CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

Ninasoma vema mjadala mzuri sana unaoendelea. Nichangiesenti sumuni

Tunahitaji mabadiliko, suala ni njia gani mabadiliko hayo yafanyike, kwa kuongozwa na nani na mwisho wake uwe nini

Mabadiliko yanaweza kuja kama upinzani na chuki dhidi ya (passive) au yanayohitajika kwa ulazima(passive aggressive) au yale ya nguvu (radical changes)

Vyama vya upinzani vimepita katika passive. Baada ya kuunda UKAWA umma ukaunga mkono kuelekea ‘passive aggressive' na kwasasa ni radical changes

Wpinzani wanapaswa si kukumbatia sherehe bali kujipanga. Tumeeleza mara nyingi kuhusu Pundits, strategists n.k.

Bandiko moja JokaKuu kazunguzia kidogo. Tutafafanua maana ya hili kadri tunavyosonga mbele

Prof Lipumba:
Katika press conference alisema 'nilishiriki kuunda UKAWA, kumkaribisha Lowassa na vikao vyote. Lakini dhamira inanisuta'

Bila kujali Prof amesimama upande gani wa ukweli au uongo kuna jambo amefanikiwa.
Kukiri ameshiriki hatua zote na kwamba nafsi inamsuta ilikuwa muhimu sana kwake

Kila anapoulizwa swali, jibu lake ni' ndiyo na nafsi inamsuta.
Kwa msingi huo, maswali yaliyotarajiwa yanakufa na kilichobak watu kusema hili au lile kuhoji uadilifu wake n.k.

Haya nikwa sababu approach yake kisiasa ilikuwa nzuri ‘ujumla'

Mansour Himid
ni mwanasiasa tunayetofautiana naye katika msimamo wake wa kuisumanga Tanganyika ingawa sote ni waumini wa S3.

Sisi tukiamini serikali 3 ni suala la mfumo na fairness, yeye akiamini ni suala la uonevu waTanganyika

Pamoja na tofauti zetu, kuna jambo amelifanya ambalo kisiasa ni zuri.
Baada ya kufukuzwa alichukua muda wa kipindi cha mpito(transition period)

Alipojiunga CUF, katika mikutano amekikiri kuwa sehemu ya mfumo uliokandamiza na uliowahukumu wapinzani kihila n.k.
Na kila mara amesema anaomba mungu na wananchi wamsamehe.Tena husema hadharani

Focus ya watu inaondoka katika kumtazama kama mhaini, inalenga kumtazama kwa mwana mpotevu na kusikiliza anasema nini, anajutia nini na anashauri nini.

Hakabiliani na maswali reja reja kwasababu alifanya approach ya jumla kama Lipumba

Tunafahamu siasa zetu si za sera wala itikadibali personality. Hilo si tatizo kubwa ukilinganisha na mfumo usiotaka mabadiliko wala kubadili mitazamo ya watukuhusu chaguzi.

Hivyo, mabadiliko yakuondoa ‘tembo' chumbani yanahitajika

Inaendelea
 
Sehemu ya II

Yapo mawazo na maoni tofauti kuhusiana na yanayoendelea.

Wapo wanaopinga ujio na wengine wakiunga mkono.

Kikubwa zaidi ni njiazinazotumika, kanuni , mitazamo ya kijamii kama maadili,itikadi na misingi.

Tofauti si mapungufu ni jambo lenye afya

Katika tofauti yapo ya kujifunza kutoka kila upande. Kwa wengine, kinachoonekana ni wapinzani kupokea ‘receive' ujio na wala si ‘accomodate''ujio. Unaweza kumpokea mgeni kwasababu tu amekuja pengine na magunia ya mahindi.

Unapoamua kumu –accommodate ni tofauti. Kwa tafsiri ndogo ‘accommodate is defined as fit in with wishes or needs of'
kwa Kiswahili,ni kuhifadhi awaye ili alingane na matakwa au mahitaji ya mahali au eneo husika

Maswali ya kujiuliza

Je, wapinzani wame ‘receive au wame accommodate' ujio uliopo?

Je, wapinzani wana pundits na strategist wanaoangalia mambo kwa upana wake?

Mfumo uliopo haujafa na wala haujakataa tamaa, unapigana katika kujilinda.

Ni kazi ngumu lakini wapo tena vema. Je,wapinzani wamejipanga kukabiliana na changamoto zinazoambatana na ujio?

Je,wapo tayari kukabiliana na chagamoto mpya kutokana na mabadiliko yanyowakumba.

Ikumbukwe, changamoto ni pamoja na distractions ambazo ni ni halali kimkakati kuwakwaza, na ni halali kuzizungumzia

Tarehe 26 August 2011 hapa duru tliandika bandiko la kwanza kuhusu damage control katika uzi huu

https://www.jamiiforums.com/great-thinkers/167157-duru-za-siasa-mgongano-wa-mawazo.html

Inaendelea...
 
Na pia, si suala la mikutano mikubwa au maandamo tu, ni suala la kuangalia kwa ukubwa na upana wake.

Tumemzungumzia Lipumba na Mansour hapo juu

Ingawaje wapo wasiokubaliana na mitazamo tofauti, kuna wakati misingi na kanuni haziwezi kuepukwa na hapa ndipo tunauliza , je, sehemu hii ya bandiko la Mzee Mwanakijiji halina funzo lolote linaloonekana?

Kwa Upande wa Mhe. Edward Lowassa
1. Mheshima Lowassa atambue na kukubali hadharani (publicly) makossa ambayo aliyafanya kama kiongozi na akiangalia leo kwa mwanga wa umbali wa historia aombe radhi taifa kwa sehemu yake na kuwa yuko tayari kujenga iman na kuahidi hayatotokea tena chini ya uongozi wake.

Ni lazima aoneshe unyenyekevu wa kukubali nafasi yake na makosa yoyote ambayo yalifanyika wakati wake kama kiongozi mkuu wa Serikali; haitoshi tena kutupa lawama kwa watu wengine.

Itakuwa hatua ya kwanza kuanza kuaminiana;

2. Alaani waziwazi na hadharani vitendo vya serikali kuminya upinzani na kuomba radhi kwa ukimya wake wakati wapinzani wananyanyaswa na vyombo vya dola umeacha doa kubwa sana la kuweza kumwamini;

Ahadi nyingine ambazo tungependa azitamke hadharani na tujue kuwa zitakuwa ni sehemu ya ahadi zake kama Mgombea wa Urais kupitia CDM.

