CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika



Hiki umeandika kitu gani?????? Dah hakika binadamu tumetofautiana..
 
**Sehemu II
MAJIBU kwa Alinda Mwalimu
Kweli Mimi ni kijana Nina umri wa miaka 30+,Nimekuelewa vizuri sana katika bandiko lako,na ile picha uliopost ambayo kwa maelezo yako ahuna uhakika umesema " Kinachoendelea Mwanza kama ni kweli basi ninaanza kuwa na wasi wasi" mwisho wa kunukuu,kwanza huna uhakika, kwanini uitimishe kwa umwagaji damu,mantiki yako kua CCM haitakubali matokeo, hivi kinara wa kukataa matokeo ni nani kati ya CCM na Upinzani (Mahaba kwa CHAMA chako yanakupofoa),Uandishi wako unataka kuonyesha kuwa Tume itaibeba CCM ata kama imeshindwa.
Swala Haki ni pana sana,linatakiwa kuanzia katika vyama vyetu vya siasa,mpaka tume ya Taifa ya uchaguzi, ulitakiwa ushahuri wa umwagaji damu uanzie katika uchaguzi wa ndani wa vyama vya siasa katika kupata wawakilishi katika uchaguzi mkuu,tumeona vurugu,kusosonekkusosoneka,kumbuka kila Mgombea anakua na wafuasi, ikitokea hariziki na matokeo vurugu zitatokea tu,haki zianzie uchaguzi wa ndani,umwagaji damu haungalii NEC TU,DR SLAA alivyobadilishiwa gia angani,nafasi yake ya Urais kuuziwa LOWASA, unazani alifurahi,je angesema hakubali na kushawishi wafuasi wake,je amani ingekuwepo,busara ile ile ya Slaa kukubaliana na hali ilivyokuwa,basi wagombea wote,matokeo yakitangazwa,wasio kubali wafuate taratibu za uchaguzi, wawaambie wawe na moyo wa SUBIRA, maana ata wewe ukukubali Lowasa kugombea, lakini sasa umekubali, kwa nini na tarehe 26 usikubali, matokeo, ata kama hujalizika, Kwahiyo Mbowe akikataa na wewe ukubali,kweli vihoja.
Pia nataka kukuonya Zitto sio BOSS wangu, Mimi nimuajiriwa wa serikali ya JMT,sijawai kukutana na Zitto ata kwa bahati mbaya katika maisha yangu,kama wewe ni secretary wa Mbowe sawa,ni wewe mtetee kwa viroja vyovyote anavyofanya,2010 nilimpigia kura Dr SLAA, ili tu alete ushindani kwa CCM, kama lengo lako kupata viti maalum,utapata tu,Mimi namkosoa yoyote.
Ninacho Amini nguvu ya ukweli ni kubwa kama tone la mafuta ya taa,tone dogo la mafuta ya taa linaondoa thamani ya UNGA, ata kama nitakua pekeyangu JF nitasimamia ukweli.
Kumwaga damu Tz si Mara ya kwanza, Ila atuhitaji itokee tena,hakuna maisha mbadara baada ya kifo, nakuona unashabikia sana umwagaji damu,kama ili linakuumiza,kwanini useme haitakua Mara kwanza kumwaga damu

Mwalimu jibu lako ni hili, usome tena bandiko langu, nimesema wazo kabisa ,TANZANIA yetu ni bora kuliko vyama vyetu, umeelewaje hapa??????

wakatatabahu
 
Last edited by a moderator:
Hiki umeandika kitu gani?????? Dah hakika binadamu tumetofautiana..

Niliemjibu katika lile bandiko ni Nguruvi3, aliuliza maswali 9,nimempa MAJIBU 9,na wewe Yale maswali yako nimekujibu hapo huu,soma maswali yako utakuta MAJIBU, nimeamua kutoa majibu tu sababu natumia simu,ningechelewa ungesema nimesema
Meseji sent and derived
 
Last edited by a moderator:



Hiki ulichoandika kinatia uvivu kusoma.. Jaribu kupangilia andishi lako ili watu wapate hamu ya kulisoma (nafikiri umejifunza kitu hicho shuleni)

Pia tatizo si kuchelewa kujibu bali tatizo ni kutokujibu.. Na nasikitika kukwambia katika maswali yangu hakujibu hata moja.. labda nikuulize tena...

"kama haki hisipotendeka kuna uwezekano wa kumwaga damu ni uchochezi? Ni uchochezi wa nini na wa nani kwenda kwa nani?

Je ni kweli haki zinatendeka ktk changuzi zetu?

kama haki hazitendeki unachoshauri ni nini?

