Bado najiuliza Gwajima ana interest gani na urais wa Lowassa? Imekuwaje mpaka Lowassa akamuamini Gwajima kiasi kikubwa hivyo. Dr. Slaa anasema Gwajima amemwambia kuwa Lowassa kawahonga maaskofu 30 ili wamuunge mkono, je iwapo hili ni kweli, siasa za mgombea wa namna hii zina athari gani kwa taifa?
Bado naamini kujadili vitu vyepesivyepesi badala ya mambo makubwa ni kutokulitendea haki taifa...
Gwajima ni rafiki wa Lowassa hii Gwajima alishasema kitambo.
Dr. Slaa baada ya kuwekewa pingamizi la kufunga ndoa na Josephina, Josephina alikasirka na kumshauri Dr. Slaa kuhama kanisa, Hivyo walihamia kanisani kwa Gwajima pia Gwajima na Dr. Slaa ni marafiki lakini sijui kama urafiki wao ulianza walipohamia kanisani kwake au kabla..
Kwa hiyo mpaka hapo unaweza kuunganisha nukta na kuona Gwajima anaingiaje kwenye ili sanga..
Inawezekana kabisa baada ya DR. Slaa kufahamu kuwa yeye ni mgombea urais, alikuwa anatafuta mtu ambaye anaweza kumsapport nje ya Chadame hivyo akaongea na Gwajima ili aongee na Lowassa haweze kujiunga nao.. Sote humu ndani tunafahamu nguvu na mikakati ya Lowassa nafikiri hata Lowassa kwenda Chadema ni pigo kubwa sana kwa CCM .
Au inawezekana Lowassa alimuomba Gwajima aongee na Dr, Slaa kama anaweza kujiunga na Chadema endapo CCM watakata jina lake.. (Na nafikiri Lowassa alimwendea Mbowe, Na Mbowe akamwambia aende kwa Dr. Slaa, hivyo akatafutwa mtu wa kumuingia DR. Slaa ambaye si mwanaUkawa au mwana CCM)
Na kwa mjibu wa ex wa Dr. ugomvi kati ya Dr.Slaa na Lowassa si mkubwa vile kama tunavyofikria sisi, hawa wao wanaelewana maana huyu mama alisema baada ya kutangaza ile "list of Shame" alikwenda kwa Lowassa na kupata dinner.
Hivyo ukianza kuunganisha hizo dot unapata picha kamili ilivyochezwa, Nafikiri Dr,Slaa alikuwa hana nia vilee ya kuwa mgombea wa urais na ndio maana alipotaka kutangazwa alikataa na kusema wasubiri ili wafanye shamra shamra.. (nafikiri hapa mambo ya Lowassa yalikuwa bado hayajakaa sawa.
Na kusapport point yangu hapo juu, ni pamoja na kufahamu kuwa nia ya Lowassa ni kugombea urais wa Tanzania iwe kwa kupitia CCM, au Ukawa au ACT ilikuwa inajulikana kwa kila mtanzania na kama Dr. Slaa angetaka kumzuia hasigombee urais kupitia Ukawa basi siku ile angekubali kutangazwa maana walishakubalina wagombe urais wote kuwa Slaa apewe nafasi.. Na pia ukisoma maelelzo ya
Tai Ngwilizi ambayo Dr. Slaa anasema "
kiongozi ambaye anaenda kuwa raisi wa nchi lazima awe na wafuasi nyuma yake.Hivyo basi unaona kuwa nia ya Lowassa ilijulikana mapema na pia ijulikana hata kwa huyu aliyemleta.
Pia tukumbuke vikao vya kumtambulisha Lowassa viliandaliwa na Dr. Slaa na mpaka hapo kulikuwa hakuna wasi wasi wote.. Kwenye Halmashauri/Kamati kuu alijieleza na walimuelewa. Baada ya hapo Dr. Slaa aligeuka ghafla maana walikuwa wamepanga wakutane wote siku ya kumtambulisha Lowassa lakini Dr. hakujitokeza na alipopigiwa simu alikuwa haipatikani ndipo Pro. Safari alimfuata nyumbani kwake na Dr. kumkabidhi Pro. barua ya kujihudhuru..
Inapofika hapo ndipo ile point ya Lissu inapoleta mantiki kuwa mama Josephina hakufurahishwa Lowassa kupeperusha bendera-- yaliyosemwa mmeyasikia. Hivi ndivyo nionavyo katika sakata ili.
Ila ninaweza kusema kuwa Dr. Slaa analeta siasa za kinafiki maana mtu amemkaribisha yeye, halafu leo analalamika kuwa ni fisadi sasa wakati anamkaribisha hakufahamu kuwa ni fisadi?
Juzi katika Press yake alikuwa na Mwakyembe (kitu ambacho si kibaya) na alipouliza alisema kuhusu kuonekana yeye na Mwakyembe (mwana CCM ambaye anapingana na mgombea urais Ukawa) alisema: "research (utafiti) lazima urudi kwenye source (chanzo) ya hilo jambo na ndiyo maana nilikuwa na jeuri ya kuzungumza kwa kujiamini"
Sasa swali la kujiuliza wakati wanazunguka nchi nzima kutangaza kuwa Lowassa ni fisadi alikuwa hajafanya research ya kutosha? Ina maana alikuwa hana uhakika ni kile anachotulisha, Je ndio maana akamkaribisha Lowassa Ukawa?
Na je vipi ile list of shame alifanya reseach ya kutosha isije kuwa nayo hana uhakika nayo.. Yaani katika wanasiasa niliyowapenda na kuamini kila watamkalo alikuwa Dr, Slaa hila huu ulaghai na uongo alionza kwa kweli amenisikitisha sana sikutegemea mzee mzima kama yule ukaa mbele ya camera ya kutulisha uongo..
Anasema Sumaye hawaongei.. Ex wake anasema alimpa No. ya simu Sumaye wiki tatu zilizopita, na waliongea vizuri tu, anasema mshahara wake alikuwa anachangia chama na wao wanakula Mihongo, anaulizwa vipi hii press nani kalipa nabaki kusema kwani nilipokwenda USA mara mbili nani alilipa maana chama kilinipa sh. Laki Tano.. Sasa jamani kama mtu mzima unaongopa kwa vitu vidogo namna hii itakuwaje kwa mambo makumbwa ambayo hatuwezi kuyafatilia na kuwa na uhakika na unachokisema? Nimeumia sana..
Kama ni swala la kutoa na kupokea rushwa, sote humu ndani tukiwa wakweli, baada ya Dr. Slaa naye kupokea mlungula ninaweza kusema tena kwa kujihamini wanasiasa wote wa Tanzania ni watoaji na wapokeaji rushwa, si Kikwete, si Kinana, si Mbowe, si Lipumba, si Zitto, si Dr. Slaa si Lowassa, si Mbatia ila hizi kelele tunazozisika kuwa ooh fulani ni mtoa rushwa, ooh fulani kapokea rushwa wanakuwa wamezidiana madili yao..
Huwezi kuniamba kuwa Dr, Slaa amejitoa Chadema ameachana na mshahara wa mil.11 kwa mwezi kwa vile ana uchungu sana na watanzania na. ndio maana anapingana na Lowassa lakini Magufuli na CCM hatii neno wakati machungu ya CCM anayafahamu vizuri.. Hizi huruma kwa watanzania zimetoka wapi?
Hivyo basi tukianza kuwahukumu watoa rushwa tuwahukumu wote bila kuangalia ni akina nani na wanafanya nini..