Mgombea wa Urais anayebeba matamanio na ahadi za vyama vya upinzani ni lazima asimamie mambo yale ambayo Upinzani Tanzania umesimamia miaka hii yote.

Litakuwa ni kosa kubwa na usaliti wa harakati za upinzani nchini kwa mgombea wake wa Urais kutosimamia wazi, hadharani na bila utata hoja kuu za upinzani nchini.

Kwa vile Lowassa ndiye ambaye CDM na vyama washirika wamekubaliana ni muhimu na lazima kutangaza hadharani kuwa atasimamia mambo yafuatayo ambayo tayari yamepaziwa sauti na CDM na vyama vingine hasa ndani ya miaka hii mitano.Atakaposhika Madaraka ya Rais;

1. Tungependa aikane Katiba ile na kuahidi atanzisha mchakato sahihi, bora, wa wazi, na utakaokidhi matarajio ya Watanzania kuhusiana na Katiba Mpya.

Mchakato huu ujao utahakikisha baadhi ya mambo yanaamuliwa kwanza kabisa kabla ya kura ya maoni

2. Ataanzisha uchunguzi wa Kimahakama (Judicial Inquiries) ya matukio ya mauaji ambayo yametokea katika mazingira ya kisiasa – wakati uliopita na wakati huu wa kampeni za Uchaguzi - ili kuhakikisha ukweli unajulikana na sheria inafuata mkondo wake kwa wahusika;

3. Serikali yake italeta miswada ya mabadiliko ya Sheria mbalimbali au miswada ya sheria mpya ambazo zimekuwa ni tatizo kwa taifa kwa miaka hii yote.

Miswada hii italetwa katika kikao cha mapema zaidi baada ya Bunge Jipya kuapishwa. Baadhi ya Sheria ambazo miswada yake itatakiwa kuletwa mara moja ili kuliondoa taifa na masalio ya sheria mbovu za utawala wa CCM na ambayo Lowassa ataahidi hadharani na wakati wa kampeni italetwa mapema ni ile inayohusu:

- Mabadiliko ya Sheria ya Usalama wa Taifa ya 1996

- Mabadiliko ya Sheria ya Usalama wa Mitandao ya 2015

- Sheria ya Uhuru wa Habari na Ulinzi wa Wafichua Maovu (Whistleblower Protection ACT)

- Mabadiliko ya Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa ya 2007

- Mabadiliko ya Sheria ya Jeshi la Polisi ya 2007

- Kupitia Sheria zile au Vipengele 40 ambavyo vilioneshwa na Tume ya Jaji Kisanga kuwa vinahitaji mabadiliko.

Ndani ya Mwaka mmoja hili liwe limetimizwa ili kuondoa Sheria zote zilizopitwa na wakati vitabuni
- Na sheria nyingine ambazo zinaonekana ni kikwazo katika kutengenza utawala bora

Endapo haya yatafanyika mapema kuelekea kampeni, na tukaona kuwa kweli hawazungumzi tu bali wako tayari kutenda basi hata sisi wengine ambao tunasita kutoa mkono wetu wa pongezi au kudandia treni la Lowassa tutakuwa tayari kuwaunga mkono na kufanya kila jitihada kuhakikisha kuwa Lowassa anachaguliwa kuwa Rais kwani atakuwa ametujengea imani kidogo na viongozi wa CDM nao watakuwa wametupa mwanga kuwa kweli wanaamini katika hii "nafasi ya pekee".

Kinyume cha hapo wengine bado tuna mioyo ya kusita sita. Hatujaona sababu au vitendo vya kutuaminisha kuwa pande hizi mbili kwel zinaamini katika kuiondoa CCM madarakani mwaka huu. Kama kweli wanaamini basi ramani ya kuunganisha fikra za wapinzani ndiyo hii.

Umoja wa Kweli Ndio Ushindi wa Kweli
Na kwa hili tunasema, hata kama watu hawakubaliani , wapinzani wana namna mbili, kufanya biashara ya ‘reja reja au jumla'

Tusemezane

MBINU NA CHANGAMOTO ZA CHAGUZI

Chaguzi huambatana na mbinu , mikakati na changamoto

Chaguzi huwa na makundi ya wapiga kura. Kwa hali ya kisiasa yapomakundi yafuatayo

(1) Kundi linalopiga kura ya hasira- hili ni lile lisilo naupande, lilichoshwa na hali iliyopo

(2)Kundi la wanachama watiifu, hili linachagua tu kutokanana vyama iwe ni CCM, UKAWA au kingine

(3) Kundi lenye mashaka- hili halina uhakika lisimame wapi namara nyingi huangalia hoja ingawa si jambo linalotazamwa sana ukilinganisha na personality

CCM inategemea makundi 2 na 3 kwasababu tayari ni mwathirika wa kundi la 1

Wapinzani wana ‘advantage' ya makundi yote. Ushindani upo kundi la 3 litakaloamua nani anashinda majimbo au dola

Wapinzani kama ilivyo kwa CCM, wana ‘disadvantage'.

Kwanza, uwezowa kufikia jamii una vikwazo tukijua CCM ina mtandao wa wakuu wa mikoa na wilaya na rasilimali za umma.

Pili,CCM wanaserikali inayomiliki vyombo muhimu.

Mfano, zipo taasisi za nishati zinazolalamikiwa kutotenda haki kwa maagizo ya serikali ili kuwanyima wananchi habari

Vyombo vya habari vinavyoegemea CCM, na vyombo vya dola kutumika vibaya

Ushindi hautaamuliwa kwa hesabu za kura, yapo mengine ambayo kama hayataangaliwa yatabadili mwenendo wa uchaguzi

Kwa mfano,hatujawahi kupata majibu ya kwanini watu wajiandikishe kwa asilimia 70 , wapiga kura wawe asilimia 30.

Kuna nini kinaendelea ambacho serikali au tume ya uchaguzi imeshindwa kubaini?

Mfumo wa pili , BVR, je, umehakikiwa kufanya kazi kamailivyokusudiwa?

Kukiwa na matatizo ya kifundi au ‘kufundwa' itakuwa ni kwa maumivu ya wapinzani

Lipo suala la ‘voters suppression' kusudio ni kuzuia watu wasitumie haki ya kura kwa udanganyifu kama ule wa 1995 watu walipoambiwa siku ya kwanza ni CCM na ya pili wapinzani

Au inaweza kuwa vitisho kwa wapiga kura (2010) kwa jeshi kutoa tamko, au kutumika nguvu za dola kwa namna yoyote.

