Mkuu
Mag3 na
Kakalende
Kwanza kabisa, Mag3 pole na safari ya 'ukonga'. Kwa muda nilikuwa na mambo mengi sikujua hata nini kilijiri. Muhimu umetoka 'kamiti max'
Pili, kuna kitu Watanzania wanapaswa kukifahamu.
Awamu ya II ilikuwa ya mpito kutoka chama kimoja kuelekea vingi Kama alivyosema Mag3, na tunaweza kuipa benefit of doubt
Tatu, awamu ya Mkapa ilikuja na uwazi na wajibikaji. Tukaona tume za rushwa zikiundwa n.k.
Mwisho wa siku hakukuwepo uwazi , uwajibikaji na rushwa ikazidi mara nyingi na ilivyokuwapo
Nne, akja JK na nguvu mpya, ari mpya na kasi mpya. Hakuna nguvu iliyoonekana wala ari yoyote.
Hakukuwa na kasi bali kudumaa kwetu kama taifa.
Rushwa imekuwa sehemu ya maisha yetu ya kila siku na kitu 'halali' Yale maisha bora hatujui yameishia wapi
Tano, sasa hivi si chama tena, tunaambiwa hapa kazi tu.
Hatujui kazi ipi maana huko nyuma kazi haikuwahi kutoa matokeo tofauti. Tunaaminishwa kuwa CCM inafanya reform
Reform ya CCM inayosemwa si ile ya moyoni. Kama ingalkikuwa ya moyoni, reform hiyo ingefanyika awamu mbili zilizotufikisha hapa.
Hii ni reform ya kuteka nyoyo za wananchi baada ya kubaini wanataka reform
Kwa mantiki hiyo, wananchi wameishi kwa kauli za kubabaisha kama tulizoona juu. Hatuambiwi kazi ni ipi tunaambiwa hapa kazi tu
Kinachotokea ni wananchi kutaka mfumo huu ubomoke. Unabomokaje hilo ni suala lingine.
Hatuwezi kuwaulumu kama wanataka hivyo. Waliopewa dhamana wameshindwa na wananchi wanataka tu kuvunja mfumo wa CCM.
Hii maana yake, wamechoka na 'status quo' wamechoka na udanganyifu wa miaka nenda miaka rudi.
Wananchi wanataka kuvunja tu mfumo wa kauli bila matendo
Ushahidi wa kuchoshwa na kauli upo kwa CCM. Hakuna sera ikiwa na mtajiwa miaka 50 ya record ya utendaji kama chama tawala.
Hawawezi kusimamia record hiyo wamebaki kutupa lawama na tuhuma kana kwamba ni wapinzani.
Wmaebaki kuwadanganya wananchi kuwa tunahitaji bouncer Ikulu ili aweze kupiga push ups
Mwalimu Nyerere hakuwahi kuchuchumaa hata siku moja katika miaka 23 ya uongozi wake.
Alizungumza na wananchi kwa kauli zake ambazo zinatumika hadi leo na wapinzani au CCM.
Miaka 30 ijayo vijana wetu wataangalia jinsi wazee wao walivyokuwa wanapiga push ups za mchangani na si za akili.
Watapita makaburini wakiyachapa viboko na kulaani watawala na watawali. Watachapa viboko makburini ya watawala, na kutemea mate kama si kunajisi makaburi ya watswali.
Watafikiria kile kizazi cha Zinjathropus lkiliendelea kuwepo Tanzania hadi miaka 30 iliyopita.
Watalia kwa uchungu wakishindwa kusoma dua au sala kwa kizazi hiki kilichovia kiakili. Watatuita kizazi cha wajinga na push ups
Katika hilo , sisi sote wa kizazi hiki hatutasalimika. Tutakuwa sehemu ya push ups kwasababu hatukufanya kitu kuzuia ujinga.
Hatukukemea wala kulaani push up ! hatukudai sera, hatukuuliza wapi tulikwama.
Tulibaki kujiunga katika misafara ya kuinama na kupiga push up tukiwa hatuna dawa, shule zetu hoi na maisha duni
Watoto watatucheka sana, hiki ni kizazi gani kilichokuwa hakijitambui
Hatujitambui kwasababu tunalishwa maneno, hatuulizi. Hapa kazi tu, ni ipi hiyo iliyoshindikana miaka 50.
Hatujiulizi ni kazi gani iliyofanyika na ipi imebaki ili tusema hapa kazi tu. Hatujitambui !