CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

Kuhusu udini kausemea, lakini hasa kajikita zaidi kwenye maadili ya viongozi wa dini. Amesema alielezwa na 'mshenga' .... kuwa kunabaadhi ya maaskofu wa maadhehebu ya kikristo(katholiko likiwemo) wamehongwa na 'wanasiasa' kuanzia kati ya mil.50 na kuendelea. Akamalizia kwa kusema kama maelezo yale (ya mshenga) yalikuwa ya kweli amesikitika sana.
Mkuu katika bandiko 2015-391 hapo juu nilisema naishia pale makusudi kabisa.

Ukisoma vizuri nimeandika 'collateral and colossal damage' naomba nifafanunue

Collateral damage ni uharibu usiokusudiwa. Kwa mfano, ndege inaposhambulia askari , mabomu yakaangusha nyumba, raia wakafa huo ndio mfano wake.

colossal damage ni uharibu mkubwa sana, wa kishindo.

Kilichotokea katika hotuba ya Dr Slaa ni vyote viwili. Lakini collateral damage ni kubwa sana kuliko watu wanavyoona

Katika nyakati hizi za uchaguzi kila kitu kinaangaliwa kutoka angel tofauti na si kila mtu atakuwa na muda au wasaa wa kutafuta ukweli. Habari zinakuwa sensitive kuliko inavyodhaniwa

Kwa mfano, tumesikia mtu akisema Lowassa hakwenda Ludewa kwasababu ya afya.

Huo unaweza kuwa uongo, wapo watakaounganisha dot zisizohusiana na kupata ukweli kutoka katika uongo.

Wapo watakaofanya spinning kupata maana waliyokusudia

Kwa hili la Dr Slaa na narudia tena, ana haki ya kujieleza kama wengine, alichosema kuhusu udini anaouzungumzia Alinda ni kibaya.

Ni kibaya si kwasababu hakupaswa kusema, bali alipaswa kusema akiwa na uhakika.

Kwa maelezo yako mstari wa mwisho anasema ' kama aliyoelezwa ni ukweli, alikitika sana'

Maana yake hakuwa na uhakika, na busara ingemlazimu akae kimya.

Kwa dhamana yake katika umma na 'credibility' anayosema, kutoa kauli kama hiyo haikuwa sahihi.

Narudia haikuwa sahihi kwasababu hakupata ukweli, kama wapo wanaotafuta ukweli kupitia hisia zake, basi watakuwa wameupata

Inaweza kuwa hakukususdia kusema hivyo, lakini ndio maana halisi ya collateral damage
 
Swali la msingi ni Je, Lowassa ni Asset ama Liability kwa CHADEMA??
Mkuu , katika uzi wa kuelekea uchaguzi tulisema hivi

'' Chadema na UKAWA wakiwa kama taasisi wanapaswa kufanya tathmini ya uhakika na kina kabla ya kuchukua maamuzi'

Tukauliza, ' kulifanyaika analysis? Tukahoji mbona kulikuwa na flip flop kuhusu suala zima? Tuliohoji, walipima kama ni asset au liability? na walikuwa na plan zozote za kukabiliana na matokeo ya maamuzi yao

Hii ilikuwa wakati picha zinazagaa zagaa , UKAWA wakisema si kweli

Tulihoji sana kuhusu mtaji wanaousema na kama walifanyia (nasisitiza) analysis ya kutosha

Mbowe nadhani alitusoma na alichosema 'Kanyaga twende katika baraza kuu'' hiyo ndiyo analysis tuliyosikia
 
Nguruvi3,

..hivi mbona mambo haya hayatokei CCM?

..yaani CCM wanaweza kufanya chochote, kwa yeyote, na hakuna mtu wa kuleta ubishi-ubishi.

..kuna mtu kama Salim Salim. kwa jinsi alivyochafuliwa ungetegemea angemwaga mboga na ugali kama alivyofanya Dr.Slaa. Au, Mzee Malecela alivyokata bila maelezo ya kuridhisha.

..Kwanini CCM wanaonekana kuwa wavumilivu na watiifu kwa chama chao, kuliko hawa walioko vyama vya upinzani?

cc Mkandara, betlehem, Mzee Mwanakijiji, Alinda, Mwalimu
Mkuu ni swali gumu sana

Nadhani approach ya watu si ya mantiki (logic) bali ya umaarufu (popularity)

Wakati Mbowe anaelezea hili suala, tulijua kabisa handling yake itakuwa ni poor. Kanyaga twende !
Na alizidi kueleza katika hali ya kutia hasira na hilo ndilo linatokea sasa.