CCM wanakiri hali ngumu inayowakabili. Istegemewe CCM itatoa dola au bunge au vyote katika kisahani cha dhahabu.

Itapigana hadi tone la mwisho ikitambua kuwa KANU imetoweka kama ilivyo UNIP

Kitakachosaidia wapinzani ni ushindi usio na shaka ‘decisive victory'.

Itawezekana wakijiweka vema kupambana na hila, kukabiliana na hoja, kujenga hoja na kujibu hoja.

Kuzuia uharibifu kwakushambulia na si kujilinda ni muhimu kwao.

Kuwepo na uthubutu ‘courage' ya kupambana na changamoto si chaguo ni lazima kwa wapinzani

Kama kuna kitu ambacho upinzani unapaswa kukipigania kufa na kupona ni kuhakikisha wote waliojiandikisha kupiga kura wanajitokeza tarehe 25 na wanapiga kura bila mizengwe yoyote. Ushindi wa 62% alioupata JK mwaka 2010 huku voters turnout ikiwa ni 42% pekee inatoa ujumbe kwamba endapo turnout ingekuwa 70% au hata 80% pengine tungekuwa tunaongea lugha nyingine sasa hivi!

Na hili wanapaswa kulisimamia kwa umakini sana hususani sasa tunapotumia huu mfumo wa BVR! Kwa matukio yaliyoripotiwa hivi karibuni ya baadhi ya viongozi kukamatwa wakikusanya kadi za kupigia kura kutoka kwa wananchi na kuzinakili namba ni dalili mbaya juu ya mambo yatakayotokea tarehe 25.
 
Hili la kuhakikisha watu wote waliojiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ni gumu kutokana na mfumo wa uchumi,kijamii na kusiasa ulipo Tanzania na mwamko mdogo wa kisiasa kwa watanzania walio wengi.

Wakati wa mchakato wa uandikishaji wa vitambulisho vya kupigia kura niliwahi kufanya uchunguzi wangu mdogo kubaini ni kwanini mwaka awamu hii watu waliojitokeza ni wengi kuliko 2010, wengi walionekana kuhitaji vitambulisho tu kwa kuwa vinatolewa bure na mfumo mpya wa kutumia mashine(BVR) umechangia kuongezeka kwa idadi ya watu wakitaka kuona tofauti ya sasa na kipindi kilichopita, hii inaweza kuonekana kama ni kushangaa tu kama ilivyo hulka ya walio wengi wetu huku wengine wakisema wanavihitaji kwa ajili ya shughuli ndogo ndogo kama usajiri wa laini za simu na kupata dhamana kwenye taasisi za fedha nk.

Nikiangalia kwenye mfumo wetu wa kimaisha/kiuchumi ni kwamba mtu hawezi kuacha shughuli yake ambayo ndio inamuingizia kipato cha kulisha familia na kwenda kupanga foleni kwa ajili ya kitu kisicho na faida ya siku hiyo na matokeo yanayoweza kupimika kwa wakati huo, pia ikumbukwe kuwa watanzania walio wengi wanafanya kazi binafsi ambazo kama hawatafanya basi siku itakuwa imeenda vibaya.

• Wafanyakazi wanaoshinda maofisini mbali na nyumbani(sehemu walizojiandikisha).

• Wasafiri wanaotoka sehemu moja kwenda nyingine, hawa utawapata kwenye mabasi makubwa, meli, ndege/ madereva wa mabasi,malori walioko mbali. nk.

• Wanafunzi wa vyuo mbalimbali waliopo nje ya vituo walivyojiandikisha.

• Watumishi wa sekta ya afya na watu watakaokuwa wakipata huduma ya afya siku ya kupiga kura/wagonjwa.

• Wale wasiojisikia kupiga kura.

• Wale watakaopiga kura pande mbili za ccm na ukawa.

• Watakaopatwa na dharura za ghafla siku ya upigaji kura.

• Wafanyakazi wa taasisi binafsi ambao hutegemewa kuleta faida ya taasisi hizo kwa siku, Hapa waajiri wengi hawatakuwa radhi kupata hasara ambayo haina nafuu ya kodi.

Hayo mambo niliyoyataja yanaweza kuonekana sio muhimu ila ndio yanayochangia ushiriki wa wananchi kwenye kupiga kura kuwa hafifu.
 
Kama kuna kitu ambacho upinzani unapaswa kukipigania kufa na kupona ni kuhakikisha wote waliojiandikisha kupiga kura wanajitokeza tarehe 25 na wanapiga kura bila mizengwe yoyote. Ushindi wa 62% alioupata JK mwaka 2010 huku voters turnout ikiwa ni 42% pekee inatoa ujumbe kwamba endapo turnout ingekuwa 70% au hata 80% pengine tungekuwa tunaongea lugha nyingine sasa hivi!

Na hili wanapaswa kulisimamia kwa umakini sana hususani sasa tunapotumia huu mfumo wa BVR! Kwa matukio yaliyoripotiwa hivi karibuni ya baadhi ya viongozi kukamatwa wakikusanya kadi za kupigia kura kutoka kwa wananchi na kuzinakili namba ni dalili mbaya juu ya mambo yatakayotokea tarehe 25.
Hili la BVR ni muhimu sana

Kuna taarifa kuwa BVR inatumika kama 'data base' na hakuna mwenye uhakika nani ana control nayo
Kuna uwezekano wa kucheza na electronic gadget watu wakapiga kura mambo yakaenda tofauti

Ndio maana tunauliza, hawa wapinzani wapo barabarani, wanajua nini kinaendelea nyuma ya pazia?

Kuna kila ushahidi kuwa tume imekuwa inafanya kazi kwa maelezo ya wakuu
Wakisema neno tume inadaka na kufanyia kazi

Pili, lazima wawe macho na walaghai hasa kuhusu shahada. CCM ni wazuri sana wa kutengeneza 'mambo'

Uchaguzi ni ''more than a ballot box'' kwa CCM na ufundi walio nao, kuna maswali ya kujiuliza sana!

Inakuwaje watu wajiandikishe 70% kwa musimama katika foleni kutwa, halafu turn out iwe 42% kwa dakika 10 za kupiga kura?
Je, kuna maelezo yaliyowahi kutolewa na serikali au taasisi husika?
Lini tume ya uchaguzi imeongelea hilo? Je, wanajua au hawajui? Wametafuta chanzo au wameridhika na majibu waliyo nayo?
 
