Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,413
- 23,592
Nafikiri hapa ndipo tunapotofautiana, mimi nasema Lowassa kwa sasa ni adui nambari one wa CCM. Ni kweli aliutaka Uraisi kupitia CCM lakini nani kweli anajua kwa uhakika malengo yake? Je yawezekana kwamba moyoni ni kweli alitaka kuleta mabadiliko from within? Kikwete anapewa benefit of doubt, Magufuli anapewa benefit of doubt, kwa nini Lowassa hapewi benefit of doubt kwa tuhuma zozote zile?Mag3; Kujibu swali lako: Lowassa si adui wa CCM. Matamanio ya kile anachokitaka (Urais), ndio chanzo cha mgogoro wa Lowassa na wenzake. Kwa vitu vingine vilivyobaki, CCM na Lowassa ni damu damu.
Hapana, I disagree, Lowassa hakuwahi kuwa Mkuu wa nchi na hakuwahi kuwa kiongozi mkuu wa chama chake, sasa aliwezaje kufanya anayodaiwa kuyafanya bila idhini ya wakubwa wake? Hizo nguvu alizitoa wapi? Pamoja na hayo tayari kasema anazikubali sera na ilani ya Chadema lakini kama ilivyo kwa malowassa-phobia hawako tayari kumpa hata hiyo benefit of doubt, kwa nini?Nafasi aliyoleta Lowassa kwenye upinzani ni kubwa. Lakini inategemea jinsi gani wananchi wataitumia nafasi hiyo. Wakimwachia Lowassa, hakutakuwa na mabadiliko yoyote. Atafanya kama yale aliyofanya akiwa CCM.
Zakumi si kila kinachosemwa humu ni ukweli uliothibitika, zingine ni hisia tu kulingana na utashi wa mchangiaji. Mimi ni katika waliokuwa mstari wa mbele kumkataa Lowassa lakini wakati huo alikuwa bado yuko kundini huko CCM. Sasa ukweli usioweza kupingika ni kwamba katoka, na ushahidi kwamba hawako tena pamoja ni, kwa mfano, uwanja anaopewa Dr Slaa na status quo kumkandia Lowassa. Miaka yote Dr. Slaa hakuwahi kupewa nafasi kama hiyo TBC hata alipokuwa anagombea Uraisi mwaka 2010, kwa nini sasa?Wachangiaji maarufu katika ukumbi huu walituambia kuwa Lowassa ali-sponsor ACT, kuisambaratisha CDM. Lowassa ali-sponsor watu mbalimbali wachaguliwe kuwa wajumbe wa NEC. Na hawa watu ndio waliokuwa wamchague Lowassa kupitia CCM. Leo baadhi ya hawa wachangia wanamkumbatia Lowassa as a game changer.
Last edited by a moderator: