CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

Wanajamvi, nimepita pita katika web na kukuta hii kitu. Sina uhakika kama tulishiriki kama nchi au serikali
Vile vile sina uhakika kama hiyo ndiyo latest edition.

Hata hivyo, tunaweza kujifunza kwa kuangalia kidogo Kama yapo yanayorandama na mazingira yetu ya sasa

http://www.ipu.org/cnl-e/154-free.htm


DECLARATION ON CRITERIA FOR FREE AND FAIR ELECTIONS
Unanimously adopted by the Inter-Parliamentary Council at its 154th session
(Paris, 26 March 1994)

The Inter-Parliamentary Council,

Reaffirming the significance of the Universal Declaration of Human Rights and the International Covenant on Civil and Political Rights which establish that the authority to govern shall be based on the will of the people as expressed in periodic and genuine elections,

Acknowledging and endorsing the fundamental principles relating to periodic free and fair elections that have been recognized by States in universal and regional human rights instruments, including the right of everyone to take part in the government of his or her country directly or indirectly through freely chosen representatives, to vote in such elections by secret ballot, to have an equal opportunity to become a candidate for election, and to put forward his or her political views, individually or in association with others,

Conscious of the fact that each State has the sovereign right, in accordance with the will of its people, freely to choose and develop its own political, social, economic and cultural systems without interference by other States in strict conformity with the United Nations Charter,

Wishing to promote the establishment of democratic, pluralist systems of representative government throughout the world,

Recognizing that the establishment and strengthening of democratic processes and institutions is the common responsibility of governments, the electorate and organized political forces, that periodic and genuine elections are a necessary and indispensable element of sustained efforts to protect the rights and interests of the governed and that, as a matter of practical experience, the right of everyone to take part in the government of his or her country is a crucial factor in the effective enjoyment by all of human rights and fundamental freedoms,

Welcoming the expanding role of the United Nations, the Inter-Parliamentary Union, regional organizations and parliamentary assemblies, and international and national non-governmental organizations in providing electoral assistance at the request of governments,

Therefore adopts the following Declaration on Free and fair Elections, and urges Governments and Parliaments throughout the world to be guided by the principles and standards set out therein :

1. Free and Fair Elections
In any State the authority of the government can only derive from the will of the people as expressed in genuine, free and fair elections held at regular intervals on the basis of universal, equal and secret suffrage.

2. Voting and Elections Rights

(1) Every adult citizen has the right to vote in elections, on a non-discriminatory basis.

(2) Every adult citizen has the right to access to an effective, impartial and non-discriminatory procedure for the registration of voters.

(3) No eligible citizen shall be denied the right to vote or disqualified from registration as a voter, otherwise than in accordance with objectively verifiable criteria prescribed by law, and provided that such measures are consistent with the State's obligations under international law.

(4) Every individual who is denied the right to vote or to be registered as a voter shall be entitled to appeal to a jurisdiction competent to review such decisions and to correct errors promptly and effectively.

(5) Every voter has the right to equal and effective access to a polling station in order to exercise his or her right to vote.

(6) Every voter is entitled to exercise his or her right equally with others and to have his or her vote accorded equivalent weight to that of others.

(7) The right to vote in secret is absolute and shall not be restricted in any manner whatsoever.

3. Candidature, Party and Campaign Rights and Responsibilities

(1) Everyone has the right to take part in the government of their country and shall have an equal opportunity to become a candidate for election. The criteria for participation in government shall be determined in accordance with national constitutions and laws and shall not be inconsistent with the State's international obligations.

(2) Everyone has the right to join, or together with others to establish, a political party or organization for the purpose of competing in an election.

(3) Everyone individually and together with others has the right:


  • To express political opinions without interference;
  • To seek, receive and impart information and to make an informed choice;
  • To move freely within the country in order to campaign for election;
  • To campaign on an equal basis with other political parties, including the party forming the existing government.
(4) Every candidate for election and every political party shall have an equal opportunity of access to the media, particularly the mass communications media, in order to put forward their political views.

(5) The right of candidates to security with respect to their lives and property shall be recognized and protected.

(6) Every individual and every political party has the right to the protection of the law and to a remedy for violation of political and electoral rights.

(7) The above rights may only be subject to such restrictions of an exceptional nature which are in accordance with law and reasonably necessary in a democratic society in the interests of national security or public order (ordre public), the protection of public health or morals or the protection of the rights and freedoms of others and provided they are consistent with States' obligations under international law. Permissible restrictions on candidature, the creation and activity of political parties and campaign rights shall not be applied so as to violate the principle of non-discrimination on grounds of race, colour, sex, language, religion, political or other opinion, national or social origin, property, birth or other status.

(8) Every individual or political party whose candidature, party or campaign rights are denied or restricted shall be entitled to appeal to a jurisdiction competent to review such decisions and to correct errors promptly and effectively.

(9) Candidature, party and campaign rights carry responsibilities to the community. In particular, no candidate or political party shall engage in violence.

(10) Every candidate and political party competing in an election shall respect the rights and freedoms of others.

(11) Every candidate and political party competing in an election shall accept the outcome of a free and fair election.


 
4. The Rights and Responsibilities of States
(1) States should take the necessary legislative steps and other measures, in accordance with their constitutional processes, to guarantee the rights and institutional framework for periodic and genuine, free and fair elections, in accordance with their obligations under international law. In particular, States should:

  • Establish an effective, impartial and non-discriminatory procedure for the registration of voters;
  • Establish clear criteria for the registration of voters, such as age, citizenship and residence, and ensure that such provisions are applied without distinction of any kind;
  • Provide for the formation and free functioning of political parties, possibly regulate the funding of political parties and electoral campaigns, ensure the separation of party and State, and establish the conditions for competition in legislative elections on an equitable basis;
  • Initiate or facilitate national programmes of civic education, to ensure that the population are familiar with election procedures and issues;
(2) In addition, States should take the necessary policy and institutional steps to ensure the progressive achievement and consolidation of democratic goals, including through the establishment of a neutral, impartial or balanced mechanism for the management of elections. In so doing, they should, among other matters:

  • Ensure that those responsible for the various aspects of the election are trained and act impartially, and that coherent voting procedures are established and made known to the voting public;
  • Ensure the registration of voters, updating of electoral rolls and balloting procedures, with the assistance of national and international observers as appropriate;
  • Encourage parties, candidates and the media to accept and adopt a Code of Conduct to govern the election campaign and the polling period;
  • Ensure the integrity of the ballot through appropriate measures to prevent multiple voting or voting by those not entitled thereto;
  • Ensure the integrity of the process for counting votes.
(3) States shall respect and ensure the human rights of all individuals within their territory and subject to their jurisdiction. In time of elections, the State and its organs should therefore ensure:

  • That freedom of movement, assembly, association and expression are respected, particularly in the context of political rallies and meetings;
  • That parties and candidates are free to communicate their views to the electorate, and that they enjoy equality of access to State and public-service media;
  • That the necessary steps are taken to guarantee non-partisan coverage in State and public-service media.
(4) In order that elections shall be fair, States should take the necessary measures to ensure that parties and candidates enjoy reasonable opportunities to present their electoral platform.
(5) States should take all necessary and appropriate measures to ensure that the principle of the secret ballot is respected, and that voters are able to cast their ballots freely, without fear or intimidation.
(6) Furthermore, State authorities should ensure that the ballot is conducted so as to avoid fraud or other illegality, that the security and the integrity of the process is maintained, and that ballot counting is undertaken by trained personnel, subject to monitoring and/or impartial verification.
(7) States should take all necessary and appropriate measures to ensure the transparency of the entire electoral process including, for example, through the presence of party agents and duly accredited observers.
(8) States should take the necessary measures to ensure that parties, candidates and supporters enjoy equal security, and that State authorities take the necessary steps to prevent electoral violence.
(9) States should ensure that violations of human rights and complaints relating to the electoral process are determined promptly within the timeframe of the electoral process and effectively by an independent and impartial authority, such as an electoral commission or the courts.
 
Zakumi

Kwamba ujio ulikuwa unasubiriwa au ulitokea tu, hilo ni swali gumu na majibu wanayo wenyewe.
Ukiangalia kutoka angle tofauti ni kama vile lilikuwa jambo la kupangwa. Vipo viahiria kama vitatu hivi. Tuachie hapo


Kwamba, mshindi kwa asilimia 50.01 au 51 atalamisha serikaliya mseto, hilo litategemea bunge likoje.
Kumbuka uchaguzi wetu Rais anachaguliwa moja kwa moja na si kutoka bungeni


Rais atakayeshinda hata kwa 0.001 bado atakuwa na nguvu iwapo atakuwa na majority katika bunge na hilo halite mlazimisha kuunda serikaliya mseto

Kwa upande mwingine, Rais atakayeshinda kwa asilimia 60 na kupoteza bunge atalazimika kuunda serikali ya mseto kwasababu hatakuwa na bunge wala wziri mkuu

Ndio maana tunawaambia wapinzani, kuacha majimbo watu wapite bila kupingwa ni hasara kubwa sana.

Kupoteza kiti kimoja cha bunge kunaweza kubadili sura ya utawala kabisa.

Kama unakumbuka bunge la katiba CCM hawakuwa na viti vya kutosha isipokuwa vya Sam six alivyounda unda na laana ikamwangukia


Tatizo ni kuwa ushindi wa asilimia 1 au chini unaweza kutuweka mahali pagumu. Mungu asaidie!

