asante sana kwa angalizo lako, nime"google" na kukuta hizo links mbili alizoleta Ng'wamapalala
Kwanza kabisa nilitgemea kukutana na clips na maandishi mbali mbali ya Mh. Lowassa kuhusu serikali 2 lakini kwa bahati mbaya kabisa nimekutana na hilo andishi la kwanza ambalo Lowassa aliongelea kanisa na hizo la pili alilohojiwa na Voa..

Andishi la pili pamoja na Lowassa kusema serikali mbili lakini bado anasisitiza kuwa wananchi waulizwe wanachotaka sasa basi kusema kuwa msimamo wa Lowassa ni serikali 2 bado hatutendi haki.
Mkuu,
Mimi nadhani unajaribu kutetea hoja ambazo hazina nguzo inazozifanya zisimame kwenye muktadha wa hoja ya msingi.

Tukubaliane tu kuwa, Lowassa mpaka sasa ni muumini wa Serikali mbili na amepiga kura kukubali Katiba Inayopendekezwa. Kama kwa sasa amebadilisha fikra baada ya kuhamia CHADEMA, hili ni suala jingine pamoja na kwamba mpaka sasa hatujasikia tamko lake la kubadilisha fikra kuhusu muundo wa Serikali ya Muungano.

Hizi hoja za kusema, alipiga kura ya kuikubali Katiba Inayopendekezwa kwa sababu huo ulikuwa ni msimamo wa CCM ni kujaribu kuzikimbia hoja za msingi.

Kama kweli Lowassa alikuwa hakubaliani na Katiba Inayopendekezwa kwa nini hakutoka nje ya bunge kama baadhi ya wabunge wengine wa CCM walivyofanya, kwa mfano, Bulaya, Filikunjombe.

Kama unataka ushahidi zaidi wa utetezi wa Lowassa kuhusu serikali mbili na siyo serikali tatu, angalia hii video yenye mahojiano yake na Swahili TV.

Last edited by a moderator:
Mkuu Kobello asante sana kwa angalizo lako, nime"google" na kukuta hizo links mbili alizoleta Ng'wamapalala
Kwanza kabisa nilitgemea kukutana na clips na maandishi mbali mbali ya Mh. Lowassa kuhusu serikali 2 lakini kwa bahati mbaya kabisa nimekutana na hilo andishi la kwanza ambalo Lowassa aliongelea kanisa na hizo la pili alilohojiwa na Voa..

Andishi la pili pamoja na Lowassa kusema serikali mbili lakini bado anasisitiza kuwa wananchi waulizwe wanachotaka sasa basi kusema kuwa msimamo wa Lowassa ni serikali 2 bado hatutendi haki.

Swala la pili "Andishi kutoka kanisani" alichoongea ndio ulikuwa msimamo wa CCM (Si Lowassa) hivyo basi ilikuwa ni wajibu au ni lazima Lowassa kutetea msimamo wa chama. Na hii si kwa Lowassa tu bali wabunge wote wa CCM walikuwa wanatetea serikali 2 kama walivyokuwa wabunge wote wa Ukawa kutetea serikali 3. Laiti kama hawa wabunge wangeachwa huru kuamua ni serikali mbili au tatu basi kama Lowassa angesema kuwa yeye anataka serikali 2 walau tungesema kuwa huu ndio msimamo wa Lowassa.. Lakini tunachokiona ni msimamo wa CCM si wa Lowassa.

Nitajaribu kutoa mfn tu.. Tunafahamu Ukawa watu waliokuwa wako mstari wa mbele kutetea serikali 3 ni Tundu Lissu na Jussa hawa watu walijenga hoja zao na hata tukisoma maandishi au hata kuangalia clips mbali mbali utaona ni kwanini wanatetea serikali 3.

Na pale mtu atakaposema kuwa Tundu au Jussa misimamo yao ni Serikali 3 mtu unaelewa kwanini ni hivyo lakini inapotokea mtu akasema kuwa Mh. Msingwa au Mh Mhonga msimamo wake ni serikali 3 huyu mtu unakuwa unamuonea kwani huo msimamo wa Ukawa ambao hawa waheshimiwa wengine wamelazimishwa kufuata, kitu ambacho mimi nakiona si sawa kwa pande zote mbili maana wabunge hawakuwa uhuru kutoa mawazo yao bali mawazo ya viongozi wa vyama vyao.