Kwa upande mwingine, Dr Slaa anaonekana kuongozwa na hasira badala ya busara
 
Sidhani kama hii press conference ya Dr. Slaa itabadili mawazo ya watu kwenye kupiga kura.
Nasema hivi kwa mantiki mbili;
1. Siasa za Tanzania sio za kuangalia hoja na sio za kuhoji viongozi au chama wamekifanyia nini kwa miaka mitano au kumi iliyopita na kuwauliza watawafanyia nini watanzania kwa sasa.
Siasa zetu ni za kuangalia 'likeable' president material na ndio maana JKikwete alishinda kwa wingi mkubwa wa kura 2005. Hata kama alikuwa ana hoja mbovu. Watu hawakuangalia hilo wameangalia ile 'populalrity' yake.
Na hata ukiangalia baada ya Lowasa kuhamia Chadema jinsi alivyoweza kuondoka na wananchi wenye mapenzi kwa CCM kuja Ukawa. Kifupi ni kwamba ujio wa Lowassa ukawa umewafanya wawe popular sana.
2. Uchaguzi wa mwaka huu hakuna msafi hata kidogo. Wanasema Lowasa ni fisadi (ikiwa na maana sio msafi), magufuli pia sio msafi, pamoja na skendo zote zilizo chini ya uongozi wake inadhihirisha jinsi gani alivyo sio msafi.
Kwahyo wananchi watabaki kupiga kura sio kuangalia usafi tena, wataangalia utashi wao.
 
HOTUBA YA DR SLAA

Wanaduru, kama ilivyo kawaida haonewi mtu , hapendelewi mtu. Kinachopendwa ni taifa

Baada ya hotuba ya Dr Slaa, tumeona upo umuhimu wa kujaribu kuiangali hotuba hiyo kwa kina na uyakinifu

1. Hotuba imeeleza mambo ya maana na ya msingi

2. Hotuba imeeleza mambo yanayokinzana ndani yake. Kwamba msemaji amejipinga mwenyewe

3. Hotuba inazidi kutoa ukweli wa kile tulichokuwa hatujui

4. Hotuba inatueleza jambo kuhusu maadili , uadilifu wa watu na viongozi

Tutakuwa na mabandiko 2 kuhusu hili.

Kwa wakati huu mjadala uendelee kama kawaida
 
Last edited by a moderator:
Kwa maelezo yaliyopo inaonekana ni wazo la Dr Slaa

Kimsingi, Dr alifikiria suala hilo hadi kuliwekea masharti

Tofauti ni ilikuja kutokana na modality ya kupokea ujio huo

Kama nitakuwa sahihi

Sasa kama Lowassa ni fisadi kama alivyotueleza, ni kitu gani kilimshawishi mpaka kutoa wazo la Lowassa kuungana na Ukawa?
Hivi hayo masharti yalikuwa ni ya Lowassa na wafuasi wake tu au yalikuwa ya kila mtanzania anayetaka kujiunga na chama (hasa sharti no.3 kama alivyoletwa na ndugu tujitegemee)

Hivi kuna mwananchi yeyote katika chama chochote hapa Tanzania anayeomba uwanachama na kupewa masharti kama waliyopewa akina Lowassa? hapa tunaongelea uanachama si urais au uongozi.. Na je masharti ya kujiunga na Chadema ni yapi?

Kama nimemsoma vizuri ndugu yangu Tujitegemee Lowassa alitimiza
Sharti no.1 (Yaani Lowassa alitamka kuachana na CCM)
Sharti no. 2 (Lowassa alijibu tuhuma ingawaje si kama tulivyotaka sisi au Dr. Slaa bali alivyoona yeye inafaa na hii ni haki yake)
Sharti no.3 (Lowassa alitangaza kuwa anahamia Chadema)
na Sharti no.4 (uongozi wa chadema baada ya kukaa vikao waliamua kumpokea Lowassa ingawaje Dr. slaa hakukubaliana nao kitu ambacho ni haki yake kwani si lazima ukubali kila kitu lakini maamuzi ya chama ni lazima yaheshimiwe)

Sasa kama alivyotaka ndivyo ilivyokuwa sasa tatizo liko wapi?