Nguruvi3;

Kwa miaka mingi Tanzania imehamua kufanya mahamuzi mepesi yenye kuakikisha usalama na kuacha kufanya yale magumu. Lakini ukweli wa mambo, maamuzi magumu yenye kuleta mafanikio kwa muda mrefu hayakwepeki.

Matokeo ya uchaguzi wa mwaka huu, yanaweza kushinikiza serikali ya mseto, serikali ya umoja wa kitaifa n.k Matatizo yaliotoea Zimbabwe na Kenya.

Baadhi ya CDM/UKAWA na sasa Team Lowassa hawana matumaini na kitu kingine zaidi ya ushindi. Haya matumaini yata-override percentage zozote zitakazoipa ushindi CCM.
 
MARUFUKU' KATIKA UCHAGUZI

Polisi wanatambua wajibu au wanatimiza wajibu?

Kutambua wajibu ni kuelewa dhana nzima ya wajibu wakinachotakiwa na kisichotakiwa katika kuwajibika.

Kumitiza wajibu ni kutenda kwa mujibu iwe kwa kuelewa aukutoelewa, kukubali au kutokubali ilimradi tu wajibu umetimia.

Nchi nyingi hujinasibu kuwa na chaguzi za haki na huru( Freeand fair elections).

Kupiga au kupigiwa kura hakutendi dhana ya haki na huru balini sehemu tu ya dhana

Lipo azimio linaloeleza dhana ya haki na huru( free andfair) pengine tulipitie kidogo

LOWASSA NA ZIARA ZA KUSHTUKIZA

Zipo sehemu kuu mbili za ziara yake

1 Akiwa waziri mkuu wa zamani, ni mtu mwenye habari nyingi za nchi.
Kwa wakati wowote anaweza kuwa ni ''target'' ya maadu wa nchi .
Lakini pia amefanya maamuzi mengi akiwa katika utumishi. Si wote waliofurahishwa pengine

2. Akiwa Mgombea wa UKAWA na hali ya kisiasa iliyopo inayotishia kukipeleka chama tawala maktaba, wakati wowote anaweza kuwa na watu wasio na ni njema naye

Hivyo, usalama wake popote alipo ni kipaumbele. Akiwa mstaafu ana walinzi wake , lakini pia kama Mgombea serikali inawajibu wa kumuandalia ulinzi. Hili linafanyika sehemu nyingi duniani.

Lengo ni kumwepusha na yasiyotarajiwa na hata serikali kuepuka lawama ikitokea isivyo tarajiwa

Bandiko la free and fair election linaeleza uhuru wa kutoa maoni , kukusanyika, kupokea na kutoa habari kwa ufahamu wa mgombea.

Ni kwa mantiki hiyo, ziara zake zinaambatana na wasi wasi wa usalama wake.

Ni vema akapewa ulinzi utakaomwezeaha kufika kule anakotaka kama haki yake ya kidemokrasia ya mgombea.

Pia, mikusanyiko mikubwa inaweza kuambatana na hali isiyotarajiwa kama vibaka kuchukua fursa kutenda uhalifu.

Kisiasa na kijamii hilo linaweza kuambatana na jina lake na UKAWA kwa ujumla na kuwa tatizo

Hivyo concern ya usalama ina mantiki kabisa

Inaendelea
 
Inaendelea


POLISI
Kwa bahati mbaya approach ya Polisi si nzuri, hoja za Polisi hazina mantiki

1 Wangeweza kuwasiliana na Lowassa na timu yake pembeni na kushaurina bila kwenda kufoka foka katika vyombo vya habari. Kufoka ni kutisha watu dhidi ya upinzani. Polisi wanatakiwa wafanye kazi kama professional na si maguvu guvu tu


2. Kauli ya Polisi kuwa watu wanaacha kazi za maendeleo kukusanyika haina mantiki.
Ni kauli inayoonyesha hakukuwa na sababu za msingi za tamko hata kama zipo

Polisi walitakiwa kuzungumzia usalama na si kazi za wizara ya kazi maendeleo na akina mama

3. Kauli ya Polisi kuhusu kazi inajichanganya sana.
Wakati wanatoa kauli hiyo, siku ya Jumatatu magufuli alikuwa Sumbawanga na mkusanyiko mkubwa sana.

Haijulikani kama Polisi walitoa kibali kwa wananchi kuacha kazi kwenda kwa Magufuli au la


Tunachoeleza ni kuwa jeshi la Polisi ni chombo muhimu katika usalama wa nchi.

Ni chombo cha umma kisichofungamana na siasa.

Inapotokea Polisi wanachukua mwelekeo unaonekana wa kisiasa tayari wanatengeneza mazingira ya kuvunja amani na usalama

Wananchi wakitambua Polisi ni mashabiki kama tunavyosikia wakiwaita Policcm ,tayari jeshi linapoteza public trust

Kukokesakana kwa public trust kunajenga kutoaminiana kati ya Polisi na wananchi. Hapo panatengenezwa kitu kinachoitwa uhasimu.

Polisi wanatakiwa washirikiane na umma. Ikitokea umma unaanza kuwaona kama sehemu ya kisiasa , hakika hali ni mbaya

Tuliona Kenya na Burundi, Polisi walipokosa imani ya umma mambo yalikuwaje

Ili kuwepo kwa amani na usalama, suala si kutisha, kutumia maguvu na kufoka hovyo.

Busara ni kutumia sheria na hekma vitu ambavyo jeshi letui halionekani kuvijali

Polisi watengeneze amani na usalama wasiwe chanzo cha kuvunja amani na usalama

''Modern ''Polisi si ile ya watu warefu, virungu na mabomu .

Sikuhizi ni Polisi shirikishi, polisi ya kitaalamu. Nguvu ni kitu cha mwisho kabisa kutumika na inapotokea ''modern ''polisi huomba radhi.

Tusemezane
 
Nguruvi3;

Kwa miaka mingi Tanzania imehamua kufanya mahamuzi mepesi yenye kuakikisha usalama na kuacha kufanya yale magumu. Lakini ukweli wa mambo, maamuzi magumu yenye kuleta mafanikio kwa muda mrefu hayakwepeki.

Matokeo ya uchaguzi wa mwaka huu, yanaweza kushinikiza serikali ya mseto, serikali ya umoja wa kitaifa n.k Matatizo yaliotoea Zimbabwe na Kenya.

Baadhi ya CDM/UKAWA na sasa Team Lowassa hawana matumaini na kitu kingine zaidi ya ushindi. Haya matumaini yata-override percentage zozote zitakazoipa ushindi CCM.

Hayo niliyawekea msisitizo ndio hali halisi ya Watanzania!

Kama kuna kitu nitamvulia kofia Lowassa ni ujasiri wake wa kuamua kuwa liwalo liwe, yupo tayari kwenda nje ya CCM na kujaribu bahati yake.

Kujiamini kwake huko pamoja na lundo la tuhuma na hali halisi kuwa ni mgonjwa taabani, ni kitu ambaocho si wengi wetu tungediriki au hata kufikiria kujitoa muhanga kupigana wazi wazi na mfumo na Chama ambacho kina nguzu za kidola na mamlaka na kinaogopeka.

Alichofanya Lowassa ni kuwaamsha watanzania kutoka unyonge wa maneno matamu ya CCM na kuthibitisha kuwa CCM si mama yake na mtu yeyote anaweza kuondoka na kuichallenge CCM.

Tofauti na kuhama kwa Mrema au hata Dokta Slaa, ni kuwa Lowassa alikuwa ni kada na mtu mwenye nguvu kubwa sana ndani ya chama. Ama kiburi, ujeuri na nguvu zake za kitajiri, uwezo kuwa karibu na wanacnhi kwa wakati mmoja na hata kuwa mstari wa mbele unamfanya apokewe kama shujaa na mkombozi na ndio pale watu wanasema "he has dared the mighty CCM with no fear"

CCM inaweweseka kwa sababu, kuna uwezekano mkubwa sana wa wananchi wapiga kura wakafuata hii blue print ya kukigeuka CCM hata dakika za mwisho na CCM kupoteza mamlaka na nguvu.

Badala ya CCM kukaa chini na kuwa -entice wananchi kwa kuwa humble na kujirudi kwa madhaifu yake kushinda umasikini, ujinga na maradhi, CCM imeleta kiburi na majivuno na hata kuongea kwa kiburi na dharau.

Hivyo, Wananchi na hata Ukawa wanaona what the heck, watakwenda head on wakiwa hawana tumaini na lolote lile tena.

Hatari yake ni kuwa kutokana na usalama wa kinafiki na mshikamano wa watu waliokaa kimya miaka yote, jambo hili la Lowassa kuhama na ukawa kumpokea kwa vifijo hata kuwa tayari kumsafisha kinapokelewa kama uhaini na kwa wanaohama CCM ni silent mutiny.

Uzuri wetu, hakuna anayekwenda mwituni! watu watatumia demokrasi kuin'goa CCM at any cost hata ama leo ni kumkumbatia Lowassa tajiri, fisadi na anayeonekana wazi kiafya hajiwezi.
 
Mkuu Rev. Kishoka , bila kujali nani atashinda au nini itakuwahatma ya taifa, lipo jambo moja muhimu umelizungumzia

Kwa miaka mingi, watanzania wamekuwa na ‘taboo' ya baadhiya mambo.

Kwa mfano, ni mwiko ' taboo and curse' wanachama kupinga vyama vyao vya kisiasa


Imekuwa ni desturi kwa watu kukubali kuanguka pamoja hata kama hawakubali anguko hilo

Imekuwa ni kawaida watu kutopingana hadharani bali chini ya meza tena kwa manung'uniko.

