CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

Alinda;13848277] Ndio Sumaye, Masha au kiongozi yeyote yule anapotaka kuhamia chama fulani huwa kuna mawasilina kabla.. Hivi unafikri Sumaye aliamka asubuhi na kusema leo naamia Chadema bila kuwa na mawasiliano na viongozi?

Hivi inakuingia akili Gwajima anyanyue simu na kwambia Dr.Slaa kuwa jamaa ameishakatwa na Dr. Slaa ajibu kuwa akaongee na Mwenyekiti? Kama ni hivi nilitegemea Dr.Slaa ajibu kuwa amekatwa kwa sababu ya ufasidi wake au ajibu kitu chochote si kusema aongee na Mwenyekiti? Hii sentensi ya Dr. Slaa inazdhhirisha alichongea Lissu ni kweli kwamba kabla ya Lowassa kukatwa kulikuwa na maongezi kati ya DR,Slaa, Gwajima na Lowassa...

Na katika simu ya Gwajima Dr. Slaa hakusema kuwa alimuombea kujiunga na Chadema bali alimpigia simu kumpa taarifa ya kukatwa! na Dr, Slaa anajibu kuwa aongee na Mwenyekiti sasa kama hawakuwa na mazungumzo kabla basi hii kauli ya niongee na mwenyekti ilikuwa ya nini?
Alinda , kama utakuwa umetusoma katika yale mabandiko 4, tumemnukuu Dr Slaa akisema 'Gwajima alimpigia simu na kusema, Lowassa kakatwa, sasa nini cha kufanya? Hiyo tu inaonyesha kulikuwa na maongezi yaliyokuwepo, alichokifanya Gwajima ni kumtaarifu rasmi kuhusu matokeo ambayo wote walikuwa wanayasubiri.
Kwani wakati Gwajima anampigia Dr. Slaa simu ya kumpokea Lowassa, huyu Dr. Slaa hakufahamu kuwa Lowassa ndio yule yule ambaye alikuwa anatutangazia kuwa ni fisadi? na kama alipigiwa na Gwajima simu alishindwa kumwambia hapana sisi Lowassa ni kapi na sisi hatuchukui makapi?
Haya pia tumeuliza. Ukisikiliza Dr Slaa alivyoongea kwa hisia na hasira kuhusu ufisadi, hakuna mtu angetegemea hata kuwa na wazo la kumpigia simu mwenyekiti

Pengine angemwambia Gwajima siku hiyo iwe ya mwisho kuongea kuhusu Lowassa.

Kwa maelezo yake Slaa akaendelea kuwa kiungo kizuri. Ndio maana tulihoji, katika point karibu 78 Dr salaa hakuona tatizo hadi point ya 68 kwenda mbelea

Kwa kupoteza uelekeo akaanza mambo ya shule za kata, kushambulia watu. Ilikuwa dhahiri, Dr alikuwa na Ombwe la hoja.

Ninamheshimu sana, lakini kwa hili tumwambie, angekaa kimya ingalikuwa bora
 
Tukubali tu kwamba kwa hali ilivyo sasa lolote linaweza kuzungumzwa kwa lengo la kutuliza/kuondoa athari/hasara itayatokana na kauli za Dk. SLAA jana....Mengi yatazungumzwa lakini ukweli wanaujua Slaa, Mbowe, Gwajima na Tundu Lissu
Ni kweli , lakini pia mantiki na hasa kauli za Dr zinatoa uelekeo mkubwa

Kuna tunayohoji ya wazi. Hivi Dr anakiri kumkaribisha Lowassa halafu mwisho wa hotuba anamkandia kwa ufisadi kuna mantiki hapo?

Halafu kashambulia watu wengine kama Guninita, Msindai n.k. akihusisha na suala lake. Kuna ukweli hapo?

Maana ukitazama matatizo yapo na viongozi wenzake, Dr ana skew info kiasi cha kuchanganya watu kama akina Guninita au Msindai ndilo tatizo

Dr Slaa katika ile press conference hakujianda kujenga hoja.

Nakubaliana naye kwa baadhi ya mambo aliyoongea. Tatizo ni kuwa hakuwa 'sober' aliongozwa na hasira zaidi badala ya hoja.

Ujenzi wa hoja zake ukageuka kuwa ule wa akina dada wanagombania Hina ya mikononi. Mwisho ugomvi wao utasikia 'ndio maana unakula maharage kila siku. Mwingine atajibu, ndio maana mama yako anavaa khanga za urafiki. Mwingine, pochi yangu bei mbaya wewe,! Atajibiwa, angalia boyfriend wako anaendesha corolla''

Mzozo utaendelea kiasi kwamba ukifika hapo hutajua ugomvi wao ulihusu Hina ya mkono ya damu ya mzee iliyokoza

Ndicho alichofanya Dr. Badala ya kueleza mambo yaliyomsibu tena kwa utaratibu trumeona akiongelea shule za kata, maji Monduli, Guninita, Sumaye na Polisi misikitini n.k yaani alikuwa disoriented kabisa

Nina respect na huyu mzee, tunawajibu wa kumuambia hapana mzee tulia hapa utavunja heshima yako
 
Hili jukwaa la great thinkers nalo mmeligeuza jukwaa la kampeni na propaganda.

Swala la Slaa kumkaribisha Lowassa Chadema sio big deal.
Tatizo ni kumsimamisha agombee urais.

Hata kule CCM walipomkata Lowassa hawakumfuta uanachama na hata angegombea ubunge wasingemkata kama ilivyo 1995 ambapo alionekana ana upungufu wa kimaadili kwa nafasi ya urais lakini akapitishwa kugombea ubunge.

Kwahiyo sioni tatizo Slaa kumkaribisha Lowassa kama mwanachama wa kawaida kuongeza nguvu kwenye timu ya kampeni.

Kama vyama vimekubali kuungana ingawa vinatofautiana itikadi, hakuna tatizo kumkaribisha mtu mmoja. Tatizo ni mtu huyo mmoja mgeni anapopewa nafasi ya kuamua hatma ya chama.
 
Wana duru, naomba kuuliza hivi Mchungaji Gwajima ana mamlaka gani ndani ya Chadema mpaka wamruhusu kushiriki kuwachagulia mgombea urais.

Na tatizo la Dr.Slaa na Lowassa ni kakaribishwa Chadema kama mwanachama wa kawaida au kusimamishwa kama mgombea urais wa Chadema.

Ahsanteni.
 
Intriguing questions
 
Hili jukwaa la great thinkers nalo mmeligeuza jukwaa la kampeni na propaganda.

Swala la Slaa kumkaribisha Lowassa Chadema sio big deal.
Tatizo ni kumsimamisha agombee urais.

Hata kule CCM walipomkata Lowassa hawakumfuta uanachama na hata angegombea ubunge wasingemkata kama ilivyo 1995 ambapo alionekana ana upungufu wa kimaadili kwa nafasi ya urais lakini akapitishwa kugombea ubunge.

Kwahiyo sioni tatizo Slaa kumkaribisha Lowassa kama mwanachama wa kawaida kuongeza nguvu kwenye timu ya kampeni.

Kama vyama vimekubali kuungana ingawa vinatofautiana itikadi, hakuna tatizo kumkaribisha mtu mmoja. Tatizo ni mtu huyo mmoja mgeni anapopewa nafasi ya kuamua hatma ya chama.
Mkuu mbona kila kitu kinajadiliwa kwa upna wake?

Hakuna anayeachwa bali hoja zinatawala. Nadhani wenye mtazamo tofauti na wako hawapaswi kuambiwa ni propaganda.

