Kwanini ni Dr.Slaa tu ndio wakuwekwa mtu kati kwanini isiwe Mbowe, Mbatia na Lissu kama bado ni wanasiasa wa kuaminiwa na kama kweli Lowassa wanamtumia kwa sababu ya mabadiliko au wana motives tofauti.
The Alibi so far on what is going on.
Prof.Lipumba
Huyu ndio wa kwanza kujitoa katika uongozi wa UKAWA kwa madai ya kuwa agenda imebadilika na vilevile dhamira inamsuta. Dhamira gani? tunajua wagombea wa uraisi wa UKAWA walikaa na kukubaliana ya kuwa Dr.Slaa ndio atapepea bendera. Hili Lipumba alilisema hadharani na Mbatia amelirudia. Kwa hivyo through series of events Dr.Slaa awezi kupokewa au kujadiliana na UKAWA kuwa mgombea wao kama CDM walikuwa awajampitisha bado.
Kwanini sasa Lipumba aondoke ghafla wakati ndio mtu aliyeandika waraka wa kumpokea Lowassa mara alipoingia kwenye mkutano wao, waraka uliosomwa na Mbatia. Ina maana mpaka dakika hiyo maamuzi ya kuwa Lowassa atakuwa mgombea wa UKAWA yalikuwa bado ayajaamuliwa na pengine maelewano ilikuwa support yake tu ndio wanayo itaka. This is the only reason why Lipumba left baada ya Lowassa kupewa unahodha wa kambi.
Dr.Slaa
Nilikuwa tayari nimeshapitishwa na chama kuwa mgombea wao kwa taratibu za ndani; kilichobaki ina maana ni ilikuwa ni public appearance tu. Jumlisha na facts za kuwa kulikuwa na mgogoro mkubwa sana kupata mgombea wa UKAWA ambao ilibidi watu watoke Dodoma na wakae mpaka saa tisa za usiku ina maana Dr.Slaa nayeye alikuwa tayari keshajiandaa kugombea uraisi pia. Kwa vyovyote vile ujio wa Lowassa kwa Dr.Slaa ni mkakati wa kuivuriga CCM kwenye campaign zake kwakuwa aliahidi kuja na wafuasi na kulikuwa na some elements of that based on his nomination campaign support aliyokuwa nayo CCM ilikuwa ni dhahiri mpaka wanachama kuimba nyimbo za kukosa nidhamu ndani ya kikao chao baada ya kukatwa kwa Lowassa.
Tundu Lissu
Dr.Slaa alishapitishwa na vikao halali vya chama kuwa mgombea wa chama chetu kwa nafasi ya uraisi. Inathibitisha zaidi by now Dr.Slaa alijua ya kuwa yeye ni mgombea tayari na ujio wa Lowassa usingeweza tengua hilo ata kama huku pembeni alikuwa anaongea na Gwajima kuhusu Lowassa sidhani kama lengo ujio wake uwe kwa sababu ya uraisi.
Baada ya hizo events nadhani kilichofuata ni hiki kutoka kwa timu ya Lowassa kwa kuitazama safu ya watu walio CDM
especially kama walianza kumfuata wakati bado yuko kwenye campaign za kuwania uongozi kupitia CCM.
"Churchill: "Madam, would you sleep with me for five million pounds?" Socialite: "My goodness, Mr. Churchill... Well, I suppose... we would have to discuss terms, of course... "
Churchill: "Would you sleep with me for five pounds?"
Socialite: "Mr. Churchill, what kind of woman do you think I am?!"
Churchill: "Madam, we've already established that. Now we are haggling about the price"
Ukiangalia tu historia yake ya kutoa vibaasha sidhani kama anawapa viongozi kwa sababu ya kura moja zao, bali anajuwa wanamakundi ya wafuasi wenye uwezo wa kumpa kura nyingi tu. Kwenye ethics wanasema uwezi defy nature ya kitu viumbe vinatabia ya kurudia mambo yaleyale given the challenge or circumstances.
Je iliwezekana vipi Lowassa kupitishwa kuwa mgombea wa CDM na UKAWA kitendo kilichopelekea prof Lipumba kuacha uongozi maana hata kama CDM walimptisha surely Lipumba utegemei nayeye akubali kirahisi kwa sababu tunajua kwa Dr.Slaa tu ilichukuwa alot of convincing from his other leaders kukubali. Na kwanini CDM ilivunja kanuni zake za ndani maana Dr.Slaa walishamteua kususa kwa Dr.Slaa sidhani kama ni kwa hoja zake tu bali kutolewa kwenye position aliyokuwa keshapitiwa na chama chake pamoja na viongozi wa vyama vingine.
Tukirudi kwenye nature ya Lowassa kwanini tusiamini hakutumia tena vibaasha vyake kununua viongozi wa UKAWA kupata support ya watu wao ili kuendeleza ndoto yake ya uraisi; je hii ndoto inaendana na vision ya UKAWA.
If you ask me there is no historical evidence to back that claim kwamba Lowassa anamapenzi na upinzani ni ndoto zake tu za uraisi na kwa njia zilezile anazotumia ndio zimemfikisha kileleni upinzani pia, why should anyone believe akiukwaa uraisi atabadilika wakati all the evidence points otherwise.
Sielewi kwanini watu amumuoni huyu mtu for what he is na jinsi gani Mbowe, Mbatia, Lissu jumlisha na Sharif Hamad walivyokuwa si watu wa kuaminiwa. Mimi bado namueshimu sana Dr.Slaa na Prof.Lipumba ndio watu pekee walio na morals ata kama walibariki ujio wa Lowassa sio kwa sababu ya kuuza nguvu zao pia na kuwapa mafisadi platform nyingine. Huyo Mbowe ndio kabisa hana loyalty yaani kejeli za jana kwa Dr.Slaa sikuamini kama anaweza rusha vijembe vya namna hile inawezekana ata Dr.Slaa alikuwa anamtumia pia kuongeza wabunge na ruzuku ya chama.