Unafiki umekuwa sehemu ya utamaduni wetu. Hata penye tatizo watu watatabasamu ili kuwafurahisha wafalme.

Kinachoendelea sasa ni ukomavu wa kisiasa. Kwamba watu kama balozi Mwapachu wanaweza kusimama na kusema hili si sawa tenakwa wakubwa zao

Mawaziri wakuu wanaweza kusema hawakubaliani na mwendo huu wakiwapinga wakubwa zao tena wengine wakiwa na habari zao

Yanayotokea yamefungua pingu za laana, desturi na utamaduni. S

asa watu wapo huru na tutashuhudia sana hata baada ya uchaguzi.

Watu wanakumbatia sera ya Nyerere kuhusu uanachama. Aliposema CCM si mama yake,sasa yanatimia


Wengi wanatambua siasa za kujikomba hazina nafasi tena.

Wakiwaangalia wahanga kama Kayanz , Jaji, Ghrb na wengine, watapata somo maridhiwa.


Uasi ndiyo fashion ya mjini na hilo linabadili ' political landscape'' kwa kiasi kubwa sana

Tusemezane
 
Swali linalokuja, je, hicho ndicho wananchi wanataka?
Je, hiyo itakuwa suluhu ya kudumu itakayojenga misingi imara ya taifa, utaifa na maendeleo?
Mkuu wangu Nguruvi3, niwie radhi kwa kukawia kukujibu lakini bado nimetamani kukujibu hivi....

Binafsi siamini katika MATAKWA YA WANANCHI hasa nikitazam political conciousness ya hao watu. Ninaamini katika KILE WANACHOPASWA KUPATA WANANCHI regardless of their political awareness or Matakwa yao. Katika hilo, hili laweza kuwa ni Takwa la wananchi lakini ninajua kuwa si kile Tunachopaswa kupata wananchi-ILLUSION.

Mkuu ni wazi sasa kuwa hii haiwezi kuwa suluhu, suluhu wanayo wananchi hawataki kuicheza ila wanakubali kuchezeshwa mchezo mchafu, ndio maana mara zote sitaacha kusema kuwa " Maendeleo ni Hesabu kali, si mchezo wa bahati nasibu. TUKAE CHINI TUPANGE NA KUPANGUA, TUWAZE NA KUWAZUA, TUTEGE NA TUTEGUE, tukiwa tunamfikiria kulwa na doto walioko matumboni mwa mama zao ambao leo wanagombea uji chekechea"
Mungu wetu sasa!
 
Last edited by a moderator:
POLISI NA KAULI ZA NGUVU

UMMA UMECHANGANYIKIWA, HISIA ZA 'UPENDELEO' ZAJITOKEZA

Tumeeleza tatizo la Polisi kutoa kauli bila kuangalia upana na madhara yake.

Marufuku ya ziara za kushutukiza za wagombea ilitolewa na kanda maalumu ya kipollisi ya Dares Salaam.

Hakukutolewa njia mbadala ya bali marufuku

Marufuku ya jambo lisilo na madhara au harufu ya uhalifu kama siasa Polisi wangeweza kushauri njia nzuri mbadala


Polisi wanaweka marufuku kutokana na sheria au hatari inayonyemelea basi Kwa nyakati, inabidi waweke mbalada wa marufku.
Kwa mfano, isitumike barabara A kwa maandamano, mbadala wake ni barabara X

Tukirudi katika marufuku, inaonekana kauli ilitolewa na jeshi laPolisi Tanzania nzima


Ukweli, ilitolewa na kanda maalumu ya Dar esSalaam kupitia viongozi wa kanda .Marufuku hayahusu mikoa au kanda nyingine
Ingalikuwa si hivyo, marufuku yangetolewa na kiongozi au msemaji kwa msisitoizo wa upana wake tofauti na kanda.

Ni haki kusema tamko lilikuwa la Dar peke yake

Mgombea wa CCM mama Samia amefanya mikusanyiko ya ghafla katika maeneo yasiyo ya kisiasa kama hospitali .

Tofauti ni kuwa CCM walikuwa nje ya kanda maalumu ya Dar, tangazo haliwahusu.

Ndivyo ilivyo kwa CCM ambapo watu wanahoji maandamano ya CCM endapo hayakuharibu shughuli na kazi za maendeleo kama ilivyodaiwa na kanda ya Dar.


KUCHANGANYIKIWA
Wapo wanaodhani CCM inapendelewa kwa wagombea wake kuruhusiwa kuchangamana na makundi katika ziara za ghafla.

Ukweli ni kuwa viongozi hao hawapo kanda ya kipolisi ya Dar es Salaam , hivyo marufuku haiwahusu huko waliko


Kwa upande mwingine, haijulikani kama UKAWA wakiwa mikoani watapewa fursa wanazopewa v CCM kwavile waponje ya kanda- Dar

Na vile vile wapo wasioelewa au wenye mashaka kuwa marufuku ya jeshi la Polisi ni ya nchi nzima na si kanda maalumu

Mchanganyiko huu ni mbaya.Unatoa nafasi za watu kuamini maoni yao kama ukweli.
Ndiyo maana tunasema katika hali hii tayari kunakutoaminia kati ya jamii na Polisi


Hali hiyo ya kukosa kuaminiana inatia shaka sana. Ni vema jeshi la Polisi likasimamia sheria za nchi.

Inapotokea kuna marufuku, basi yazingatie sheria za nchi bila kubagua. Kuzuia baadhi ya watu kukutanana na watu ni kuwamnyima uhuru ule ule wanaonufaika nao wengine na ni ubaguzi ikitokea

Kumnyima mtu uhuru ni kwenda kinyume na katiba. Kutoa upendeleo ni kukiuka misingi ya azimio la uchaguzi huru na za haki



Tusemezane

 
MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA

HILI LA MAGUFULI UMELIONA? UMELISIKIA?

UNA KAULI YOYOTE AU NI KANYAGA TWENDE?


Mgombea-CCM mh Magufuli alikuwa Mbeya na Songwe katika kampeni za uchaguzi

http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Magufuli--Msikimbilie-mabadiliko-ya-uongozi/-/1597296/2849386/-/h6jwrvz/-/index.html

Ikumbukwe , mh Magufuli ni mgombea wa CCM kamawalivyo wengine wa nafasi hiyo kutoka vyama vya siasa.

Magufuli anapokuwa katika jukwaa, ni mgombea wa CCM si waziri wa serikali. Mamlaka ya uwaziri si sehemu ya kampeni za siasa

Ukisoma habari hapo juu, mh Magufuli ameagiza watendaji wa wakala wa barabara kutoa tenda za ujenzi wa barabara, katoa amri

Kumbuka, hapa hakutoa ahadi kama zingine tunazosoma. Alichokifanya ni kumwagiza mtendaji wa serikali kutangaza tenda

Kwa maneno mengine Magufuli ametumia uwaziri kuamuru jambo akiwa mgombea

Hapa kuna sura mbili

Kwanza, Magufuli amekiuka taratibu za kampeni kwa kutumia ofisi ya umma kutekeleza ahadi zake

Pili, ame tumia ofisi ya umma kutangaza tenda katika kampeni, ni harufu kali ya rushwa. Kwamba, apewe kura kwasababu ya......

Katika uchaguzi huru na wa haki, wagombea hupewa fursa sawa. Haijulikani fursa hizo zitawafikaije wapinzani wa CCM.

Msajili wa vyama anapaswa kuangalia haya na kuyachukulia hatua. Kinyume chake, msajili atakuwa ni wa baadhi ya vyama vinginevikipewa 'pass'. Hatudhani kama msajili ameliona hili. Angalikuwa ameliona angeshatoa kauli.

Na hatudhani kama hakuona hili kwa ukubwa wake, kama ndiyo , atawezaje kuona mengine?


Ni kwa msingi huo, tunasisitiza, uchaguzi wa haki na huru haushii kwa mtu kwenda kwenye sanduku la kura

Tujiulize, hivi tunapotuma wazee wetu kama akina Salim na Warioba kuwa wasimamizi nje, wanapokutana na haya ya Magufuli wanakauli gani?

Tusemezane
 
UDHAIFU MKUBWA WA MGOMBEA WA UKAWA KATIKA HOTUBA/KUJIELEZA.

Ndg wana jamvi, leo nimefuatilia kwa karibu sana uzinduzi wa kampeni za ndg zetu UKAWA kama vile nilivyofuatilia kwa karibu uzinduzi wa CCM kwenye uwanja huo huo wa jangwani, nikiri wazi UKAWA walijipanga sana kiorganisation ya mkutano na kuhamasisha watu kiasi kwamba watu walifurika mno zaidi sana ya wenzao, na watu walikua na hamasa kubwa mno, na kila ukiwaona unasema hawa wana kiu ya mabadilko.

Ukiacha hayo mazuri niliyosema, kuna jambo nmeligundua ambalo ni baya sana kwa upande wa ndg zetu UKAWA ambapo lazima wajipange, kama nilivyosema mkutano ulikua na hamasa za hali ya juu na watu walikua wanaonekana kabisa wana kiu sana ya UKAWA na kutamani slogan yao ya mabadiliko, bt mgombea wao ambae ni nembo yao kwenye uchaguzi ndg E.N. Lowassa anaudhaifu mkubwa kwenye self expression na hotuba kiujumla ambayo kwa kweli kujirekebisha ni jambo la lazima kama anataka kuwin public mentality ambayo ni muhimu kuhamasisha kura.