Hili la kuhakikisha watu wote waliojiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ni gumu kutokana na mfumo wa uchumi,kijamii na kusiasa ulipo Tanzania na mwamko mdogo wa kisiasa kwa watanzania walio wengi.

Wakati wa mchakato wa uandikishaji wa vitambulisho vya kupigia kura niliwahi kufanya uchunguzi wangu mdogo kubaini ni kwanini mwaka awamu hii watu waliojitokeza ni wengi kuliko 2010, wengi walionekana kuhitaji vitambulisho tu kwa kuwa vinatolewa bure na mfumo mpya wa kutumia mashine(BVR) umechangia kuongezeka kwa idadi ya watu wakitaka kuona tofauti ya sasa na kipindi kilichopita, hii inaweza kuonekana kama ni kushangaa tu kama ilivyo hulka ya walio wengi wetu huku wengine wakisema wanavihitaji kwa ajili ya shughuli ndogo ndogo kama usajiri wa laini za simu na kupata dhamana kwenye taasisi za fedha nk.

Nikiangalia kwenye mfumo wetu wa kimaisha/kiuchumi ni kwamba mtu hawezi kuacha shughuli yake ambayo ndio inamuingizia kipato cha kulisha familia na kwenda kupanga foleni kwa ajili ya kitu kisicho na faida ya siku hiyo na matokeo yanayoweza kupimika kwa wakati huo, pia ikumbukwe kuwa watanzania walio wengi wanafanya kazi binafsi ambazo kama hawatafanya basi siku itakuwa imeenda vibaya...

...Hayo mambo niliyoyataja yanaweza kuonekana sio muhimu ila ndio yanayochangia ushiriki wa wananchi kwenye kupiga kura kuwa hafifu.
The Intelligent, sijui unafuatilia kwa ukaribu kiasi gani takwimu zinazotolewa wakati wa Uchaguzi Mkuu na mwitikio wa wananchi kila baada ya miaka mitano. Ukweli ni kwamba idadi ya wanaojiandikisha kupiga kura imekuwa ikiongezeka kila uchaguzi ila yaliyotokea mwaka 2010 kwa sababu ambazo hadi leo hazijaweza kutolewa ni kweli yalizua maswali kuliko majibu. Ni mwaka huo pekee ambapo idadi ya wapiga wanaodaiwa kujitokeza ilikuwa asilimia chini ya hamsini ya idadi ya waliojiandikisha tofauti kabisa na miaka ya nyuma. Hebu tafakari hili jedwali hapa chini;

[TABLE="class: cms_table"]
[TR]
[TD="align: center"]Mwaka[/TD]
[TD="align: center"]Waliojiandikisha[/TD]
[TD="align: center"]Waliopiga kura[/TD]
[TD="align: center"]Asilimia[/TD]
[TD="align: center"]Kura halali[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="align: center"]1995[/TD]
[TD="align: center"]8,928,826[/TD]
[TD="align: center"]6,846,681[/TD]
[TD="align: center"]77%[/TD]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="align: center"]2000[/TD]
[TD="align: center"]10,088,484[/TD]
[TD="align: center"]8,517,598[/TD]
[TD="align: center"]84.43%[/TD]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="align: center"]2005[/TD]
[TD="align: center"]16,407,318[/TD]
[TD="align: center"]11,365,477[/TD]
[TD="align: center"]72.4%[/TD]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="align: center"]2010[/TD]
[TD="align: center"]20,137,303[/TD]
[TD="align: center"]8,397,963[/TD]
[TD="align: center"]42.8%[/TD]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Linaloleta hofu kuliko hata hayo matokeo ya mwaka 2010 ni kukosekana kwa tathmini ya hali kama hiyo ilivyoweza kujitokeza; si Tume ya Uchaguzi, si serikali, si bunge, si vyama vya siasa, si wanaharakati, si wasomi...hakuna kikundi chochote kilichoweza kukaa kujadili, kutafakari na kutoa tathmini ya uchaguzi huo na kutoa sababu kwa nini hali kama hiyo ilijitokeza.

Kama ni kweli kuwa walioweza kujiandikisha mpaka sasa kupitia BVR ni zaidi ya milioni 22, hiyo ni sawa kabisa kwani inaendana na takwimu za nyuma na ilitegemewa iwe hivyo. Dai lako la watu kujiandikisha tu eti kwa lengo la kupata kitambulisho halina mantiki na si sahihi. Unaelezaje waliojitokeza kujiandikisha kabla ya BVR huko nyuma? Mbona siku ya kura waliojitokeza walikuwa ni wengi tu?

Kama alivyosema Mwalimu tuzidi tu kuwashawishi wote waliojiandikisha wajitokeze kwa wingi siku ya upigaji kura na kwa technolojia ilipon tuhakikishe kwamba hiyo idadi haitachakachuliwa. Tupange namna ya kuhakiki kwamba taarifa zinazofikishwa Tume ni sahihi kwa kila kituo cha kupigia kura, kila jimbo, kila mkoa ili kuziba kabisa mianya ya wezi wetu hawa waliokubuhu.
 
Mkuu Mag3

Rais Kikwete alipokuwa Songea aliwaambia wana CCM, uchaguzi wa mwaka huu utakuwa wa kihistoria na hivyo wajiandae.
Kauli hiyo ilitoka kabla ya Dodoma uchinjaji ulipofanyikia

Prof Lipumba alikaririwa katika video akisema ' ... hali ilivyokuwa ngumu na tulivyosaidiakuokoa jahazi'

Hayo mawili yanaonyesha kwa ufupi jinsi gani uchaguzi wa 2010 ulivyokuwa na ugumu na pengine kutupa mwanga wa idadi ya wapiga kura kwa kulinganisha na waliojiandikisha

Kwa Muktadha huo, serikali inajua nini kilitokea, lakini lengo si limefikiwa? Maelezo wanayo wenyewe

Tume ya uchaguzi inafahamu nini kilitokea, lakini lengo si lilitimia? Maelezo zaidi ya nini?

Wasomi wetu ndio kama Prof wa chuo kikubwa cha Tanzania Bensen Bannah.

Kazi ya taasisi tanzu ya CCM inayoitwa 'REJECT' au REDT kazi yao ni kupamba wagombea, kutoa tathmini za kununuliwa n.k.