Na kama kweli kuwa labda Dr. Slaa alichotaka kutoka kwa Lowassa sicho alichofanya je kulikuwa na sababu ya kutoa maneno yote yale mpaka kufikia mambo ya maaskofu?

Kulikuwa na ulazima wa kuungana Sitta na Mwakyembe kweli?

Kulikuwa na haja ya kutoa tuhuma lukuki za kuhongwa kweli?

Hivi busara ya Dr. slaa imekwenda wapi? Je Sumanye na viongozi wengine waliohamia Chadema wanahusikaje na mambo ya Richmond? Sumaye si Chadema yeye ni mpambe wa Lowassa je Dr. Slaa alikuwa na haja gani ya kumshambulia Sumanye?

Dr.Slaa kwa kweli leo ameniacha na maswali mengi kuliko majibu.

Lowassa ni mchafu kama alivyotuaminisha je alistahili hata kumpigia Mwenyekiti wake kumwambia jkuhsu ujio/kukatwa kwa Lowassa?

Tulishinda tunamrushia mawe Mbowe kumbe mtu kaletwa na Slaa halafu Slaa kala kona zigo katushwa Mbowe.. hama kweli dunia ni tambala bovu..
 
Dr. Slaa inavyoonekana ni anataka kustaafu kwa shari na si kwa amani kama anavyosema. Kwanini aseme anawasubiri Chadema/Lowasa wamjibu? Inamaana ameficha ushahidi ili wakimjibu na yeye aje kuwajibu kwa ku-reveal huo ushahidi kidogo kidogo?
Hapa ndo napata shaka kuwa Dr. Slaa anaucheza muziki aliowekewa na watu maalumu. Huku sio kustaafu siasa kwa amani hata kidogo na inavyoonekana ni kustaafu siasa kwa wote tukose.
Prof. Lipumba na Dr. Slaa wote wamejitoa kwenye vyama vyao baada ya Ukawa kuwatosa wote na kumpa Lowasa. Inamaana yalikuwa mapandikizi ya CCM kwamba yamebuma na hawakuwa na plan nyingine zaidi ya wao kutolewa?
Pia kwa wakati huu nawashauri Ukawa na Chadema wasimjibu chochote Dr. Slaa, waishi kama hakuna kilichotokea. I tell you, ndani ya week Dr. Slaa atakuwa ameshasahaulika.
Sasa huo ushahidi anaosema anao sijui ataita tena press conference kuumalizia kuutoa?
 
Sasa kama Lowassa ni fisadi kama alivyotueleza, ni kitu gani kilimshawishi mpaka kutoa wazo la Lowassa kuungana na Ukawa?
Hivi hayo masharti yalikuwa ni ya Lowassa na wafuasi wake tu au yalikuwa ya kila mtanzania anayetaka kujiunga na chama (hasa sharti no.3 kama alivyoletwa na ndugu tujitegemee)

Hivi kuna mwananchi yeyote katika chama chochote hapa Tanzania anayeomba uwanachama na kupewa masharti kama waliyopewa akina Lowassa? hapa tunaongelea uanachama si urais au uongozi.. Na je masharti ya kujiunga na Chadema ni yapi?

Kama nimemsoma vizuri ndugu yangu Tujitegemee Lowassa alitimiza
Sharti no.1 (Yaani Lowassa alitamka kuachana na CCM)
Sharti no. 2 (Lowassa alijibu tuhuma ingawaje si kama tulivyotaka sisi au Dr. Slaa bali alivyoona yeye inafaa na hii ni haki yake)
Sharti no.3 (Lowassa alitangaza kuwa anahamia Chadema)
na Sharti no.4 (uongozi wa chadema baada ya kukaa vikao waliamua kumpokea Lowassa ingawaje Dr. slaa hakukubaliana nao kitu ambacho ni haki yake kwani si lazima ukubali kila kitu lakini maamuzi ya chama ni lazima yaheshimiwe)

Sasa kama alivyotaka ndivyo ilivyokuwa sasa tatizo liko wapi?

Na kama kweli kuwa labda Dr. Slaa alichotaka kutoka kwa Lowassa sicho alichofanya je kulikuwa na sababu ya kutoa maneno yote yale mpaka kufikia mambo ya maaskofu?

Kulikuwa na ulazima wa kuungana Sitta na Mwakyembe kweli?

Kulikuwa na haja ya kutoa tuhuma lukuki za kuhongwa kweli?

