CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika


mkuu Alinda ni kweli kabisa, nimesikia mwenyewe EATV na pia wakamhoji mwabasheria fulani, nimemsahau jina kuhusu hilo, na akashangaa sana huku akisema polisi haina haki ya kumzuia yyt kutembea, bt ndio hivyo ruling imeshatolewa na polisi Dsm, sasa sijui watatii au watakomaa na sheria? Kazi ni kwao
 

Polisi ni chombo cha usalama wa raia. Kampeni za siasa ambazo zinaweza kuleta usumbufu wa watu zinaweza kukatazwa na polisi japokuwa hazifunji sheria.

Kwa mfano foleni ya magari ni kubwa sana jijini DSM. Kampeni ambazo zitaongeza foleni hizo zinaongeza usumbufu tu ambao unapunguza kiwango cha uzalishaji.
 
Mkuu wakati naandaa bandiko ningependa kukumbusha kuwa hizo unazosema si sababu za Polisi

Polisi wanasema, ziara hizo zinawaondoa wananchi katika shughuli zao za maendeleo

Concern ya Polisi si usalama per se, ni wananchi wanaondoka katika kazi zao. Swali, jeshi la polisi linafanya kazi za wizara ya kazi na maendeleo ya jamii? Ni wajibu wa polisi kusimamia kazi za watu? Jeshi linajua watu wangapi wanafanya kazi maeneo hayo? Jeshi limeweza kutoa ajira kwa wahusika?

Kazi ya jeshi la polisi ni kuzuia, kulinda amani na usalama wa wananchi.

Kama ni suala la kazi, vipi Magufuli jana kule Sumbawanga, wananchi hawakuacha kazi zao? Mbona jeshi linaona kazi za eneo moja la Dar na si Sumbawanga? Kwanini lisihimize wananchi warudi mashambani na kutumia mbegu bora za kilimo?
 

Yaani Tanzania kuna mambo ya ajabu hadi yanakufanya wakati mwingine uone hata aibu kuwa Mtanzania.

Ipo siku huyo Kova atampiga marufuku Lowassa kuwa hai kisa tu uwepo wake hai unasababisha mparaganyiko jijini.
 

Mimi sioni huu kama ni uchaguzi. Naona kama ni vita vya ndani vya wapenda madaraka na rafu zote wanazochezeana ni sawa tu. Kama Lowassa angepita kwa tiketi ya CCM asingetumia daladala. So let him test the other side.
 
Yaani Tanzania kuna mambo ya ajabu hadi yanakufanya wakati mwingine uone hata aibu kuwa Mtanzania.

Ipo siku huyo Kova atampiga marufuku Lowassa kuwa hai kisa tu uwepo wake hai unasababisha mparaganyiko jijini.



NN

Ulitaka huyu jamaa aingie magogoni kilaini? Yaani achumie kivulini, alie kivulini, aende magogoni kivulini.
 
NN

Ulitaka huyu jamaa aingie magogoni kilaini? Yaani achumie kivulini, alie kivulini, aende magogoni kivulini.

Upande mwigine huko sawa kabisa ngoja walau hata wao waonje yale machungu wayapatayo wapinzani. Na hiki tunachokiona kwa Lowassa au Masha ni cha mtoto wapinzani wamepitia mengi.. Mfn uchanguzi wa serikali za mitaa huko Monduli, wapinzani alivyodharirishwa na kupigwa na polisi waliokuwa wametumwa na Lowassa.

Jana sikuumia kuomuona Masha akipanda karandinga bali nilifarijika maana alikuwa waziri wa mambo ya ndani, alikuwa na uwezo kuwa kupeleka miswada bunge ya kurekebisha sheria kandamizi lakini hakufanya hivyo kwani waliokuwa wanaumizwa na hizo sheria walikuwa ni wapinzani ambao hawana haki katika nchi hii. Leo hii zile sheria alizotumia kuwakandamiza "wale" ndizo hivyo zinazotumika kumkandamiza hata yeye..
 

Habari yako Zakumi
Nina uhakika asilimia 100 kuwa polisi wana 'double standard' kwenye hili.
Leo hii Magufuli akisema anafanya kama Lowassa alivyofanya utaona hao polisi hawatoi tamko lolote na zaidi watampa ulinzi.
Kwa mfano, polisi walisema hakutakuwa na maandamano ya watu na wagombea wao pindi wanapochukua na kurudisha form zao.
Umeona Zanzibar Dr. Shein alichofanya? Ameandamana na wafuasi wake kwenda na kuchukua form. Sasa hapo unaweza kusema polisi wanasimamia haki?
This is too much...
 

Wanasiasa wengi hawana kumbukumbu na hawaweki maneno na matendo yao kama 'reserve' kwa matukio ya mbeleni.
Hawa wanaohamia upinzani wamehamia wakati jua linatua. Walitakiwa wahamie wakati jua lipo kwenye utosi linaunguza kwelikweli ndo wajue maswahibu wanayoyapata upinzani.
 

Na zaidi ya yote sijaona kama kuna uvunjifu wa amani wowote ambao lowassa ameusababisha.
Sijaona watu kupigana wala kurushiana maneno ya aina yeyote.
Hapa polisi wanatakiwa kujisafisha na hizi 'double standards' wanazozionesha.
 

Labda sasa ndo anaweza kuwa na 'a balanced perspective' baada ya kuonja udhalimu wa CCM.
 

Labda sasa ndo anaweza kuwa na 'a balanced perspective' baada ya kuonja udhalimu wa CCM.

Atleast Masha kwa kuishi kwake USA alikumbuka walahu ubinadamu wa kuleta mabasi kubeba mahabusu badala ya yale makarandinga ya polisi.
Nitamkumbuka kwa hilo angalau watuhumiwa sasa wanapelekwa mahakamani kutoka magerezani kwa njia yenye ubinadamu japo kidogo.
 
Yaani siasa za nchi hii zinanizidishia 'kizunguzungu'. Ni kweli kabisa sikukubaliana na Lowassa kujiunga UKAWA lakini kujiunga kwake huko hakutakiwi kutumika kuinyanyasa UKAWA. Hivi wanajua kweli madhara hasi juu ya haya wanayoyafanya...!? Na kwa kweli taratibu wanaanza kubadili mtazamo wangu juu ya Lowassa na UKAWA nikiwa na 'kizunguzungu' changu hivyo hivyo.
 

Alinda:

Angekuwa Dr. Slaa, Lipumba, Zitto, Mbowe, au Seif Sharrif wanafanyiwa hivyo, ningekuwa nao. Lakini kwa Lowassa, Masha, naona hivyo ni vita vya wenyewe na wenyewe. Waache wachukue mikong'oto tu.
 
Na zaidi ya yote sijaona kama kuna uvunjifu wa amani wowote ambao lowassa ameusababisha.
Sijaona watu kupigana wala kurushiana maneno ya aina yeyote.
Hapa polisi wanatakiwa kujisafisha na hizi 'double standards' wanazozionesha.

Huyu jamaa hajawai kuwa nje ya shughuli za kiserikali. Ameitumia serikali kufika hapo alipo. Mwache aonje kuwa nje ya serikali kabla ajarudi kama rais.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…