JE watu wakae kimya wakiangalia baadhi ya wataule wakisigina haki zao?

au watu wapaze sauti zao?

na je unafahamu watu wakipaza sauti zao ni nini kinachotokea?


Pia kwani watanzania kumwaga damu ni mara ya kwanza?

Si ulisikia kiongozi wako mkuu akisema "wakati wanakigoma wakipigwa mabomu watu wa Arusha Iringa walikuwa wanakumbatia watawala! Labda nikuulize je hiyo damu uliyomwagika miaka ya 1990 huko mkoani Kigoma ilikuwa ni damu ya
Mbuzi au ya binadamu? Na je hii damu ilimwagika kwa ajili ya madaraka au kwa ajiri ya kutaka haki sawa?


HAYO NDIO MASWALI NILIYOULIZA SASA SOMA MAJIBU YAKO UONE KAMA YANAJIBU MASWALI YANGU.
 

hakuna swali nisilojibu labda uamue kujitoa UFAHAMU, fuatalia mtililiko wa maswali yako, utaona MAJIBU yangu yamefuata mtililiko wa maswali yako,ungeweka namba ningekujibu kwa mtililiko wa namba
 

" Ni wajibu wa tume ya uchaguzi kusoma alama za nyakati, na kuandaa mazingirai mazuri ambayo yatatoa haki bin haki kwa pande zote mbili yaani chama tawala na vyama vya upinzani la sivyo tujiande kwa nchi yetu kumwaga damu.. Huu ndio ukweli ambao tunapaswa kuusema."

Wewe ukaamua moja kwa moja kuihusisha kauli hii na upinzani kuwa ndio vinara wa umwagaji damu ukitoa mfano wa Mbowe! Bila kuangalia upande wa pili ni kwa jinsi gani wenye dhamana wanaweza pia kuwa ni chanzo cha uvunjifu wa amani na hata umwagaji damu....

AMANI ni tunda linalostawisha na HAKI, USAWA... kukosekana kwa vitu hivi ni kuhatarisha uwepo wa AMANI yenyewe. Alinda amejitahidi kuweka tahadhari juu ya hatari iliyopo endapo waliopewa dhamana ya kusimamia uchaguzi kuhakikisha unakuwa ni huru na wa haki wanashindwa kutimiza wajibu wao. Tumeshuhudia wenyewe jinsi zoezi la kujiandikisha kupiga kura lilivyokwenda kwa kigugumizi huku kukiwa na kasoro lukuki.

Bahati mbaya sana wewe unachoona ni kauli za Mbowe tu! Umeshindwa kukemea pia kauli na vitendo vya wana CCM, vyombo vya dola pamoja na vyombo vya habari vinavyomilikiwa na serikali vinavyoashiria kuwa wako tayari kwa lolote kuhakikisha CCM inaendelea kubaki madarakani hata kwa GOLI LA MKONO!
 

Unajifanya kipofu katika maandishi, nimeonya vyama vya siasa vyote akiwepo aliesema gori la Mkono,na wale waliposema afe kipa,afe beki Lowasa RAIS, na yule aliesema atatangaza matokeo kabla ya Tume
 
UDHIBITI WA SERIKALI KWA WAPINZANI UNAENDELEA

ILANI YA CCM NA VIPAU MBELE VISIVYO NA MASHIKO

Serikali imepiga maruku matumizi ya uwanja wa taifa kwa shughuli za kisiasa.

Kupitia msemaji wake, serikali imesema viwanja hivyo vitabaki kutumika kwa shughuli za kisiasa tu.

Hii inafuatia ombi la wapinzani kutaka kuzindua kampeni zao katika viwanja hivyo

Viwanja vingi vya michezo kama Sheikh Amri Abeid na Kirumba vinamilikiwa na CCM.

Hii maana yake, CCM itatutimia viwanja vilivyojengwa na wananchi kwa shughuli zaowapinzani wakilazimika kutafuta viwanja mbadala

Mara kadhaa tumeshuhudia sherehe za CCM zikifanyika katika viwanja vya taifa.

Tunajua uwanja wa zamani umetumika kwa shughuli za kisiasa au kijamii kama kuombea dua taifa na mwaka mpya

Haieleweki endapo tangazo la serikali ni la kudumu au ni katika uchaguzi tu.

Zipo hisia kuwa hatua hiyo ikiambatana na ile ya kuzuia wagombea kuambatana na maandamano imeletwa 'mahususi'

Hatua za zimamoto zinajenga hisia zisizotakiwa katika jamii. Mfululizo wa 'udhibiti' hautoi fursa sawa kuelekea uchaguzi.