Muhimu ni wewe kueleza position yako kama ambavyo wengine wanaeleza yao

Kuhusu uanachama, maelezo ya Dr Slaa hayapo wazi. Nadhani angefafanua kama ulivyouliza mjadala ungekuwa kwingine. Utakubaliana nami kuwa alirukia hoja zisizo husiana na mada kabisa

Kuhusu kumkaribisha, nadhani kama ksuingekuwa na walakini hakukuwa na haja ya kuzuia wanachama wa mtu

Kama tatizo ni kugombea, wapi Dr Slaa ameonyesha hilo kama kiini cha tatizo?

Ukisoma maelezo yake anazungumzia ufisadi, well, kama alijua hilo angeweza kusema kwa urahisi, Lowassa kachukue fomu ya uanachama tawi lolote.

Ilipokwenda mahali anaweka masharti na hata kukaa vikao ni wazi alikubaliana na suala hilo katika 'condition fulani'
Tunahoji ufisadi unaweza kusafishwa na mtu mwenyewe kama alivyotaka?

Ukimsoma , ni ngumu kupata ground ya malalamiko yake. Kuondoka kwake ni kutokana na kutofautiana na wenzake.

Hii haina maana wenzake walikuwa sahihi, la hasha! alichotakiwa kueleza ni simple, hakubaliani na wenzake kwasababu haamini ABCD

Kwenda kuzungumzia Sumaye na misikiti ilikuwa off point kubwa sana. Mbona hakuyasema alipokuwa katika kiti cha enzi?
Na wala Sumaye hakuwahi kuwa sehemu ya mzozo na wenzake.

Tuliandika siku picha ziliposammbaa katika uzi wa kuelekea uchaguzi.
Ukipata wasaa pitia uone tusivyofungwa na mtu au chama chochote katika mitazamo

Katika watu wanaokubaliana na hatua zake, tupo katika rekodi.
Tuliandika hivi

'Dr Slaa anazidi kuwa mfano wa viongozi. Kama hukubaliana na jambo njia nyepesi ni kuachana na suala hilo kwa kujiuzulu. Na hapa ndipo tunaposema, Lowassa alitakiwa kujiuzulu kama hakukubaliana na suala la Richmond''

Hayo tumesema wazi, sasa kuna tatizo lipi tukisema kile tunachoona hakipo sahihi japo kwa mitazamo yetu?
 
Waungwana,

Na mimi nichangie mawili matatu kwa nilivyomuelewa Dr. Slaa. Nadhani tatizo kubwa watu hawafanyi chronological order ya kile alichokisema na matokeo yake mambo mengi yanatafsiri out of context. Kama tu utaweka time factor katika hoja za Dr. Slaa nafikiri vitu vingi vinakaa mahala pake vizuri kabisa.

Labda nitoe angalizo, ninayoandika hapa ninaegemea katika vitu vifuatavyo;

  • · Nilivyomuelewa Dr. Slaa jana katika press yake
  • · Kauli na tabia ya viongozi wa CDM katika kipindi chote ambacho Dr. Slaa amekuwa kimya
  • · Kinachoendelea sasa kwenye kampeni ya Uraisi ya bwana Lowasa
  • · Na utashi wangu katika kuchambua mambo

Hoja zangu nyingi, zitajikita katika vitu hivyo hapo juu.

LENGO LA DR. SLAA KUVUNJA UKIMYA
Lengo kuu ninaloona mimi kwa hiki kilichotokea jana, ilikuwa ni kutoa maelezo ya kwa nini Dr. Slaa kama katibu mkuu amekuwa kimya tangu ndugu Lowasa ajiunge na CDM na baadae kuteuliwa na kutangazwa kuwa mgombea wa uraisi kupitia chama hicho kwa muamvuli wa UKAWA. Hapa kuna maswali yafuatayo;

  • · kwanini amekaa muda mrefu sana kutoa maelezo yake:
  • JIBU: Katika maelezo yake Dr. Slaa ameleza wazi kuwa uamuzi wake wa kujiuzulu ulikuwa immediate. Na barua yake kwanza ilichanwa na Prof. Safari. Na kama mtu ni mfuatiliaji mzuri kulikuwa na juhudi mbalimbali za kimazungumzo zilizokuwa zinafanywa na uongozi wa CDM kumrudisha kundini. Nadhani sote ni mashahidi wa hili. Na pia, Dr. Slaa alikuwa na haki ya kuchukua muda wa kutosha kupima na kupata ushauri juu hiki alichokifanya jana. Sasa nadhani swali hili halina mashiko na haliongezi chochote katika muktadha wa mambo.

  • · Na kwanini ameamua kusema sasa:
  • JIBU: Je, kusema muda huu ambao tayari CDM wameshachanganya kwenye kampeni na kuliongelea pale mwanzo kabla hawajaanza wapi kungekuwa na athari kubwa zaidi kwa CMD? Katika njia moja, mi nadhani kwa yeye kusema sasa hivi kuna fanya mambo mawili kwa wakati mmoja; Kwanza katoa dukuduku lake, hili ni lisingeweza kubaki hivi hivi daima. Pili, Kusema kule mwanza kabla hata kampeni kuanza kungekuwa na athari kubwa zaidi kwa CDM, kwa hiyo kwa njia moja aidha kwa kupanga au kutokupanga amekisaidia chama katika hili. Hii imekuwa nusu ya shari.

MAUDHUI YA LENGO
Kutoka na lengo hilo, ni dhahiri kuwa maudhui ya mazungumzo yake yangekusa mambo makubwa yafuatayo;

  • · Mchakato wa kumpata Lowasa kama mgombea uraisi wa CDM

  • · Kwa nini hamkubali Lowasa na hapa ndio kwenye maneno mengi (mzizi wa tatizo).
  • · Mstakabali wake ndani ya CDM
  • · Mengineyo
MCHAKATO WA KUMPATA LOWASA:

Kwa mujibu wa Dr. Slaa, alipigiwa simu na Mch. Gwajima (ambae amesema wana mahusiano ya kirafiki) baada ya Lowasa kukatwa CCM akimuuliza wafanye nini. Mchangiaji Alinda, amerudia kuuliza sana nani amemleta Lowasa CDM na nadhani (niko tayari kusahihishwa) anatumia maelezo haya ya Dr. Slaa kuonesha ni kuwa jibu ni Dr. Slaa. Nikubali kuwa maelezo haya yanaonesha tayari kulikuwa na maongezi kati ya Slaa na Gwajima. Gwajima alieitwa “mshenga”, kwa sababu ya urafiki wake na Slaa kwa vyovyote vile kama alitaka kuinzisha mazungumzo kati ya Lowasa na CMD ilikuwa ni by natural law angepitia kwa rafiki yake. Na Slaa kama katibu mkuu, hakuwa na maamuzi ya moja kwa moja akiliwasilisha hili suala kwa mwenyekiti wake na baadae likafika mpaka kamati kuu ya chama. Angalizo hapa ni kuwa, Slaa kama katibu mkuu hana haki ya kumnyima mtu ruhusu ya kujiunga na chama. Slaa kuwa first point of contact kati ya Lowasa na CMD hakumaanishi kuwa yeye binafsi hakuwa na tatizo na ufisadi wa Lowasa kwa kipindi hicho. Alichofanya hapa ni simply kufuata utaratibu wa kama kukubaliwa ama kukataliwa kwa Lowasa kufanywe na CDM. Ni vizuri kunote kuwa, mpaka kwenye hatua hii, hakuwa ametoa msimamo wowote. Kwa hiyo nadhani kusema kuwa Slaa ndie aliyemkaribisha Lowasa CDM kwa hoja hiyo sio sahihi hata kidogo.