Hivi busara ya Dr. slaa imekwenda wapi? Je Sumanye na viongozi wengine waliohamia Chadema wanahusikaje na mambo ya Richmond? Sumaye si Chadema yeye ni mpambe wa Lowassa je Dr. Slaa alikuwa na haja gani ya kumshambulia Sumanye?

Dr.Slaa kwa kweli leo ameniacha na maswali mengi kuliko majibu.

Lowassa ni mchafu kama alivyotuaminisha je alistahili hata kumpigia Mwenyekiti wake kumwambia jkuhsu ujio/kukatwa kwa Lowassa?

Tulishinda tunamrushia mawe Mbowe kumbe mtu kaletwa na Slaa halafu Slaa kala kona zigo katushwa Mbowe.. hama kweli dunia ni tambala bovu..

Kuna kitu nyuma ya Dr. Slaa. Ili tujibu hayo maswali aliotuachia inabidi tumjue anamchezesha huu muziki.
Usikute yeye ndo amekuwa mdomo wa mtu fulani kusemea haya.
 
Nimetumiwa audio ya Lissu akihojiwa na chombo cha habari ila sijui ni chombo gani..

Nitajaribu kumnukuu.

""Ilipofika mwezi wa tano Dr. Slaa alianza maongezi ya kumleta Lowassa.. ""
(hapa rejea kauli ya mshenga Gwajima akimpigia simu kwambia kuwa Lowassa amekatwa)

Mwanandishi anauliza kilichoharibika ni nini kama Dr. Slaa ndiye aliyepanga?

Lissu anajibu "Nilichoharibika ni first lady! mama amekataa, siku ambayo kamati kuu imempokea Edward Lowassa Dr. Slaa alilala kwenye gari, alitupiwa mabegi yake na kesho yake akasema anataka kujihudhuru (rejea Prof. safari kuchana barua yake ya kujihudhuru).. (hii kitu niliwahi kuisoma ktka jukwaa la siasa)

Mwandishi: Ni hatua gani mnafanya maana yeye amesema hajiusishi katika chama?

Lissu anasema " Kama nimemsikia sawa sawa amesema yeye hana chama hajiusishi tena na siasa lakini mtu anayesema hajihusishi na Chama mwezi huu amepokea mshahara wa chama, anaishi katika nyumba aliyonunuliwa na chama,anatembea na gari ya Katibu mkuu wa chama analindwa na walinzi wa chama halafu anatukana chama..""
Na atwambie nani aliyemuandalia mkutano wa leo wa Serena Hotel?

Tundu tulizungumuza kwenye kamati kuu, Lowassa alijibu tuhuma zake kwenye kamati kuu na akatwambia kwamba aliyeruhusu mkataba wa Richmond alikuwa Rais Kikwete na Dr. slaa alikuwepo pamoja na wajumbe wa kamati kuu.

Kuhusu wabunge wengi Lissu anasema yeye kama mwanasheria mkuu wakati Dr. Slaa anamtafuta Lowassa hakumshirikisha na swala la wabunge hakuna lilipoandikwa""

Najaribu kufatilia ni redio gani ila ni redio za nje ya nchi... BBC au Voa au Deutsch welle
 
Naona kama Lissu amekurupuka kumjibu Slaa....

Binafsi siwezi kuamini eti u First lady ndio chanzo cha yote haya...

Habari za kutupiwa mabegi nje na kulala kwenye gari ni kichekesho kingine kwenye maelezo ya Lissu...

Ni bora Lissu angepiga kimya tu ama angejipanga kujibu hoja baada ya hoja kwenye 'maelezo' ya Daktari Slaa...
 
Ila swali la msingi ni kwanini Dr. Slaa alimtafuta Lowassa? Maana mazungumzo ya Dr. Slaa na Lowassa yalianza tangu May tena bila viongozi wa chama kufahamu.. na alipokatwa ndo Gwajima alimpigia simu na kupeleka wazo kwa Mwenyekiti..

Jioni - Sauti ya Amerika Kuanzia dk ya 11
 
Kwa mambo yanayotokea sasa hivi inahitaji utulivu sana kuamini hizi kauli za wanasiasa...

Kwa kauli alizozitoa leo na alizozitoa kipindi cha nyuma kuhusu Lowassa ni vigumu sana kuamini kwamba Dk. SLAA alianza kuzungumza na Lowassa kuanzia May....Hata uso wake tu Dk. SLAA unaeleza kila kitu...