Hatutegemei mtu aliyetengewa fungu la Ikulu kwa katiba mpya kama Bensen, kushugjulisha akili akijua ni 'mwajiriwa'

Lazima wapinzani watumie resource kuelimisha umma na kusimamia mwenendo mzima wa uchaguzi hasa upande wa wapiga kura.

Ipo hoja ya vyombo vya habari vya umma kutumiwa na CCM. Ni kweli lakini hiyo haiwezi kuwa suluhu ya tatizo.

Suluhu ipo ambayo naiandikia bandiko litakalopanda muda si mrefu wa jinsi gani wanaweza kutumia resource zao vyema hasa katika mawasiliano na umma kwa kutumia vyombo vya habari bila kusigishana na vile vya umma tena ikawa effective zaidi
 
Last edited by a moderator:
The Intelligent, sijui unafuatilia kwa ukaribu kiasi gani takwimu zinazotolewa wakati wa Uchaguzi Mkuu na mwitikio wa wananchi kila baada ya miaka mitano. Ukweli ni kwamba idadi ya wanaojiandikisha kupiga kura imekuwa ikiongezeka kila uchaguzi ila yaliyotokea mwaka 2010 kwa sababu ambazo hadi leo hazijaweza kutolewa ni kweli yalizua maswali kuliko majibu. Ni mwaka huo pekee ambapo idadi ya wapiga wanaodaiwa kujitokeza ilikuwa asilimia chini ya hamsini ya idadi ya waliojiandikisha tofauti kabisa na miaka ya nyuma. Hebu tafakari hili jedwali hapa chini;

[TABLE="class: cms_table"]
[TR]
[TD="align: center"]Mwaka[/TD]
[TD="align: center"]Waliojiandikisha[/TD]
[TD="align: center"]Waliopiga kura[/TD]
[TD="align: center"]Asilimia[/TD]
[TD="align: center"]Kura halali[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="align: center"]1995[/TD]
[TD="align: center"]8,928,826[/TD]
[TD="align: center"]6,846,681[/TD]
[TD="align: center"]77%[/TD]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="align: center"]2000[/TD]
[TD="align: center"]10,088,484[/TD]
[TD="align: center"]8,517,598[/TD]
[TD="align: center"]84.43%[/TD]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="align: center"]2005[/TD]
[TD="align: center"]16,407,318[/TD]
[TD="align: center"]11,365,477[/TD]
[TD="align: center"]72.4%[/TD]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="align: center"]2010[/TD]
[TD="align: center"]20,137,303[/TD]
[TD="align: center"]8,397,963[/TD]
[TD="align: center"]42.8%[/TD]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Linaloleta hofu kuliko hata hayo matokeo ya mwaka 2010 ni kukosekana kwa tathmini ya hali kama hiyo ilivyoweza kujitokeza; si Tume ya Uchaguzi, si serikali, si bunge, si vyama vya siasa, si wanaharakati, si wasomi...hakuna kikundi chochote kilichoweza kukaa kujadili, kutafakari na kutoa tathmini ya uchaguzi huo na kutoa sababu kwa nini hali kama hiyo ilijitokeza.

Kama ni kweli kuwa walioweza kujiandikisha mpaka sasa kupitia BVR ni zaidi ya milioni 22, hiyo ni sawa kabisa kwani inaendana na takwimu za nyuma na ilitegemewa iwe hivyo. Dai lako la watu kujiandikisha tu eti kwa lengo la kupata kitambulisho halina mantiki na si sahihi. Unaelezaje waliojitokeza kujiandikisha kabla ya BVR huko nyuma? Mbona siku ya kura waliojitokeza walikuwa ni wengi tu?

Kama alivyosema Mwalimu tuzidi tu kuwashawishi wote waliojiandikisha wajitokeze kwa wingi siku ya upigaji kura na kwa technolojia ilipon tuhakikishe kwamba hiyo idadi haitachakachuliwa. Tupange namna ya kuhakiki kwamba taarifa zinazofikishwa Tume ni sahihi kwa kila kituo cha kupigia kura, kila jimbo, kila mkoa ili kuziba kabisa mianya ya wezi wetu hawa waliokubuhu.

Mpo sawa wakuu,
Ila mm kuna jambo linanipa hofu kubwa sana kuhusu kura, nimeangalia cheating manipulation za kura kwenye kura za maoni za wabunge na madiwani wa CCM nimeogopa mno, nimemsikia Chegeni analalamika kuwa Kamani alikua anaongeza kura hadi manne kwa kituo, nikasema dah!!!! Kwenye chama ni haya je general election itakuaje?

Watu wengine wanapuuza haya mambo yanayoendelea kwenye kura za maoni za chama tawala na mauza uza yake, lakini ukiangalia kwa jichola tatu kuna cha kujifunza kinachoreflect General elections, hapo ndio namkubalia Nguruvi3 kwamba uchaguzi nizaidi ya kuhamasisha kupiga kura tu bali ni kujipanga kwa mikakati na mbinu. Ushindi hauji kiuwepesi kama wengine wanavyodhania. Bt hayo ngoja tuwaachie Elections strategists watuambie hizo mbinu na ufundi mwingine.
 
Tunafuatilia kwa ukaribu sana kura za maoni za CCM.

Kama wanaweza kucheza 'off side na rough' wakiwa wenyewe, hilo linaeleza kwa upana nje ya wigo wao wapoje

Wanachokifanya ni mazoezi, wakati wa mechi watakuwa na uzoefu mkubwa sana
Kitendo cha bunge kuwaongezea mamilioni kililenga 'kuwawezesha' kufanya yao, na ndicho kinaendelea

Uchaguzi unaporudiwa katika majimbo 5 inatosha kabisa kutoa picha kamili ya jinsi walivyo mafundi

Lakini pia tujiulize, uchaguzi wa serikali za mitaa unaosimamiwa na serikali ya CCM ulikuwaje

Tuliona uchakachuaji wa kiwango kizuri tu. Katika mazingira ya kawaida wapinzani wangesginda kwa 30- 40% au zaidi

Kule walikoshinda, kulikuwa na umakini wa wananchi wenyewe na ushindi haukuweza kutiwa maji 'chakachuliwa'

Hilo linatuambia kuwa, uwezekano wa kupata 50.1% kwa bao la mkono unawezekana kama wataachiwa upenyo

Muhimu ni kuhakikisha wapinzani wanashinda kiasi cha kushindwa kuchakachua

Wanasimamia uandikishaji na upigaji kura

Wanahamasisha kulinda shahada za wapiga kura

Wana mawakala wa kutosha na wa kuaminiwa

Wanatumia media si kueleza sera tu, bali udanganyifu mwingine unaoambata na chaguzi