Hatua ya pili katika mchakato ilikuwa ni mjadala wa ujio wa Lowasa na viongozi wa juu wa chama. Hapa sasa kila mwenye dukuduku, wasiwasi, kukataa au kukubali ndio alitakiwa aseme. Na hapa kwa mujibu wa Dr. Slaa yeye kwa msimamo wake alitaka Lowasa apewe masharti kadhaa. Kuna hoja kuwa kwanini Lowasa apewe masharti wakati katiba ya chadema haimpi mtu masharti hayo kujiunga kuwa mwanachama. Wanaouliza swali hili wanasahau kuwa, Lowasa hakutaka kuja CMD kuwa mwanachama wa kawaida. Kama angetaka hivyo hakuwa na haja ya kupitia kwa Gwajima. Yeye alitaka kuja CDM ili awe mgombea uraisi kupitia CMD baada ya kukataliwa CCM. Kama hapo bado mtu haoni tofauti itakuwa ameamua tu kutokuiona hiyo tofauti. Masharti yenyewe ni haya, (order haijazingatiwa);

  • · Lowasa atangaze IMMEDIATE kuachana na CCM na atangaze kujiunga CDM.
  • · Ajisafishe yeye mwenyewe juu ya tuhuma zake za ufisadi.
  • · Aseme ni asset gani analeta CMD.
Tatizo la watu wengi katika hayo masharti ni kuwa nadhani hawajaelewa msingi wa hayo masharti kama ambavyo mimi nimeyaelewa. Ni kutokana na masharti haya mimi naona kuwa Dr. Slaa kamwe hakutaka Lowasa ajiunge na CDM. Ni sawa na Zitto alivyosema kama Lowasa anataka kuja ACT aje lakini inabidi afate masharti yetu ya kutangaza mali zake, watu wakasema angalia Zitto amemkaribisha Lowasa. Lakini kama ukiangalia kwa umakini wake, hayo masharti yalikuwa hayatekelezeki kwa Lowasa. Asingeweza kuyatekeleza hayo masharti in a million years tena kwa muda aliokuwa anautaka Slaa. Lowasa aliwaambia CDM nitakuja na wabunge 50 na lundo ya mwenyeviti wa mikoa na wilaya wa CCM. Dr. Slaa aliona huu sio ukweli, na kama ni ukweli basi hao waje wakiwa ni asset sio liability. Kuja kama asset, ni kuondoka wao wenyewe kabla ya kusubiri mchakato wa ndani wa CCM. Wajitoe kabla hawajakataliwa. Ukisubiri kukatwa ndio ukaja wewe ni liability. Na hichi kitu nadhani watu wengi wameshindwa kukielewa. Wanauliza kwa hiyo hii asset ingekuja, je Lowasa asingekuwa fisadi? Mbona mnasahau hayo masharti mengine. Sharti lililokuwa linamuondoa Lowasa kwenye Ufisadi ni la yeye mwenyewe kujisafisha. Kujisafisha kwa ushahidi na kuwaweka wazi wahusika halisi wa hizo tuhuma. Hivi ndio nilivyomuelewa mimi Dr. Slaa. Kifupi ni kuwa, kwenye akili yake alijua kwa jinsi anavyomjua huyu mtu haya masharti kamwe Lowasa asingeweza akayatimiza. Kusema kuwa mwanzo alikubali halafu baadae akakataa ni kushindwa tu kuyaelewa mambo katika mapana yake. Na nadhani katika upana wake, hapa Dr. Slaa alikuwa anajaribu kulinda credibility ya chama kwa kutumia hoja na vitendo sio kwa ubabe. Na ni lazima ikumbukwe kuwa mpaka hapa hoja kuu ya CDM bado ilikuwa ni ufisadi sio kuindoa CCM whatever the cost/means.

SABABU ZA KUMKATAA LOWASA.
Hapa nadhani hata hakuhitaji maelezo mengi kwa sababu mengi ya yaliyosemwa yalikuwa ni marudio. Lakini nataka nijibu swali moja linaloulizwa sana. Inakuje Dr. Slaa anajikita katika kuzungumzia Richmond ya miaka 8 iliyopita anaacha madudu ya EPA, ESCROW, Meremeta etc yaliyotokea baada ya Richmond. Kwani haya madudu mengine yanamuhusu Lowasa moja kwa moja? Hivi kuna mtu hajui msimamo wa Dr. Slaa kwenye haya mengine? Hili halikuwa lengo la press yake ya jana. Richmond imekuja kwenye mjadala kwa sababu huwezi kumzungumzia Lowasa bila kuizungumzia hiyo. Alijiuzulu uwaziri mkuu kwa sababu ya hiyo, sio kitu kidogo hiki. Lowasa alikuwa katika ajenda yake jana.

MUSTAKABALI WAKE NDANI YA CHAMA.
Hapa sina maelezo ya zaidi.

MENGINEYO.
Hapa kwenye mengineyo nako kuna matatizo kadhaa. Na nakubaliana na Nguruvi, na King Suleimani katika hili, inawezekana Dr. Slaa alienda mbali tofauti na mahitaji. Hakuwa na haja ya kuiaddress issue ya babu Seya, masheikh wa Zanzibar wala hongo inayosemwa (kaambiwa na Gwajima) kuwa wamepewa maaskofu. Inawezekana wakati anaanza kuyaongelea haya hakupanga kufika huku ila yaliyompanda yalimpanda. Binafsi Slaa hawezi kuniambia kuwa hakuwa na hasira. Atakuwa sio mtu wa kawaida. Muda na nguvu aliyoiweka kwenye chama ni lazima awe na hasira. Lakini haya mimi nimeyaweka katika mengineyo kwa sababu kwa uoni wangu yalikuja in the heat of the moment. Hayakuwa madhumuni makuu.

Ahsanteni.
 
GalaxyS3

Karibu jamvini

Mkuu umeongea mengi, naomba nipitie machache

Kukaa kimya: Hili tumelizungumza sana kuanzia siku alipojiuzulu katika nyuzi mbili moja ikiwa ya kuelekea uchaguzi na nyingine ya ACT mpini

Kukaa kimya kwake kulimjengea hsehima sana. Ni lazima mtu ajipe muda wa kutathmini hatma yake baada ya kutulia.
Hilo tupo katika rekodi tukimsifu kwa dhati kabisa. Na ilikuwa busara sana kuepusha shari, sifa nyingine ya Slaa

Kusema sasa hivi: Hilo tumelizungumza jana . Ana haki ya kuzungumza, kutoa maoni, kujitetea au kueleza kilichotokkea ili tupate upande wa pili wa shilingi. Si kwa faida yake, ni kwa faida yetu sote. Wla hakuna muda anaopangiwa kuzungumza.

Tatizo: Jana alipoongea hakuzungumzia tatizo na wenzake. Alikwenda mbali na kuzungumzia mambo nje ya yale yaliyokusudiwa. Hivi shule za kata, maji, Guninita, Sumaye na misikiti yanahusika vipi na hoja yake?
Hilo ndilo linazua sintofahamu kwa baadhi ya watu kuhisi timing yake ilikuwa na motive

Hapa lazima ajilaumu maana hakupaswa kwenda huko. Alikuwa na haki ya kueleza kilichotokea.