Ni changamoto kwa wapinzani kutafuta maeneo mbadala. Zipo nafasi zinazoweza kuchukua idadi yoyote

Kwa upande mwingine, wananchi wana ufahamu, ni vigumu kutoa sababu kuwashawishi hatua zichukuliwazo ni muhimu

Endapo huu ni mkakati, basi utakuwa na matatizo hasa kwa chama tawala CCM

Wananchi wanaweza kutafsiri hatua za serikali ambayo ni ya CCM zina lengo la kisiasa hata kama si hivyo

CCM itajijengea mazingira ya chuki zisizo za lazima na hilo ni kwa hasara yao kuelekea uchaguzi


ILANI YA CCM Inaendelea
 
ILANI YA CCM 2015

CCM imetoa ilani yao kwama ilivyonukuliwa na gazeti la Mwananchi.

Duru tutaangalia ilani hiyo tukizingatia CCM ni chama tawala na kama lipo jipya linaloweza kujadilika.

Moja ya sera za CCM ni kujenga uwanja wa ndege wa Dodoma katika kiwango cha kimataifa.

Tunaweza kusema, CCM imeshindwa kuhamisha makao makuu Dodoma.

Uwanja uliopo una kidhi ya mawasiliano. Dodoma si mji wa mikataifa na wala hauhitaji ndege za kimataifa kutua hapo

Pengine kuimarisha uwanja wa sasa unaokidhi haja ni jambo muhimu kuliko kujenga uwanja ambao tuna uhakika hautakuwa na manufaa ya aina yoyote.

Gharama za ujenzi wa uwanja zingeElekezwa maeneo kama uwanja wa JKN ili kuvutia mashirika ya kimataifa kutumia kuliko ilivyo sasa

Uwanja wa KIA unakabailiwa na matatizo makubwa ikiwa ni pamoja na ushaindani.

Ujenzi wa uwanja wa Kenyatta Kenya na ule wa Voi nchini humo unatishia sana hali ya baadaye ya sekta ya utalii.

Kuliko kujenga 'ghost airport' Dodoma, pesa zingelekezwa kwa viwanja kama cha Mwanza, KIA, na JKN

Ahadi na sera ya CCM zimelenga zaidi kisiasa na si kiuchumi.

Hapa ndipo wapinzani wakitumia vichwa vyao, wanaweza kuonyesha wananchi kwanini CCM inapaswa kupumzika

Tutaendelea na kuangalia ilani ya CCM
 
ILANI YA CCM 'RUSHWA''

Inaendelea...

Rushwa ni jambo linaloitesa serikali ya CCM na chama chake.
Uchaguzi wa kura za maoni ni ushahidi wa rushwa kuwa utamaduni wa CCM na nchi kwa ujumla

Ilani ya CCM inasema wataunda mahakama na vyombo maalumu vya kushugulikia rushwa kama suluhu ya tatizo

Wananchi wanapaswa kuona CCM walivyoishiwa mbinu za kuongoza nchi.

Haya si kwa mujibu wetu bali matendo yanayoonekana wazi kama ushahidi usio na shaka

1. Kwa miaka taarifa 10 CAG zinazoonyesha ufujaji, ubadhirifu na rushwa iliyotawala na zinakabidhiwa kwa Rais/mwenyekiti wa chama

2. Taarifa zote za bunge zimefanyiwa miziengwe. Tunakumbuka Escrow karibuni. Mwanasheria mkuu alitetea hakukuwepo rushwa

Kikao cha bunge liliona lipo jambo. Kwa 'namna' ya kawaida, suala likarudishwa serikalini ili wahusika wachukuliwe hatua.

Serikali ikawasafisha baadhi tofauti na uilivyojadiliwa. Ni kama lille la katibu mkuu wa wizara aliyegawa rushwa,akaachwa astaafu

3. Meno ya tembo yamekamtwa yakipitishwa uwanja wandege.
Ingawa uchunguzi unaendelea, inatosha kusema ni dalili nzuri jambo hilo ni mazoea , pengine safari hii imekuwa bahati mbaya tu

4. Mikataba mingi iliyoitia taifa hasara ipo miaka nenda rudi. Shirika la Reli ni mfano, mataruma yaligeuzwa vyuma chakavu.

5. Serikali ya CCM iliona wabunge wakidai mafao ''wawezeshe'' miswada. Ingawa si wazi, ni ' rushwa' katika mazingira ya uhalali

Inatosha kusema kuwa kila jambo lilogusa rushwa IPO tabia ya ima kukingia kifua au kwa kuunda tume zisizo na majibu

Inaendelea..
 