Hapa pa media ndipo tutajadili muda si mrefu
 
MAZISHI YA MZEE KISUMO NA SIASA

KASORO ZINAZOCHAGIZWA NA UCHAGUZI

OMBWE LA BUSARA KUTOKANA NA USHAURI MBAYA

Waswahili husema kufa kufaana. Hayo ndiyo yanayotokea katikasiasa za Tanzania

Habari kubwa ni kuzuiwa kwa msafara mgombea wa UKAWA kuhudhuriamazishi ya mzee Peter Kisumo,Usangi-Mwanga

Mzee Kisumo ni mmoja wa wadhamini wa CCM. Ameshika nyadhifa serikali kama ukuu wa mikoa , uwaziri na Ubunge

Marehemu Kisumo ni kati ya ‘wanafunzi' wa Mwalimu Nyerere, pamoja na akina Marehemu Amri Jamal,Msuya,Warioba, Salimu Ahamed Kingunge kwa uchache wa kuwataja

Heshima ya Kisumo ndani ya CCM ni kubwa, akiwa mlezi wa wanasiasa kama Rais Kikwete, Lowassa na wengine

Inatosha kusema hata akina Slaa wakiwa CCM mzee alikuwa mwanadamizi na kiongozi wao

Yapo Mahusiano ya kijamii na kisiasa ya wanasiasa waliopo CCM na walioondoka

KIFO CHA MZEE KISUMO

Msiba wa Mzee Kisumo una sura ya kitaifa kwa kuzingatia mchango wake kama kiongozi wa aserikali miaka mingi iliyopita
taifa lililpokuwa changa likikabiliwa na Changamoto nyingi. Ni kati ya wale wasiotajwa katika kulifisi taifa bali kulihudumia

SAKATA LA MAZISHI
Msiba wa Kisumo ni wa familia kwa kuanzia. Ndugu wamempoteza mzee, duru tunatoa mkono wa pole kwa tukio hili

Pili, msiba wa Kisumo una uhusiano na CCM kutokana nafasi zake ndani ya chama kama udhamini .

Ukweli kuwa huu ni msiba wa watu wote alioishi nao, CCM ina nafasi ya kumuenzi mmoja wa waasisi wa Chama

Tena katika kipindi hiki CCM ikiporomoka, Kisumo ni role model ya watu waliosimamisha chama kwa uadilifu na kujitolea

Inaendelea.......
 
Sehemu ya II

SAKATA LA MAZISHI

Kutokana na nafasi yake katika jamii , msiba wa Kisumounagusa taasisi na vyama vya siasa .

Mfano, ni wiki chache tu, Mzee Kisumo naLowassa walikuwa chama kimoja
Haina maana kwa mahusiano ya muda mrefu kuvurugwakwasababu za kisiasa

Ingelikuwa faraja na umoja kwa wapinzani kutumamwakilishi kwasababu za nafasi ya marehemu katika ujenzi wa taifa

Lowassa kuhudhuria mazishi haliwezi kuwa shida. Tatizo nikuwa yeye sasa ni mgombea wa Urais na hatuna uhakika alikwenda akiwa na kofiagani, ya kuwakilisha upinzani au muombelezaji au Mgombea.

POLISI WASEMA MISAFARA HAIRUHISIWI

Taarifa ya Polisi iliyonukuliwa na gazeti moja inasema,Polisi hawakuruhusu msafara wa Lowassa na wapambe wake kwasababu ya umati utakaokuwepo

Polisi hawakueleza kwa ufasaha kwasababu, umati si sababu yakuzuia mikusanyiko.

Sababu inaweza kuwa ya kuhatarisha amani na usalama. Hakuna dalili kama msafara huo ungehatarisha amani.

Si mara ya kwanza vyama tofauti kukutana misibani naamani kutawala. Kama ipo sababu, waliyotoa haikidhi haja ya zuio

Kwa upande mwingine, familia ya Kisumo ingefadhaika endapoCCM wangechukulia msiba huo kwa wepesi

Lakini pia familia isingefarajika wakati wa majonzi kutumika kisiasa kwa pande hasimu kuanza siasa misibani

Hakukuwa na sababu za Lowassa kuambatana na msafara wawanachama waliovalia kichama katika msiba wa

Halikuwa kosa, bali busara zinaelekeza, lazima unyenyekevu utawale na si kila mahalipanatawaliwa na siasa.

Inaendelea
 
sehemu ya I

KUELEKEA UCHAGUZI

Wapinzani wanapaswa kuwa na busara kuelekea uchaguz

Hali kwa upande wa CCM si njema, hata hivyo, wameapa kutumia kila njia na goli la mkono kufikia malengo yao

Maswali, je polisi walitumia nguvu zao kwa busara? Jibu ni ndio na hapana
Ni ndio kwasababu, kwa mtazamo wetu eneo la msiba haliwezi kuwa eneo la siasa. Si kimaadili, kiutamaduni au kibinadamu.

Jibu la pili ni Hapana. Kwa maelezo yao, sababu walizotoa hazikidhi haja ya zuio.
Ni nyepesi zisizo na mashiko. Hivyo, kama lipo zuri, hilo lilitokea kwa bahati mbaya inayoweza kuonekana ni nzuri.

Je, Lowassa alipaswa kuhudhuria mazishi.
Jibu ni Ndiyo, akiwa raia ana haki hiyo. Akiwa ‘mwakilishi' kama ilikuwa ni hivyo ana haki hiyo

Je, Lowassa na timu yake walifanya jambo jema?

Kuhudhuria msiba ni jambo la faraja na la kibinadamu.

Msiba haupaswi kuwa sehemu ya siasa kwa kiwango kilichoonekana.

Ingawa hakuna kosa, kuna kukosekana kwa busara

WASHAURI

Tatizo la Lowassa kuambatana na timu yenye mavazi linaweza kuchangiwa na kukosekana ushauri.

Ombwe la ushauri ni hatari kuelekea uchaguzi. Tumesema uchaguzi si kuhesababu kura bali mahesabu ya kupata kura.

Katika mazingira yetu, unyenyekevu na busara ni sehemu ya kushinda nyoyo.