Na haki hiyo ilipaswa iambatane na credibility. Mtu mzito kichama na kimaadili kuanza kuzungumzia mambo ya kufikirika yenye hisia kwa jamii halikuwa jambo sahihi

Kwa mfano, alipozungumzia kuhusu Sumaye na misikiti, kuhongwa kwa maaskofu n.k. ni mambo yasiyo na ushahidi at least kwa sasa kwasababu hakuweka ushahidi

Kuhusu kuwa 'f'ocal point'' , ukisoma maelezo yake ' Gwajima alimpigia simu na kwamwambia, amekatwa sasa tufanye nini""
Hapa inaonyesha kulikuwa na mawasiliano endelevu kuhusu suala hilo

Kuhusu masharti, ukimsoma anasema 'tulipokuwa tunakwenda katika kikao nilikuwa na msimamo wangu' Hivyo ni vema kusema alikuwa na msimamo tayari nje ya vikao . Si jambo baya lakini lazima liunganishwe na mlolongo mzima wa habari

Masharti aliyoweka ni Lowassa kukana CCM, kujisafisha kuhusu Richmond na kueleza anakwenda chama gani
Kukana CCM halikuwa jambo gumu, kueleza anakwenda wapi halikuwa jambo gumu. Pengine ugumu ulikuwa wa Richmond

Tuliwahi kuuliza kama analysis ilifanyika ya kutosha. Sasa hilo ni moja ya hoja zake nzito, lakini haliondoi ukweli kuwa Lowassa angesema kilichotokea basi Slaa angekuwa na mtazamo tofauti.

Inaelekea alikubaliana naye kuanzia mwanzo na wala hakuona ufisadi.
Hoja ya ufisadi ameieleza mwisho baada ya kueleza ushiriki wake. Hapo huoni kuna walakini?

Kuhusu Lowassa kuja na watu, hili nalo tumelihoji mapema sana. Tulisema inakuwaje CDM wana kura za maoni wakati huo huo wanasema wana mtaji? Tulizungumza kuhusu asset and liability.
Tunaweza kusema kwa dhati, tumezungumzia hili kabla ya Slaa. Na bado linazizima masikioni mwa wengi

Mkuu hoja kubwa ni kupitia kauli zake mwenyewe na kuzi dissect ili tupate mitazamo tofauti

Jambo moja lisilo na ubishi, maudhui ya hotuba yake yameacha maswali mengi

Slaa aliongozwa na hasira na si busara zake tunazojua. Hilo limempunguzia heshima na uzito wa hoja zake , ni ukweli tu tuuseme

Shule za kata, maji na kuzunguka kupiga kampeni akiwa mstaafu havi add up katika kile alichotaka kueleza.

Zinabadili mjadala kabisa na hilo halikuwa sahihi na ni kosa. Alikuwa off point kuanzia kati kati hadi mwisho wa hotuba akiongozwa na jaba na hasira. Ukisoma maswali aliyoulizwa, yote aliyajibu akiwa disoriented kabisa
 
GalaxyS3,

..asante sana kwa mchango wako.

..umetupa mwanga zaidi kuhusu mtafaruku uliotokea.

..mimi nadhani tatizo lipo hapo ktk MENGINEYO.

..kunapotokea matatizo/migogoro/sintofahamu kama hii iliyotokea CDM wahusika wanatakiwa watoe maelezo na misimamo yao, halafu watuachie wasikilizaji tufanye conclusions zetu. kwa maana nyingine wasikilizaji ndiyo tunashughulika na "mengineyo."

..Dr.Slaa alikuwa na hoja nzuri sana, lakini kaiharibu kwa kuongeza hayo "mengineyo." kuna tofauti kubwa sana kati ya jinsi alivyozungumza Prof.Lipumba, na jinsi alivyofanya Dr.Slaa.

..Hata mwenyekiti Mbowe nadhani alitaka suala hili liishe ktk namna ya kistaarabu, na kwamba wahusika wataendelea kuwa marafiki. Nasema hivyo kutokana na kauli alizozitoa kwamba Dr.Slaa ameamua "kumpumzika."

..Alichofanya Dr pale ni kama mtu aliyekwenda kujilipua. Matokeo yake watu wameacha kujadili hoja zake, sasa wanamjadili yeye.

..VERY SAD kwa baadhi yetu, ukizingatia kwamba huyu ndiye aliyetufanya wengi wetu tukaanza kuipenda CDM.
Rev. Kishoka, Nguruvi3, Alinda, TUJITEGEMEE, Mkandara, Mwalimu
 
Last edited by a moderator:
Asante sana GalaxyS3 kwa mchango wako nzuri ambao kwa namna moja au nyingine umenipa mwanga kuhusu ujio wa Lowassa ndani ya Chadema, pamoja na hayo bado sina mashaka na Dr. Slaa...

Kwanini nasema hivyo? Nasema hivyo kwa sababu:

Kwa jinsi Dr. Slaa alivyomueleza Lowassa jana, hivi kulikuwa na umhimu wa yeye kuwa "mposaji" wa Lowassa kuingia Chadema? Hivi hakuona kuwa kitendo cha Lowassa kuwa mwanachama wa kawaida tiyari kilikuwa kinatia doa kubwa ndani ya Chadema?

Na kama katibu mkuu anawajibu wa kulinda chama chake, kuhakikisha kuwa kila kiongozi anafuata maadili ya chama, hivyo basi inapotokea mtu anayetaka kujiunga na chama kwa minajri ya kugombea urais (kama ulivyoeleza hapo juu) lakini maadili yake ni machafu mtu huyu hakupaswa hata kujadiliana naye maana anaelewa kuwa ni fisadi na chama chake hakipokei mafisadi..Kwa hili tusimtetee Dr. Slaa tatizo limetoka kwake.

Na huu mjadala wa Gwajima Dr. Slaa na Lowassa hakuanza baada ya Lowassa kukatwa bali ulianza muda mrefu na ndio maana Gwajima alipompigia simu " alimwambia kuwa jamaa kakatwa" na Dr, Slaa akajibu niongee na Mwenyekiti kwa hii sentesi inaonyesha kuwa walishapanga kuwa akikatwa tu basi aje Chadema.

Nafikiri tuangalie haya mambo bila upendeleo unapompeleka mtu sehemu fulani iwe kwenye chama au kazini au sehemu yeyote ile basi ili apokelewa kutatokana na jinsi ulivyomuelezea kwa wanachama/au boss/Mwenyekiti wako. Haiwezekani leo ulete mwanachama ambaye anampango wa kuwa mwakilishi wa chama/kampuni yenu mwenye madoa doa na baaadaye usema "nimemleta nyie ndio waamuzi wa mwisho" Jamani kama ninafahamu fulani ni wezi/jambazi/fisadi tena fisadi kwanini nimpe hata nafasi ya kuongea na boss wangu?

Kama Lowassa angeletwa na mtu mwingine na Dr. Slaa akareact kama alivyo react jana ningemuelewa tena ningemtetea sana,
Kama Dr. Slaa hasingekuwa anamfahamu Lowassa vizuri juu ya ufisadi wake na akaja kufahamu baada ya kuwa ameishamtambulisha katika chama na hapo pia ningemuelewa lakini si sasa, alimfahamu vizuri kuwa Lowassa ni fisadi, alifahamu vizuri kuwa chama chake kinapingana na ufisadi na Lowassa na yeye ndiye alikuwa mpiga debe wa Lowassa kujiunga na chadema kuingia. Jamani jamani wanasiasa kuweni na aibu tena kwa watu wenye umri kama Dr. Slaa kwa kweli inasikitisha.
 