Binafsi tangu mchakato wa kumuingiza Lowassa CHADEMA/UKAWA nimekosa kabisa imani na Mbowe...Lissu et al....Si wa kweli...Hasa walipokanusha kwa nguvu zote Lowassa kuhushuria CC ya CHADEMA kwa mara ya kwanza...

Hivyo nashawishika kuamini kwamba kauli nyingi alizoongea Lissu leo ni za kutunga....Hazina mashiko kwa kweli...
 
Mkuu TUJITEGEMEE wazo la kumkaribisha Lowassa Ukawa7Chadema lililetwa na nani?
Nisamehe kama itakuwa usumbufu kuweka maelezo yote haya. Ila Mkuu jibu lako liko namba 8 mpaka 10
-------------------------
HOTUBA YA Dr. SLAA
====================
1.Napenda kumshukuru mwenyezi mungu kwa kutujali uzima.

2. Nimeamua kujitokeza leo hii ili kumesha upotoshaji na kuuweka wazi ukweli.

3.Sina tabia ya kuyumbishwa na ninasimamia ninachokiamini.

4.Sina ugomvi na kiongozi yeyote maana siasa sio uadai.

5. Siasa inapoongozwa kwa misingi ya upotoshaji, matokeo yake ni vurugu.

6. Naweka wazi kuwa mimi sikuwa likizo na hakuna aliyenipa likizo yoyote.

7.Kilichotokea ni kuwa niliamua kuachana na siasa tangu 28.7.2015 saa sita usiku baada ya kutoridhishwa na kilichokuwa kinaendelea ndani ya chama changu.

8.Ni kweli nilishiriki kumleta Lowassa CHADEMA Lakini nilikuwa na misimamo yangu ambayo ilitufanya tusielewane.

9. Baada ya Lowassa kukatwa pale Dodoma, Gwajima ambaye ni mshenga wa Lowassa alinipigia simu kutaka kujua nii cha kufanya.

10. Nilimpigia Mwenyekiti Mbowe kumjulisha na tukakubaliana kupanga muda wa kuwasikiliza.

11. Kabla ya kuanza kuwasikiliza, msimamo wangu ulikuwa ni kumtaka Lowassa kwanza atangaze kuhama chama, aweke wazi ni chama gani anaenda na ajisafishe juu ya tuhuma zake

12.Tangu akatwe jina, Lowassa hakutangaza kujitoa CCM na wala hakujisafisha na tuhuma zake, kitu kilichonifanye nitofautiane naye.

13. Niliwauliza wanachadema wenzangu kuwa Lowassa anakuja kama Mtaji au Mzigo?

14. Swala sio urais kama watu wanavyozusha, mimi nilikuwa nataka mgombea mwenye uwezo na sifa ambaye ataweza kuitoa CCM. Sikuwa na tamaa ya urais kama watu wanavyosema

15. Tangu Gwajima atupe taarifa za ujio wa Lowassa, Swali langu la Lowasssa kuwa Mtaji au mzigo halikuwahi kujibiwa.

16. Nilitaka kujua ni mtaji gani lowassa atakuja nao na ni viongozi gan atakuja nao.

17. Nilijibiwa kuwa anakuja na wabunge 50 wa CCM, wenyeviti 22 wa mikoa na wenyeviti 80 wa wilaya.

18.Baada ya ahadi hiyo, nilitaka sasa nipewe majina ya hawa watu lakini mpaka tarehe 25 july sikupewa hayo majina

19. Wenzangu waliniambia kuwa tarehe 27 niitishe kikao cha dharura ila niligoma kwa sababu nilikuwa sijapewa haya majina

20. Ndani ya kikao hicho, tulianza kwa mabishano makali kati yangu na Mbowe, Lissu na Gwajima, viongozi wenzangu ni shahidi na mungu anajua. Msimamo wangu ulikuwa ni uleule kujua mchango wa Lowassa

21. Kikao kile kikavunjika, baadae tukaingia kamati kuu lakini bado msimamo wangu ulikuwa ni uleule. Baadae nikaandika barua ya kujiuzulu.

22.Profesa Safari aliichana ile barua.