Yule Lowassa wa miaka nane iliyopita hodari wa kuongea sio huyu wa sasa, anaonekana dhaifu mno kwenye kuongea, sijajua kwa nn, anaongea bila kujiamini na pia kama anakuwa na uoga kukiongea kwa umakini kile anachokiamini.
JP Magufuli yeye amebahatika sana kipindi hiki, amekua mzungumzaji hodari sana, yupo kwenye chama ambacho wengi wanakiona kama kimechoka lakini kwa namna anvyoongea na kujieleza, wapo watu wanaamini kumbe mabadiliko yanaweza kupatikama ndani ya CCM, amejua namna ya kuwarubuni wapiga kura kisiasa vizuri sana na kwa hoja za nguvu hata kama hazina uhalisia.

Lowassa anatatizo kwenye maeneo yafuatayo hapa chini kama nilivyoshuhudia leo Jangwani na siku za karibuni, wadau mtanikosoa au kuongezea kwenye huu mtazamo wangu.

1.muda wa kuongea, mgombea Uraisi ni mtu anaepaswa kuzungumza kwa muda mrefu zaidi ya wapambe wake na anapswa kujieleza vizuri kabisa ili tumpime kwamba atakuja kufanya nn huyu mtu sio dakika zisizozidi kumi na tano tena nazo zikiwa na matatizo mengine mengi yatakayowapa mwanya wapinzani wake kumshambulia kama nitakavyoendelea hapa chini. Ukawa inabidi wajiongeze kwenye suala la muda, the same niliona wakati wa kura za maoni CCM kingunge alikua anaongea sana kuliko mhusika.

2. Kujadili Non Issues, hapa sijui hajapata washauri vizuri wa kumueleza nn cha kuongea, mambo kama ya Babu Seya, Mashehe wa Zanzibar na Balali, those ar non issues, alipaswa tu kuelezea bila hata kutaja majina wala kuonyesha uelekeo wake, kuna baadhi ya mambo ni ya kimahakama, so utii wa sheria ni muhimu mno na hakupaswa kudiscuss hayo mambo, nilikua naongea na jamaa yangu mmoja akaniambia kuna shida kwa hao watu so lazima asema, nikamwambia hayo mambo ayaache kwa mashabiki hata kama pana mkono wa nani sio vema kudiscuss jukwaani nikosa kubwa sana la kimantiki na kumpa adui nafasi ya kumuattack kwa mambo mengi.

3. Self confidence, hili nalo ni tatizo kubwa sana kwa mgombea wa UKAWA hajiamini kabisa na kama vile haamini anchokisema, muangalie Maalimu Seif, hata kama anakikana alichokisema jana, utaona anaongea kwa confidence sana kiasi cha kuwaainisha wafuasi wake, pia mkumbuke Dr.Slaa, anaongea kwa confidence sana kuaminisha watu wake kile anchoamini, pia hata mgombez wa CCM Magufuli utamuona anavyoongea kwa confidence hata kama cho kitu kinapingana na kile ambacho kinaaminiwa na wanchi. Hii i aleta uhakika sana kwa watu unwaoaleza, sasa EL naonakosa hiiki kitu, ni lazima sasa watu wa UKAWA wamsaidie kupandisha confidence yake.

4. Kuwaza sana kura bila kuelezea ni kwa nn apewe yeye kura, hii ni kama summary ya hayo juu, mgombea wa UKAWA kwa kiasi kikubwa anachowaza na kuongea ni kuomba kura tuu bila kuwashawishi hao watoa kura kwamba nichagueni niweze kuwasaidia kuwatoa kwenye matatizo yenu kwa mikakati na mipango hii sio kuishia tu kuwaza kura bila kusema why upewe kura, hapa JPM anapata crdt kwa kujieleza why apewe kura, na UKAWA lazima wabadilike.

mwisho,
nimalize kwa kuwashauri UKAWA wakati wa siasa za majibizano hasa kwenye non issues zimepitwa na wakati kabisa, kikubwa nikuwaeleza wanachi mambo makuu matatu, kwanini wawachague wao sio CCM, Watawafanyia nini na watafanyaje, habari za individuasm na vijembe zimepitwa na wakati, ni lazima kufanya kampeni kimkakati na mipango timilifu sio majungu na vijembe. Na hii pia inawahusu CCM vijembe na majungu sivyo wananchi wanataka kusikia.

Mgombea wa UKAWA awe monitored vitu gani vya kuongea na kujipanga kwa mtazamo mzuri bila kuharibu taswira ya kampeni zake na pia kuwapa wapinzani wake vitu vya kuongea, fanya kampeni za kushambulia na sio kujilinda.

Karibuni tujadiliane wana jamvi,
 
HOTUBA YA MGOMBEA URAIS KUPITIA CHAMA CHA CHADEMA NA UKAWA MH. EDWARD NGOYAI LOWASSA

YA KUZINDUA ILANI NA KAMPENI YA UCHAGUZI MKUU

Jangwani-Dar-es-Salaam, 29 AGOSTI 2015

Ndugu Wana Dar es salaam na Watanzania wenzangu

1. Leo ni siku ya kihistoria. Baada ya miaka ishirini na tano tangu mfumo wa vyama vingi urejeshwe, vyama vya upinzani wa CHADEMA, CUF, NCCR na NLD umeungana chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi kupigania uchaguzi mkuu wa mwaka huu na kuwa na mgombea mmoja katika ngazi zote.

2. Miaka zaidi ya hamsini ya utawala wa serikali za CCM na waasisi wake, umekuwa utawala wa wachache walio hodhi madaraka na mali za nchi.

3. Leo tunaanza safari ya uhakika ya kuleta mabadiliko ya kweli nchini.

a. Mabadiliko yaletayo neema na kujenga upya mfumo wa uchumi, haki na sheria nchini.

b. Mabadiliko ya kuimarisha huduma za jamii kama elimu, afya, maji na makazi.

c. Mabadiliko ya kuondoa umaskini.

d. Mabadiliko tunayatoahidi ni mabadiliko ya kurejesha matumaini kwa Watanzania kwa kubadili hali zao za maisha.

4. Kila mwaka hali na ubora wa maisha ya Watanzania imeshuka wakati tunaambiwa kuwa pato laTaifa linakuwa.

5. Lakini Watanzania wanachotaka siyo takwimu bali kuona kipato chao kinakua, shule, hospitali na barabara bora zinajengwa.

6. Wanataka kupata maji safi na salama ya kunywa. Wanataka makazi bora.

7. CHADEMA na UKAWA, tuna dhamira ya kuleta mabadiliko ya kweli ili kuona azma ya Watanzania tangu uhuru ya kuondoa umaskini, maradhi,na ujinga inahitimishwa.

8. Ili tufanye hivyo tuahitaji tufanye mabadiliko ya fikra, uongozi, sera na utendaji.

9. Leo Tanzania inakabiliwa na changamoto nyingi za ki-uchumi, kisiasa na kijamii. Changamoto hizi ni matokeo ya sera za utawala wa Chama kimoja wa miaka hamsini. Sote ni wahanga wa siasa na sera hizi.

10. Miaka Hamsini ya CCM imetosha. Tunataka mabadiliko na siyo ahadi zile zile kila mwaka.

11. Tusidanganyike, CCM hawana jipya.

12. Chagueni UKAWA wenye dira ya kubadili maisha ya wananchi.

13. Mimi ninauchukia umaskini na mimesimamia maendeleo kwa vitendo. Nilipokuwa Waziri Mkuu nilijaribu kubadili hali hii. Nilisimamia ujenzi wa shule za kata, Chuo Kikuu cha Dodoma. Nilihakikisha mikataba mibovu ya maji inavunjwa na sasa wananchi wa kanda ya ziwa wanapata maji safi.

Ndugu watanzania
14. CCM wanauliza tuna mpango gani wa kumaliza umaskini. Sisi hatuahidi tu. Tutatenda.

15. Ilani yetu ni dira ya kuondoa umaskini kwa mikakati sahihi na siyo nadharia.

16. Mkakati wa kuondoa umaskini si wa sekta kwa sekta bali wa sekta zote kwa pamoja. Ni ujumla wa utendaji na utekelezaji wa sera za kila sekta utakao leta maendeleo.

17. Mkakati wangu na UKAWA wa kuondoa umaskini utakuwa na nguzo tano:-
a. Kupunguza matumizi ya serikali na mashirika yake na kuimarisha utendaji na uwajibikaji.
b. Kukuza pato la serikali kwa kudhibiti ukwepaji na misamaha ya kodi holela na kuhakikisha nchi inawekeza katika sekta muhimu na inapata gawio halisia kutoka wawekezaji
c. Kukuza uchumi kwa sera na sheria endelevu ikiwa ni pamoja na kukuza biashara na uwekezaji hasa katika sekta za madini, kilimo, viwanda, ufugaji na uvuvi na kuondoa kodi kwa wanyonge.
d. Kuimarisha huduma za umma kama elimu, afya, maji na makazi, na mazingira
e. Kuimarisha utawala bora na mfumo wa haki na sheria chini ya Katiba ya Wananchi.

18. Chini ya misingi hii na ili kufanikisha mkakati wa kuondoa umaskini, serikali yangu itafanya yafuatayo:-

ELIMU BORA KWA KILA MTANZANIA
Nimelisema hili huko nyuma. Nalisema tena leo. Elimu kwanza, Elimu kwanza, Elimu kwanza.