Kwenye mkutano wa jana Dr Slaa ameonyesha madhaifu makubwa kwenye maeneo kadhaa;

1. Upande mmoja anakubali kushiriki mchakato wa kumkaribisha Lowasa kwenye chama kwa kuwa na mawasiliano na "mshenga" Askofu Gwajima, lakini anaanzia katikati pale anapopigiwa simu kwamba "Amekatwa wafanyeje" na yeye kwenda kujadiliana na mwenyekiti wake. Ameshindwa kueleza hii idea ya kumualika Lowassa imeanzishwa na nani haswa? nani aliyeanzisha mazungumzo na "mshenga"? Kwani kwa taratibu za posa si yule mwenye uhitaji wa "mke" ndio anawasiliana na "mshenga" na kumtuma kwenda ukweni?

2. Anakubaliana na ujio wa Lowasa baada ya kutimizwa "masharti" aliyoyaweka "yeye" (sio taratibu za chama kwa kama ilivyofanyika kwa wengine waliojiunga na chadema) kwamba yakitimizwa basi yuko radhi kumkaribisha. Kwa mtu ambaye amemtuhumu juu ya kashfa za ufisadi kwa kiwango kile kulikuwa na haja kweli ya kujadili ujio wake kwenye chama kwa masharti? Suala la ujio wake halikupaswa kuwa ni "out of the question" kutoka mwanzo? Lakini yeye huyuhuyu bado akashiriki kwenye mazungumzo ya kumkaribisha ndani ya chama? Kwani hizo tuhuma alizifahamu kabla au baada ya mazungumzo na "mshenga" kuanza?

3. Kwa kuanza kushambulia wengine kina Sumaye, Masha n.k. alipoteza focus nzima ya mazungumzo yake ambayo yalipaswa kujikita kwenye kiini cha kutofautiana kwake na viongozi wenzake juu ya ujio wa Lowasa! Kina Sumaye wamejiunga baada ya Lowasa kuteuliwa kuwa mgombea urais. Akazidi kupoteza uelekeo kwa kurusha mashambulizi kwa maaskofu wa kanisa katoliko kuwatuhumu kwa rushwa huku akijaribu kujenga picha kwamba kanisa la kilutheri tayari linamuunga mkono mlutheri mwenzao! Wakati huo huo akimnanga Sumaye kwamba ndie aliyetuma askari waingie msikitini mwembechai kupiga waislamu! Mashambulizi haya yalikuwa na kila alama kuwa ni script iliyoandaliwa na CCM sababu ni kitu ambacho wameshawahi kukifanya hapo awali!

4. Kwenye suala zima la kashfa za ufisadi amekosa kuwa muwazi kwa kuanika kila kitu hadharani huku akichagua ukweli upi auweke wazi na upi auhifadhi kwa matumizi ya baadae! Kwangu mimi hio si kwa ajili ya manufaa ya wananchi bali kujinufaisha binafsi kisiasa. Hii same old trick ya "nina nyaraka na mkinichokoza ntazilipua" imekuwa sasa ni utoto tu manake nyaraka zina faida gani ikiwa vyombo vya dola hazizitumii kushitaki wahalifu na haziwekwi hadharani zote bali hawa jamaa kujitapa kuwa wanazo?

5. Alipopoteza uelekeo kabisa ni kuanza kuzungumzia juu ya mke/mchumba wake kwamba wameoana kihalali na ndoa imefungwa na Mwenyezi Mungu! Mungu yupi huyo anaruhusu kuoa mwanamke ambaye tayari amewahi kufunga ndoa ya kanisani?

Ni wazi kwamba kwenye hotuba ile hakujipanga vema na ni kama vile kuna mambo ambayo hakuwa akiyazungumza yeye kama yeye... ni kama vile kaandikiwa script ya nini cha kuongea! Kaonyesha wazi jazba, chuki na kufanya maelezo yake kwa ujumla kuwa ni personal vendetta dhidi ya Lowasa!

Amejiharibia credibility yake na for sure his political legacy kwenye nchi hii!
 
Kuhusu kuwa 'f'ocal point'' , ukisoma maelezo yake ' Gwajima alimpigia simu na kwamwambia, amekatwa sasa tufanye nini""
Hapa inaonyesha kulikuwa na mawasiliano endelevu kuhusu suala hilo

Kuhusu masharti, ukimsoma anasema 'tulipokuwa tunakwenda katika kikao nilikuwa na msimamo wangu' Hivyo ni vema kusema alikuwa na msimamo tayari nje ya vikao . Si jambo baya lakini lazima liunganishwe na mlolongo mzima wa habari

Masharti aliyoweka ni Lowassa kukana CCM, kujisafisha kuhusu Richmond na kueleza anakwenda chama gani
Kukana CCM halikuwa jambo gumu, kueleza anakwenda wapi halikuwa jambo gumu. Pengine ugumu ulikuwa wa Richmond

Tuliwahi kuuliza kama analysis ilifanyika ya kutosha. Sasa hilo ni moja ya hoja zake nzito, lakini haliondoi ukweli kuwa Lowassa angesema kilichotokea basi Slaa angekuwa na mtazamo tofauti.

Inaelekea alikubaliana naye kuanzia mwanzo na wala hakuona ufisadi.
Hoja ya ufisadi ameieleza mwisho baada ya kueleza ushiriki wake. Hapo huoni kuna walakini?

Kuhusu Lowassa kuja na watu, hili nalo tumelihoji mapema sana. Tulisema inakuwaje CDM wana kura za maoni wakati huo huo wanasema wana mtaji? Tulizungumza kuhusu asset and liability.
Tunaweza kusema kwa dhati, tumezungumzia hili kabla ya Slaa. Na bado linazizima masikioni mwa wengi

Mkuu

Kwenye bandiko langu nimeandika kwa uchache sana kwenye sehemu ya MENGINEYO. Kwa sababu sipendi kujadili vitu ambavyo kimsingi havina mashiko. Nimeangalia katika press yake nikachukua mambo ambayo mimi binafsi niliyaona yanahadhi ya kujadiliwa kwa sababu na yanahusika moja kwa moja na maudhui makuu ya press ile. Na nikasema inawezekana in the heat of the moment, alienda nje sana na maudhui makuu. Lakini nampa Dr. Slaa benefit of a doubt kutokana na historia na credibility yake aliyojingea kwa muda mrefu kuwa alikuwa sincere katika maudhui makuu ya press yake.

Nasema tena, hasira ya Dr. Slaa is understandable! Jiweke kwenye viatu vyake, uongozi wa chama umemsema kuwa yuko likizo kwenye mkutano mkuu wa chama wakati si kweli. Vijana wanajulikana kuwa ni wana CDM wamemsema vibaya kwenye mitandao ya jamii kabla ya yeye kusema chochote wote tumeona na hakuna alikataza hili suala kutoka kwenye uongozi. Mabango na mabango hapa JF yakimkashifu yeye Slaa na mkwewe toka kwa vijana wa CMD tumeyaona humu. Lissu amemuondoa kama author wa list of shame akajiweka yeye wakati ni Slaa alikuwa jukwaani akitaja yale majina. Tuangalie huku na huku jamani na tujaribu kuangalia mambo kwa macho ya wale wanaotendewa pia.

Tuje kwenye hoja, bado nadhani hujaya angalia hayo masharti kwa mapana yake kama ninavyo yaona mimi. Kama Lowasa angeweza kuyameet yale masharti angekuwa si Lowasa huyu tunaemsikia siku zote. Tatizo nafikiri bado liko kwenye nini kilisemwa na nani na lini? Moja, Kuukana CCM na kutangaza kuja CDM ilikuwa rahisi ndio, hasa ukizingatia kuwa mtu hawezi kuwa mwanachama wa vyama viwili. Mbili, kujisafisha na tuhuma hili ni gumu sana na mpaka sasa hivi hajifanyika katika uhalisia wake. Tatu, ni suala la asset vs liability ambalo hata wewe mwenyewe mpaka sasa hivi bado linakuzizima masikioni mwako. Kwa hiyo kati ya matatu aliyoyataka katibu mkuu ni moja tu ndio limefanyika mpaka hii leo. Sasa ukakasi hapa unatoka wapi? The guy has been right for over 10 years, he was on the right track yesterday and then his emotions got the better of him hakufanyi alichokuwa anakisema sio sahihi.

