Nguruka
Senior Member
- Dec 6, 2006
- 189
- 129
MAPEMA Juma hili tumesikia baadhi ya vyama vya siasa nchini vinavyoshiriki Uchaguzi Mkuu wa 2020 vikitoa maneno makali dhidi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kile ambacho wao wanasema kuwa Tume imekosa meno dhidi ya wanaokiuka Maaduili ya Uchaguzi.
Mgombea Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lisu alitumia dakika kadhaa jukwaani wakati wa kampeni zake huko mkoani Songwe kujibu mapigo dhidi ya taarifa ya Tume ya kuvionya vyama ambavyo vinakiuka maadili ya uchaguzi wakati wa kampeni zao.
Tume kupitia Mkurugenzi wa Uchaguzi, haikumtaja mtu wala Chama cha Siasa anacho kituhumu kukiuka maadfili ya uchaguzi (Hii vijana tunaita kurusha jiwe gizani, utakaesikia anaguna ujue limempoata).
Hivyo Tume ilitupa jiwe gizani lakini binafsi nadhani liliwapata Chadema maana kitendo cha mgombea wao wa Urais kuijibu Tume ni ishara kuwa jiwe hilo liliwapata na huenda limewaumiza.
Mimi naamini kuwa limewaumiza na ndio maana wamesimama kujibu mapigo. Lakini ni Dhahiri kuiwa Chadema kupitia mgombea wao huyo ndio walianza kukiuka maadili ya uchaguzi ambayo waliyasaini kama ishara ya kuyafuata wakati wa kampeni.
Sehemu ya pili ya Maadili hayo ya Uchaguzi inaeleza wazi yanayotakiwa kufanywa na vyama Siasa na Wagombea Katika Kuendesha Shughuli za Siasa wakati wa Kampeni.
Moja ya wajibu wa Vyama vya Siasa na Wagombea kuheshimu na kufuata Katiba ya Nchi sheria za uchaguzi, kanuni za uchaguzi, maadili ya uchaguzi na maelekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi pamoja na sheria nyingine za nchi katika kipindi chote cha uchaguzi.
Sasa kwanini nasema Chadema jiwe la tume limewapata ni kwakua wenyewe wamekua wakifanya baadjhi ya vitu ambavyo hawapasi kufanya kwa m,ujibu wa Maadili ya uchaguzi.
Mambo yasiyotakiwa kufanywa na Vyama vya Siasa kulingana na Kanuni za Maadili ya Uchguzi na ambayo Chadema imekua ikiyafanya ni pamoja na .
Kufanya fujo au kuchochea vurugu ya aina yoyote katika mikutano ya vyama vingine; hili limefanmyika katika mkutano wao wa kwanza walihamasisha watu waandamane.
Kutumia lugha ya matusi, kashfa, kejeli, udhalilishaji na vitisho au lugha inayochochea uvunjifu wa amani au kuashiria ubaguzi wa kijinsia, ulemavu, rangi au maumbile kwenye mikutano na kwenye shughuli zote za kampeni;ya kampeni ya vyama vingine vya siasa na matangazo ya uchaguzi yanayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi;
Pia kutokubali au kutokuheshimu maamuzi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi yanayofanywa kwa mujibu wa sheria za uchaguzi.
Hivyo Chadema wanatakiwa kutoa boriti katika macho yao ndipo waende kutoa Boriti kwa tume ya taifa ya Uchaguzi ambayo kimsingi inapaswa kutoa ingiliwa na mtu au chama chochote wakati inatekeleza majukumu yake.