CHADEMA: Ukimya wa Rais dhidi ya vitendo vya ukandamizaji unaoendelea ni wa kutia wasiwasi

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,183
Reaction score
2,100
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinalaani kwa nguvu zote tukio la kushambuliwa, kupigwa na kukamatwa kwa mwanaharakati wa haki za binadamu, demokrasia na mwanachama wetu, Mdude Nyagali, usiku wa kuamkia tarehe 2 Mei 2025, nyumbani kwake mkoani Mbeya.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa majirani na mashuhuda, watu waliojitambulisha ni polisi walivamia makazi ya Mdude, wakampiga vibaya na kisha kumchukua kwa nguvu bila hati ya ukamataji wala kufuata utaratibu wa kisheria.

Tukio hili linadhihirisha kwa mara nyingine hali ya kuzorota kwa haki za kiraia na kisiasa nchini. Ni dhahiri kuwa hatua hizi ni sehemu ya mkakati mpana wa kunyamazisha wakosoaji
wa serikali na wapigania haki.

Soma Pia: Mdude Nyagali adaiwa kukamatwa na kupigwa na watu waliojitambulisha Polisi

Chadema inaitaka Serikali kupitia Jeshi la Polisi kutoa taarifa ya haraka kuhusu alipo Mdude, hali yake ya kiafya, na sababu halali za ukamataji wake. Pia tunasisitiza kufanyika kwa
uchunguzi huru na kuwajibishwa kwa wahusika wote wa tukio hili.

Aidha, tunamkumbusha Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa ukimya wake wa mara kwa mara dhidi ya vitendo vya ukandamizaji wa sauti huru ni wa kutia wasiwasi.

Tunamtaka atoe kauli ya wazi ya kulaani na kuchukua hatua za dhati za kulinda haki za Watanzania wote
bila ubaguzi.

Chadema itaendelea kusimama kidete kupigania haki, demokrasia na utawala wa sheria.
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinalaani kwa nguvu zote tukio la kushambuliwa, kupigwa na kukamatwa kwa mwanaharakati wa haki za binadamu,
demokrasia na mwanachama wetu, Mdude Nyagali, usiku wa kuamkia tarehe 2 Mei 2025, nyumbani kwake mkoani Mbeya.

Mna taka aongee nini wakati yeye ndie ana watuma??
 
Matendo yote haya yana baraka zake na anayafurahia kwani anaamini ndiyo yatamuweka tena madarakani.
 
Yeye ndiye Mnufaika Mkuu wa huu ukandamizaji wa HAKI unaoendelea.
 
mdude kaingia kwenye 18 za wenyewe aliokuwa anawatukana na kuwaambia vibaka sasa wanaenda kumbaka aone ubakaji ulivyo
 
Kauli yake ya mwisho kuhusiana na tukio kama hilo alisema
'kifo ni kifo'
mstarajie matumaini au kauli isiyo ya kibabe
 
Acha kukurupuka basi .subiri kufa CCM kwanza maana kinachofanyika sasa CCM ndio inajitangaza kuwa wao ni Hatari wa kwanza duniani
 
Lissu alisema Mbowe ndio anawauza hawa vijana akiwa mwenyekiti haya mambo yatakwisha. Dunia hii ina watu wabaya sana leo anaumbuka.
 
Back
Top Bottom