Uchaguzi 2020 CHADEMA vipi, jiwe la Tume ya Uchaguzi liliwapata gizani

Uchaguzi 2020 CHADEMA vipi, jiwe la Tume ya Uchaguzi liliwapata gizani

Nguruka.
Umekaa unaandika ujinga huku unajifanya huoni ?! Huoni vyama vinavyonyanyaswa kwa kuenguliwa wagombea wao ?! Unajifanya kipofu kutoona vyama vingine vinafanya kampeni kwa lugha kisukuma ?! Hujui nini , kwamba uonewe ukae kimya ndiyo nidhamu ?!.
kwani nyie mmekatazwa kufanya kampeni kwa KINYIRAMBA?mwenzenu ni mahiri ktk lugha kila sehemu anapofika lazima salimie kwa lugha ya eneo husika ndio aendelee na lugha ya Taifa.vilevile ingekuwa ni kuonewa kwa vyama vingine hata hao NEC wasingepot.eza muda kukaa kushughulikia RUFAA Zaidi ya 500
 
kwani nyie mmekatazwa kufanya kampeni kwa KINYIRAMBA?mwenzenu ni mahiri ktk lugha kila sehemu anapofika lazima salimie kwa lugha ya eneo husika ndio aendelee na lugha ya Taifa.vilevile ingekuwa ni kuonewa kwa vyama vingine hata hao NEC wasingepot.eza muda kukaa kushughulikia RUFAA Zaidi ya 500
Tafuta hotuba ya Musukuma (mbunge) wakiwa Chato na Rais . Muombe mtu akutafsirie uone ukabila ulivyo sumu
 
Namba bado haziongopi, takwimu za uhakika bado zinaonyesha ya kwamba, endapo uchaguzi kama ungalifanyika mwishoni mwa juma hili l, matokeo yangekuwa kama ifuatavyo;
TAL kwa upande wa CDM 69%
JPM kwa upande wa CCM 21%
Vyama vingine 10%

Prediction bado inaonyesha TAL anaweza kuchukua 3% kutoka kila upande ifikapo mwisho wa mwezi huu na kufikisha 75% huku akimuacha mgombea wa CCM kwa mbali akijikongoja kwa 19% na vyama vingine kwa 7%

Mfalme Sauli aliua kwa mamia lkn Daudi mtumishi wa Mungu aliua kwa mealfu. Hii ndizo sauti zisikikazo kutoka kwa wapigakura.
Hahahaaa hii ndio raha ya Watanzania. Enhe huo utafiti uemefanywa na taasisi gani hapa duniani. Je unakumbuka Sheria ya Mitandao maarufu kama “Cyber Crime Act ya 2015”. Je Unajua kuna Sheria ya Takwimu 2019 Sura 351.

Sheria hiyo sasa katika kifungu cha 37(2) kinasema kuwa mtu yeyote ambaye anamiliki taarifa yoyote ya kitakwimu, ambayo kwa ufahamu wake anajua zimetolewa kinyume na masharti ya sheria hii, anachapisha au anasambaza kwa watu wengine taarifa hizo, anatenda kosa, na akipatikana na hatia atahukumiwa faini isiyopungua shilingi milioni tano au kifungo cha muda usiopungua miezi kumi na mbili, au vyote kwa pamoja. Sasa shauri lako. Ila mimi nitakuletea japo maji ya kunywa na sabuni.
 
Sheria zinasemaje kuhusu lugha ya campaign ?! Na unadhani ni kwanini mgombea hata mmoja wa udiwani hakuenguliwa kwa sababu za pingamizi za wapinzani ?!.

Usijifanye kipofu dogo
Sheria iko wazi kuhusu Lugha ya Kampeni kua ni Kiswahili au Kiingereza na pindi lugha hizo zisipoeleweka mgombea atatakiwa kutumia Mkalimani. Hii unaipata sehemu ya pili ya Maadili ya Uchaguzi, ambayo inaelezea kwa kina Maadili ya Vyama vya Siasa na Wagombea katika kuendesha Shughuli za Kampeni. (Ingia Tovuti ya tume www.nec.go.tz usome maadili ya Uchaguzi). Sasa 2.1 (k) inakuelezea hilo.

