Kwa jinsi tunavyomuelewa Dr. Slaa kwa swala la Lowassa hisingekuwa rais Gwajima ampigie simu tu from nowhere kumueleza kukatwa kwa Lowassa na Dr. Slaa ajibu mpaka niongee na Mwenyekiti..
Ndio maana kauli ya Lissu kwangu inaleta mantiki kuwa Dr. Slaa, Gwajima na Lowassa walikuwa na maongezi kabla ya Lowassa kukatwa inaweza kuwa ni May au June au hata July mwanzo...Sasa kama anafahamu uchafu wa Lowassa na huu uchafu wa Lowassa ndio ulimfanya yeye kuachana na siasa ni kwanini yeye kupeleka wazo la Lowassa kuhamia Chadema?
Dada yangu Alinda,
KUna kitu kinapingana hapa! Dr. Slaa alidai kwenye hotuba yake hakutaka kuwa Rais.
Lakini inaelekea wazi kuwa alikuwa tayari Lowassa aje. Aidha habari zisizothibitishwa, ujio wa Lowassa na wafuasi wake ulikuwa uongeze nguvu CDM na hata kumpa fursa mgombea wa CDM (Dr. Slaa) uwezo wa kunyakua Urais.
CDM waliweka sharti ndani ya UKAWA la kupewa Urais ambalo lilimshinda Lipumba (again, hizi ni habari za mizunguko na michepuko na hata udini pia unatajwa hasa Ukatoliki versus Uislamu).
Again, kutokana na maudhui ya mkutano wake na kiwango cha hisia (emotions), suala la yeye kusema hakuwa na nia ya Urais linaonekana kama ni uongo (aidha za michepukoni ni kuwa yeye na wapambe walitaka Lowassa aje aonegze nguvu, tatizo lilikuja Mbowe alipoona opportunity from another angle na kuamua kumwachia Lowassa agombee urais).
Kiukweli, hotuba nzima imeamsha maswali mengi ya credibility za wanasiasa wengi (not Lowassa, he is known thug, master of manipulation and opportunist that is not a secret at all) wazee wetu wiki hii hasa Sitta, Slaa na Mwakyembe.
Ukiangalia kauli za hawa wazee watatu, kila mmoja anatoa vitisho na blackmail kuwa ana mengi ya kumwaga mboga na kudai kama Lowassa na wenzake wnaa ubavu wathubutu kujibu hoja.
This is a mockery to good governance and transparency. It is absolute denial of justice and tarnish credibility of so called Wapiganaji au Wapambanaji.
Leo hii tukianza kusema wewe bwana tuna siri zao hebu nyamaza tusikuumbue, ilhali tunakutuhumu mwizi au tunakujua ni mhalifu bila kukufikisha pale panapostahili, hatuoni kuwa bado tunaendeleza utamaduni mchafu tunaoupiga vita wa mtandao, ufisadi, vificho, visasi na hata kupoteza credibility ya kusimamia haki na utu?
Inanikumbusha reaction ya watu nilipohoji kukiukwa kwa kanuni na katiba ya CCM kwenye mchakato wa kuchagua mgombea wa CCM, nilipohoji kufurahia kudhihkiwa na kunajisiwa demokrasia na kanuni ndani ya CCM, kisa Lowassa kakatwa mpaka nikatuhumiwa kukatiwa kitu.
Nikauliza, kama leo tunaruhusu na kufurahia CCM walichofanya ndani yao, kesho wakifanya kwenye uchaguzi mkuu na magoli ya mikono tutakuwaje na sauti za kulalamika au kukemea?
Natambua sisi ni binaadamu an tuna double standards. Lowassa is public enemy
#1 , lakini pia ni kipenzi cha wengine wengi tuu pamoja na uanaharamu na uharamia wake wote.
Kama kweli tunataka mabadiliko, basi tuwe mstari wa mbele kuisimamia haki bila selectiveness au kufanya mambo ya mizengwe maana ugonjwa huu wa mizengwe tuliomlaumu Mwalimu Nyerere 1995, tumeuendeleza 2000, 2005, 2010 na leo hii 2015 tumeufurahia kutokana na Mizengwe kutoa goli la mkono kumkata Lowassa na wengine.
Kama tulishangilia uhuni wa CCM na safu ya viongozi wake kumkata Lowassa na wengine, iweje leo tumkasirikie Mbowe kwa kutumia fursa "kuleta" ushawishi wa mizengwe ambao Ukawa na CDM waliupigia kura ya ndio?
Ni aibu leo tunasema heri Magufuli ana ufisadi mdogo tunaweza kuishi nao, huku tunajua walimleta machoni petu tupige kura ni mafisadi wenye nguvu kubwa na kwa ushirika kama fisadi Lowassa!
We should not have double standards on anything, otherwise huo ni ushetani mkubwa kuliko machafu na madhaifu ya wale tunaowajua kuwa ni wahalifu.
Tuache unafiki na hizi selective justice na selective minds za kujenga upya nchi au hata kuchambua mambo!