RUSHWA INAVYOITESA CCM

Mbinu zimetumika kuhakikisha wahusika hawafikishwi mbele ya vyombo vya sheria. hata ikitokea hivyo, wahusika hupeta kutokana na udhaifu wa mashtaka. Tuliona kesi ya balozi mmoja aliyetuhumiwa kutumia mapesa ya umma ikimalizika 'salama salimini'

Tunaposikia CCM inataka kuweka mahakama za rushwa, inachekesha, inashangaza sana.

Ni lini tumekuwa na tatizo la mahakama? Ni lini kesi zimefikishwa mahakamani ikishindikana kwasababu ya kutokuwa na mahakama?

Tunaweza kuwa na mahakama lukuki. Kama dhamira haipo,wala rushwa waendeshea mashtaka,mahakama haiwezi kuwa suluhu

Rushwa ni uhalifu kama uhalifu mwingine. Kuitengenezea mahakama ni kugawa uhalifu katika makundi.

CCM wanataka mahakama ya rushwa, kesho ya hongo, mwaka mwingine ya wezi wa kuku tu.

Ipo siku tutasikia CCM ikishauri uwepo wa mahakama ya wachepukaji, wagoni na wazinzi, ndiyo CCM ya leo

Hizi ni dalili za ''dilly dally'' kuhadaa umma wakati CCM imeshindwa kushughulikia miaka zaidi ya 30

CCM inaposema itaunda vyombo maalumu ni kichekesho cha mchana wa leo.

Kuna PCCB iliyopo chini Rais, kuna DPP, kuna DCI ambao wote ni wafanyakazi wanawaowajibika kwa serikali. T

umeona PCCB ikishindwa majukumu kutokana na kutokuwa chombo huru. Tumesikia msuguano kati ya DCI na PCCB n.k kwa uchache

Hatuwezi kuwa na vyombo vingine vikaja na matokeo tofauti. Kinachoumiza ni mfumo uliojengwa katika urasimu na kulindana.

Tume ya Warioba ilikuja na mapendekezo ya kutengenisha vyombo vya umma, kugawa majukumu na kumpunguzia Rais majukumu

CCM wanaotaka mahakama walipinga tume wakiita kazi ya tume 'hatukuwatuma' kutuletea mengine.
Leo wanashauri yale yale walioambiwa tena wakija na karatasi inayoitwa Ilani

Huu ni udanganyifu usio na mashiko. Ilani kama hizi zinapaswa kuangaliwa na wananchi kama hadithi

Ni hadithi kwasababu CCM iliyoshindwa ikiwa na vyombo vyote inaomba ridhaa itekeleze kile ilichoshindwa!!

CCM isiyoweza kupambana na rushwa ndani ya chama chao, inatuaminisha inaweza kupambana nje ya chama!

kama huyu si mbuzi wa gunia anayeuzwa, basi atakuwa tembo mweupe

Tutajadili ilani kuhusu deni la taifa na ilani ya CCM
 
ILANI YA CCM . VITUKO VINAENDELEA.

CCM WANADHIBITI DENI LA TAIFA

WATAJENGA HOSPITALI ZA RUFAA

Katika kile kinachoonekana na CCM kuendelea na maigizo ikiacha watu hoi kwa vicheko ni hii sera ya kudhibiti deni la taifa

Mtakumbuka hapa JF tumeongelelea sana madhara ya kukua kwa deni la taifa.

Serikali ya CCM ilisimama hadharani na kusema 'ni lazima nchi ikope ili kutekeleza majukumu' na kwamba deni si kitu kibaya

Tena walisema tunakopesheka kwasababu bado tupo katika viwango vya kimataifa vinavyokubalika kukopeshwa

Hakuna aliyeona tatizo ndani ya CCM na kulizungumzia. Wote walishangilia CCM kutekeleza miradi kama ilani isemavyo

Tume ya Warioba ilizungumzia kuhusu hili na CCM hao hao wanaoandika ilani ya kudhibiti deni la taifa waliiikataa rasimu

Hivi CCM waliposema tunakopesheka na hakuna tatizo, hawakuona umuhimu huo? Leo akili ya kudhibiti deni la taifa wameipata wapi?

Tuliposema kuwepo na namna ya kudhibiti kukopa, CCM hawakuona hilo, leo akili ya kuliona wameipata kutoka wapi?

