CHADEMA waache kutumia neno Kamanda bila sifa stahiki

Ryan Holiday

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2018
Posts
3,499
Reaction score
5,956
Habari,

Nimekuwa kimya kwa miaka mingi, kutokana na miangaiko ya hapa na pale.
Lakini kila ninapopita mitaani, vichochoroni na kwenye madimbwi ya maji na kutana na neno hili 'KAMANDA" nikirudi kwenye Uso kitabu, X, Insta, nikienda JF nakutana na neno hili "KAMANDA". Yaani mtu hata chakula chake cha siku kinamshinda anajiita ''KAMANDA''. Kiujumla KAMANDA ni neno kubwa sana na lenye uzito sana, nikisema hivi, nafikiri wale Makamanda wenzangu wa Jeshi wananielewa. Hili neno kiujumla Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wanalitumia kimkakati na wameshindwa kulitendea haki.

Basi Kamanda ni nani? neno "Kamanda" kwa ujumla linahusiana na uongozi, mamlaka, na uwezo wa kusimamia au kuongoza katika nyanja mbalimbali, hasa za kijeshi, usalama, na hata harakati za kijamii, katika hali yoyote ile ya mvua au jua na kuwa na msimamo wa kujitoa mhanga kwa ajili ya wenzako au misimamo yako.

Unaweza kuwa "umekula mbuzi mzima lakini mkia umekushinda", hapa kwenye kujitoa "mhanga", mseme tu ukweli na muwe-honest na nafsi zenu kumewashinda, hivyo nasema hivi "CHADEMA acheni kujipa vyeo vya movie za action, wakati hata kujificha msituni kwa siku moja kunawashinda!"

:Tssk:
 
Kwa hiyo unaumia saana jamaa wakiitana makamanda?Basi ziba masikio usiwasikie wakiitana hivyo.
 
Wewe ni CCM unawapangiaje CHADEMA?
wao wakisema CCM waache kutumia neno COMRADE pasipo stahiki .. una jua maana ya comrade?
 
Mimi sio CCM wala sio CHADEMA, kwenye ukweli lazima tuseme ukweli.
Pilipili ya Shamba inakuwashia nini kama wewe siyo CCM , kwanini una deal na CHADEMA ambayo inasemekana imekufa, haina uongozi, cham cha wachagga, kitapeli, hakina dira na kuacha vyama vikubwa kama CCK, CUF, ACT , NLD na NRA?

Ukiingiza kichwa mchangani, funika kalio watoto watakucheka.
 
Shida umekariri kwamba mtu akitoa hoja yenye mantiki basi ni CCM, mtu ana uhuru wa mtazamo na maoni yake. Siasa ni jambo pana, na kila chama kina wafuasi wake kwa sababu tofauti. Badala ya kushindana kwa maneno, ni vyema tuchambue hoja kwa mantiki na tuelekeze nguvu kwenye mijadala yenye tija.
 
Huwezi chambua hoja bila kujua mrengo wa mleta hoja.
umesikia watu wanaokwambia MAMA HADAIWI KITU, huko jimboni hakuna madawati, walimu, ajira, umeme, barabara, huyo mtu ukimchungiza ni MBOGAMBOGA, kwanini mnajificha kwenye mwavuli wa "sina chama" wakati una kadi ya kijani?
 
Wewe unaonaje?
Navoona ni kwamba utateseka bure kama utakua unakerwa na vitu vidogo vidogo kama hivi.
Harmonize anajiita jeshi, umeona jeshi limemmaind?
Lady Jay dee anajiita komando,umesikia makomando wakikereka?
Hata wewe unaweza kujiita unavotaka kikubwa kama unaona hilo jina linakua nguvu na ari fulani!
Ndio maana wengi wanajiita maraisi na wafalme lakini hakuna rais anayekereka na hilo.vitu vingine ni just for fun tu..
 
Huwezi chambua hoja bila kujua mrengo wa mleta hoja.
umesskia watu wanaokwambia MAMA HADAIWI KITU, huko jimboni hakuna madawa, walimu, ajira, umeme, barabara, huyo mtu ukimchungiza ni MBOGAMBOGA, kwanini mnajificha kwenye mwavuli wa "sina chama" wakati una kadi ya kijani?
Kuheshimu mitazamo tofauti ni msingi wa demokrasia. Kujadili changamoto za wananchi kama vile madawa, walimu, ajira, na miundombinu ni muhimu bila kujali mrengo wa kisiasa. Badala ya kuhukumu watu kwa misimamo yao. Tatizo si rangi ya kadi ya mtu bali kusema kitu chenye mantiki kwa jamii.
 
Navoona ni kwamba utateseka bure kama utakua unakerwa na vitu vidogo vidogo kama hivi.
Harmonize anajiita jeshi, umeona jeshi limemmaind?
Lady Jay dee anajiita komando,umesikia makomando wakikereka?
Hata wewe unaweza kujiita unavotaka kikubwa kama unaona hilo jina linakua nguvu na ari fulani!
Ndio maana wengi wanajiita maraisi na wafalme lakini hakuna rais anayekereka na hilo.vitu vingine ni just for fun tu..
Kuna mambo makubwa ya kuwekea nguvu na muda kuliko kukasirishwa na vitu vidogo kama hivyo. Watu wanajiita majina mbalimbali kwa sababu zao iwe ni kwa mzaha, kiasili, kidini, kichawi au hata chapa yao binafsi. Kama Harmonize anajiita jeshi na Lady Jaydee komando, halina madhara kwa mtu mwingine. Lakini CHADEMA ni chama ambacho kinawakilisha na kugusa maisha ya watu wengi moja kwa moja hivyo ni lazima wajitafakari na kujiita majina yenye maana nayanayo wakilisha sifa ya jamii wanayoiongoza.
 
Habari,

Nimekuwa kimya kwa miaka mingi, kutokana na miangaiko ya hapa na pale.
Lakini kila ninapopita mitaani, vichochoroni na kwenye madimbwi ya maji na kutana na neno hili 'KAMANDA" nikirudi kwenye Uso kitabu, X, Insta, nikienda JF nakutana na neno hili "KAMANDA". Yaani mtu hata chakula chake cha siku kinamshinda anajiita ''KAMANDA''. Kiujumla KAMANDA ni neno kubwa sana na lenye uzito sana, nikisema hivi, nafikiri wale Makamanda wenzangu wa Jeshi wananielewa. Hili neno kiujumla Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wanalitumia kimkakati na wameshindwa kulitendea haki.

Basi Kamanda ni nani? neno "Kamanda" kwa ujumla linahusiana na uongozi, mamlaka, na uwezo wa kusimamia au kuongoza katika nyanja mbalimbali, hasa za kijeshi, usalama, na hata harakati za kijamii, katika hali yoyote ile ya mvua au jua na kuwa na msimamo wa kujitoa mhanga kwa ajili ya wenzako au misimamo yako.

Unaweza kuwa "umekula mbuzi mzima lakini mkia umekushinda", hapa kwenye kujitoa "mhanga", mseme tu ukweli na muwe-honest na nafsi zenu kumewashinda, hivyo nasema hivi "CHADEMA acheni kujipa vyeo vya movie za action, wakati hata kujificha msituni kwa siku moja kunawashinda!"

:Tssk:
Hao hilo jina liliondoka na slaa miaka ilee petrobas katambi akalizika na kuwapa jipya wakijulikana kwa jina la makarai!
 
Back
Top Bottom