Kwa hiyo mkakati wetu wa msingi utakuwa kutoa Elimu itatayogharamiwa na serikali kwa kila Mtanzania kutoka elimu ya msingi hadi Chuo Kikuu na pia:-

1. Kuimarisha elimu ya teknolojia, ustadi na ufundi inayojenga uwezo wa kujiajiri na ushindani katika soko la ajira.
2. Ujenzi na uimarishaji wa miundombinu ya elimu ikiwa ni pamoja na shule za Kata.
3. Kusimamia ubora wa viwango vya elimu kote nchini.
4. Kuimarisha taaluma na mitaala katika mashule.
5. Kuondoa utoro darasani, na kuboresha afya za wanafunzi.
6. Kuboresha maslahi na vitendea kazi kwa walimu ikiwa ni pamoja na nyumba, posho ya kufundishia, usafiri na zana za teknolojia.
7. Kufuta michango ya maabara ya shule za kata

AFYA
1. Afya na tiba ya kila Mtanzania itagharamiwa kupitia bima za gharama nafuu na mifuko ya hifadhi ya jamii
2. Tutaimarisha afya ya msingi pamoja na kinga kupunguza gharama za tiba.
3. Serikali itahakikisha kuna uwiano na upatikanaji wa watumishi wa afya katika kada mbalimbali ili kuleta tija na huduma stahiki.
4. Itaimarisha miundombinu ya afya pamoja na kujenga hospitali za kisasa ili kusogeza huduma za afya karibu na jamii na pia kuepukana na tiba za nje ya nchi.
5. Tutarejea kwa lengo la kuboresha maslahi na vitendea kazi katika sekta ya Afya ikiwa ni pamoja na nyumba na usafiri.
6. Tutathibiti ongezeko la gharama za huduma za afya bila kuathiri uendeshaji wa watoaji huduma za afya kama vile serikali na hospitali za sekta binafsi.

ARDHI, MAJI NA KILIMO

1. Tutaimarisha mfumo wa umiliki wa ardhi kwa Watanzania na kudhibiti migogoro ya ardhi hasa kati ya wakulima na wafugaji.
2. Tutapima ardhi yote ya Tanzania na kumilikisha vijiji na wakulima kwa hati za serikali ili kuipa thamani.
3. Tutaleta mapinduzi ya kilimo kwa kuimarisha elimu, ufundi na teknolojia ya kisasa na kumkomboa mkulima kutoka jembe la mkono.
4. Tutasimamia kilimo, ufugaji na uvuvi wa kisasa na kuunganisha sekta hizo na ya viwanda.
5. Kuhakikisha kuwa wananchi wanatunza na kulinda vyanzo vya maji.
6. Tutakuza kilimo cha umwagiliaji kwa kuwapa wakulima elimu na mikopo ya riba nafuu ya kuvuna maji na kujenga miundombinu husika.
7. Tutaweka mazingira rafiki yatakayomhakikishia kwa kila Mtanzania kupata maji safi na salama. Kumaliza kero za maji nchini kutamkomboa mwanamke kutokana na adha ya kuchota maji kwa kichwa
8. Nitafuta kodi zote za mazao na mifugo kwa wakulima na wafugaji.
9. Tutasimamia kilimo cha biashara kinachozingatia maslahi ya nchi na ya Watanzania.
10. Tutaanzisha programu maalum ya kufufua mazao asilia ya Tanzania hususan mkonge.
11. Tutaanzisha Benki ya Maendelo ya Ufugaji na Uvuvi.

MIUNDOMBINU
1. Tutaboresha bandari zilizopo na kujenga mpya kama vitega uchumi vya Taifa ili kurejesha biashara tulizopoteza kwa bandari za nchi jirani.
2. Tutajenga barabara nchini kwa kuzingatia ubora hasa zile za vijijini.
3. Tutajenga reli ya kati kwa viwango vya kisasa
4. Tutajenga shirika la Ndege la Taifa linalojiendesha kwa misingi ya faida.
5. Tutajenga miundombinu ya kisasa na kuondosha misongamano ya magari hasa katika majiji ya Dar es salaam, Mwanza, Mbeya na Arusha
6. Tutaimarisha uzalishaji na usambazaji wa umeme vijijini ili kufikia zaidi ya asili mia sabini na tano ya Watanzania

VIWANDA

1. Tutaimarisha sekta ya viwanda kuwa mhimili wa uchumi kwa uzalishaji wa bidhaa na ajira endelevu
2. Tutajenga viwanda vipya vya kusindika mazao ya kilimo, uvuvi na ufugaji.
3. Tutahakikisha kuwa ndani ya miaka mitano mali ghafi zote za Tanzania zinasindikwa kabla ya kusafirishwa nje ili kuongeza mapato na ajira ya mamilioni ya vijana.
4. Tutaanzisha Benki ya Ukuzaji wa Viwanda

UCHUMI
1. Tutabadili mfumo wa Uchumi wa nchi ili kuhakikisha kuwa mfumo wa uchumi wa Tanzania unakuwa ni wa soko-kijamii ambapo nguvu za soko zitatumikia jamii kwa serikali kuweka uwiano wa mapato unaohakikisha huduma za kijamii zinapatikana kwa ufanisi.
2. Tutalinda sekta binafsi na bidhaa za ndani kwa kuwapa Watanzania upendeleo wa maksudi kwa kipindi cha mpito ili waimarike na waweze kuhimili ushindani. Tutawapa wafanyabiashara wetu upendeleo katika manunuzi ya serikali na kuwajengea mazingira mazuri ya biashara na kodi endelevu.
3. Tutawawezesha Watanzania kupata mitaji ya biashara kwa masharti nafuu kabisa.
4. Tutavutia uwekezaji na wawekezaji wenye tija. Kuweka udhibiti wa wahamiaji wasioleta tija wala maslahi kwa Taifa.
5. Tutaimarisha sera ya ubia baina ya Serikali na Sekta binafsi kwenye maeneo muhimu ya kiuchumi na kibiashara. Pia, kuwawezesha Watanzania kuwekeza kwa njia ya ubia na wawekezaji wenye mitaji mikubwa bila kujali wanapotoka.
6. Tutaimarisha usimamizi kwa kubadilisha mfumo wa Vyama vya Ushirika nchini ili utokane na uendeshwe na wakulima wenyewe ikiwa na pamoja na kuwawezesha kuboresha makazi kwa mpango wa kushirikiana kujenga nyumba bora
7. Tutaanzisha na kuwezesha uanzishaji wa viwanda vidogovidogo vinavyotoa ajira kwa wingi kwa kuvihusisha na vyuo vya ufundi na benki maalum kwa lengo hilo.

AJIRA
1. Tutasimamia swala la ajira hasa kwa vijana kwa kukuza elimu ya ufundi ili waweze kujiajiri
2. Tutazipa kipaumbele sekta zinazozalisha ajira kwa wingi hasa za viwanda, kilimo, ufugaji, uvuvi na utalii na kuzipa unafuu wa kodi ili zikue kwa haraka.
3. Tutawapa wawekezaji wakubwa katika sekta hizi upendeleo maalum na viwango vya kodi nafuu.

NISHATI NA MADINI
1. Serikali itashiriki kikamilifu katika uzalishaji wa nishati
2. Itatengeneza mazingara mazuri ya kisera yatakayovutia na kuwezesha ushiriki wa Watanzania na ubia kati yao na wageni.
3. Serikali yangu itaupa uzalishaji mkubwa wa umeme wa maji kipaumbele namba moja, umeme wa makaa ya mawe kipaumbele namba mbili, umeme wa gesi asilia kipaumbele namba tatu na umeme wa urana kipaumbele namba nne.
4. Serikali itatoa vipaumbele muhimu kwenye usambazaji wa huduma kubwa ya umeme sehemu za uzalishaji uliyolenga masoko ya ndani, ya nchi jirani na ya nchi za kigeni.
5. Itapitia upya mikataba yote mikubwa ya nishati na madini ili kubaini iliyo mibovu na kuifanyia maboresho.
6. Serikali yangu itatumia sehemu ya hisa zake kwenye raslimali kubwa ya gesi asilia iliyopatikana hapa nchini kama rehani kwenye kujichukulia mikopo kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu ya mabomba ya gesi.
7. Serikali itatoza kodi na ada ndogo zaidi kwa wazawa wenye ubia kati yao na wageni kuliko zitakazotozwa kwa wageni wasiowekeza kwa kushirikisha wazawa.

8. Serikali itasitisha utoaji wa misamaha ya kodi isiyo lazima kwenye sekta ya madini, na badala yake itawekeza kwenye kuongeza thamani ya raslimali zake za madini.
9. Tutakuza nishati mbadala kutamkomboa mwanamke kutokana na adha ya kukata kuni

MALIASILI NA UTALII
1. Tutasimamia uvunaji na matumizi ya rasilimali za Taifa kwa manufaa ya kila Mtanzania wa kizazi hiki na kijacho
2. Tutapiga vita ujangiri na kuimarisha utunzanji wa hifadhi za taifa na mazingira
3. Tutachochea ujenzi wa miundombinu ya utalii nchini ikiwa ni pamoja na ujenzi wa mahoteli na kuimarisha mafunzo
4. Tutaongeza idadi ya watalii kufikia milion mbili ifikapo 2020.