Lakini pamoja ya hayo nimeuliza hapo awali kuwa je kwani msimamo wa Lowassa hauwezi kubadilika? Kama Lowassa metoka CCM na kwenda Chadema ni nini kitachomfanya hasibadilishe uamuzi wake wa awali?

Pia ndugu zangu Tanzania muhimu si serikali ngapi umuhimu ni kupata mhafaka kwa pande zote mbili ili kusudi kila upande uweze kutembea kifua mbele ukijivunia Mama yetu Tanzania.

Ng'wamapalala
Unakumbuka hapa""""

Mimi ninaheshimu uwezo wa Lowassa kwenye resource mobilization and mass mobilization kwenye uwanja wa siasa za Tanzania. Hakuna mwingine nchini zaidi ya Lowassa kwenye maeneo haya.

Hata wapinzani walikuwa wanampigia magoti aende kwenye vyama vyao kwa sababu wanafahamu uwezo wake mkubwa katika resource mobilization and mass mobilization kwenye uwanja wa siasa za Tanzania.

Nadhani ameamua kubaki CCM kwa sababu anahofia atapoteza vingi alivyonavyo!"""

Hizo ndio siasa
Haya, tuseme kuwa hizo sources hazitoshi au hazipo kabisa na hazina maana yeyote.
Twende kwenye logical analysis.
1. Kama mwana CCM just three weeks ago, ungemuweka kundi gani?
a. Nyerere's Fondation na kina Judge Warioba, Butiku, Humphrey Polepole.

b.Magamba michongo kama vile Rostam Aziz, Chenge,Iddi Simba et al.
c.Magamba mizigo kama vile Pinda,Membe, Bilal etc...
d.Wasiojali mabadiliko kama Deo Filikunjombe
Au kundi lolote like based on common characteristics bila kumtumia kabila and such things.
Halafu ujaribu kuangalia kama kambi hiyo, ndani ya CCM imeonyeshaje Hata siku moja ku-compromise na wapinzani kwenye suala la kikatiba.
Ukiacha hilo, umeshawahi kumsikia Lowassa akizungumzia suala lolote LA kikatiba, aki analyse policies in deep,au akiandika articles kama kina Msekwa, Nyerere,Jumbe,etc au Hata January?
Lowassa Ana papers alizoandika ambazo unaweza kutupatia?
So, why would you expect a "clip" or any other form of proof?
Also, kama unasema muundo wa serikali siyo muhimu sana,hapo nitakubaliana na wewe, lakini upande aliopo Lowassa sasa hivi mfumo wa serikali is the "nucleus" of their existence na kwenye campaigns tegemea hilo, apart from ufisadi ambao sina shaka Hata yeye anajua kuna vielelezo vitamwagwa.
 
Kwa bahati mbaya karibia viongozi wote wa CCM nimewaweka katika group moja ambalo ni wala rushwa na wezi wa mali za umma.
Mtazamo wangu kwa Mh. Lowassa huko wazi (kwa bahati mbaya nimekula propogada za CCM ) na ndo maana niko hapa kutafuta ukwel wa kujua ni kweli Lowassa ni fisadi? ni kweli Lowassa ni mla rushwa? je ni kweli Lowassa msimamo wake ni serikali 2?

Na katika kutafuata ukweli wa msimamo wa Lowassa kuhusu swala la serikali mbili bado sijaona msimamo wa Lowassa ila nilichoona ni maoni yake.

Maoni ya mtu na msimamo wa mtu ni vitu viwili tofauti.. Mtu anapokuwa na msimamo mara nyingi huwa habadiliki kirahisi lakini mtu anapotoa maoni/mapendekezo basi huyu mtu naweza kubadilika kutoka na mazingira aliyomo, na hiki ndicho ninachokiona kwa Lowassa na kinadhihirishwa na pale anaposema "ltuwaachie wananchi watoe maoni".

