Mwalimu hapo juu , tulisema turudi kwenye mada, hata hivyo tunatoka nje kidogo kuweka hoja inayotuondoa katika mada , sawa .
Tunaomba jamvi radhi kuchepuka
Hili la Richmond tuliongelee kwa upana wake tukijua ima ni mbinu za kuwaondoa Watanzania katika hoja, au mbinu za kutafuta ushindi kwa njia za udanganyifu
Richmond imeibuka baada ya ukimya wa miaka 8. Wengine tumepiga kelele sana hadi kuonekana wendawazimu
Tulisema , ni lazima chimbuko la tatizo na wahusika wawekewe bayana ili kulinusuru taifa siku za mbeleni
CCM hawakukubali kwa kutumia wingi na madaraka kama yale ya Spika.
Wanaishi na watuhumiwa kwa miaka 8 bila kusemana si ndani ya kamati , vikao au mikutano.
CCM wana nyaraka zote kama wanavyodai akina Mwakyembe na Sitta
CCM wameshindwa kufikisha nyaraka katika vyombo husika, hatua zichukuliwe kwa miaka 8
Kwa kutambua watanzania ni watu wa matukio na si hoja, bila aibu wanasema hilo ndilo tatizo la umeme na chanzo cha bei kubwa
Wanaotoa madai ni hao wanaoomba ridhaa ya kuongoza. Wamo katika mfumo uliolea matatizo. wanadhani tatizo ni baadhi ya watu.
Richmond haikuanguka kama comet kutoka space. Ilitengenezwa. Inakuwaje mafundi wameachwa kwa miaka 8?
Tunafahamu mgao wa umeme ni tatizo. Serikali iliyopo imengia kukiwa na tatizo hilo, na hadi sasa lipo.
Matatizo yapo katika maeneo mawiili. Kwanza rushwa, kama tulivyowahi kusikia mgao wa kutengeneza ili watu waagize mafuta, na majuzi tulikuwa na escrow ambayo haisemwi kwasababu tu inagusa maeneo kadhaa nyeti
Juzi tumesikia mgao wa umeme kwasababu ya kuunganisha gridi ya taifa. Unganisho hilo linahusu baadhi ya siku.
Mfano, zipo siku nchi nzima inapata umeme, kuna siku umeme unakosekana kwa masaa kadhaa. Hakuna sababu za msingi
Kama Richmond ni tatizo, kwanini wananchi wasijiulize, wale wazazi wanaolala sakafuni na vichanga nao ni sababu ya Richmond?
Wale wanafunzi wanaosoma chini ya mibuyu nao ni tatizo la Richmond? Wale walimu wanaotembea siku nzima kufuata haki zao za mishahara ni Richmond? Akina mama wanaotembea KM 2 na vichanga vyao migongoni kutafta maji nao ni sababu ya Richmond?
Wizi wa taarifa za CAG nao ni Richmond? Misamaha ya Trilioni za kodi inahusiana vipi na Richmond?
Utegemezi wa bajeti nao ni sehemu ya Richmond? Ajali zinazomaliza ndugu zetu nao ni Richmond?
Rushwa hadi kura za maoni, nalo ni tatizo la Richmond?
Escrow na mgao wa vigogo nalo ni tatizo la Richmond? Kukosekana kwa dawa muhimbili kwa kiasi nalo ni tatizo la Richmond?
Wagomjwa kualala mzungu wa nne Amana , Liwale na kwingineko nalo ni Richmond?
Orodha ni ndefu ya matatizo mazito tuliyo nayo. Hili la Richmond ni sehemu tu ya matatizo mazito tuliyo nayo.
Inaendelea..