ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,040
- 7,303
Mkuu nadhani kuna wakati tukubaliane kuwa tofauti ya mawazo inajenga. Pia tuangalie mambo kwa upana wake
Kama utamuuliza Alinda hilo swali la mlungula basi pia usiache kumjibu, kwamba, wale wanaosema EL ni fisadi wana evidence yoyote?
Mama Tibaijuka kachukua za mboga, tumeambiwa kimaadili hapaswi. Lakini je, ilikuwa ni jambo pristine?
Tumesikia ya Escrow, kamati zimeundwa. Je, unataka kusema hakuna aliyehusika kwavile tu hakuna ushahidi huo?
Yule mzee aliyegawa kutoka mabenki amefanya hivyo kwa kutumia mikataba. Lakini je, hakukuwa na mziangira ya 'rushwa'?
Point yangu ni kuwa tuangalie mambo kwa mtazamo mpana si kwa kutaka kusikia tunachotaka bali hata tusichokitaka
Hao wengine wametoka wapi wakati tunajadili issue ya Dr. Slaa na kuchukua mlungula?
Ndio maana nasema tunakosea kuligeuza jukwaa la great thinkers kuwa sehemu ya propaganda.
Mtu akisema kuhusu escrow muulize kuhusu escrow na ajibu escrow. Lakini mtu anaposema Dr. Slaa kachukua mlungula halafu anapoulizwa anajibu escrow ni ishara ya kutokulitendea haki hili jukwaa.
Nadhani wote tunajuana kwenye majukwaa ya kejeli kuwa tunaziweza, ila sifa mojawapo ya usomi ni kujua kuwa kila kitu na mahali pake. Kwa kutambua hilo ndio maana jukwaa hili likaanzishwa.