UTAWALA BORA, ULINZI WA NCHI NA USALAMA WA RAIA
1. Tutasimamia Katiba mpya inayolinda haki za msingi za wananchi na kuweka bayana mipaka ya madaraka ya serikali na viongozi, Bunge na Mahakama.
2. Tutaboresha miundobinu ya sheria na kuimarisha utendaji wa Mahakama na maslahi ya wafanyakazi
3. Tutasimamia haki za raia na kuangalia upya sheria kandamizi ili wananchi kama Masheik wa Zanzibar hawasoti jela kwa sababu za kisiasa.
4. Tutaimarisha mafunzo ya vyombo ya Polisi hasa wapelelezi na waongoza mashtaka ili wapate uwezo wa kusimamia utoaji wa haki.
5. Tutavipa vyombo vyote vya ulinzi na usalama nyenzo na kuboresha mazingira yao ya kazi na maslahi


UZALENDO, UTENDAJI NA UWAJIBIKAJI
1. Tutajenga uzalendo ili kila Mtanzania aweze kutathmini mchango wake kwa taifa kila siku
2. Tutaimarisha nidhamu, utendaji na uwajibikaji katika Sekta ya Umma
3. Tutaimarisha mchango wa Wataalam wetu, wanawake na vijana katika kusimamia uchumi na kuwajengea mazingira stahiki ya kazi pamoja na mafao.
4. Tutapiga vita rushwa na ubadhirifu katika sekta ya Umma na binafsi
5. Tutadhibiti na kupunguza matumizi ya serikali ikiwa ni pamoja na kufuta safari za watumishi serikalini zisizokuwa muhimu pamoja na zile za Rais na kupiga marufuku matumizi ya mashangingi serikalini.
6. Tutadhibiti deni la Taifa kwa kuanza na ukaguzi wa madeni ya serikali ili kuhakiki jinsi yalivyotumika
7. Tutaimarisha uwazi na kuondoa usiri katika shughuli za serikali na kuweka bayana mikataba yote ya nchi ikiwa ni pamoja na ile ya mafuta, madini na gesi asilia


KUKUZA PATO LA SERIKALI

1. Tutadhibiti mapato kutokana na raslimali kwa kupitia upya viwango vya mirabaha kutokana na madini na gesi asilia ili kuhakikisha kuwa Tanzania inapata gawio stahiki.
2. Serikali itaanzisha Wizara maalum itakayosimamia nishati ya gesi na mafuta.
3. Tutaimarisha ofisi ya Msajili wa Hazina ili kusimamia vema uwekezaji wa Serikali katika mashirika na mapato yake.
4. Tutahakikisha kuwa mashirika ya umma yanaendeshwa kwa misingi ya faida na uadilifu.
5. Tutadhibiti ukwepaji kodi za ushuru wa forodha na kupiga marufuku misamaha ya kodi holela ili kuokoa mabilioni ya fedha yanayopotea kila wiki.
6. Sambamba na hilo tutarahisisha utaratibu wa kulipa kodi ili kuondoa kero na mazingira ya rushwa. Kwa kudhibiti makusanyo ya kodi tutakusanya fedha za kugharimia huduma za msingi kama afya na elimu kikamilifu.


KUIMARISHA MUUNGANO

1. Tutaimarisha umoja, usalama na udugu wa Watanzania na Muungano kwa misingi ya haki na usawa

WANAWAKE, WATOTO NA WAZEE

1. Wanawake watapewa fursa na haki sawa katika elimu na uchumi ili waweze bila kuwezeshwa.
2. Tutahakikisha wazazi wanapata fursa ya kuwa walezi na wafanyakazi kwa kuongeza urefu wa likizo ya uzazi
3. Tutaimarisha elimu ya watoto hasa wasichana na kukuza fursa zao na kukomesha ndoa za watoto wadogo.
4. Tutaongeza uwakilishi wa akina mama katika ngazi zote serikalini na mashirika yake kufikia asili mia hamsini ifikapo 2020.
5. Wazee na wasiojiweza watapewa posho ya kujikimu inayokidhi mahitaji ya msingi itakayowawezesha kuishi kwa heshima na kulinda utu wao ndani ya familia na jamii zao.

SANAA, UTAMADUNI NA MICHEZO


1. Tutaendeleza na kuwezesha vipaji vya sanaa na michezo
2. Tutarudisha viwanja vya michezo vilivyovamiwa
3. Tutafuta kodi zote za vifaa vya michezo.
4. Tutadhibiti viwango na maadili ya bidhaa za nje zinazoingizwa nchini na kuzitoza kodi halisia
5. Tutajenga taasisi na vyuo vya kukuza michezo ili kuhakikisha kuwa ndani ya miaka mitano Tanzania inashiriki kwa ushindi katika mashindano ya kimataifa ya soka na riadha
6. Tutalinda Hakimiliki za sanaa nchini
7. Tutafuta kodi za sanaa kwa wasanii chipukizi ili kuwapa muda kwa kujijenga.

SERA YA MAMBO YA NJE YENYE TIJA KWA TAIFA


1. Tutakuza ushirikiano wa Kimataifa wenye tija na Ujirani mwema.

2. Tutatetea haki za binadamu, usawa wa nchi na kuimarisha ushiriki wa Tanzania katika diplomasia ya kimataifa.

3. Tutakuza umoja na ushirikiano wa Umoja wa Afrika, Jumuia ya Afrika Mashariki, SADC na Umoja wa Mataifa.

4. Tutaimarisha Umoja wa Mataifa ikiwa ni pamoja na kudai mabadiliko ya mfumo ili kuleta usawa wa nchi shiriki.

Ndugu Watanzania

Naomba nimalizie kwa kusema yafuatayo

1. Natambua kuwa uongozi ni dhamana. Mkinichagua nitaienzi dhamana hiyo kwa utendaji uliotukuka.

2. Nawaahidi Watanzania kuwa kwa uwezo, akili, uzoefu na nguvu zangu zote nitawatumikia. Nawaomba nanyi mniahidi jasho lenu na uwezo wenu wote ili kwa pamoja tuvuke. Tutajikomboa toka utawala wa CCM unaodumaza uchumi na maendeleo. Tutaanza safari ya uhakika kuondoa umaskini.

3. Mabadiliko pia ni kuthamini utu na kukataa hadaa ya hongo ili kuuza haki yako ya kuchagua. Msikubali rubuni za uchaguzi kwa kupewa pesa au vitu. Rushwa ya uchaguzi ndiyo sera ya CCM. Ukikubali basi umeuza pia haki na sauti yako ya kuwalalamikia walio madarakani. Imetosha. Tukatae. Tulinde utu na haki zetu. Tuchague mabadiliko.

4. Mabadiliko ni fikra. Ni kufikiri na kutenda tofauti. Hatuwezi kuendelea kufikiri na kutenda kama kwamba hatuna dharura ya maendeleo. Kwanza tuanze kwa kufanya mabadiliko na tujiamini kuwa sisi kama Taifa tunaweza. Tunaweza kujitegemea na kuleta maendeleo yetu wenyewe bila kutegemea wafadhili. Hii si ndoto. Nchi nyingi zimefanikiwa kuondoa umaskini katika kizazi kimoja. Tujifunze kutoka kwao.

5. Tuwe taifa linalotumia raslimali zake kujiendeleza na siyo kuwanufaisha wageni na kuwafanya Watanzania watwana katika nchi yao. Inabidi tuache kuwa taifa ombaomba. Tuache kuukubali na kuvaa umaskini kama joho la fahari.

6. Mabadiliko ya kweli hayawezi kuletwa na CCM. Tusitegemee kuwa leo wana jipya. Ndiyo maana ahadi walizotoa miaka thelathini iliyopita ndizo wametoa juzi. Tukatae hadaa. Miaka hamsini ya CCM imetosha.

7. Tunaamani kwamba tutashinda kwa sababu Watanzania mpo nyuma yetu. Watanzania mmeamua kuleta mabadiliko. Kura yako ndiyo itakayokuwa mkombozi wako. Hakikisha unapiga na kuilinda kura yako. Wakati wa mabadiliko ni sasa.

Mungu ibariki Tanzania. Asanteni sana
Tunaamini habari hii imetoka kwenye reliable sources
 
Swali ni kuwa kwa miezi hii karibu miwili iliyobakia wataendelea kutuma hotuba zake kwenye mitandao?

Au siku moja atasimama na kuelezea kwa kina? Au wapiga kura wanatakiwa kumkubali tu kwa imani hata kama hawajui yeye mwenyewe anasimamia nini hasa?

Kama yeye mwenyewe hakisemi kila anachosimamia katika mambo muhimu tutajuaje kile kinachosemwa atasimamia kweli anakiamini?
 
Tunaamini habari hii imetoka kwenye reliable sources


Ni reliable mkuu maana ndio alisoma jana ITV na radio 1 pamoja na vyombo vingine vya habari mara tu baada ya taarifa ya habari, nadhani waligundua mgombea wao kaharibu kwenye uwanja kuongea muda mchache tena bila kuingia in details kwenye important issues, wakaona warescue situation kwa kumtafutia air time haraka.

hapa nawapongeza kdg strategist wa UKAWA kwa kuliona hilo mapema, lakini je huko mikoani na kwingineko watafanya nn kmsaidia akichemka tena? Na watafanya mara ngapi na je muda upo? The best option japo ni kipindi kifupi sana awe monitored wenye kuongea yaani wajipange mapema, na apewe muda usipungua dk 30 kujieleza ili wananchi wamjaji kwa haki, hii kutumia chini ya dk 15kwa kisingizio cha muda ni kuwapa nafasi wapinzani kushambulia.