Kuhusu mawasiliano ya Gwajima na Slaa kuwa on going hilo sio tatizo. Hao ni marafiki (sijui kama bado upo huo urafiki). Bado hiki hakioneshi kuwa Slaa ndio alimkaribisha Lowasa CDM. Lowasa hakutana kujiunga na Dr. Slaa, alitaka kujiunga na CDM na Gwajima alipopiga simu yake Slaa kama kiongozi alimpeleka kwenye vikao vya maamuzi vya chama. Slaa hajakubaliana na vikao vya chama, akajiuzulu. Leo kaja akasema ni kwa nini hajakubaliana na vikao vya chama. Na hapo ni lazima amuongelee lowasa. Ukimuongelea Lowasa ni lazima uongelee Richmond. Na bado Slaa anasema ana ushahidi unaonesha ushiriki wa wazi wazi wa Lowasa katika Richmond. JJ Mnyika pia alishasema kuwa anao ushahidi mwingi tu unamuhusisha moja kwa moja Lowasa na Richmond. Utetezi wa Lowasa wa uongozi wa juu hata wewe nadhani unajua kuwa ni weak sana. Waziri mkuu hafanyi kazi kwa kuambiwa kuwa mkuu (Asiye na Jina) amesema tufanye.

Slaa amesema ili kuweka vitu on records. Waliokuwa wamepanga kumchagua Lowasa, wote wameshasikia aliyoyasema jana mara nyingi tu. Sidhani kama kuna ataekabadili mawazo kwa sababu ya press ya jana. Hakuna sababu ya kumfanya Slaa kuwa ni Villain kwa sababu tu kasema yake. Nasema tena, kusema kwake jana kuna faida kwa CMD kwa sababu, maneno yake ja jana kwa hali ilivyo yana effect ndogo sana katika kampeni zinazoendelea na hapo hapo CDM hawana haja ya kumuwaza tena katika mipango yao kwa hizi siku 50 na kadhaa zilizobaki.
 
Asante sana GalaxyS3 kwa mchango wako nzuri ambao kwa namna moja au nyingine umenipa mwanga kuhusu ujio wa Lowassa ndani ya Chadema, pamoja na hayo bado sina mashaka na Dr. Slaa...

Kwanini nasema hivyo? Nasema hivyo kwa sababu:

Kwa jinsi Dr. Slaa alivyomueleza Lowassa jana, hivi kulikuwa na umhimu wa yeye kuwa "mposaji" wa Lowassa kuingia Chadema? Hivi hakuona kuwa kitendo cha Lowassa kuwa mwanachama wa kawaida tiyari kilikuwa kinatia doa kubwa ndani ya Chadema?

Na kama katibu mkuu anawajibu wa kulinda chama chake, kuhakikisha kuwa kila kiongozi anafuata maadili ya chama, hivyo basi inapotokea mtu anayetaka kujiunga na chama kwa minajri ya kugombea urais (kama ulivyoeleza hapo juu) lakini maadili yake ni machafu mtu huyu hakupaswa hata kujadiliana naye maana anaelewa kuwa ni fisadi na chama chake hakipokei mafisadi..Kwa hili tusimtetee Dr. Slaa tatizo limetoka kwake.

Na huu mjadala wa Gwajima Dr. Slaa na Lowassa hakuanza baada ya Lowassa kukatwa bali ulianza muda mrefu na ndio maana Gwajima alipompigia simu " alimwambia kuwa jamaa kakatwa" na Dr, Slaa akajibu niongee na Mwenyekiti kwa hii sentesi inaonyesha kuwa walishapanga kuwa akikatwa tu basi aje Chadema.

Nafikiri tuangalie haya mambo bila upendeleo unapompeleka mtu sehemu fulani iwe kwenye chama au kazini au sehemu yeyote ile basi ili apokelewa kutatokana na jinsi ulivyomuelezea kwa wanachama/au boss/Mwenyekiti wako. Haiwezekani leo ulete mwanachama ambaye anampango wa kuwa mwakilishi wa chama/kampuni yenu mwenye madoa doa na baaadaye usema "nimemleta nyie ndio waamuzi wa mwisho" Jamani kama ninafahamu fulani ni wezi/jambazi/fisadi tena fisadi kwanini nimpe hata nafasi ya kuongea na boss wangu?

Alinda,

Ukilisema hivyo unapingana kabisa na misingi ya kidemokrasia. Katika justice, ndio maana hata convicted killers bado wanakuwa na haki ya ku appeal. D katika CDM inasimamia Demokrasia. Sasa kusema Slaa kwa sababu tu alidecide Lowasa ni mchafu hakuwa na haja ya kusemezana na mwenyekiti wake that is a slippery slope! Pili, hili suala aliletewa na rafiki yake and probably mtu ambaye (at the time) alikuwa anamuheshimu, kwa hiyo alilipeleka lakini tayari akijua kwa misingi ya chama chake itakuwa ni ngumu kwa huyu mtu kupita. Boy, was he surprised!! Nukta yangu ya msingi hapa ni kuwa, kila mtu ana haki ya kusikilizwa bila kujali tuhuma zake hata kama kuna lundo la ushahidi juu ya hizo tuhuma. Hiyo ndio MISINGI. Hakuna kucut corners, inatakiwa kufuatwa kikamilifu hasa hasa ukiwa una deal na watu usiowakubali ili usiwe muonevu.

Kama Dr. Slaa hasingekuwa anamfahamu Lowassa vizuri juu ya ufisadi wake na akaja kufahamu baada ya kuwa ameishamtambulisha katika chama na hapo pia ningemuelewa lakini si sasa, alimfahamu vizuri kuwa Lowassa ni fisadi, alifahamu vizuri kuwa chama chake kinapingana na ufisadi na Lowassa na yeye ndiye alikuwa mpiga debe wa Lowassa kujiunga na chadema kuingia. Jamani jamani wanasiasa kuweni na aibu tena kwa watu wenye umri kama Dr. Slaa kwa kweli inasikitisha.

Mimi sijui ile nadharia kuwa Slaa alimpigia debe Lowasa unaitoa wapi ndugu yangu. Kama nilivyokujibu hapo juu, vyama vya siasa sio vya watu fulani. Vina viongozi wanaoviongoza kutokana na katiba za vyama hivyo. Mtu yoyote anahaki ya kujiunga na chama chochote hilo liko wazi. Maamuzi kwenye vyama hufanywa kwa hoja na sio visasi, kuchukiana wala kubagua. Ukiona hukubaliani na maamuzi ya wengi ndani ya chama chako na huwezi kukaa kimya, unajitoa kwenye hicho chama. Na hicho ndicho alichofanya Slaa jana. Sidhani kama kulikuwa na kupiga debe hapa.
 
GalaxyS3,

..ppl r just reacting to what Dr.Slaa did.

..viongozi wa cdm kusema Dr amepumzika ilikuwa ni juhudi tu kuepusha haya ambayo Dr alifanya jana.

..bahati mbaya Dr didnt see it that way, badala yake aliona huo ni UWONGO na UZUSHI dhidi yake.

..Dr angetumia approach aliyofanya Prof.Lipumba sidhani kama tungekuwa tunamjadili yeye binafsi badala ya hoja zake.