Lakini kama kuna mgombea amekiuka maadili hayo ya Uchaguzi kuna Hatua za kuchukuliwa na Wagombea husika ambapo Malalamiko yatafikishwa mbele ya Kamati, na kamati inawajumbe ambao ni kutoka Vyama vya Siasa vyenye wagombea. Sasa wewe na mimi pamoja na vyama vya Siasa tunachofanya ni Kunung'unika Mitandaoni aidha JF, Insta, Twitta na kwingineko kuwa Tume haitendi haki, tunapaswa Tuyafikishe MALALAMIKO katika Kamati ya Maadili ya Kitaifa. Sehemu ya 5 ya Maadili ya Uchaguzi imeainisha hayo. Kuna Kamati 4. Ingia mtandaoni usome kama mimi nilivyosoma.
 
Chadema kuwajibu tume si kwa sababu wamekiuka maadili, Ni kwa sababu Mgombea ambae anatarajiwa na wengi katika Uchaguzi ni mgombea kutoka Chadema, Hivyo yeye kama mgombea lazima awajibu maana abaewindwa ni yeye, wale wengine hawana madhara.
 
View attachment 1573572
MAPEMA Juma hili tumesikia baadhi ya vyama vya siasa nchini vinavyoshiriki Uchaguzi Mkuu wa 2020 vikitoa maneno makali dhidi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kile ambacho wao wanasema kuwa Tume imekosa meno dhidi ya wanaokiuka Maaduili ya Uchaguzi..
Meko Alipokuwa Bunda alisema hawana Taa kwa sababu walichagua Upinzani. Alipokuwa Busega ( Lamadi ) akasema mkichagua Upinzani hataleta Maendeleo. Alipofika Kigoma akasema Haya Maendeleo Haya ni yangu nimeleta, Maendeleo hayana Vyama[emoji3][emoji3][emoji3]

Zote Ni kauli za Mtu mmoja katika Uchaguzi mmoja! Sijui ndio kuchanganyikiwa kumeanza.
 
Ukisikia "pa" ujue imekukosa,Sasa hawa jamaa zetu liliwapata ndio maana yowe lilikuwa jingi
Alipokuwa Bunda alisema hawana Taa kwa sababu walichagua Upinzani. Alipokuwa Busega ( Lamadi ) akasema mkichagua Upinzani hataleta Maendeleo. Alipofika Kigoma akasema Haya Maendeleo Haya ni yangu nimeleta, Maendeleo hayana Vyama Ni kauli za Mtu mmoja katika Uchaguzi mmoja!
 
Nguruka.

Umekaa unaandika ujinga huku unajifanya huoni ?! Huoni vyama vinavyonyanyaswa kwa kuenguliwa wagombea wao ?! Unajifanya kipofu kutoona vyama vingine vinafanya kampeni kwa lugha kisukuma ?! Hujui nini , kwamba uonewe ukae kimya ndiyo nidhamu ?!.
Jadhuong, wagombea wanaenguliwa bila sababu au kwa mujibu wa sheria? Kama fomu ina dosari kama sheria inavyosema unataka waachwe?
 
View attachment 1573572
MAPEMA Juma hili tumesikia baadhi ya vyama vya siasa nchini vinavyoshiriki Uchaguzi Mkuu wa 2020 vikitoa maneno makali dhidi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kile ambacho wao wanasema kuwa Tume imekosa meno dhidi ya wanaokiuka Maaduili ya Uchaguzi...

Double standard zipo maeneo mengi na zinaoendelea upande Fulani na ndio maana wanajikuta njia panda na kushindwa kumkemea yeyote moja kwa moja.
 
Double standard zipo maeneo mengi na zinaoendelea upande Fulani na ndio maana wanajikuta njia panda na kushindwa kumkemea yeyote moja kwa moja.
Waache KUNUNG'UNIKA badala yake WALALAMIKE kwa kufikisha hayo Malalamiko kwa Kamati husika.
 