Kama nilivyosema hapo awali watu wenye msimamo wa serikali 3 ni Tundu Lissu na Jussa hawa wanaweza kubadilika (kutoka na hulka ya mwanadamu) lakini hawatabadilika kirahisi rahisi maana wana uhakika wa hoja zao zinasimama zenyewe na mpaka sasa hakuna hoja upande wa pili inayoweza kusimama dhidi ya hoja zao.

Swala la Lowassa kutoongea au kuto toa hotuba katika mambo mbali mbali hilo ni kweli na hata nilishawai kuliuliza humu ndani kuwa "inakuwaje Lowassa anawapenzi wengi wakati sikuwahi kumsikia wakati wa bunge la katiba akitetea wananchi, katika swala la Escrow alikuwa kimya, katika swala la unyanyasaji wa wananchi "na operation tokomeza majangili alikuwa kimya na nk haya mapenzi ya wananchi kwa Lowassa yanatoka wapi? Mpaka sasa sikuweza kupata majibu kama nilivyouliza kuhusu rushwa zake ni zipi??

Swala la vielelezo:Je watamwaga vielelezo vya Lowassa peke yake au watamwaga vielelezo vya kila mtu aliyekula rushwa? Kwa sasa hivi ndani ya CCM hakuna kiongozi safi na hili hata wananchi wanalifahamu sasa sijui kama hivyo vielelezo vitawashtua wananchi hawa ambao Richmond haikuwashtua na Lowassa alirudii Bungeni kwa kishindo.

Chenge amepita kwa kishindo, Mama Tibaijuka anaye ameshinda kwa kishindo hivi unafiri swala la rushwa na ufisadi bado ni kikwazo kwa watanzania? Kwa sasa watanzania tumeisha kuwa sugu na ufisadi hata ungesema Lowassa amevuja benki na kuiba kama watu wameamua kumchagua watamchagua tu.Wananchi hawachangui wasafi kama wangekuwa wanachagua wasafi leo hii Dr. Slaa angekuwa Ikulu.
 
Mkuu,
Mimi nadhani unajaribu kutetea hoja ambazo hazina nguzo inazozifanya zisimame kwenye muktadha wa hoja ya msingi.

Tukubaliane tu kuwa, Lowassa mpaka sasa ni muumini wa Serikali mbili na amepiga kura kukubali Katiba Inayopendekezwa. Kama kwa sasa amebadilisha fikra baada ya kuhamia CHADEMA, hili ni suala jingine pamoja na kwamba mpaka sasa hatujasikia tamko lake la kubadilisha fikra kuhusu muundo wa Serikali ya Muungano.

Hizi hoja za kusema, alipiga kura ya kuikubali Katiba Inayopendekezwa kwa sababu huo ulikuwa ni msimamo wa CCM ni kujaribu kuzikimbia hoja za msingi.

Kama kweli Lowassa alikuwa hakubaliani na Katiba Inayopendekezwa kwa nini hakutoka nje ya bunge kama baadhi ya wabunge wengine wa CCM walivyofanya, kwa mfano, Bulaya, Filikunjombe.

Kama unataka ushahidi zaidi wa utetezi wa Lowassa kuhusu serikali mbili na siyo serikali tatu, angalia hii video yenye mahojiano yake na Swahili TV.

Asante ana kwa video yako.. Ila swali langu kwako je hii video umeiangalia kweli? Katika hiyo video hakuna msimamo wa Lowassa wa serikali 2 bali ni maoni yake na anasema sababu ya kukataa hizo serikali 3 ni uwogo wa vita ambayo inaweze kutokea (propoganda za CCM kama tulivyozoea) na pia anasema "ninaomba Mungu apishe mbali hata kama tutakubaliana na serikali hizo.." hapa unaona kuwa huyu tayari kubadilika..