..kwangu mimi Dr did not show CLASS/UNYENYEKEVU/UKOMAVU. Sijui kazi ya PR firm iliyoandaa mkutano ule ilikuwa ni nini haswa.
 
Last edited by a moderator:
GalaxyS3 nadhani unaliangalia suala kwa utetezi zaidi ya kutusoma katika maoni yetu

Narudia, suala la kutukanwa. Tulikemea kuhakikisha anatendewa haki, tuliwaambia viongozi wa CDM , kitendo cha vijana wawe TeamLowassa au M4C kuanza matusi si cha kiungwana .Tulisema wazi ni vijana wa Lowassa wanaoona Slaa kama tishio la mtu wao?

Pili, watu wakiwa na ganzi kuhusu nini kimetokea , tuliweka maswali zaidi ya 20 kwa viongozi wa CDM . Katika hayo zipo hoja za Slaa tulizoziwekea mantiki kabisa .Tulihoji huo mtaji, political base ya CDM na UKAWA itakuwa hali gani n.k.

Tatu, kuhusu press ya Dr Slaa, tumesema hivi ' Aliyoongea yana mntiki' kwamba hahuKukumiwi kwa maoni yake

Nne, Kuhusu uadilifu, kazi yake ya kujenga chama chake haina mfano.
Ali sacrifice maisha na hata fursa kwa ajili ya Chama. Ndio ilikuwa hoja mahususi kuwa vijana waache kumtukana na familia yake

Tano, watu wenye akili walimuelewa Dr Slaa, matusi ya vijana yalikoma. Busara zake zilionekana lulu, muhimu ni yeye kutokuwa sehemu ya asichiokubaliana nacho. Huo ndio uongozi ambao Lowassa alipaswa kufanya akiwa PM. Clear!

Sita,tatizo kaharibu maana kaenda mbali akijichanganya, azima tuwe wakweli.
Credibility yake ni hali ya juu. mabandiko ya nyuma, tumesema wazi credibility yake imekuwa compromised na jazba na hasira

Kwa mwezi mzima ameishi vizuri, wenye akili wakimwelewa. Mwisho wa siku anakuja na hoja zinatotia shaka.

Kwa mfano, hoja za udini, hii ni mbaya sana na kwakweli ni mbaya kuliko unavyoiona na kusema mambo madogo. I wish ungejua
Tumesema kuna collateral damage and colossal. Kama hukutuelewa wakati ule basi umekosa point muhimu

Ujumbe wake mwanana unafunikwa na mengine sensitive aliyoongea.
Hapo anapoondoa watu kwenye message yake na kuanza kujadili hoja zake laini alizotoa bila kupima madhara yake kwa jamii nzima

Mkuu, hatuwezi kudharau kauli zake wasababu ana ujumbe. Kwa wengine kila alichosema tumekijadili, tulitaka kujua ana nini cha ziada. Kwa bahati mbaya ,sijui kwa ushauri wa nani, akaondoa watu kwenye hoja na kutumia muda mwingi kujadili mambo yasiyo na uhusiano wala maana bila kupima madhara yake

Hivi shule za kata na suala lake vina uhusiano gani? Hivi maji Monduli na suala lake vinahusiana vipi?
Hivi Sumaye na viatu misikini vinahusiana vipi na matatizo aliyokutana nayo?

Orodha ya hovyo imefunika kabisa dhahabu aliyokuwa nayo.
Tunaiona dhahabu kwasababu tumeiongelea, kwa bahati mbaya upup unawasha zaidi

Saba, hakuna na sisi wengine tupo katika rekodi ya kusema akina Mbowe na Kanyaga twende haijajibu hoja.

Akina Lissu na ficha ficha ya picha haikuwa na maana. Maelezo yao na jinsi wanavyo handle suala zina ni disaster

Hebu kasome kuhusu Desert storm pale Jangwani. Tumeenda mabali na kusema, Mbowe akae pembeni kama Slaa

Yote hayo yanawekwa wazi kwasababu sisi wengine utaifa kwanza.

Hatujadili kwa kuangalia sura au vyama. Hatujadili kwa kuangalia nani kafanya nini, tunajadili kilichopo

Wiki iliyopita ilikuwa desert storm, jana Slaa kaja na habari. Kwa bahati mbaya kaongozwa na hasira ambazo hazikuwa na maana yoyote. Kasema mambo kiasi cha kuiweka credibility yake on the line

He could simply borrow a leaf from Lipumba. Natofautiana sana na Lipumba lakini jambo zuri alilofanya ni kutoa statement ambayo pamoja na mapungufu yake haikuonyesha ukakasi kama wa Slaa.

Dr kwa heshima yake hakupaswa kuvutika na mameno ya kina Lissu. ange maintain tu abaki na heshima yake ambayo mimi binafsi namuheshimu sana.

Hakutaka, akaenda kutoa chakula cha habari kwa kusema mambo ya hovyo badala ya core issue.

Hakuwa na sababu za kuongelea akina Guninita, atazunguka kumpinga Lowassa akiwa mstaafu, mambo ya dini dini na, shule za kata, maji na mambo mengine ya kiwango duni.

Alikuwa na message kali sana, tumeiona. Hakutumia fursa hiyo , tutasema !
 
Mbowe anaweza kulaumiwa kwa mengi lakini kwa jinsi alivyouhandle mgogoro huu na katibu mkuu wake ameonyesha kiwango cha juu cha ustaarabu, uvumilivu na ukomavu wa kisiasa. Chadema na Ukawa walikuwa wanapitia kipindi kigumu sana katika kufikia muafaka wa nani atapepea bendera yao kwenye uchaguzi huku muda ukiwa hauko upande wao.

Inapotokea mnatofautiana kimtazamo kwenye maamuzi fulani ni uungwana "kukubaliana kutokukubaliana/agree to disagree", na hiki naamini ndicho Mbowe alichomaanisha aliposema katibu mkuu amepumzika na atawakuta mbele ya safari. Pengine alikuwa na matumaini kwamba pamoja na kutofautiana kwao wanaweza kufikia muafaka kwenye masuala mawili matatu kwa mustakali mwema wa upinzani nchini.

Bahati mbaya Mheshimiwa Slaa ame-react vingine kabisa!
 
Mbowe anaweza kulaumiwa kwa mengi lakini kwa jinsi alivyouhandle mgogoro huu na katibu mkuu wake ameonyesha kiwango cha juu cha ustaarabu, uvumilivu na ukomavu wa kisiasa. Chadema na Ukawa walikuwa wanapitia kipindi kigumu sana katika kufikia muafaka wa nani atapepea bendera yao kwenye uchaguzi huku muda ukiwa hauko upande wao.

Inapotokea mnatofautiana kimtazamo kwenye maamuzi fulani ni uungwana "kukubaliana kutokukubaliana/agree to disagree", na hiki naamini ndicho Mbowe alichomaanisha aliposema katibu mkuu amepumzika na atawakuta mbele ya safari. Pengine alikuwa na matumaini kwamba pamoja na kutofautiana kwao wanaweza kufikia muafaka kwenye masuala mawili matatu kwa mustakali mwema wa upinzani nchini.

Bahati mbaya Mheshimiwa Slaa ame-react vingine kabisa!
GalaxyS3,

..ppl r just reacting to what Dr.Slaa did.

..viongozi wa cdm kusema Dr amepumzika ilikuwa ni juhudi tu kuepusha haya ambayo Dr alifanya jana.

..bahati mbaya Dr didnt see it that way, badala yake aliona huo ni UWONGO na UZUSHI dhidi yake.