HOSPITALI ZA RUFAA

Katika kichekesho kingine, ni CCM kutaka kujenga hospitali za rufaa za kanda

Ni kichekesho kwasababu mwenyekiti wa CCM alishatangaza kuzipandisha baadhi ya hospitali kama ya Morogoro, na Ligula Mtwara

Leo ilani inataka kuwepo na hospitali za rufaa za kanda, ni zipi hizo ukiacha zile zilizopandishwa hadhi?

Je, si kweli kuwa hospitali zote za mikoa zimekuwa za rufaa? Tunaomba msaada kuhusu hili kama ni tofauti

Lakini pia tuJiulize, kwani hoja ni kuwa na majengo mengi au kuwa na maeneo yenye huduma za kisasa na zinazopatikana kwa unafu?

Wndapo hospitali za rufaa ni muhimu, iweje ''watu'' wanaokwenda kutibiwa nje wengine wakiwa na matatizo yanayotibika nchini?

Je hospitali za rufaa zilizopo zimetoa huduma gani nzuri kiasi kwamba tufikirie kila 'kata' inahitaji moja?

Nini kinafanyika kuimarisha zilipo sasa kwa vifaa na wataalamu?

Yote yanayosemwa katika ilani kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi, ni kichekesho!

Kama hutacheka kwa ilani ya CCM katika baadhi ya vipengele, ni wakati uombe serikali ilipie gharama za matibabu ya kicheko India.

Tutaendelea...
 
Mahakama ya Rushwa

Huku ni kuwahadaa watanzania wasiojielewa kuwa suluhisho la rushwa Tanzania ni mahakama 'special' kushugulika nalo...

PCCB haipo huru, haina meno na haiwezi kuthibiti rushwa katika mazingira tuliyonayo..rushwa ambazo 'puppet master' ni 'mamlaka ya juu' haziguswi..PCCB inatakiwa kuboreshwa na kuwa huru....

Taasisi za serikali zinazosimamia haki za wananchi mfano Tume ya Uchaguzi zinapaswa kuwa huru..na hilo haliwezekani bila kubadilishwa kwa katiba..katiba yetu inampa mamlaka makubwa Rais...

John F Kennedy kabla ya kuonana na Nyerere Marekani mwaka 1963, alisema katiba ya Tanzania inaweza kumfanya Rais wa Tanzania akawa dictator...hatujawahi kuwa na mabadiliko ya maana yenye msingi wa uwajibikaji kwenye katiba yetu zaidi ya jaribio lililochakachuliwa...

Rushwa ni utamaduni (culture) ambayo vita vyake inabidi ishirikishe wadau wote...kuna wananchi wanaotoa rushwa bila kuombwa...inabidi ifike mahala wote tukubaliane kuwa 'enough is enough'..sheria peke yake haziwezi kuondoa tatizo la rushwa lililokithiri Tanzania na nchi nyingi kusini mwa jangwa la Sahara....

Hata hivyo tunahitaji kuwa na sheria bora zitakazosaidia kuthibiti na kuzuia rushwa, sheria hizo zisimamiwe na PCCB iliyosukwa upya..na wahusika wafikishwe katika mahakama zetu hizi hizi zitazokuwa zimeboreshwa kwa kuzingatia vipaumbele vya mahitaji ya mahakama za Tanzania....
 
Jack sheria bora zipo tena nyingi sana.

Tatizo si upungufu wa sheria, majaji au vyumba vya mahakama.

Tatizo ni mfumo uliojengwa wenye kutoa nafasi kwa wahalifu kutumia sheria hizo hizo kujilinda wakitekeleza uhalifu

PCCB ipo chini ya ofisi ya Rais, DCI na DPP ni wateule wa Rais.
Polisi ni chombo cha dola ambacho mkuu wake ni mteule wa Rais. Bunge halina meno kwa baadhi ya wateule wa Rais

Unakumbuka Escrow , bunge lilishindwa kutimiza wajibu wake kwasababu waliohusika walirudishwa kwa mteule wao.

Yeye ndiye aliamua nini kifanyike wale si mkono wa sheria

Angalia, serikali imepewe nguvu za kuunda tume. Siku hizi Polisi kazi yao ni kukimbizana na waalifu kama wezi wa 'kuku'

Tume zinazoundwa kisheria haziwajibiki popote bali kwa mhusika na hapa ni serikali.

Kwamba, maamuzi ya tume hizo yanaweza kupata 'veto' ya mtu mmoja

Tume zimebadiki kuwa machaka ya kuficha wahalifu. Ndio maana likitokea tatizo, viongozi hukimbilia kuunda tume

Kikubwa zaidi, katiba inampa mamlaka Rais kiasi kwamba hakuna chombo chochote kinachoweza kuhoji jambo juu yake

Hawa CCM wanafahamu hilo kwasababu wameishi katika mfumo huo.