23.Cha kusikitisha ni kuwa Kesho yake picha zikaanza kusambaa mtandaoni zikimuonyesha la lowassa japo viongozi wangu walizikana zile picha. Kibaya ni kuwa viongozi waliuficha ukweli

24. Kesho yake niliandika tena barua rasmi ya kujiuzulu.

25. Baada ya pale zikaanza propaganda za uongo zikimuhusisha hadi mke wangu eti kanizuia.

26. Naomba watanzania wajue kuwa mke wangu hakuwahi kunizuia kwa lolote, lkn hata angefanya hivyo sio mbaya maana hata yeye ni mwanaharakati mwenye uchungu na nchi hii.

27. Mke wangu aliwahi hadi kuumia wakati akipigania ukombozi wa nchi hii.....Lakini sio mbaya, familia yangu imezoea propaganda.

28. Kikubwa katika harakati ni credibility ambayo lazima uilinde na mimi sitaki jina langu liharibiwe na ni haki yangu.

29. Maslah mapana ya taifa ndiyo yaliyotufikisha hapa na sio maslahi binafsi.

30.Lowassa na wapambe wake ni waongo maana hakuna hata kipengele kimoja walichokitekeleza.

31. Tulitaka hao wabunge 50 waje kwanza kabla ya mchato wa uteuzi ccm

32. Napinga kuchukua makapi ya CCM kuyaita MTAJI.

33.Mtu kama Sumaye ni FISADI na nilikuwa siongei naye

34. Sumaye aliwahi kusema CCM wakimchagua Lowassa atahama chama. Leo Lowassa kawaje msafi??

35. Tulitaka Mtaji toka kwa Lowassa na sio MAKAPI

36. Wenyeviti walioletwa na Lowassa ni MZIGO na namjua vizuri. Akithubutu kunijibu ntamwaga UOZO wake wote

37.Nani asiyejua Guninita pia ni mzigo??

38: Nawataka viongozi wangu wanijibu ni mtaji upi walioupata toka kwa Lowassa.

39. Mimi ni Padri Mstaafu, sipendi siasa za uongo.

39. Ukisema unataka kuiondoa CCM ni lazima ujikumbushe misingi ya CHADEMA ambayo ilikuwa ni uadilifu. Leo chadema hii ina Uadilifu gani??

40. Namshangaa sana Lowassa eti kusimama mbele ya watu akijinasibu kuwa ni msafi.....kwamba mwenye ushahidi aende Mahakamani. Ni dhambi kupotosha watu.

41. CCM hawana ujasiri, ni waoga na ndiyo maana wamewalea watu kama akina Lowassa

42. Ukitoa kinyesi chooni na kukipeleka Chumbani maana yake hata chumba chako ni CHOO na kitakuwa kinanuka zaidi kulicho choo cha kawaida

43.Mimi nilikuwepo wakati sakata la Richmond likijadiliwa.Mimi nina ugomvi wa muda mrefu na Lowassa.

44. Mwaka 2010 mimi nilimtaka Lowassa atangaze Richmond ni ya nani.

45. Leo tena namtaka Lowassa namtaka Lowassa atoke hadharani atangaze Richmond ni ya nani. Unaposema ni ya mkubwa, atuambie mkubwa gani

46. Ukitaka kuijua Richmond rejea Ripoti ya Mwakyembe. Nampongeza Mwakyembe na Sitta kujitokeza hadharan kuusema ukweli.

47. Siku moja kabla ya ripoti kusomwa, nililetewa Rushwa ya milioni 500 ili tukaupindishe ukweli bungeni lakini nilikataa

48. Ripoti ya mwakyembe iliamua mambo mawili, moja; Lowassa ajipime au bunge lijadili na lichukue ripoti. Lowassa kuona hivyo akaamua kukimbilia kujiuzulu kukwepa aibu ya kung'olewa na bunge

49: Lowassa haaminiki, ni muongo na hastahili kuwa Rais wa nchi....

50. Lowassa ni FISADI na kama mimi ni muongo ajitokeze hadharani akanushe

51. Anasema Lowassa ataleta maji, mbona jimbo lake la Monduli halina Maji???

52. Mnasema Lowassa kaanzisha shule za kata, iv mjua msingi wa shule za kata? waandishi rudini shule mkajifunze upya.

53.Nilifanikiwa kuijenga Chadema na ikawa tumaini jipya la watanzania.....Vijana wangu wa Chadema, naomba niwe mkweli propaganda imekivamia chama.

54. Inasikitisha kuona CHADEMA inajaza mabasi pale jangwani badala ya watu.....alafu mnawadanganya watu eti ni MAFURIKO

55. CHADEMA ya kipindi changu ilikuwa inakemea Rushwa. Niambien leo chadema watasema nini kwenye majukwaa?

56. Mnaomtetea Lowassa na nyie jitokezen hadharani...mimi nasema kwa sababu nina ushahidi na sio lazima ushahidi huu niupeleke mahakamani.

