Masalu Jacob
JF-Expert Member
- Jul 26, 2017
- 1,013
- 1,183
Habari Tanzania!
Leo napendezwa niongee na enyi vijana kizazi kipya kwenye masuala ya Utaawala na Siasa Kazi.
1. Siasa; Unapobomoa " Legacy " ya utawala wowote/ yoyote ukumbuke utawajibika kiutawala na utapata adhabu yenye kukupa adabu aidha uache nia ovu uliyonayo kwa kujua au kutokujua; au upotezwe mazima kwa manufaa ya Taifa (Rejea Siasa CHADEMA na kinachoendelea)
Kikawaida kabisa hata CHADEMA endapo mngekuwa mmeunda Serikali mngefanya yaleyale kwa mtu au watu wenye mawazo au nia ya kuondoa "Legacy" ya Utawala uliopo au uliopita kwa gharama yoyote.
Namna ya kujiepusha: Yafaa siasa safi, ubunifu wa sera matokeo na uchochezi wa fikra au maarifa mapya kwa jamii; mwisho jamii ndio itatoa ushindi kwa upande wenu.
2. Kazi na Utawala; Kijana unapopata kazi au unapokuwa kwenye majukumu yako hasa ya kitendaji zingatia sana sheria. Wengi wa vijana hawasomi au kuweka mazingatio wanapoingia kwenye majukumu aidha Mapya au yaliozoeleka kwenye kutimiza wajibu wao. Mfano; Kwa mujibu wa Sheria kama sitakosea inaeleza kuwa kifungu cha mwisho cha mafungamano aidha maneno au maandishi ndio hubeba maana kamili ya kile mlichokubaliana.
Ikitokea kijana upo kwenye ajira au ukaajiriwa na ukatumwa au kupokea maelekezo yoyote ya kiongozi au mkuu wako katika kazi; piga kazi itapendeza zaidi ukipata nyaraka. Mfano; Ukitumwa au kutekeleza jambo au jukumu na Mkuu wako huna kosa kisheria endapo kama kwenye mkataba wako wa kazi kulikuwa na kipengele cha mfano huo hapo chini.
Ref: Uwe tayari kufanya kazi yoyote utakayoelekezwa na mkuu wako. ( Mfano usio rasmi).
Rejea Kesi pendwa kwa Vijana - Mshkaji hana kosa ni jambo la muda tu.
Vijana acheni ushabiki hausaidii lolote zaidi kuongeza hasira ndani yako.
Vijana jikiteni kwenye kusoma na muwe wabunifu.
NB
Kwa mujibu wa KATIBA nimetoa maoni yangu binafsi yasihusishwe na jambo au kitu chochote.
Asalaam.