Lakini pia wapinzani watambue, vyombo vya dola vinatafuta sababu kuzuia nguvu inayoonekana kuielemea CCM

Hivyo, ni muhimu kutumia busara, kinyume chake wapinzani wanaweza kuwa katika wakati mgumu

Tumesikia tangazo la jeshi la Polisi kuzuia misafara,tumesikia tangazo la kamisheni ya mawasiliano dhidi ya ITV na Radio one

Hayo tutayajadili kwa kina, kwa ufupi,tujiulize. je, kile kinachoitwa Machinery of Governemnet (MoG) kimeanza kazi???
Tuajadili

Tusemezane
 
Nguruvi3,

..tatizo ccm huanzisha jambo au utaratibu fulani. Sasha wengine wakiiga na kuanza kuwazidi malaria basi ccm huleta vyombo cya dola kuzuia jambo hilo.

..ccm ndiyo waasisi wa utaratibu wa mazishi ya "kichama ". Wao ndiyo walioanzisha utaratibu wa kuvaa sare za chama kwenye misiba na kuvika majeneza bendera za ccm na vijana wa chama kuteka nyara shughuli za misiba.

..Kama ccm wanavaa sare zao kwenye misiba kwanini iwe makosa kwa waombolezaji wanachama wa vyama vingine kuvaa sare za vyama vyao?

..mimi simlaumu lowassa kwa kusindikizwa na umati wa watu kila anapokwenda. Hulu ni wakati wa uchaguzi, what do u expect??! Nitamlaumu na kumdharau kama atashindwa kuwafanya hawa wasindikizaji wawe wapiga kura.

..halafu huu umati na jinsi unavyokuwa mkubwa una effects zake ktk saikolojia ya wapinzani wa lowassa. Umati huu unawafanya ccm wafikirie mara mbili-'mbili kuhusu jinsi ya kukabiliana na ukawa/ccm/lowassa.

..lowassa amawatupia "chambo" ccm na polisi na wao wakakimeza. Polisi hawakupaswa kumzuia lowassa. Kitendo kile kimewafanya waonekane wanamuonea na kumuandama lowassa. Siku watakayompiga mabomu ndiyo watakuwa wamemtakasa machoni mwa wapenda mageuzi wa nchi hii na wanachama wenzake wa cdm. Kama utakumbuka mkutano mkuu wa cdm ulisheni wahanga wa ukatili wa namna mbalimbali wa polisi.

..busara ya lowassa ktk Sakata hili ni pale alipokataa agizo la polisi kwenda msibani bila washabiki wake waliokuwa wakimsindikiza. Kitendo kile kimejenga imani na ukaribu Kati yake na mashabiki wake.
 
mkuu upo sawa, ila naomba niongeze kdg,
at first nilivyosoma kwenye mitandao nilimlaumu sana Lowassa kwa kukosa busara kwa kuhamasisha watu waende nae msibani, huku ni kupolitisize msiba jambo ambalo si jema, nikasema loo huyu mzee vipi hajui huu ni msiba, nikafikiri sio jambo jema na busara kabisa nikadhania ameharibu.

baadae nilisikiliza taarifa ya habari nikagundua nilikosea kufikiri mwanzo maana nilimsikia akiwakataza wafuasi wake wasiambatane nae msibani, na akawaahidi atarudi Moshi kisha wampokee, lakini wafuasi wake walikataa kata kata kwamba nao wana3nda msibani, mpaka hapa huwezi kabisa kumlaumu Lowassa kama amekosa busara maana aliwazuia from begining kwamba jamani msinifuate, so hakukua na shida kabisa kwa upande wake maana alifanya jitihada zikashindikana.

polisi wangeweza kuwaruhusu wale watu lakini kule msibani wakawazuia wasiingie kanisani au popote penye eneo la msiba maana wako wengi, kitendo cha kuwazuia kilileta hisia za kuzuiwa kisisa kuliko uhalisia wa kimsiba zaidi.

Je Lowassa angewatosa wafuasi wake na kwenda mwenyewe baada ya kuzuiwa na polisi?? Jibu ni hapana, asingeweza kwend mwenyewe kwa hali ilivyokua mpaka pale wanazuiwa, alitumia busara na yeye kutokwenda baada ya watu wake kuzuiwa pale na polisi baada ya yeye kuwasihi toka airport wasimfuate. why? Kinadharia ingewauma sana kwamba Lowassa amewaignore na kuwaona hawafai, so kwa busara ile, wale watu walifarijika kwamba kumbe huyu Bwana yuko pamoj nao.

Mkuu Nguruvi3, hili jambo linamahusiani sana na zuio la polisi la maandamano, wakati huu UKAWA wanapomtambulisha mgombea wao, naomba uje na uchambuzi juu ya ZUIO LA POLISI KWA MAANDAMANO NA YANAYOFANANA NA HAYO, tujadili pamoja
 
Nguruvi3,

..tatizo ccm huanzisha jambo au utaratibu fulani. Sasha wengine wakiiga na kuanza kuwazidi malaria basi ccm huleta vyombo cya dola kuzuia jambo hilo.

..ccm ndiyo waasisi wa utaratibu wa mazishi ya "kichama ". Wao ndiyo walioanzisha utaratibu wa kuvaa sare za chama kwenye misiba na kuvika majeneza bendera za ccm na vijana wa chama kuteka nyara shughuli za misiba.

..Kama ccm wanavaa sare zao kwenye misiba kwanini iwe makosa kwa waombolezaji wanachama wa vyama vingine kuvaa sare za vyama vyao?

..mimi simlaumu lowassa kwa kusindikizwa na umati wa watu kila anapokwenda. Hulu ni wakati wa uchaguzi, what do u expect??! Nitamlaumu na kumdharau kama atashindwa kuwafanya hawa wasindikizaji wawe wapiga kura.

..halafu huu umati na jinsi unavyokuwa mkubwa una effects zake ktk saikolojia ya wapinzani wa lowassa. Umati huu unawafanya ccm wafikirie mara mbili-'mbili kuhusu jinsi ya kukabiliana na ukawa/ccm/lowassa.

..lowassa amawatupia "chambo" ccm na polisi na wao wakakimeza. Polisi hawakupaswa kumzuia lowassa. Kitendo kile kimewafanya waonekane wanamuonea na kumuandama lowassa. Siku watakayompiga mabomu ndiyo watakuwa wamemtakasa machoni mwa wapenda mageuzi wa nchi hii na wanachama wenzake wa cdm. Kama utakumbuka mkutano mkuu wa cdm ulisheni wahanga wa ukatili wa namna mbalimbali wa polisi.