Swala la akina Esther Bulaya: Jamani tufike sehemu tuwe wakweli hivi nani hasiyejua kuwa swala serikali mbili ni msimamo wa CCM na serikali 3 ni Ukawa? Hivi katika akili zako unaweza kukubali kweli kuwa wanachama wote wa CCM walitoa mawazo yao huru na kupendekeza serikali 2 au wana Ukawa wote walitoa maoni yao kwa huru na kupendekeza serikali 3? Kama ni kweli basi taifa letu sisi sote ni matahira na hakuna Taifa hapo. Maana Taifa linahitaji watu wenye maono tofauti huwezi kujenga taifa kama unakuwa watu wenye maono sawa, mawazo sawa, mitazamo sawa, wote ni kusema ndio au hapana, na nk ili taifa halipo katika hii dunia.

Na ndio maana nilawahi kusema kuwa mchakato uliharibiwa na wanasiasa baada ya kuingiza uvyama.
 
Last edited by a moderator:
Asante ana kwa video yako.. Ila swali langu kwako je hii video umeiangalia kweli? Katika hiyo video hakuna msimamo wa Lowassa wa serikali 2 bali ni maoni yake na anasema sababu ya kukataa hizo serikali 3 ni uwogo wa vita ambayo inaweze kutokea (propoganda za CCM kama tulivyozoea) na pia anasema "ninaomba Mungu apishe mbali hata kama tutakubaliana na serikali hizo.." hapa unaona kuwa huyu tayari kubadilika..
Alinda, ninavyofahamu na kulingana na ripoti ya mwanzo ya Tume ya Warioba, hata Kikwete mwenyewe awali alikubaliana na muundo wa serikali tatu. Tume ilishangazwa sana na msimamo huo wa Kikwete ulivyobadilika ghafla siku alipohutubia Bunge Maalum La Katiba na kama sikosei hii ndiyo ilikuwa sababau kubwa iliyolisukuma taratibu na kanuni za BMLK kubadilishwa na ripoti ya kamati kusomwa kwanza kabla ya hotuba ya Kikwete. Kulikuwa na woga kwamba kama Warioba angesoma hiyo ripoti na kulitolea ufafanuzi baada ya Kikwete kulihutubia BMLK kungetokea na hali ya sintofahamu ndani ya bunge hilo na si ajabu wabunge wengi wangeafiki ripoti hiyo.

Swali ambalo wengi walibaki wakijiuliza ni kitu gani kilikuwa nyuma ya kitendo cha Raisi kuisaliti tume aliyoiunda na aliyofuatilia kazi yake hatua kwa hatua na kubariki mapendekezoi yake kipindi chote! There was something very fishy behind all this na hicho kitu tutaweza kukijua tu hawa walaghai watakapotolewa madarakani mwezi Oktoba. Ndio maana ujio wa Lowassa Chadema/UKAWA unawapa kiwewe CCM kwa kiwango hiki tunachoshuhudia.
 
Last edited by a moderator:
Hivi ni lipi na wapi Lowassa alitamka mambo ya serikali 2 au 3?

Huu uumini wa Lowassa wa serikali mbili hauwezi kubadilika kuwa serikali tatu?

Kama huyu Lowassa amezaliwa na kulelewa na CCM lakini leo hii kahama CCM je kinachomshinda ni nini kuwa muumini wa serikali 3?

Hivi wakati anajiunga na Ukawa si alifahamu kuwa Ukawa wanapigania katiba ya Wananchi ambayo ni rasmu ya Warioba?

Simpendi Lowassa, lakini napenda kumhukumu kwa haki si kwa maneno ya kulishwa na CCM Kama ni mla rushwa tuambiwe ni rushwa ya nini, ni lini ilitokea na ni wapi na serikali ilimchukulia hatua gani na kama serikali haikuchukua hatua tuambiwe ni kwanini? zaidi ya hapo yatakuwa ni majungu ya akina Nape und co.

Kwenye red: Mjini Dodoma wakati wa Bunge Maalum la Katiba.

Kwenye blue: Lowassa, kwa maneno yake, hakuhama CCM kwa sababu ya serikali 2 au 3. Au Hakuhama CCM kwa sababu hakubaliani na sera zake. Kilichomkimbiza CCM ni jina lake kukatwa Dodoma. Basi! Na hataki kuwa kwenye Chama chochote ambacho hakitampitisha kuwa mgombea wa urais. CCM wamekata jina akaondoka. Kaingia CHADEMA na washirika na kupewa kiti cha enzi!