Mgombea anatakiwa kuchunga sana maneno yake na namna ya kuzungumza ili kulinda Hadhira yake n wengine anaowasiliana nao. Kwa mfano kuwaambia watu wakasome website, huu ni upotofu wa hai ya juu na pasilofanyika umakini inaweza kuzua hasira kwa watu wako ambao wengi ni wa kipato cha chini access na net yenyewe shida.

Angeweza tu kusema "muda hautoshi, hapa nitaeleza kwa muktaari/kwa kifupi vipaumbele vya ilani na mm mgombea, zaidi mtasikia kwenye kampeni tunavyoendelea, kwenye vyombovya habari na kwa wale wenye uwezo wa kupata mtandao tutaiweka kwenye website ya Chama". Angalau hapa itaonyesha kauli isiyo tata kama ya uwanjani pale kwamba mkasome kwenye website nyie wasomi, sijui alijisahau akadhania anaongea na walimu wa vyuo vikuuhakujua pale wengi ni malofa wa halimya chini hata mtandao hawaujui.

Ni lazima abadilike na asipobadilika alazimishwe kubadilika, na ikishindikana atapoteza imani ya watu wengi sana wanaomuamini maana huku mwenzake anajieleza sana mpaka anaongea kwa makabila mengi kukonvice hadhira yake na kuwapa comfidence
 
Swali ni kuwa kwa miezi hii karibu miwili iliyobakia wataendelea kutuma hotuba zake kwenye mitandao?

Au siku moja atasimama na kuelezea kwa kina? Au wapiga kura wanatakiwa kumkubali tu kwa imani hata kama hawajui yeye mwenyewe anasimamia nini hasa?

Kama yeye mwenyewe hakisemi kila anachosimamia katika mambo muhimu tutajuaje kile kinachosemwa atasimamia kweli anakiamini?

Swali la msingi sana hilo...

Wanatumia muda mwingi kumsafisha Lowassa badala ya kuinadi Ilani...Kilichofanyika jana Jangwani ni kichekesho...Sumaye na wenzake wametumia muda mwimgi kumsafisha Lowassa ilhali jukwaa lilikuwa kwa ajili ya Lowassa na Babu Duni Haji...Lowassa naye anatumia muda aliopewa kueleza nini atawafanyia watanzania anasahau vipaumbele mpaka anakumbushwa badala yake anajikita kwenye mambo ya Babu Seya, Balali na Masheikh wa Uamsho...Macho yote ya watanzania yalikuwa Jangwani jana...Wengi walitegemea Lowassa atatumia jukwaa la Jangwani kueleza mabadiliko anayojinasibu atayafanya...Hotuba ya ITV ilikuwa kwa ajili ya kufukia mapungufu yaliyotokea Jangwani...

Ile hotuba ya jana ITV ilikuwa ni kama damage control kwa kile kilichotokea Jangwani...Which was even damaging....

Sasa sijui na kule mikoani hotuba zake zitakuwa zinarushwa usiku kwenye TV ama la...

Tutashuhudia mengi sana miezi hii miwili....

Fikiria watu wanaelezwa hotuba/Ilani inapatikana kwenye website ya chama...Kumbe uongo...

Lowassa ni Kamari kwa kweli...
 
Swali ni kuwa kwa miezi hii karibu miwili iliyobakia wataendelea kutuma hotuba zake kwenye mitandao?

Au siku moja atasimama na kuelezea kwa kina? Au wapiga kura wanatakiwa kumkubali tu kwa imani hata kama hawajui yeye mwenyewe anasimamia nini hasa?

Kama yeye mwenyewe hakisemi kila anachosimamia katika mambo muhimu tutajuaje kile kinachosemwa atasimamia kweli anakiamini?

Mkuu hayo mambo nimeyaeleza sana hapo juu kwenye bandiko namba 351, napata shida sana na kujieleza kwa huyu mgombea na kisingizio chao cha muda ambacho kiukweli hakina maana sana, kwasababu wangeweza kuwapunguza wazungumzaji ambak sio wagombea na kupunguza mambo mengi ya msingi ili apate walau 30 minits kuainisha vipaumbele vyake in details.

Kama ataendelea na utaratibu wa kupeleka hotuba kwenye website ya chama kila anakokwenda bila yeye mwenyewe kujieleza, atapoteza public trust aliyonayo na atawavunja moyo hata wale wanazi wake, Na bahati mbaya mshindani wake ni bingwa sana wa kujieleza kiasi cha kuongea hata kimakabila ili kuvutia wasikilizaji wake, sasa je huyu jamaa ataweza?

Wananchi wanataka mgombea ajieleze why achaguliwe yeye na sio mwingine, atawatendea nn, na kwa njia zipi, sasa mgombea lazima ajijengee uwezo wa kuzungumza tena kwa kujiamini na kuhakikisha anafanya utaratibu wa kupata muda mzuri kutetea sera zake, mambo ya websitehayatakiwi, kwanza watu wenye access na mtandao ni wachache sana.

Waratibu wa kampeni za huyu Bwana kiukweli wana kazi kubwa sana, na ninachokiona sasa inabidi yeye na Duni ambae ndio muongeaji mzuri inabidi watengani ili kuongeza coverage, sasa hapo ndio balaa linakuja, atamudu kuongea kwa kujiamini mikutano mitatu mpaka minne kwa siku moja.
Anahitajika kupangiwa muda mzuri wa kutosha kuongea na waratibu wake wapunguze wazungumzaji na mambo yasiyo ya msingu mgombea aongee kwa muda wa kujitosheleza, mambo ya website yatachochea hasira badala ya kusaidia.
 
UDHAIFU MKUBWA WA MGOMBEA WA UKAWA KATIKA HOTUBA/KUJIELEZA.

Ndg wana jamvi, leo nimefuatilia kwa karibu sana uzinduzi wa kampeni za ndg zetu UKAWA kama vile nilivyofuatilia kwa karibu uzinduzi wa CCM kwenye uwanja huo huo wa jangwani, nikiri wazi UKAWA walijipanga sana kiorganisation ya mkutano na kuhamasisha watu kiasi kwamba watu walifurika mno zaidi sana ya wenzao, na watu walikua na hamasa kubwa mno, na kila ukiwaona unasema hawa wana kiu ya mabadilko.

Ukiacha hayo mazuri niliyosema, kuna jambo nmeligundua ambalo ni baya sana kwa upande wa ndg zetu UKAWA ambapo lazima wajipange, kama nilivyosema mkutano ulikua na hamasa za hali ya juu na watu walikua wanaonekana kabisa wana kiu sana ya UKAWA na kutamani slogan yao ya mabadiliko, bt mgombea wao ambae ni nembo yao kwenye uchaguzi ndg E.N. Lowassa anaudhaifu mkubwa kwenye self expression na hotuba kiujumla ambayo kwa kweli kujirekebisha ni jambo la lazima kama anataka kuwin public mentality ambayo ni muhimu kuhamasisha kura.

Yule Lowassa wa miaka nane iliyopita hodari wa kuongea sio huyu wa sasa, anaonekana dhaifu mno kwenye kuongea, sijajua kwa nn, anaongea bila kujiamini na pia kama anakuwa na uoga kukiongea kwa umakini kile anachokiamini.
JP Magufuli yeye amebahatika sana kipindi hiki, amekua mzungumzaji hodari sana, yupo kwenye chama ambacho wengi wanakiona kama kimechoka lakini kwa namna anvyoongea na kujieleza, wapo watu wanaamini kumbe mabadiliko yanaweza kupatikama ndani ya CCM, amejua namna ya kuwarubuni wapiga kura kisiasa vizuri sana na kwa hoja za nguvu hata kama hazina uhalisia.

Lowassa anatatizo kwenye maeneo yafuatayo hapa chini kama nilivyoshuhudia leo Jangwani na siku za karibuni, wadau mtanikosoa au kuongezea kwenye huu mtazamo wangu.

1.muda wa kuongea, mgombea Uraisi ni mtu anaepaswa kuzungumza kwa muda mrefu zaidi ya wapambe wake na anapswa kujieleza vizuri kabisa ili tumpime kwamba atakuja kufanya nn huyu mtu sio dakika zisizozidi kumi na tano tena nazo zikiwa na matatizo mengine mengi yatakayowapa mwanya wapinzani wake kumshambulia kama nitakavyoendelea hapa chini. Ukawa inabidi wajiongeze kwenye suala la muda, the same niliona wakati wa kura za maoni CCM kingunge alikua anaongea sana kuliko mhusika.

2. Kujadili Non Issues, hapa sijui hajapata washauri vizuri wa kumueleza nn cha kuongea, mambo kama ya Babu Seya, Mashehe wa Zanzibar na Balali, those ar non issues, alipaswa tu kuelezea bila hata kutaja majina wala kuonyesha uelekeo wake, kuna baadhi ya mambo ni ya kimahakama, so utii wa sheria ni muhimu mno na hakupaswa kudiscuss hayo mambo, nilikua naongea na jamaa yangu mmoja akaniambia kuna shida kwa hao watu so lazima asema, nikamwambia hayo mambo ayaache kwa mashabiki hata kama pana mkono wa nani sio vema kudiscuss jukwaani nikosa kubwa sana la kimantiki na kumpa adui nafasi ya kumuattack kwa mambo mengi.