Ni mfumo unaowasaidia katika kutekeleza azma zao

Leo wanakuja na sera ya mahakama maalumu kana kwamba, DCI,DPP, PCCB wameshafanya kazi tatizo ni mahakama

Huu ni ulaghai usio na chembe ya akili na unaonyesha jinsi gani tulivyo na tatizo nchi hii

Hao waliokaa na kupenedekeza Upuuzii huo ndio 'think tank' ya CCM. Kweli hawajui wala rushwa pango lao ni CCM!!!

Jiulize, wanapokuwa wamelala au wamekunywa pombe hali yao inakuwaje

Wananchi wanaletewa kila aina ya maono kuwa CCM imechoka kifikra, hawana jipya la kuonyesha, ni mafundi wa kulaghai tu

Wahalifu wamejengewa uzio na wapo ndani ya CCM wakitumia mfumo huo

CCM inaaminisha umma kuwa tatizo ni vyumba vya mahakama na upungufu wa majaji

Vijisenti, senti za mboga na kila aina ya dharau kejeli na kashfa zinatoka kwa wana CCM tena wnaotarajiwa kurudi bungeni.

CCM haioni hilo kama tatizo, eti wanaandika sera, ilani yao ni kujenga vyumba vya mahakama na majaji maalumu kwa wala rushwa!

Hawa ndio wanafikiria kupunguza deni la taifa, wanafikiria kupunguza mfumuko wa bei!
 
HAYA YAMEANZA LINI NAKWASABABU GANI?

MSAJILI WA VYAMA NAMWENYEKITI WA TUME MLIKUWA WAPI?

NINI KINAWASUKUMASASA HIVI?

Kanda maalumu ya Polisi Dar imepiga marufuku zomea zomea ya watu wenye mavazi ya chama fulani.

Haijasemwa chama gani bali ‘fulani'


Kauli hiyo ya fulani ni mahususi ili kukwepa kueneza habari za chama kinacho zomewa

Kwavile ni chama ‘fulani' Kauli yaweza kuwa ya kweli au ya kutunga, haku naanayethibitisha ni chama gani bali chama fulani

Hii inafuatia marufuku ya
;

1. maandamano wakati wa kurudisha fomu

2.kufungia vyama vya siasa uwanja wa taifa.

3. Ipo taarifa ya kuzuia vikundi vya ulinzi vya vyama vyasiasa

4.Na kauli ya kuwataka viongozi wa dini wasihubiri kampeni kwenye nyumba za ibada

Kauli na marufuku ukitolewa na Polisi,tume ya uchaguzi na msajili wa vyama zinahitaji kuangaliwa kutoka pande zote

1. Zomea Zomea

Kumekuwepo na utani wa ‘magamba na magwanda' , ‘Ufipa' na ‘Lumumba'

Tumesikia nyimbo za vikundi vya vyama kama zile za CCM Dodoma zikinanga vyama vingine

Tumesikia wabunge kuzomeana katika bunge la JMT na BMLK kwa maneno makali zaidi ya zomea zomea inayosemwa.

Kwa nyakati zote hizo ofisi ya msajili wa vyama ilikuwa kimya

Leo kimesibu nini na kwa msukumo gani ofisi inakemea jambolililopo kwa muda mrefu?

2.. Vikundi vya ulinzi

Wakati wa TANU kulikuwepo na TYL(Tanu youth League) baadaye UVCCM chini ya ‘Makamanda',juzi mmoja kafukuzwa

Tunaona UVCCM na sare na kuonyesha ishara ya ‘saluti'inayotumika majeshini

Vyama kama CUF vikaunda matawi yao (Blue guard) na CHADEMA(Red Brigade)

Yote haya yakifanyika, Polisi, Msajili wa vyama walikuwawanayaona.

Leo kwanini ionekane kundi fulani ni tatizo na si makundi yote likiwemo lililoasisi mtindo huo CCM na UVCCM?

Tatizo ni nini hasa hadi makundi haya matatu yaonekane tofauti!


Inaendelea…..
 
Inaendelea sehemu ya II

3. Viongozi wa dini

Nao wameaswa kutohubiri kampeni kwani ni kinyume cha taratibu. Ni kweli utaratibu huo unakiukwa.
Jambo la kujiuliza, utaratibu huo umekiukwa kuanzia lini? Na kwanini ni sasa si wakati wa kura za maoni!