Na kujibu swali lako kwenye blue, kama Lowassa atakubaliana na UKAWA kuhusu serikali 3, watu watakuwa na haki ya kuhoji dhamira ya yeye kufanya hivyo sasa na sio wakati UKAWA inaundwa. Kumbuka UKAWA ni umoja wa vyama vinavyopinga kile Lowassa na wenziwe walichopitisha Dodoma. Na huko nyuma hakusema chochote wakati Lipumba na wenzake wanatoka nje. Leo hii anatumia UKAWA kama daraja la kufikia azma yake ya kwenda Ikulu, na sio mambo ya serikali 3.

Kwa ufupi bado hii saga ya Lowassa inaacha maswali mengi sana.
 
Kwenye red: Mjini Dodoma wakati wa Bunge Maalum la Katiba.

Je unaweza kutupa andishi lake au clips yake ni nini alichangia kuhusu serikali 2/3? Si ulizi hivi kwa ubaya bali ninapenda kusikia alisema nini. (sikumbuki kama alichangia kitu chochote katika bunge la katiba labda kwenye vikao vyao)

Kwenye blue: Lowassa, kwa maneno yake, hakuhama CCM kwa sababu ya serikali 2 au 3. Au Hakuhama CCM kwa sababu hakubaliani na sera zake. Kilichomkimbiza CCM ni jina lake kukatwa Dodoma. Basi! Na hataki kuwa kwenye Chama chochote ambacho hakitampitisha kuwa mgombea wa urais. CCM wamekata jina akaondoka. Kaingia CHADEMA na washirika na kupewa kiti cha enzi!

Kwa bahati mbaya au nzuri hizi ndio siasa za Tanzania na hawa ndivyo watanzania walivyo kuna viongozi wengi na wagombea ubunge/udiwani wenyeviti wa vijiji wanahama kutoka chama kimoja kwenda chama kingine si kwa ajili ya sera au ilani ya chama fulani au si kwa kwa ajili ya kupenda kuwatumikia watanzania bali ni kwa ajili ya matumbo yao na famili zao kwa hili tusimhukumu Lowassa peke yake bali tuwahukumu wote waliohama vyama vyao kwa sababu za kukatwa katika chaguzi mbali mbali. Niliwahi kusikia tetesi (ila sijui kama ni kweli au la) kuwa Rais Kikwete naye alishajiandaa kuhama chama kama wasingepitishwa kugombea urais, Mh Sitta naye alikuwa ahame ili kugombe rais kupitia chadema ila walimshawishi kubaki CCM kwa ahadi ya uwaziri kwa hivyo utaona kuwa hii ni hulka ya wanasiasa wetu.

Na kujibu swali lako kwenye blue, kama Lowassa atakubaliana na UKAWA kuhusu serikali 3, watu watakuwa na haki ya kuhoji dhamira ya yeye kufanya hivyo sasa na sio wakati UKAWA inaundwa. Kumbuka UKAWA ni umoja wa vyama vinavyopinga kile Lowassa na wenziwe walichopitisha Dodoma. Na huko nyuma hakusema chochote wakati Lipumba na wenzake wanatoka nje. Leo hii anatumia UKAWA kama daraja la kufikia azma yake ya kwenda Ikulu, na sio mambo ya serikali 3.
Kwa ufupi bado hii saga ya Lowassa inaacha maswali mengi sana.

Ni kweli watu wana haki ya kuhoji na ni vizuri watu wakahoji na wakihoji tunategemea kupata majibu kutoka kwa mhusika na hii ndio Tanzania ninayoitaka ya watu kuhoji, watu kutokosagwa kama kondoo na nk. Ila tukumbuke Lowassa si Biblia kuwa habadiliki, Lowass ni binadamu na binadamu tunabadilika kutokana na watu waliotuzunguka na mazingira tunayoishi hivyo basi kama Lowassa atabadilika ni jambo jema na nzuri na ndivyo tunavyotegemea maana hatutegemei Lowassa kuibadilisha Ukawa bali Ukawa kumbadilisha Lowassa.
 
Kwenye red: Mjini Dodoma wakati wa Bunge Maalum la Katiba.