57. Wenye uwezo wa kumpeleka Lowassa Mahakamani ni Serikali, na mwakyembe alisema juzi kuwa kesi ya jinai haina kikomo, mtu anaweza kushitakiwa muda wowote

58. Sitaki kuingila swala la Babu Seya, lakini waliolawitiwa ni watoto waliokuwa chini ya umri. kwa nini haki yao ipotee?

59. Rais hana mamlaka ya kumtoa Babu Seya. Lowassa asiwadanganye.

60. Kuhusu swala la Masheikh, Sumaye ndiye aliyeamuru mapolisi wavamie misikiti wakiwa na mbwa......Watanzania msikubali kudanganywa. hizo ni propaganda za wasaka urais

61. Masikubali Rais Muongo na mimi naapa ntapiga kelele kila kona kumpinga Lowassa.

62.Lowassa alipokuwa waziri mkuu, matatizo yanayotokea leo hayakuwepo? mapigano ya wakulima na wafugaji hayakuwepo?

63. Lowassa akiwa waziri mkuu alisababisha migogoro mizito sana kati ya monduli na karatu. Rais wa aina hii wa nini?

64. Naomba nisiongee mengi kwa sababu ntakosa ya kusema siku nyingine.....Nawataka Lowassa na Sumaye wajitokeze kunijibu.

65. Siku nyingine ntakuja kuongelea kuhusu hisa za Lowassa kwenye makampuni

66. Nahitimisha kwa kusema kuwa Nimestaafu siasa na sina chama lakini nina nchi, hivyo ntaendelea kuwatumikia watanzania kwa jinsi mungu alivyonipa vipawa

67. Narudia tena, Sina chama na sitajiunga na chama chochote.

Waandishi wanauliza Maswali:
Mwandishi: Umesema ujiungi na chama chochote, utawasaidiaje watanzania? Rais gan unamuunga mkono?

Mwandishi Guardian: Ulisema Lowassa atakuwa assert kama atakuja na wabunge na hao wenyeviti. Je angekuja kama assert ungeyasema haya yote?

Mwandishi binafsi: Umesema na Chadema ni makapi? Mwaka 1995 Uliihama CCM, Je na wewe ni KAPI?

Mwandishi-Azam: Umetangaza kustaafu siasa, lakini bado unakadi ya CCM na CHADEMA? Je utazirudisha?

Mwandishi Blog: Unaonekana baada ya chedema kukutosa ndo maana unamshambulia Lowassa, je ni kweli?
 
Last edited by a moderator:
Watanzania wengine ni watu wa ajabu sana. Sijui wanataka mabadiliko ya aina gani? EL mwenyewe alikubali makosa na kuachia uwaziri mkuu hilo nalo wanaliona dogo sijui watakua lini. EL ni Jamabazi sugu ambalo uroho wake wa madaraka umeharibu upinzani. Kama kweli alikuwa na nia ya kuwaendeleza Watanzania ilikuwaje alishindwa wakati alipokuwa waziri mkuu? Mbona Sokoine aliachia ngazi kwa sababu ya afya yake na baadaye alirudi na alionekana kiongozi makini, sasa huu umakini wa EL ni upi? Wa kugawa pesa za peremende?

Mark my word this country will never be governed if EL win, but he will never come what may be.
 
Mark my word this country will never be governed if EL win, but he will never come what may be.
Mkuu, hebu naomba uitafsiri hii kwa kiswahili, wengine ung'eng'e ulitupitia kando. Siulizi kwa kejeli tafadhali, nisingependa nitie neno kwanza mpaka hapo nikiwa na uhakika nimeelewa kinachoongelewa.
 
Kama umemsikia vizuri Dr. Slaa amesema kuwa alikuwa mmoja wa watu waliomleta Lowassa Chadema .. alipigiwa simu na Gwajima na yeye akasema mpaka aongee na Mwenyekiti hivyo utaona Lowassa alitoka kwa Dr. Slaa si kwa Mbowe kama tulivyokuwa tunaaminishwa..

Naam, hata mimi nilidhani Mbowe ndio alifuatwa aka shauri wenzie, kumbe mposaji alikuwa Slaa Gwajima mshenga
 
Back
Top Bottom