Lakini pia kuna jambo la kushangaza kidogo.
Waziri wa serikali alikwenda Kanisani kuhubiri siasa za katiba akitoa maneno makali yenye hisia kuliko zomea zomea.

Waziri huyo yupo kazini na hatukusikia msajili wa vyama akikemea siasa katika nyumba za ibada au CCM.
Nini kimemshtua safari hii hadi kutoa kauli?


Mara nyingi serikali imewaomba viongozi wa dini kuombea Amani taifa.

Kama dini na siasa hazichanganywi, viongozi hao wa dini wanaombwa kwenda kwenye siasa kwa mwamvuli gani?

Je, ni vema kuchanganya siasa na dini na si dini na siasa?


Katika mazingira yaliyopo , wananchi waachwe huru kutimiza haki yao ya kushiriki siasa.

Ima kuna anayerusha mawe huyo anakiuka sheria za nchi.

Hatudhani zomea zomea ni tatizo kwani haikuanza leo na imeachwa ikakomaa na hao wanokemea.

Msajili wa vyama, Polisi na tume ya uchaguzi wanaweza kufikia mahali pa kukataza alama za vyama.


Hivi mtu akionyesha vidole viwili bila kusema neno, hiyo nizomea zomea, hatujui kama nayo ipo mbioni kuwekewa marufuku

Jitihda za kuminya uhuru wa watu, kuegemea upande mmoja zinachochea hali kuliko kuleta sualuhu.

Wananchi watakosa Imani na vyombo husika! Ndivyo ilivyoanza kwa nchi kama Kenya.

Mwisho wa siku nguvu ya umma ikazidi uwezo wa vyombo vya dola, yaliyoendelea ni hadithi


Amani na utulivu ni zao la haki. Vyombo husika kama wadau wa Amani na utulivu havipaswi kuhubiri Amani na utulivu bali kutenda haki ili zao la Amani na utulivu lipatikane.

Kuendeleana matamko au kauli za kutisha hakutendi haki kwa chama kama CCM.

Wananchi wanaaingalia CCM kama serikali na hivyo si busara kuiweka CCM katika wakatiusiostahili.

Tuache vyama vya siasa vifanye yao, watendaji wasimamie haki. Hilo tu.


CCM kama chama tawala itendewe haki. Wapinzani kama wadau wasiasa watendewe haki.

Tusijenge mazingira yatakayowasukuma wananchi kujenga chuki dhidi ya upande mmoja kwa kuona lipo neno, lipo jambo.

Msajili wa vyama, mwenyekiti wa tume au jeshi la Polisivisimamie haki na si kuchukua jukumu la ‘mashataka' viendeshe shtaka na kutoa'hukumu'

Kama CCM ina tatizo ni vema itumie vyombo vya sheria. Kamawapinzani wana tatizo nao watumie njia hiyo hiyo.

Si kazi ya msajili,mwenyekiti wa tume au Polisi kuendesha mashtaka yasiyokuwa na malalamikaji.Nani kazomewa?

Vyama vya siasa vijibebe na vibebe mizigo yao. Umma uachweu amue hatma ya nchi

Tusemezane
 
Nguruvi3


Nakubaliana na wewe kuwa kuna tatizo la mfumo ambalo suluhisho lake ni mabadiliko ya katiba yatakayompungizia Rais madaraka...

Ukitazama hukumu zinazotolewa kwa wala rushwa ni ndogo, sio kali na haziwezi kusaidia kuondoa tatizo, ndio maana kuna haja ya kuziangalia upya sheria zinazohusika...

Tuna Baraza la maadili ya viongozi wa umma unaofanya uchunguzi wa malalamiko baada ya sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma (ambayo ipo chini ya ofisi ya Rais) kukamilisha uchunguzi wa awali na 'kujiridhisha' kuwa kuna hoja ya msingi...

Muundo wa Baraza hilo ni wa wajumbe watatu wanaoteuliwa na Mh. Rais.....

Hata Director wa PCCB anateuliwa na Rais bila kuidhinishwa na Bunge, mambo kama haya hayawezi kuzuia rushwa zinazotokea 'juu'...

Kuanzisha mahakama ya rushwa ni kuongeza matumizi yasiyo ya lazima, ni kushindwa kuona chanzo cha tatizo au kulenga mishale sehemu siyo...

CCM wangesema kuboresha miundombinu ya mahakama zetu na kuongeza majaji ili kupunguza mrundikano wa mashauri ingekuwa sawa...
 
Last edited by a moderator:

Kinachofanyika ni kuwa upande wa CCM unajaribu kudhibiti umaarufu wa UKAWA na kufifia kwa CCM katika ramani ya siasa za Tanzania mwaka huu....