Kwenye blue: Lowassa, kwa maneno yake, hakuhama CCM kwa sababu ya serikali 2 au 3. Au Hakuhama CCM kwa sababu hakubaliani na sera zake. Kilichomkimbiza CCM ni jina lake kukatwa Dodoma. Basi! Na hataki kuwa kwenye Chama chochote ambacho hakitampitisha kuwa mgombea wa urais. CCM wamekata jina akaondoka. Kaingia CHADEMA na washirika na kupewa kiti cha enzi!

Na kujibu swali lako kwenye blue, kama Lowassa atakubaliana na UKAWA kuhusu serikali 3, watu watakuwa na haki ya kuhoji dhamira ya yeye kufanya hivyo sasa na sio wakati UKAWA inaundwa. Kumbuka UKAWA ni umoja wa vyama vinavyopinga kile Lowassa na wenziwe walichopitisha Dodoma. Na huko nyuma hakusema chochote wakati Lipumba na wenzake wanatoka nje. Leo hii anatumia UKAWA kama daraja la kufikia azma yake ya kwenda Ikulu, na sio mambo ya serikali 3.

Kwa ufupi bado hii saga ya Lowassa inaacha maswali mengi sana.
FJM sitakuita muongo lakini sidhani kama unasema kweli...ndani ya BMLK Lowasssa sikumbuki kama aliwahi kusimama na kutetea muundo wa serikali mbili ila kuna wakati aliongea akitoa maoni yake kuhusu dira ya taifa. Hakuongelea tu muundo wa serikali aligusia na mambo mengine kama elimu, umiliki wa ardhi, ajira na vitu kama hivyo na kwa kifupi ni kwamba alionesha kutokubaliana na sera za chama chake. Kuhusu muundo wa serikali tatu alitoa tu tahadhari kwamba kunaweza kuhatarisha uhai wa Muungano.

Hoja yako, kwamba akiunga mkono msimamo wa UKAWA wa serikali tatu watu watakuwa na haki ya kuhoji dhamira ya yeye kufanya hivyo sasa na sio wakati UKAWA inaundwa, haina mshiko. Nasema hivyo kwa sababu kama ameweza kuhama chama na kwenda chama kingine, hiyo pekee ni ishara ya kuunga mkono msimamo wa chama hicho ikiwa ni pamoja na muundo wa serikali tatu.

Huyo anayehoji kwa nini kabadilisha msimamo atakuwa ni mtu wa ajabu kwani ilitakiwa ahoji kwanza kwa nini kaikacha CCM na sababu mojawapo ni kwamba anao uhuru wa kufanya hivyo kwa sababu CCM si baba wala mama. Pili kama umefuatilia vizuri Lowassa amewahi kuhoji mengi tu ya sera za CCM k.m. kilimo kwanza ni moja ya mambo aliyoyakosoa nayo wazi wazi akidai ingefaa kama msisitizo ungekuwa elimu kwanza.

Na mwisho naomba nikutoe hofu kwa kukukumbusha kwamba Lowassa ni binadamu na si malaika, hajapigiliwa msumari hapo aliposimama hadi ashindwe kubadili msimamo. Duniani kote watu huenda na wakati na msimamo wa mtu leo hauwezi kuwa kigezo cha kumnyima haki ya kubadilika ikilazimu kulingana na hali ya wakati huo. Ingekuwa hivyo, watu wasingetafuta maendeleo kwa sababu maendeleo ni matokeo chanya ya mabadiliko.

FJM, binadamu huwa na wito na wito wa Luwassa ni kulifikisha Tanzania kwenye matumaini na kama hakuweza kupewa nafasi hiyo ya kutimiza ndoto yake ndani ya CCM akaamua kupitia chama kingine, kaharibu nini? Si bado ni mwananchi mwenzetu hapa hapa Tanzania, je kuwa na nia ama dhamira ya kufanikisha kitu ni kubaya? Mbonaa kila mtu anakuwa na mipango yake ya baadaye, kwa nini kwa Lowassa iwe nongwa? Kwa sababu humpendi? Huo sasa ni wivu.
 
Back
Top Bottom