..Dr angetumia approach aliyofanya Prof.Lipumba sidhani kama tungekuwa tunamjadili yeye binafsi badala ya hoja zake.

..kwangu mimi Dr did not show CLASS/UNYENYEKEVU/UKOMAVU. Sijui kazi ya PR firm iliyoandaa mkutano ule ilikuwa ni nini haswa.
.... Ndio maana tunasema reaction yake haikuwa na ulazima

Kwa mfamo. angesema 'niliacha siasa tarehe 28 July saa sita usiku' bila neno jingine, leo angekuwa amerudisha mzigo kwa akina Mbowe ambao nao wasingeona busara kusema tofauti na suala lingeishia hapo.

Dr kakimbilia maneno Uongo na uzushi ambayo yanaweza kuwa na ukweli bila kuwa na maana kwa wakati uliokuwepo.
Kwamba, busara, ukweli na uongo na uzushi vilitakiwa kuangaliwa. Kwa hili Dr hakuwa makini hata kidogo

Jingine ni lile la maaskofu ambao leo anaombwa ushahidi. It was unnecessary kuzungumzia mambo asiyo na ushahidi nao

Halafu akarukia akina Sumaye, Guninita na wengine. Akaacha akina Mbowe na Lissu ambao ndio wenye hoja

Hilo lilionyesha Dr alivyokuwa miffed and perturbed kwanza, halafu bewildered iliyompelela kuwa rogue and finally disoriented

Alitakiwa abaki kwenye mada. Kuzungumzia shule za kata na maji ilikuwa climax ya disorientation.

Yaani Slaa tunayemjua akawa anazungumzia trivial and flimsy issue,hazina connections, mara Sumaye na Polisi mara viatu mara maji.

It was disaster kwake najisikia vibaya maana huyu mzee namheshimu sana.

Ican't wrap up my head kilimtokea kitu gani jana na kuwa disoriented kiasi kile

........
 
Alinda,

Ukilisema hivyo unapingana kabisa na misingi ya kidemokrasia. Katika justice, ndio maana hata convicted killers bado wanakuwa na haki ya ku appeal. D katika CDM inasimamia Demokrasia. Sasa kusema Slaa kwa sababu tu alidecide Lowasa ni mchafu hakuwa na haja ya kusemezana na mwenyekiti wake that is a slippery slope! Pili, hili suala aliletewa na rafiki yake and probably mtu ambaye (at the time) alikuwa anamuheshimu,.

Aliyemtuhumu Lowassa kuwa ni fisadi ni Dr. Slaa/Chadema na anayetaka kumsikiliza Lowassa kwanza ni Dr. Slaa/Chadema sasa wakati wanamtuhumu kuwa yeye ni fisadi walishindwa nini kumsikiliza kwanza? Na je inamaana wakati Dr. Slaa anaitisha mkutano pale Mwembeyanga hakuwa na uhakika na anachokisema?

Na je kama ingetokea Lowassa akatekeleza yale masharti aliyopewa angekuwa safi? na tangu lini Chadema wanasafisha mtu? na je vipi ili list of shame ingebaki vile vile au jina la Lowassa ingetolewa?

kwa hiyo alilipeleka lakini tayari akijua kwa misingi ya chama chake itakuwa ni ngumu kwa huyu mtu kupita. Boy, was he surprised!! Nukta yangu ya msingi hapa ni kuwa, kila mtu ana haki ya kusikilizwa bila kujali tuhuma zake hata kama kuna lundo la ushahidi juu ya hizo tuhuma. Hiyo ndio MISINGI. Hakuna kucut corners, inatakiwa kufuatwa kikamilifu hasa hasa ukiwa una deal na watu usiowakubali ili usiwe muonevu. .

Kama alifahamu msingi ya chama chake kuwa hakiwezi kumpitisha mtu kama Lowassa je alishindwa nini kumwambia Gwajima ukweli? Hiyo heshima gani inayokushinda kusema unachoamini na kusimamia misingi ya chama chako. Maongezi ya Gwajima alianza tangu May hivyo alikuwa na muda mzuri wa kutafakari na kuona je Lowassa anafaa kujiunga na Chadema ua hafai? na kama aliona kuwa hafai angemwambia Gwajima ukweli, kama alisimama mbele ya mamilion wa watanzania na kusema Lowassa hafai alishindwa nini kusema haya akiwa na Gwajima?

Mimi sijui ile nadharia kuwa Slaa alimpigia debe Lowasa unaitoa wapi ndugu yangu. Kama nilivyokujibu hapo juu, vyama vya siasa sio vya watu fulani. Vina viongozi wanaoviongoza kutokana na katiba za vyama hivyo. Mtu yoyote anahaki ya kujiunga na chama chochote hilo liko wazi. Maamuzi kwenye vyama hufanywa kwa hoja na sio visasi, kuchukiana wala kubagua. Ukiona hukubaliani na maamuzi ya wengi ndani ya chama chako na huwezi kukaa kimya, unajitoa kwenye hicho chama. Na hicho ndicho alichofanya Slaa jana. Sidhani kama kulikuwa na kupiga debe hapa.

Ni kweli kuwa vyama vya siasa vina viongozi wanaongoza kutokana na katiba za vyama vyao je masharti aliyowekewa Lowassa yalitoka katika katiba ipi?

Sina tatizo na Dr. Slaa kutoa lake moyoni, maana kama angekaa kimya zigo angetushwa Mbowe lakini mpaka sasa tunaona zigo lililetwa na Dr. Slaa, kalipigia debe yeye sasa analiruka na kumwachia Mbowe.

Lakini nashindwa kuelewa nini madhumuni ya Dr. Slaa kumkaribisha Lowassa?

Je alitaka Lowassa awe mgombea urais?
Je alitaka Lowassa awe katika kampeni zake?
au alitaka Lowassa kuwa mwanachama wa Chadema kama walivyo wanachama wengine na kama ni hivi nini faida za kuwa na Lowassa.. Na je nani alimtafuta nani je ni Lowassa alimtafuta Dr. Slaa kupitia Gwajima au ni Dr. Slaa alimtafuta Lowassa?

Naombeni wanajamvi tuunganishe dot.
 
Kama alifahamu msingi ya chama chake kuwa hakiwezi kumpitisha mtu kama Lowassa je alishindwa nini kumwambia Gwajima ukweli? Hiyo heshima gani inayokushinda kusema unachoamini na kusimamia misingi ya chama chako. Maongezi ya Gwajima alianza tangu May hivyo alikuwa na muda mzuri wa kutafakari na kuona je Lowassa anafaa kujiunga na Chadema ua hafai? na kama aliona kuwa hafai angemwambia Gwajima ukweli, kama alisimama mbele ya mamilion wa watanzania na kusema Lowassa hafai alishindwa nini kusema haya akiwa na Gwajima?

Je alitaka Lowassa awe mgombea urais?

Je alitaka Lowassa awe katika kampeni zake?
au alitaka Lowassa kuwa mwanachama wa Chadema kama walivyo wanachama wengine na kama ni hivi nini faida za kuwa na Lowassa.. Na je nani alimtafuta nani je ni Lowassa alimtafuta Dr. Slaa kupitia Gwajima au ni Dr. Slaa alimtafuta Lowassa?

Naombeni wanajamvi tuunganishe dot.
Alinda , kumbe ni kuanzia May wapo katika maongezi. Naunganisha na ile kauli ya 'amekatwa Dodoma, tunafanyaje'

Maswali yako yanahitaji majibu kwakweli. Na majibu yapo katika ''maongezi'' kati ya May-July
 
Back
Top Bottom