3. Self confidence, hili nalo ni tatizo kubwa sana kwa mgombea wa UKAWA hajiamini kabisa na kama vile haamini anchokisema, muangalie Maalimu Seif, hata kama anakikana alichokisema jana, utaona anaongea kwa confidence sana kiasi cha kuwaainisha wafuasi wake, pia mkumbuke Dr.Slaa, anaongea kwa confidence sana kuaminisha watu wake kile anchoamini, pia hata mgombez wa CCM Magufuli utamuona anavyoongea kwa confidence hata kama cho kitu kinapingana na kile ambacho kinaaminiwa na wanchi. Hii i aleta uhakika sana kwa watu unwaoaleza, sasa EL naonakosa hiiki kitu, ni lazima sasa watu wa UKAWA wamsaidie kupandisha confidence yake.

4. Kuwaza sana kura bila kuelezea ni kwa nn apewe yeye kura, hii ni kama summary ya hayo juu, mgombea wa UKAWA kwa kiasi kikubwa anachowaza na kuongea ni kuomba kura tuu bila kuwashawishi hao watoa kura kwamba nichagueni niweze kuwasaidia kuwatoa kwenye matatizo yenu kwa mikakati na mipango hii sio kuishia tu kuwaza kura bila kusema why upewe kura, hapa JPM anapata crdt kwa kujieleza why apewe kura, na UKAWA lazima wabadilike.

mwisho,
nimalize kwa kuwashauri UKAWA wakati wa siasa za majibizano hasa kwenye non issues zimepitwa na wakati kabisa, kikubwa nikuwaeleza wanachi mambo makuu matatu, kwanini wawachague wao sio CCM, Watawafanyia nini na watafanyaje, habari za individuasm na vijembe zimepitwa na wakati, ni lazima kufanya kampeni kimkakati na mipango timilifu sio majungu na vijembe. Na hii pia inawahusu CCM vijembe na majungu sivyo wananchi wanataka kusikia.

Mgombea wa UKAWA awe monitored vitu gani vya kuongea na kujipanga kwa mtazamo mzuri bila kuharibu taswira ya kampeni zake na pia kuwapa wapinzani wake vitu vya kuongea, fanya kampeni za kushambulia na sio kujilinda.

Karibuni tujadiliane wana jamvi,
You said it all Mfalme...

Napata shida ya nini atafanya Lowassa akiwa katika ziara za kampeni mikoani...Magufuli ni muongeaji mzuri sana...Na ameonekana kuwateka watu kwa uongeaji wake huu...

Lowassa anapendwa na watu hilo halina ubishi...Lakini hawezi kuongea jambo ambalo limewaogopesha hata wafuasi wa Ukawa...Jana pale Jangwani baadhi ya watu walionesha kwenye TV wakianza kuondoka wakati Lowassa akiwa anaongea hali ambayo iliashiria kwamba hawakuridhishwa na kile alichokuwa akikiongea...

Pia kitendo cha Lowassa kusema kwamba alikubaliana na Mwenyekiti Mbowe kuwa kutokana na muda hotuba yake iwekwe kwenye website ya Chama kilikuwa ni kichekesho kingine...Kwani macho na masikio ya watanzania yalikuwa Jangwani...Ule ulikuwa ni wakati na mahali muafaka pa yeye na Mgombea mwenza wake kueleza kwa kina dhana ya mabadiliko wanayoinadi...Lakini haikuwa hivyo...Badala yake wanawaambia watu waende kuisoma hotuba kwenye website!!...Ni watu wangapi wana access na mtandao(internet)?...

Hata ile hotuba ya ITV saa 3 usiku jana ilikuwa ya kukurupuka kwa lengo la kuondoa mapungufu yaliyotokea Jangwani...Sina uhakika kama watu wengi walikuwa na taarifa ya hotuba hiyo na kama iliwafikia watu wengi kutokana na ughafla wake...

Kama ulivyosema hapo juu...Huu ni wakati wa UKAWA na CCM kujikita katika kunadi Ilani zao...Si wakati wa kufanya yale yanayofanywa na akina Sumaye...Makongoro Nyerere..Tambwe Hiza et al...Unatumika muda mwingi kueleza vijembe badala ya kunadi Ilani...Lowassa jana ametumia dk.10 kuinadi Ilani...Muda mwingi umetumiwa na kina Sumaye et al...Magufuli yeye alitumia zaidi ya saa 1 kuinadi Ilani na bado muda ukawa hautoshi...

Hilo la Non Issues za akina Babu Seya...Balali...Masheikh wa Zanzibar tayari nimelieleza pale juu...Haya ni mambo yanayoonekana madogo lakini yanaweza kumgharimu sana Lowassa na Ukawa kwa ujumla...Vipi familia ya Balali ikimjia juu Lowassa kwa kutumia jina la mpendwa wao ambaye ni marehemu kutaka kura?...Vipi wadau wa Mahakama wakihoji kitendo cha Lowassa kuzungumzia hukumu ya Babu Seya (ambayo mpaka Mahakama ya Rufaa iliona kuna hatia ya unajisi na kulawiti?)...Lowassa anahitaji ushauri katika hili maana hii ni mara ya pili analizungumzia...

Pia kitendo cha Lowassa kuwaomba watu wa Dar es salaam kumuombea kura kwa watu wa Bara na ni kichekesho kingine...

Bala.
 
Lowassa Lowassa Lowassa umetuangusha.

Niliwahi kuuliza huko nyuma huyu Lowassa mwenye wafuasi lukuki wanachofuata kwake ni nini?
Lowassa kuongea hawezi hawezi kabisa, sifa mojawapo ya kuwa mwanasiasa ni kujua kuteka jukwaa, uwe muongeaji mzuri, uwe mjenga hoja na nk. Hizi sifa zote Lowassa hana,yaani anazidiwa na Lema.

Na hii inatupa tabu kwetu sisi wanamageuzi tumezoea kusika wajenga hoja, watu ambao ukiwasilizia wanakupa matumaini ya Tanzania ya kesho, wanakutia hamasa ya kupenda na kusikiliza wanasiasa, anapoongea unatamani hazimalize lakini kwa huyu Mh. ni aibu.

Nashindwa kuelewa kama alijiandaa kwa tukio la jana au ndio zile sifa za wanaccm dharau kwa wananchi kama kawaida. Na pia sijuia kama ni macho yangu au ni fikra zangu lakini naona kama Mbowe anampa heshima kubwa Lowassa yaani Mh. anaonekema kama "king" fulani hivi hizi heshima za kinafiki sisi wanamageuzi hatujazizoea.

Pia Mh. Lowassa hivi ulishindwa kufanya mazoezi ya kuongea huku nyumbani kwako? Ukishajifahamu kuwa unaupungufu fulani, na kuna tukio kubwa ambalo unatakiwa "kuwin" watu ni bora ufanye mazoezi ya kuongea nyumbani kwako ukiwa na mkeo pamoja na watoto wako kuliko kutia aibu kama alivyofanya jana? Na hii kitu ufanya watu wengi tu. Tunafahamu kuwa unatatizo la hotuba lakini hii hakufanyi kutojaribu kutatua hilo tatizo. Upinzani ni pamoja na kuuza sera zake na ili uze hizi sera/Ilani kwa wananchi ni lazima uwe muuongeaji mzuri, huku si CCM ambapo mlizoea kubebwa bebwa na jina la chama chenu.

MH. Mbowe tulikupa taadhari kuhusu Lowasa na sasa kunakupata taadhari tena msipokuwa makini mtapokeza hata ile imani ndogo iliyobaki kwenu. Mzee afanye mazoezi ya kutoa speech zenye kueleweka msimuone haya wambieni ukweli maana hotuba ingawaje ni za dk 10 lakini zina makosa mengi.
 
' JANGWANI DISASTER-UKAWA'

MAAFA YA KISIASA VIANJA VYA JAGWANI


Wanajamvi, tume tathmini kwa kina na uyakinifu kuhusu hotubaya UKAWA jangwani

Tutakuwa na mabandiko kuangalia nini kimetokea hadi UKAWA wakajikuta kwenye disaster kubwa kiasi kile

Tunawashukuru wachangiaji walioona mambo mengi na hapa naomba niwanukuu kwa uchache

Mzee Mwanakijiji ' miezi iliyobaki itakuwa hotuba zamitandao? Je, wapiga kura wakubali personality au substance? Watu watajuaje anasimamia alichosema kama hakusema''

King Suleiman ‘maandalizi na uhamasisha ulikuwa mzuri. Maudhui (contents) zilikuwa hafifu sana. Hotuba ilizungumzia trivial matter. Waratibu wa kampeni ya Lowassa na UKAWA wana kazi kubwa sana''

Balantanda ''hotuba yaITV ilikuwa damage control, hotuba ya Jangwani imetisha hata UKAWA wenyewe''

Alinda '' Mh Mbowe tulikutahadharisha kuhusu Lowassa, sasa tunakupa tahadhari nyiningine. Nashindwa kuelewa kama alijiandaa kwa tukio lajana. Lowassa Lowassa Lowassa umetuangasha''

Hayo ni baadhi tu ya maneno ya wanajamvi yaliyosimama wima,yenye mantiki, ukweli , hofu na angalizo.

Tutakuwa na mabandiko 3 kuhusu hili la jangwani na kichwa kidogo cha habari katika uzi huu ni

''JANGWANI DISASTER'

MAAFA KATIKA VIWANJA VYA JANGWANI

CC Tumaini Makene Molemo CHADEMA KWANZA Pasco
 
Back
Top Bottom