Kuzuia zomea zomea, uwanja wa taifa n.k ni mlolongo wa mwenendo wa CCM kumdhibiti Lowassa na UKAWA kwa faida yao katika dhana ileile ya kuua na kudhoofisha nguvu ya upinzani...

Huku ni kujitoa ufahamu kuwa upinzani wa leo ni sawa na miaka hiyo...ukweli ni kuwa upinzani wa leo una nguvu na unatishia uhai wa CCM kuliko wakati wowote toka mfumo wa vyama vingi uanze...

Chama tawala kinatumia vyombo 'vyake' vya dola katika kutimiza azma yake hiyo..ukweli ni kuwa CCM imechokwa na wengi..na huu ukweli hawawezi kuuficha chini ya ardhi, utajitokeza tu....

Sheria za kuwepo vikundi vya ulinzi kwa vyama vya siasa haijakiukwa na upinzani (kwa sababu hawajasema) zaidi ya kujaribu kueneza propaganda....

Kuna viongozi wa dini kadhaa wamezungumza katika maeneo ya ibada kuhusu, kwa mfano, suala la kukithiri kwa rushwa katika kura ya maoni CCM kwenye uteuzi wa wagombea wao..huku ni kuwashusha zaidi CCM na serikali inaona bora kuwanyamazisha ukizingatia kuwa wana ushawishi mkubwa kwa waumini wao....

Ifike mahala serikali iache kuingilia uhuru wa wananchi wasiovunja sheria yoyote...kwa kufanya hivyo wanazidi kudhihirisha ukweli kuwa wanahangaishwa na upinzani....
 
USHINDI NI ZAIDI YA KURA
UKAWA WANATAMBUA UKWELI HUO?
Kwa nchi za kiafrika, uchaguzi si suala lakura tu, bali namna gani kura zinaweza' kupatikana'

Katika nchi masikini, vyombo vya umma ni mali ya serikaliiliyopo madarakani.

Mara nyingi hufanya kazi kwa maagizo ya watawala. Ndivyodemokrasia ya Afrika ilivyo


Ni kama tunavyoona personality zikiwa juu ya sera na ilaniza uchaguzi.

Kwa muktadha huo, vyama vya upinzani hukutana na vikwazo lulukikabla ya kuingia katika sanduku la kura


Wapo wasomaji watakaohoji, iwapo vyama tawala vina nguvu zausaidizi, iweje nchi kama Kenya, Malawi, Zambia, Nigeria n.k. zimefanikiwakubadilisha serikali, vyama tawala kuangushwa na wapinzani?

Hoja hii ina jibu moja, kwamba, ili wapinzani washindewanatakiwa kushinda katika kiwango ambacho nguvu ya ushindi italazimisha chamakilichopo madarakani kuachia ngazi.

Ushindi wa karibu hutoa nafasi kwaudanganyifu kwavile tu kuna usaidizi wa vyombo vingine


Uchaguzi unapokaribiana sana kimatokea ‘too close to call'historia inaonyesha mambo mawili kutokea.

Moja, chama tawala kutumia nguvuilizonazo za kidola kulamisha matokeo.

Pili , au kunatokea vurugu na machafuko.Ndivyo tumeona mara nyingi katika nchi zinazoendelea au masikini


Tukirijea uchaguzi wa 2015 hapa nchini, inaelekeautakaribiana sana'too close to call' au chama tawala kupoteza umiliki wamihimili 2 ya dola, au kupoteza vyote

Kama ilivyo sehemu nyingine duniani, wapinzani Tanzaniahawana chaguo.
Ni ima washinde kwa kishndo au wapoteze uchaguzi kwaujumla. Ushindi wa nguvu utawahakikishia mambo haya


1 Kwamba, wanashika dola kwa ujumla wake(Bunge na serikali)

2 Wanamiliki sehemu ya bunge kupitia 2/3

3 Wanamiliki bunge kwa ujumla wakiwa na idadi kubwa yawabung
Hii ina maana, CCM hawawezi kuunda serikali wakiwa na Rais,waziri mkuu mpinzani.

Hapa pana mtego sana na inavyoonekana, wapinzani wamepoteza mtazamo(focus) kuhusu jambo hili.

Wasipokuwa makini watalipa gharama kubwa.

Tunafafanua sehemu ya pili
 

waiting for the next part kisha nitachangia maana hata mm nina muono kama huo, uchaguzi ni zaidi ya kura kwenye box ni mipango haswa, na hili ni zaidi kwa nchi zenye democrasia changa kama yetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…