Nilipokuja swala la Chadema kukosa muelekeo kwa kweli ninakuunga mkono, ni kweli Mh.
Mbowe amefanya mambo mengi, kuna mambo ambayo yalikuwa mazuri sana, na kuna mambo ambayo yalikitia chama doa kubwa, Mh. Mbowe baada ya matokeo ya uchaguzi basi ilikuwa ni lazima yeye na team yake wajihudhuru lakini kama walivyo viongozi wa kiafrika wote swala la kuwajibika ni mwiko...
Chadema si Chadema ile iliyobeba umoja na matumaini, si Chadema ya viongozi waliokuwa na ujasiri si Chadema iliyokuwa inamsemea mnyoge bali hii ni Chadema iliyokosa mwelekeo.
Ni wakati sasa Mh. Mbowe awaachie vijana wake aliyowandaa zaidi ya miaka 10 kwani huu ni wakati wao na Chadema kinawahitaji sana. Ni wakati wa Mnyika, Mwalimu, Lissu, Lema, kuongoza chama..Mh. Mbowe uliyofanya yanatosha sasa pumzika tuone matunda ya malezi yako.
Nianze ulipomalizia. Moja ya kazi kubwa za Mh Mbowe ni kutoa chama kutoka 'club' ya wastaafu na kuwa chama cha siasa kilichobeba matumaini ya Watanzani. Kazi hiyo ni pamoja na recruitment ya vijana
Vijana wamekuwa chachu iliyoineza Chadema katika maeneo mengi ikiwemo ya vijijini
Tuliona uchaguzi wa serikali za mitaa miaka michache iliyopita ilivyokuwa na nguvu
Kuna picha ya watu kama 20 wakishangilia kutwaa kitongoji huko vijijini kabisa
Tukaona watu wakijitoa na plot zao kule Iringa kujenga ofisi katika sakata la Mwandosya
Chama kikapata wabunge wengi kutoka maeneo ambayo CCM ilikuwa haifikirii
Maeneo salama ya CCM kama Morogoro, Tanga , Lindi ikawa si salama tena
Hayo hayakutokea kwa bahati mbaya ilikuwa ni jitihada za wanachama kufikia matarajio
Tatizo lilianza kuelekea 2015. Tulisema katika uzi huu,kundi lililohamia Chadema kwa muda mfupi na katika taharuki haikuwa jambo jepesi,kama ililazimu busara zilitakiwa kuhakikisha smooth transition
Tatizo la kufanya 'amalgamation' ni kitu kinachohitaji umakini, weledi na maarifa
Tuliposikia 'kanyaga twende' wengine tulifahamu hakukuwa na mipango wala vision
Tatizo hilo linaendelea, ni kama kuna makundi ingawa hayapo wazi.
Kazi alitakiwa kuifanya Mbowe katika amalgamation kupunguza effect ya upungufu wa awali.
Tatizo la pili,katibu mkuu. Dr Slaa alikuwa kama chama na hilo halikuwa utamaduni mzuri.
Kilichopaswa kufanya ni kupata katibu mkuu atakayekuwa na vision ya chama next level
Mbowe kwa mujibu wa katiba kamchagua Katibu mkuu ambaye hakuna sababu ya kutosema kapwaya
Mbowe amejikuta akiwa na wajibu wa KUB. Kama mtakumbuka tuliwahi kusema kazi hiyo anaweza kuifanya mtu mwingine Bungeni ili kumpa nafasi ya kushughulikia mengine, haikuwa hivyo
Ipo hoja dhaifu kuwa katika miaka zaidi ya 15 Mbowe amewezesha chama kuwa na wabunge wengi , kutwaa miji na majiji pamoja na vitongoji.
Ni hoja dhaifu kwasababu si suala la kupigia hatua, ni suala la unapiga hatua kwa kasi gani
Miaka 15 wabunge 30 kutoka 2,wanachama wasubiri mingine 15 kuwa na 60 inaeleza kasi ndogo.
Yes kama ameweza kufikisha hapo sasa atoe kijiti kwa mashine mpya inayoweza kutimua mbio zaidi
Mbio si mikutano tu bali kufanya chama cha upinzani kibeba hadhi yake kama mbadala wa serikali
Katika hayo ni muhimu kikajielekeza katika mambo ya Taifa na kimataifa.
Ni lazima kihakikishe kinagusa maisha ya kawaida ya wananchi na kinakuwa ndiyo 'loud speaker' na ''nyenyere'' wa kuiamsha serikali inapozembea au kulala.
Yapo amkundi ya jamii yenye kuhitaji sauti na sauti hiyo ndiyo ilitegemewa kutoka Chadema
Kwasasa hakuna kinachoendelea zaidi ya kuilamu CCM kwa uonevu.
CCM na serikali wanapofanya hayo ndilo lengo lao,si kuwalaumu kutimiza malengo ya kuua upinzani
Kunahitaji fikra mpya za kukabiliana na tatizo.
Fikra hizo zinaweza kutoka kwa watu nje ya uongozi wa sasa, wawe wazoefu au wenye maono tofauti.
Mbowe haonekani kuwa sahihi tukiangalia anavyoshughulikia mambo ndania ya chama chake.
Na kwa kukosa fikra mpya, sasa Bongofleva inaonekana kama ndiyo njia
Ukitazama madhaifu mengi ikiwemo kuongoza Chadema katika failures nyingi na bado amekuwa excused na ukiangalia anapokipeleka chama, nitashangaa kama kuna mtu atakuwa na matumaini
Katika kuzuia uharibifu unaoendelea hatua za haraka na za dharura zinahitajika
Hii ni pamoja na kumtaka Mbowe atoe nafasi kwa fikra mpya au ashinikizwe kutoa nafasi hiyo
Kusubiri hadi 2018 ni kulea ubovu na pengine kumkabidhi ajaye gari lisilo na taa wala matairi, linaunguruma tu, na abiria wana matumini litaondoka kwasababu kuna dereva mpya
Hapana, kama Chadema wanataka kujirudi na kujitathmini, waache kulalamikia externa factors wa deal na internal factors na hapa pa kuanzia ni kwa Mwenyekiti aliyepelekea chama kudorooora!
Tusemezane