..busara ya lowassa ktk Sakata hili ni pale alipokataa agizo la polisi kwenda msibani bila washabiki wake waliokuwa wakimsindikiza. Kitendo kile kimejenga imani na ukaribu Kati yake na mashabiki wake.

lowassa1.jpg

lowassa2.jpg

Matokeo ya kumzuia Lowassa asiende msibani ndio haya!

Nakubaliana na wewe kwa asilimia kubwa tu JokaKuu...kila nikijaribu kujiuliza mantiki ya polisi kumzuia Lowassa na msafara wake sipati jibu. CCM hofu kubwa imewashika na kitendo kama hicho ni katika muendelezo tu wa yale ambayo yamewafanya wananchi wengi kuamua kutowapenda kama si kuwachukia.

Kwa vitendo vyao hivyo wanadhani wanaudhoofisha upinzani, wakisahau kwamba kwa sasa mambo yamebadilika na wananchi wanao mwamko mpya tofauti na zamani. Huu upuuzi wao unazidi tu kujenga chuki baina ya watawala na wananchi na kuna siku hata hivyo vyombo vya dola wanavyovitumia vitawageuka na dalili zote tayari zinaonesha kuwa hiyo siku haiko tena mbali.
 
Nguruvi3,

..tatizo ccm huanzisha jambo au utaratibu fulani. Sasha wengine wakiiga na kuanza kuwazidi malaria basi ccm huleta vyombo cya dola kuzuia jambo hilo.

..ccm ndiyo waasisi wa utaratibu wa mazishi ya "kichama ". Wao ndiyo walioanzisha utaratibu wa kuvaa sare za chama kwenye misiba na kuvika majeneza bendera za ccm na vijana wa chama kuteka nyara shughuli za misiba.

..Kama ccm wanavaa sare zao kwenye misiba kwanini iwe makosa kwa waombolezaji wanachama wa vyama vingine kuvaa sare za vyama vyao?

..mimi simlaumu lowassa kwa kusindikizwa na umati wa watu kila anapokwenda. Hulu ni wakati wa uchaguzi, what do u expect??! Nitamlaumu na kumdharau kama atashindwa kuwafanya hawa wasindikizaji wawe wapiga kura.

..halafu huu umati na jinsi unavyokuwa mkubwa una effects zake ktk saikolojia ya wapinzani wa lowassa. Umati huu unawafanya ccm wafikirie mara mbili-'mbili kuhusu jinsi ya kukabiliana na ukawa/ccm/lowassa.

..lowassa amawatupia "chambo" ccm na polisi na wao wakakimeza. Polisi hawakupaswa kumzuia lowassa. Kitendo kile kimewafanya waonekane wanamuonea na kumuandama lowassa. Siku watakayompiga mabomu ndiyo watakuwa wamemtakasa machoni mwa wapenda mageuzi wa nchi hii na wanachama wenzake wa cdm. Kama utakumbuka mkutano mkuu wa cdm ulisheni wahanga wa ukatili wa namna mbalimbali wa polisi.

..busara ya lowassa ktk Sakata hili ni pale alipokataa agizo la polisi kwenda msibani bila washabiki wake waliokuwa wakimsindikiza. Kitendo kile kimejenga imani na ukaribu Kati yake na mashabiki wake.
Mkuu taratibu za CCM ni za kuvia nafasi. Pengine wapinzaniwangeongoza kwa kuonyesha utu misibani.

Mzee Kisumo amefariki akiwa CCM mwanzilishi, mwanachama namdhamini

Ningechangia hoja ya King Suleiman kwa pamoja.

Hakuna kosa la Lowassa kuhudhuria msiba zaidi ya utu naubinadamu.

Haikuwa sahihi kwake kuwaacha wafuasi wake. Lakinialichelewa kuchukua hatua

Kuwaambia atarudi Moshi ni jitihada za mwisho kuzuiamtafaruku na Polisi.

Ilikuwa ni jambo jema kufanya hivyo kutotoa nafasi kwaPolisi kuanza kushambulia.

Kwa busara za kawaida, kuzuia ni bora kuliko kuponya.

Inajulikana, uwepo waLowassa mahali unaambatana na makundi ya watu.

Angeweza kuepuka kwa kutotoa ratiba. Uwepo tu ingekuwahabari juu ya unyenyekevu

Angeliweza kusafiri hadi Usangi bila kuwaudhi wafuasi wakeau kuleta distractions

Habari kubwa iliyokuwepo jana ni Gununita na Mgheja.

Focus isingeondoka, ingekuwa moja ya mambo ya kutia kiweweCCM
 
Nguruvi3,

..umeona picha toka msibani??

..jeneza alimowekwa marehemu lilikuwa na bendera ya ccm.
 
Last edited by a moderator:
Kama kuna kitu ambacho upinzani unapaswa kukipigania kufa na kupona ni kuhakikisha wote waliojiandikisha kupiga kura wanajitokeza tarehe 25 na wanapiga kura bila mizengwe yoyote. Ushindi wa 62% alioupata JK mwaka 2010 huku voters turnout ikiwa ni 42% pekee inatoa ujumbe kwamba endapo turnout ingekuwa 70% au hata 80% pengine tungekuwa tunaongea lugha nyingine sasa hivi!

Na hili wanapaswa kulisimamia kwa umakini sana hususani sasa tunapotumia huu mfumo wa BVR! Kwa matukio yaliyoripotiwa hivi karibuni ya baadhi ya viongozi kukamatwa wakikusanya kadi za kupigia kura kutoka kwa wananchi na kuzinakili namba ni dalili mbaya juu ya mambo yatakayotokea tarehe 25.
,,,
Kujitokeza kupiga kura pekee haitoshi, tukumbuke mwaka 2010 mistari ya foleni za kupiga kura ilikuwa sawa, au kupita 2005 (at least kwenye eneo langu), lakini kuna vijanaa walienda kupiga kura wakaambiwa majina yao hayapo kwenye daftari japokuwa walijiandikisha.

Inabidi kuhakiki kwa umakini mkubwa na kulinda kura, mwaka 2010 matokeo yalichukua mda mrefu kutangazwa, sina uhakika na utaratibu wa safari hii ila ingekuwa vyema kama matokeo yote yangebandikwa kwenye vituo mara baada ya kuhesabiwa na wakala wa vyama na sio kukusanywa maboxi yote na kupelekwa makao makuu
 
Back
Top Bottom