View attachment 1573572
MAPEMA Juma hili tumesikia baadhi ya vyama vya siasa nchini vinavyoshiriki Uchaguzi Mkuu wa 2020 vikitoa maneno makali dhidi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kile ambacho wao wanasema kuwa Tume imekosa meno dhidi ya wanaokiuka Maaduili ya Uchaguzi.
Mgombea Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lisu alitumia dakika kadhaa jukwaani wakati wa kampeni zake huko mkoani Songwe kujibu mapigo dhidi ya taarifa ya Tume ya kuvionya vyama ambavyo vinakiuka maadili ya uchaguzi wakati wa kampeni zao.
Tume kupitia Mkurugenzi wa Uchaguzi, haikumtaja mtu wala Chama cha Siasa anacho kituhumu kukiuka maadfili ya uchaguzi (Hii vijana tunaita kurusha jiwe gizani, utakaesikia anaguna ujue limempoata).
Hivyo Tume ilitupa jiwe gizani lakini binafsi nadhani liliwapata Chadema maana kitendo cha mgombea wao wa Urais kuijibu Tume ni ishara kuwa jiwe hilo liliwapata na huenda limewaumiza.
Mimi naamini kuwa limewaumiza na ndio maana wamesimama kujibu mapigo. Lakini ni Dhahiri kuiwa Chadema kupitia mgombea wao huyo ndio walianza kukiuka maadili ya uchaguzi ambayo waliyasaini kama ishara ya kuyafuata wakati wa kampeni.
Sehemu ya pili ya Maadili hayo ya Uchaguzi inaeleza wazi yanayotakiwa kufanywa na vyama Siasa na Wagombea Katika Kuendesha Shughuli za Siasa wakati wa Kampeni.
Moja ya wajibu wa Vyama vya Siasa na Wagombea kuheshimu na kufuata Katiba ya Nchi sheria za uchaguzi, kanuni za uchaguzi, maadili ya uchaguzi na maelekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi pamoja na sheria nyingine za nchi katika kipindi chote cha uchaguzi.
Sasa kwanini nasema Chadema jiwe la tume limewapata ni kwakua wenyewe wamekua wakifanya baadjhi ya vitu ambavyo hawapasi kufanya kwa m,ujibu wa Maadili ya uchaguzi.
Mambo yasiyotakiwa kufanywa na Vyama vya Siasa kulingana na Kanuni za Maadili ya Uchguzi na ambayo Chadema imekua ikiyafanya ni pamoja na .
Kufanya fujo au kuchochea vurugu ya aina yoyote katika mikutano ya vyama vingine; hili limefanmyika katika mkutano wao wa kwanza walihamasisha watu waandamane.
Kutumia lugha ya matusi, kashfa, kejeli, udhalilishaji na vitisho au lugha inayochochea uvunjifu wa amani au kuashiria ubaguzi wa kijinsia, ulemavu, rangi au maumbile kwenye mikutano na kwenye shughuli zote za kampeni;ya kampeni ya vyama vingine vya siasa na matangazo ya uchaguzi yanayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi;
Pia kutokubali au kutokuheshimu maamuzi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi yanayofanywa kwa mujibu wa sheria za uchaguzi.
Hivyo Chadema wanatakiwa kutoa boriti katika macho yao ndipo waende kutoa Boriti kwa tume ya taifa ya Uchaguzi ambayo kimsingi inapaswa kutoa ingiliwa na mtu au chama chochote wakati inatekeleza majukumu yake.
Wewe siyo kijana kiakili bali kijana umri tu bali akili zako ni kikongwe,
Kijana hawezi fikiri kama wewe,
Hawezi pambanua mambo kama wewe.

Kilichojaa kwako ni upumbavu ambao ni ugonjwa usiokuwa na dawa.

Hakuna asiyejua ccm, nec, polisi, Tiss, uhamiaji, mahakama nk, adui yao mkubwa ktk nchi hii ni chadema na mgombea wao Lissu.
HII HATA DUNIA INAFAHAMU.

Ni wewe peke yako usiyejua hili kwasababu ya
 
Wewe siyo kijana kiakili bali kijana umri tu bali akili zako ni kikongwe,
Kijana hawezi fikiri kama wewe,
Hawezi pambanua mambo kama wewe.

Kilichojaa kwako ni upumbavu ambao ni ugonjwa usiokuwa na dawa.

Hakuna asiyejua ccm, nec, polisi, Tiss, uhamiaji, mahakama nk, adui yao mkubwa ktk nchi hii ni chadema na mgombea wao Lissu.
HII HATA DUNIA INAFAHAMU.

Ni wewe peke yako usiyejua hili kwasababu ya
Ulichokisema ni sawa na maiti kushindana na wafukiaji. Mmeshashikiwa akili na hamjui mbinu Basi mnakalia kutukana tu.
 
Back
Top Bottom